Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
3,511
2,000
Wanabodi,
Huu ni wito tuu kwa wana jf kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa tuu, yaani tufanye "a constructive criticism" kama kuna mahali amekosea, au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme kwa lugha ya heshima na staha, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji huu utakuwa unamsaidia rais wetu na kuisaidia nchi yetu.

Nakiri kupandisha uzi huu kutokana na mchango wa mwana jf huyu

Rais wa nchi ni kama baba wa familia, anahitaji kuheshimiwa.

Hata akikosea anakosolewa kwa heshima fulani.

Hata akidanganya haitwi muongo.

Hata akichelewa kwenye shughuli haambiwi kachelewa maana mkubwa hachelewi bali anakuwa hajafika.

Simaanishi Magufuli ni malaika au hawezi kufanya makosa, Magufuli naye ni binaadamu tuu kama binaadamu wengine na siku zote binaadamu ni viumbe dhaifu, hivyo Magufuli naye ana madhaifu yake ikiwemo kupenda misifa, kuropoka na kufanya maamuzi ya papara na kukurupuka ila kwa vile ndie kiongozi wetu Mkuu, kuna mambo ambayo hatupaswi kuyasema hata kama ni kweli, ikiwemo kumuita rais ni muongo hata kama ni kweli sometimes ni muongo hatupaswi kusema rais ni muongo bali rais alikuwa ana joke au anatania tuu.

Mfano rais alipozungumzia Kufyatua watoto atasomesha bure. Tamko hili lilikwenda kinyume cha uzazi wa mpango, hapa rais aliropoka lakini haiwezi kusemwa rais karopoka, maana hata mimi nilishitushwa na tamko lile ( Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni Yake au ni ya Wale Wazee wa..?!.)
bali Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu aliibuka na kulitolea ufafanuzi tamko like kuwa lilikuwa sii kweli bali ni utani tuu akiwatania watani zake Wazaramo.

Mfano kwenye hoja ya udikiteta, ni kweli Magufuli ni dikiteta na hivyo ndivyo alivyo, na sio kwamba anajifanyisha, ila Tanzania hapa tulipo fikia, tulihitaji dikiteta na Mungu ametupatia Magufuli, badala ya kushukuru ndio kwanza tunalaumu.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Watu walipoitwa Vila.za, hatukunyamaza, tulitoa ushauri humu.
Wito kwa Baba Jesca: Watendee Haki Kina Jesca Wote Ili Nao Wapate Bahati Kama Jesca!.

Hata alipozungumzia mishahara ya peponi, pia tulitoa ushauri humu
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Hata majumbani mwetu baba ambaye ni Mkuu na kichwa cha nyumba, kuna mara kibao anakosea hasa sisi mababa wa Kiafrika kutokana na mambo ya kiasili ya Uafrika wetu, na pia sio malaika hivyo ana madhaifu mengi tuu ambayo wamama huyajua huyaona, huyavumilia lakini hawayasemi hadharani.

Kuna namna ya ukosoaji wa heshima wenye lengo la kujenga, a constructive criticism ambao hufanywa in good faith na kuna ukoasoaji wa udhalilishaji ambao hufanywa in bad faith, ridiculously kumdhalilisha, kumjengea chuki, achukiwe, kumshushia hadhi na heshima etc ambayo japo is the truth but the motive behind is ill motive.

Simaanishi sasa ndio wote kazi yetu iwe ni kumuimbia nyimbo za sifa na mapambio, no tumkosoe kwa heshima na kwa nia njema kabisa kwa lengo la kumrekebisha na kumsaidia na sio kumdhalilisha.

Tanzania ni yetu sote, sio Tanzania ya Magufuli pekee, we all have a role to play and a responsibility of duty of care kujenga na sio kubomoa.

Kuna watu katika kumbonda Magufuli, kila siku kazi yao ni kumbomoa tuu na kumsifia Nyerere, yaani kumtumia Nyerere as a reference, ila ukimwangalia Magufuli kwa jicho la karibu, huyu jamaa yuko kama Nyerere kwa karibu kila kitu
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia,Sio Kama Nyerere!.

Katika kujenga nchi the motive iwe ni kujenga kila kitu ikiwemo kujenga watu akiwemo rais anahitaji kuendelea kujengwa na sio kubomolewa tuu.

Japo nafahamu katika kujenga, kuna sehemu itakubidi ubomoe ndipo ujenge, ubomoaji huo hufanyika kwa makini sana ili usibomoe kusiko husika na kila ubomoaji huo ukifanyika hufuatiwa na ujenzi papo kwa papo! .

Nitapenda kuiona jf ya hivyo, wale waashi mahiri wa jf ambao kazi yao ni kubomoa tuu, wapewe jukumu la kujenga pia sio kila siku wao ni kubomoa tuu, mwisho watapewa sifa ya kuitwa wabomoaji tuu ili hali tuna wajenzi imara na mahiri humu tena waliopitia kozi za uanagenzi kwa wale mahiri kabisa.

Wana jf tuwe wakweli kumhusu Magufuli toka ndani ya nafsi zetu sio kwa kuvaa miwani yenye kuona mabaya tuu, mapungufu tuu na makosa pekee, bali kama kuna mema pia tuyaone, kama kuna mazuri pia tuyaangazie na kuyasema as encouragement kwa rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Ni sahihi unachokisema. Ila ni vizuri tujifunze kukosowa kwa staha siku zote na kwa watu wote na siyo kwa Rais tu.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Katiba katika Ibara ya 46(1-3) inazuia kumshitaki kwa sababu ya ''madudu'' aliyoyafanya wakati akiwa Rais wa Tanzania.

Hata akifanya ‘’madudu’’ na kuondoka, sioni retrospective legislation ikipata nafasi katika uwanja wa siasa za Tanzania.
Mkuu Msemaji Ukweli, ni kweli kifungu hicho ni Kinga ya rais kutokushitakiwa mahakamani, ila kinga hiyo inahusu rais kutokushitakiwa mahakamani katika utekelezaji wa majukumu ya kirais tuu na sio kila kitu.

Mfano Ben alipofanya biashara akiwa Ikulu, kufanya biashara Ikulu sii miongoni mwa majukumu ya kirais akiwa Ikulu hivyo anashitakika kwa kosa la abuse of office, na kutokushitakiwa ni kwa heshima tuu ya kumstahi aachwe apumzike kwa amani.

Au JK alipoyasamehe yale majizi ya EPA, hakuna kifungu chochote cha katiba yetu kinachompa rais mamlaka ya kuzuia sheria isichukue mkondo wake. Yaani jitu ni lijizi la malí ya umma, limekamatwa red handed, badala ya sheria kuachwa ichukue mkondo wake, majizi yale yalisamehewa!.

Kwa mujibu wa katiba, mwenye mamlaka ya kufungua mashitaka au kutofungua ni DPP na sio rais. Mamlaka ya rais ni kumsamehe mfungwa yoyote baada ya kuhukumiwa na sio kuzuia majizi yasishitakiwe, hivyo JK anashitakika ile kinga ya kutokushitakiwa haimhusu ila kwa heshima ameachwa apumzike kwa amani kama Ben, hivyo hata aliyepo ni kweli hata afanye madudu gani ikiwemo uvunjaji wa katiba, hatafanywa chochote, ataachwa apumzike tuu kwa amani.

Usikute hizi ni miongoni mwa sababu zinazopelekea bao la mkono au zisipotosha zitatosheshwa.

