Wivu kwa mchepuko

R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,278
5,319
Habari za wakati huu wana MMU,

Jumamosi ya juzi nilivyotoka kazini nikawa sina mahali pakwenda kupumzika kama mnavyojua hiyo siku huwa tunafanya kazi nusu siku.

Mke wangu kipenzi alikuwa amesafiri so nikaona niende kwa mchepuko wangu bila kutoa taarifa kwake. Nilivyofika mlangoni nikaona kuna sandals za kiume sikuwa na shaka ila radio ilifunguliwa kwa sauti ya juu sana.

Niligonga mlango wala sikupata majibu yoyote ikabidi nimpigie simu lakini haikupokelewa.Ikabidi nisepe ila roho ilikuwa inaniuma sana.

Baada ya dakika tano wala sikuwa nimefika mbali akanibip nikampigia. Akasema nipo kwenye gari simu ilivyoita sikuisikia, nikamuuliza nyumbani kuna mtu akasema nyumba ameifunga so hakuna mtu. Nikasikia hasira sana yaani amenifanya mimi boya.

Ikabidi nigeuze nirudi mpaka pale kwake ili nihakikishe kama kweli hakuna mtu au niliangalia vibaya. Bahati nzuri pale nilimfungulia biashara ya kuuza duka na duka lilikuwa wazi nikaenda dukani nikajifanya nahitaji kununua bidhaa pale mara akatoka yeye alivyoniona alipata mshtuko mpaka akawa ameganda tu pale hata hajanisemesha mbaya zaidi alikuwa amevaa upande tu wa kanga.

Nikamuuliza umerudi saa ngapi hakujibu nikamwaambia endelea na maisha yako mama siwezi kupigana mimi.

Jana Jumapili ilipita kimya hakunisumbua wala nini ila leo nashangaa ghafla nakuta msg ya kuomba msamaha na maelezo kibao wala sijamjibu mpaka sasa na nilishatia nia ya kumuacha moja kwa moja kwasababu sina nguvu za kupigania papuchi.

Kwa wale wazoefu hivi roho inapouma kwa mchepuko wako kuchepuka katika nyumba unayolipia kodi ni dalili ya wivu au ni kujihisi umefanywa mjinga?
 
Mara nyingi ndivyo ilivyo, kuwa unalipia kodi ya chumba/nyumba, biashrara umemfungulia, gari umemnunulia lakini bado kuna Msaidizi wako. Hapo wala usiwe mkali, endelea naye tu maana hata wewe ni mwizi hapo, huenda aliye kuwemo ndani ndiye mume mtarajiwa naye analipia hicho chumba na biashara kamfungulia.
 
Hapana mkuu huyu mwanamke nilimtoa Dodoma akafikia kwenye hiyo nyumba na alikuja hapa akiwa mgeni kabisa wa hili jiji la Makonda.

So huyo jamaa kama amempata basi huenda jamaa anajua kuwa yule mwanamke amelewa na yeye anachepuka kwa sababu eneo la pale anapoishi wengi wanajua mimi ndiye mume wake hata wpangaji wenzie huwa wanajua hivyo.

Sasa sijui ameutoa wapi ujasiri wa kuingiza mwanaume kwenye nyumba ile na yule jamaa sijui ndio wale msingi kiuno maana haogopi kwenda kulala kwenye nyumba ambayo hauilipii kodi.
 
Unamuonea wivu mchepuko kwa lipi labda?au wameisha?sijawai kumuonea mchepuko wivu wala kujiona mjinga..!
Mkuu nahisi kwa sababu mimi ndiye ninayemlipia hela na ya ile pango katika nyumba anayoishi na biashara ya duka nimefungulia .Lakini bado analeta kidume kwenye hiyo nyumba na kitanda nilichonunua mimi nahisi ndio kitu kinachoniuma roho.
 
Duuuhh kazi kweli kweli, mtenda akitendewa.

Kinachokuuma ni kile ulichowekeza kwa huyo mchepuko. Lakini pia ni dhana uliyojijengea kwa mchepuko, na dhana hiyo ni "kwa mchepuko wako ni free stress zone".

Hata hivyo ni Muda muafaka wa wewe kujitathimini. Je, kama wewe umeumia kiasi hicho na mkeo akijua una "spare tire" bila ridhaa yake ataumia kiasi gani.

NB : Pumzika au Acha mechi za mchangani.
 
Mkuu umenongea pointi nitajitathimini tena nijue wapi nilikosea ili nianze upya.
 
Tatizo anajua hata wewe si mali yake, unakwenda ukitaka, ukiwa na shida naye sio akiwa na shida nawe, hutakiwi kuumia roho kwasababu maneno kama hayo ya mpnz mkeo ndio ambayo yamemfanya akawe na wake. Usiumie huna mamlaka ya kukasirika
 
Mara nyingi ndivyo ilivyo, kuwa unalipia kodi ya chumba/nyumba, biashrara umemfungulia, gari umemnunulia lakini bado kuna Msaidizi wako. Hapo wala usiwe mkali, endelea naye tu maana hata wewe ni mwizi hapo, huenda aliye kuwemo ndani ndiye mume mtarajiwa naye analipia hicho chumba na biashara kamfungulia.
Ni kweli mkuu, hawa wawili wote ni wezi, inabidi wawe wadogo kwa muda. Wayamalize kiutu uzima
 
Badala roho ikuume kumsaliti mke wako roho inakuuma kuona mchepuko unagegedwa mxiouuu
Kwani nini iniume kwa mke wangu wakati sijasababisha matatizo yoyote kwa upande wake?Hivi wewe ukichepukaga na yule mtu wako huwa unaumia roho?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom