Wito watolewa kwa jamii kutoa taarifa za vitendo vya kikatili .

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Msaidizi wa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha ACP J. Kaijanante ametoa wito kwa jamii kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na vitendo vya kikatili kwa kutoa taarifa za vitendo hivyo katika vituo vya jeshi hilo.

Pia wadau wa haki za wanawake na watoto wemeaswa kutorudi nyuma pale wanapopata vitisho bali kushirikiana na jeshi hilo kutokomeza vitendo vya kikatili kwenye jamii.

Wadau mbalimbali wamesema kuwa vitendo vya kikatili vipo hata kwa wanaume ni wakati wa kila mtu kutoa elimu ili kujenga uelewa na kujua namna ya kuviripoti.

Vitendo vya kikatili sio vya kuvumilia, Karipoti sasa upate haki yako na pia saidia wengine waliopo katika hali hiyo kwa kuripoti sehemu husika.
 
Mpangaji mwenzangu ananinyanyasa kimapenzi jamani, nisaidieni kuripoti Polisi dawati la jinsia.
Karipoti kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nawe utapata msaada wa haraka
 
Back
Top Bottom