Paskali
 
treborx

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,634
2,000
Mimi nakubaliana na mleta uzi ingawa kuna mahali napata shida sana. "Constructive criticism" ni ya namna gani kwa common sense ya kawaida? Mimi nafikiri watu waseme mawazo yao mbadala. Na wayaseme vizuri kabisa, hata kama watasema hawakubaliani kabisa na mawazo ya mtu mwingine. Bado sioni tatizo liko wapi. Tuondokane na hii tabia ya kupenda kukubaliana kwa kila kitu kama penguins. Kuna dhana ya diversity inasema, kila mtu ana utofauti wa namna yake na wa kipekee. Hata wachangiaji wa Jf tuna mawazo mseto yenye kuakisi diversity zetu. Mtu asiyependa kusikia mawazo tofauti au asiyependa kukosolewa hajawahi kuishi katika sayari hii bado, ni mtu aliyejifungia kwenye box lake linaloitwa "illusion".
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Wanabodi,
Huu ni wito tuu kwa wana jf kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa tuu, yaani tufanye "a constructive criticism" kama kuna mahali amekosea, au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme kwa lugha ya heshima na staha, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji huu utakuwa unamsaidia rais wetu na kuisaidia nchi yetu.

Wana jf tuwe wakweli kumhusu Magufuli toka ndani ya nafsi zetu sio kwa kuvaa miwani yenye kuona mabaya tuu, mapungufu tuu na makosa pekee, bali kama kuna mema pia tuyaone, kama kuna mazuri pia tuyaangazie na kuyasema as encouragement kwa rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
huyu Magufuli ambaye kwa Upumbavu sana! Na Nasema Kwa Upumbavu sana Kwa Kuwa Yeyote anayeshabikia Approach ya Magufuli kwenye hili swala la Madini ni Mpumbavu kiasi cha kuhurumiwa. Awe ni Rafiki au Ni adui kwangu Nitasema kwa Masikitiko sina Jina Lingine la Kumpa ni Mpumbavu!.
Mkuu ,TL Marandu, hili ni angalizo tuu!.

Paskali
 
shinyangakwetu

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
1,756
2,000
Wanabodi,
Huu ni wito tuu kwa wana jf kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa tuu, yaani tufanye "a constructive criticism" kama kuna mahali amekosea, au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme kwa lugha ya heshima na staha, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji huu utakuwa unamsaidia rais wetu na kuisaidia nchi yetu.

Nakiri kupandisha uzi huu kutokana na mchango wa mwana jf huyu

Rais wa nchi ni kama baba wa familia, anahitaji kuheshimiwa.

Hata akikosea anakosolewa kwa heshima fulani.

Hata akidanganya haitwi muongo.

Hata akichelewa kwenye shughuli haambiwi kachelewa maana mkubwa hachelewi bali anakuwa hajafika.

Simaanishi Magufuli ni malaika au hawezi kufanya makosa, Magufuli naye ni binaadamu tuu kama binaadamu wengine na siku zote binaadamu ni viumbe dhaifu, hivyo Magufuli naye ana madhaifu yake ikiwemo kupenda misifa, kuropoka na kufanya maamuzi ya papara na kukurupuka ila kwa vile ndie kiongozi wetu Mkuu, kuna mambo ambayo hatupaswi kuyasema hata kama ni kweli, ikiwemo kumuita rais ni muongo hata kama ni kweli sometimes ni muongo hatupaswi kusema rais ni muongo bali rais alikuwa ana joke au anatania tuu.

Mfano rais alipozungumzia Kufyatua watoto atasomesha bure. Tamko hili lilikwenda kinyume cha uzazi wa mpango, hapa rais aliropoka lakini haiwezi kusemwa rais karopoka, maana hata mimi nilishitushwa na tamko lile ( Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni Yake au ni ya Wale Wazee wa..?!.)
bali Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu aliibuka na kulitolea ufafanuzi tamko like kuwa lilikuwa sii kweli bali ni utani tuu akiwatania watani zake Wazaramo.

Mfano kwenye hoja ya udikiteta, ni kweli Magufuli ni dikiteta na hivyo ndivyo alivyo, na sio kwamba anajifanyisha, ila Tanzania hapa tulipo fikia, tulihitaji dikiteta na Mungu ametupatia Magufuli, badala ya kushukuru ndio kwanza tunalaumu.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Watu walipoitwa Vila.za, hatukunyamaza, tulitoa ushauri humu.
Wito kwa Baba Jesca: Watendee Haki Kina Jesca Wote Ili Nao Wapate Bahati Kama Jesca!.

