Wanabodi,
Huu ni wito tuu kwa wana jf kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa tuu, yaani tufanye "a constructive criticism" kama kuna mahali amekosea, au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme kwa lugha ya heshima na staha, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji huu utakuwa unamsaidia rais wetu na kuisaidia nchi yetu.
Nakiri kupandisha uzi huu kutokana na mchango wa mwana jf huyu
Rais wa nchi ni kama baba wa familia, anahitaji kuheshimiwa.
Hata akikosea anakosolewa kwa heshima fulani.
Hata akidanganya haitwi muongo.
Hata akichelewa kwenye shughuli haambiwi kachelewa maana mkubwa hachelewi bali anakuwa hajafika.
Simaanishi Magufuli ni malaika au hawezi kufanya makosa, Magufuli naye ni binaadamu tuu kama binaadamu wengine na siku zote binaadamu ni viumbe dhaifu, hivyo Magufuli naye ana madhaifu yake ikiwemo kupenda misifa, kuropoka na kufanya maamuzi ya papara na kukurupuka ila kwa vile ndie kiongozi wetu Mkuu, kuna mambo ambayo hatupaswi kuyasema hata kama ni kweli, ikiwemo kumuita rais ni muongo hata kama ni kweli sometimes ni muongo hatupaswi kusema rais ni muongo bali rais alikuwa ana joke au anatania tuu.
Mfano rais alipozungumzia Kufyatua watoto atasomesha bure. Tamko hili lilikwenda kinyume cha uzazi wa mpango, hapa rais aliropoka lakini haiwezi kusemwa rais karopoka, maana hata mimi nilishitushwa na tamko lile ( Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni Yake au ni ya Wale Wazee wa..?!.)
bali Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu aliibuka na kulitolea ufafanuzi tamko like kuwa lilikuwa sii kweli bali ni utani tuu akiwatania watani zake Wazaramo.
Mfano kwenye hoja ya udikiteta, ni kweli Magufuli ni dikiteta na hivyo ndivyo alivyo, na sio kwamba anajifanyisha, ila Tanzania hapa tulipo fikia, tulihitaji dikiteta na Mungu ametupatia Magufuli, badala ya kushukuru ndio kwanza tunalaumu.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Watu walipoitwa Vila.za, hatukunyamaza, tulitoa ushauri humu.
Wito kwa Baba Jesca: Watendee Haki Kina Jesca Wote Ili Nao Wapate Bahati Kama Jesca!.
Hata alipozungumzia mishahara ya peponi, pia tulitoa ushauri humu
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote
Hata majumbani mwetu baba ambaye ni Mkuu na kichwa cha nyumba, kuna mara kibao anakosea hasa sisi mababa wa Kiafrika kutokana na mambo ya kiasili ya Uafrika wetu, na pia sio malaika hivyo ana madhaifu mengi tuu ambayo wamama huyajua huyaona, huyavumilia lakini hawayasemi hadharani.
Kuna namna ya ukosoaji wa heshima wenye lengo la kujenga, a constructive criticism ambao hufanywa in good faith na kuna ukoasoaji wa udhalilishaji ambao hufanywa in bad faith, ridiculously kumdhalilisha, kumjengea chuki, achukiwe, kumshushia hadhi na heshima etc ambayo japo is the truth but the motive behind is ill motive.
Simaanishi sasa ndio wote kazi yetu iwe ni kumuimbia nyimbo za sifa na mapambio, no tumkosoe kwa heshima na kwa nia njema kabisa kwa lengo la kumrekebisha na kumsaidia na sio kumdhalilisha.
Tanzania ni yetu sote, sio Tanzania ya Magufuli pekee, we all have a role to play and a responsibility of duty of care kujenga na sio kubomoa.
Kuna watu katika kumbonda Magufuli, kila siku kazi yao ni kumbomoa tuu na kumsifia Nyerere, yaani kumtumia Nyerere as a reference, ila ukimwangalia Magufuli kwa jicho la karibu, huyu jamaa yuko kama Nyerere kwa karibu kila kitu
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia,Sio Kama Nyerere!.
Katika kujenga nchi the motive iwe ni kujenga kila kitu ikiwemo kujenga watu akiwemo rais anahitaji kuendelea kujengwa na sio kubomolewa tuu.
Japo nafahamu katika kujenga, kuna sehemu itakubidi ubomoe ndipo ujenge, ubomoaji huo hufanyika kwa makini sana ili usibomoe kusiko husika na kila ubomoaji huo ukifanyika hufuatiwa na ujenzi papo kwa papo! .
Nitapenda kuiona jf ya hivyo, wale waashi mahiri wa jf ambao kazi yao ni kubomoa tuu, wapewe jukumu la kujenga pia sio kila siku wao ni kubomoa tuu, mwisho watapewa sifa ya kuitwa wabomoaji tuu ili hali tuna wajenzi imara na mahiri humu tena waliopitia kozi za uanagenzi kwa wale mahiri kabisa.
Wana jf tuwe wakweli kumhusu Magufuli toka ndani ya nafsi zetu sio kwa kuvaa miwani yenye kuona mabaya tuu, mapungufu tuu na makosa pekee, bali kama kuna mema pia tuyaone, kama kuna mazuri pia tuyaangazie na kuyasema as encouragement kwa rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Ni sahihi unachokisema. Ila ni vizuri tujifunze kukosowa kwa staha siku zote na kwa watu wote na siyo kwa Rais tu.