Hata alipozungumzia mishahara ya peponi, pia tulitoa ushauri humu
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Hata majumbani mwetu baba ambaye ni Mkuu na kichwa cha nyumba, kuna mara kibao anakosea hasa sisi mababa wa Kiafrika kutokana na mambo ya kiasili ya Uafrika wetu, na pia sio malaika hivyo ana madhaifu mengi tuu ambayo wamama huyajua huyaona, huyavumilia lakini hawayasemi hadharani.

Kuna namna ya ukosoaji wa heshima wenye lengo la kujenga, a constructive criticism ambao hufanywa in good faith na kuna ukoasoaji wa udhalilishaji ambao hufanywa in bad faith, ridiculously kumdhalilisha, kumjengea chuki, achukiwe, kumshushia hadhi na heshima etc ambayo japo is the truth but the motive behind is ill motive.

Simaanishi sasa ndio wote kazi yetu iwe ni kumuimbia nyimbo za sifa na mapambio, no tumkosoe kwa heshima na kwa nia njema kabisa kwa lengo la kumrekebisha na kumsaidia na sio kumdhalilisha.

Tanzania ni yetu sote, sio Tanzania ya Magufuli pekee, we all have a role to play and a responsibility of duty of care kujenga na sio kubomoa.

Kuna watu katika kumbonda Magufuli, kila siku kazi yao ni kumbomoa tuu na kumsifia Nyerere, yaani kumtumia Nyerere as a reference, ila ukimwangalia Magufuli kwa jicho la karibu, huyu jamaa yuko kama Nyerere kwa karibu kila kitu
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia,Sio Kama Nyerere!.

Katika kujenga nchi the motive iwe ni kujenga kila kitu ikiwemo kujenga watu akiwemo rais anahitaji kuendelea kujengwa na sio kubomolewa tuu.

Japo nafahamu katika kujenga, kuna sehemu itakubidi ubomoe ndipo ujenge, ubomoaji huo hufanyika kwa makini sana ili usibomoe kusiko husika na kila ubomoaji huo ukifanyika hufuatiwa na ujenzi papo kwa papo! .

Nitapenda kuiona jf ya hivyo, wale waashi mahiri wa jf ambao kazi yao ni kubomoa tuu, wapewe jukumu la kujenga pia sio kila siku wao ni kubomoa tuu, mwisho watapewa sifa ya kuitwa wabomoaji tuu ili hali tuna wajenzi imara na mahiri humu tena waliopitia kozi za uanagenzi kwa wale mahiri kabisa.

Wana jf tuwe wakweli kumhusu Magufuli toka ndani ya nafsi zetu sio kwa kuvaa miwani yenye kuona mabaya tuu, mapungufu tuu na makosa pekee, bali kama kuna mema pia tuyaone, kama kuna mazuri pia tuyaangazie na kuyasema as encouragement kwa rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Aanze kubomoa nyumba za serikali alizouza,arudishe hela za samaki Na meli mbovu arudishe hela zetu tutamuona anafanya la maana,yeye anagusa walikokosea wenzake tu Bali alikoboronga yeye anatutisha eti ataehoji MV DSM anahoji kifaru cha jeshi!!!!???huku ni kulipiza visasi maana ya kwake ni mengi Na hayaguswi Na ukijaribu wataku Ben SAA 8
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Pascal issue ya kukosoa JPm itabadilika pale atakapobadili lugha yake against Wapinzani wake Wa kisiasa.Pale atakapojua Uchaguzi umekwisha na Tanzania ni yetu sote.

Pale Wanachama wa CCM watakapojua miiko ya sheria na haki za RAIA kwamba hakuna aliye juu ya Sheria.

Matusi, Majigambo,udhalilishaji,ubaguzi,vitisho na visasi lazima vikemewe siyo wakati wake.

Tumepata Rais ambaye anaabudu na kuheshimu visasi,chuki na ubaguzi. Anayoyasema.mdomo ni si anayoyatenda.Yuko tofauti na Makamu wake a jitahidi kubadili ka amasivyo ameligawa Taifa na limegawanyika aone matendo yake kwamba ni maovu asikimbilie niombeeni.

Tutaliombea Taifa lakini si MTU mwenye Chuki, visasi na ubaguzi. Na katika marais atachukiwa na wengi sana.
 
Siyo hivyo tu aache chuki,visasi na ubaguzi havijengi Bali vinabomoa Taifa.
 
Mafuluto

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
1,770
2,000
Huu uzi sikuwahi kuuona kabla. In a way nashukuru sikuwa nimeuona !
Ila pia kama huyu ni yule yule Mayala sasa naelewa kwa nn ktk ule mkutano na waandishi wa habari yaliulizwa maswali ya kitoto !
Tatizo sugu kwa ss wa TZ ni unafiki !! Na utatumaliza milele na milele. Sasa sijui ni ukanjanja au, tuanze kufundishana siasa 101 ?

Zama hizi sio zama za ujima, people have to speak up their mind, na siyo mambo ya kupewa ubwabwa na kofia na kushangilia kila kitu !! Mikataba mliingia, mkaitetea kwa mbwembwe na kushangilia kwa kura za ndiyoooooo then leo mjifanye mna uchungu eti wazalendo ?

Mnasema tuwaombee kwa mungu kila siku huku nyuma mnakula rambirambi za watoto, na kutoa lugha chafu kwa waathirika wa tetemeko !!

Pascal issue ya kukosoa JPm itabadilika pale atakapobadili lugha yake against Wapinzani wake Wa kisiasa.Pale atakapojua Uchaguzi umekwisha na Tanzania ni yetu sote.

Pale Wanachama wa CCM watakapojua miiko ya sheria na haki za RAIA kwamba hakuna aliye juu ya Sheria.

Matusi, Majigambo,udhalilishaji,ubaguzi,vitisho na visasi lazima vikemewe siyo wakati wake.

Tumepata Rais ambaye anaabudu na kuheshimu visasi,chuki na ubaguzi. Anayoyasema.mdomo ni si anayoyatenda.Yuko tofauti na Makamu wake a jitahidi kubadili ka amasivyo ameligawa Taifa na limegawanyika aone matendo yake kwamba ni maovu asikimbilie niombeeni.

Tutaliombea Taifa lakini si MTU mwenye Chuki, visasi na ubaguzi. Na katika marais atachukiwa na wengi sana.
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,200
2,000
Uzi wa kijinga kabisa kupostiwa na MTU anaejiita GT hapa jamii forum, vyovyote iwavyo binadamu hapangiwi namna ya kufikiri,kutoa maoni n.k

Kuweni wema mtaona tu mambo yanabadirka yenyewe
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,533
2,000
Aanze kubomoa nyumba za serikali alizouza,arudishe hela za samaki Na meli mbovu arudishe hela zetu tutamuona anafanya la maana,yeye anagusa walikokosea wenzake tu Bali alikoboronga yeye anatutisha eti ataehoji MV DSM anahoji kifaru cha jeshi!!!!???huku ni kulipiza visasi maana ya kwake ni mengi Na hayaguswi Na ukijaribu wataku Ben SAA 8
amtoe na bashite ,
 
Thinktz01

JF-Expert Member
Feb 24, 2014
272
250
Wanabodi,
Huu ni wito tuu kwa wana jf kuhusu ukosoaji wa Rais wa nchi, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli,
kama kuna mahali amekosea, au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme kwa unyenyekevu kwa lugha ya heshima na staha, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji kwa rais,
ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa, yaani tufanye "a constructive criticism" hivyo ukosoaji huu utakuwa na nia ya kumsaidia rais wetu kuwa rais bora zaidi na kulisaidia taifa kusonga mbele na sio kurudi nyuma.

Nakiri kupandisha uzi huu kutokana na mchango wa mwana jf huyu

Rais wa nchi ni kama baba wa familia, anahitaji kuheshimiwa.

Hata ikitokea baba mwenye nyumba au baba nyumbani amekosea jambo fulani, anakosolewa kwa heshima kiutu uzima kwa kutumia lugha ya heshima na staha na sio lugha ya machukizo au matukano! .

Hata akidanganya haitwi muongo anaitwa hayuko sahihi sana, au ameshauriwa vibaya!.

Hata akichelewa kwenye shughuli haambiwi kachelewa maana mkubwa hachelewi bali anakuwa bado hajawasili kutokana na kutingwa na shughuli muhimu, na asipotokea kabisa ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu!.

Simaanishi rais Magufuli yeye ni malaika hivyo hawezi kukosea au kufanya makosa, no!, rais Magufuli naye ni binaadamu tuu kama sisi binaadamu wengine wrote, na siku zote sisi binaadamu ni viumbe dhaifu, hivyo rais Magufuli naye ana madhaifu yake ikiwemo kuonekana kama ni mtu wa kupenda misifa, anapoongea kuna wakati anaonekana kama ni msema hovyo au kama anaropoka, na katika kufanya maamuzi, kuna wakati anaonekana kama anatenda kwa pupa au papara na baadhi ya maamuzi yake, kuonekana kama ni maamuzi ya kukurupuka ila kwa vile yeye ndie kiongozi wetu Mkuu, kuna mambo ambayo hatupaswi kuyasema hivyo yalivyo, hata kama ni kweli, ikiwemo kumuita rais ni muongo hata kama ni kweli sometimes anaweza kusema kitu cha uongo hatupaswi kusema rais ni muongo bali rais alikuwa hajashauriwa vizuri au alikuwa ana joke tuu, au anazungumza kwa utani tuu, yaani rais anatania.

Mfano rais alipozungumzia Kufyatua watoto atasomesha bure. Tamko hili lilikwenda kinyume cha uzazi wa mpango, hapa rais ni kama aliropoka tuu lakini haiwezi kusemwa rais karopoka, bali rais alikuwa anatania tuu watani zake, wazaramo!. Siku alipotamka hivyo, hata mimi nilishitushwa na tamko lile ( Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni Yake au ni ya Wale Wazee wa..?!.)
Lakini baada ya siku mbili tatu, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu aliibuka na kulitolea ufafanuzi wa kina tamko lile kuwa lilikuwa sii kweli bali rais alikuwa akiwatania tuu watani zake Wazaramo!.

Mfano kwenye hoja ya udikiteta, ni kweli rais Magufuli ni kama dikiteta fulani havi, lakini hivyo ndivyo alivyo, na sio kwamba anajifanyisha, ila pia, Tanzania hapa tulipo fikia, tulihitaji sana mtu mwenye silika za udikiteta na Mungu akaisikia sala yetu ametupatia rais Magufuli ambaye ni dikiteta kweli ila ni dikiteta mzuri benevolent dictator hivyo badala ya watu kuulaumu huu udikiteta wa rais Magufuli, tunapashwa kushukuru Mungu!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Watu walipoitwa Vila.za, hatukunyamaza, tulitoa ushauri humu.
Wito kwa Baba Jesca: Watendee Haki Kina Jesca Wote Ili Nao Wapate Bahati Kama Jesca!.

Hata alipozungumzia mishahara ya peponi, pia tulitoa ushauri humu
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Hata majumbani mwetu hasa majumba ya Kiafrika na Kiswahili, baba ambaye ni mkuu na kichwa cha nyumba, kuna mara kibao anakosea hasa sisi mababa wa Kiafrika tunaofuata mila zetu za kiasili ya Uafrika wetu, na pia sio malaika hivyo tuna madhaifu mengi tuu ambayo wamama huyajua huyaona, huyavumilia lakini hawayasemi hadharani.

Kuna namna ya ukosoaji wa heshima na staha wenye lengo la kujenga, a constructive criticism ambao hufanywa in good faith na kuna ukoasoaji wa udhalilishaji wenye lengo la kubomoa ambao hufanywa in bad faith, ridiculously au kumdhalilisha, mkosolewa kwa nia ya kumjengea chuki, achukiwe, kumshushia hadhi na heshima ili aonekane ni mtu wa hovyo, etc huu sio ukosoaji mzuri hata kama ni kweli amekosea, yaani japo is the truth but the motive behind is ill motive.

Simaanishi sasa ndio wote kazi yetu iwe ni moja tuu, kumhusu rais wetu, iwe ni kumuimbia tuu nyimbo za sifa na mapambio, no !, tumkosoe rais Magufuli kwa heshima na kwa kutumia lugha ta staha kwa nia njema kabisa kwa lengo la kumrekebisha na kumsaidia na sio kumdhalilisha.

Tanzania ni yetu sote, sio Tanzania ya Magufuli pekee, we all have a role to play and a responsibility of duty of care kujenga nchi yetu na sio kuibomoa na kumjenga rais wetu na sio kumbomoa.

Kuna watu katika kumbonda rais Magufuli, kila siku kazi yao ni kumbomoa tuu na wengine humsifia Nyerere, yaani kumtumia wasifu wa Nyerere as a reference, ila kiukweli ukimwangalia rais Magufuli kwa jicho la karibu, yuko kama Nyerere kwa karibu kila kitu
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia,Sio Kama Nyerere!.

Katika kujenga nchi the motive iwe ni kujenga kila kitu ikiwemo kujenga watu akiwemo rais anahitaji kuendelea kujengwa na sio kubomolewa tuu.

Japo nafahamu katika kujenga, kuna sehemu inaweza ikakubidi ubomoe kwanza ndipo ujenge, ubomoaji huo hufanyika kwa makini sana ili usibomoe kusiko husika na kila ubomoaji huo ukifanyika hufuatiwa na ujenzi papo kwa papo! .

Nitapenda kuiona jf ya hivyo, wale waashi mahiri wa jf ambao kazi yao ni kubomoa tuu, wapewe jukumu la kujenga pia sio kila siku wao ni kubomoa tuu, mwisho watapewa sifa ya kuitwa wabomoaji tuu ili hali tuna wajenzi imara na mahiri humu tena waliopitia kozi za uanagenzi kwa wale mahiri kabisa.

Wana jf tuwe wakweli kumhusu rais Magufuli toka ndani ya nafsi zetu sio kwa kuvaa miwani yenye kuona upande mmoja tuu wa mabaya tuu, mapungufu tuu na makosa pekee, bali kama kuna mema pia tuyaone, kama kuna mazuri pia tuyaangazie na kuyasema as encouragement kwa rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Utumwa ni Utumwa Tuu, hata wa Fikra nao ni Utumwa.
 
Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,344
2,000
Mwenye kuhitaji kuheshimiwa anapaswa kuanza kujiheshimu mwenyewe na kuwaheshimu wale wanaomzunguka nk. Zile kauli za bukoba na moshi zilikupendeza wewe? Uvunjaji wa dhahiri wa katiba kuhusu mikutano ya vyama vya siasa wewe unaridhika nao? Hebu tufike mahali kijiko tukiijua kijiko tu
 
Who Cares?

JF-Expert Member
Jul 11, 2008
3,518
2,000
Mwenye kuhitaji kuheshimiwa anapaswa kuanza kujiheshimu mwenyewe na kuwaheshimu wale wanaomzunguka nk. Zile kauli za bukoba na moshi zilikupendeza wewe? Uvunjaji wa dhahiri wa katiba kuhusu mikutano ya vyama vya siasa wewe unaridhika nao? Hebu tufike mahali kijiko tukiijua kijiko tu
Mkuu upo sahihi...ila post hii ilitolewa kipindi kile cha kujipendekeza kupata UKUU wa mikoa na wilaya.
sahivi huyu Pasco mwenyewe anamnyea mukulu ipasavyo...maana hatamani tena kupata hata ujumbe wa 10 houses
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Utumwa ni Utumwa Tuu, hata wa Fikra nao ni Utumwa.
Naunga mkono hoja, tena Mwalimu Nyerere alitufundisha, hakuna umasikini mbaya kama umasikini wa fikra. Ila pia heshima ni kitu cha bure. Katika vitabu vyote vya dini tunafundishwa utii wa mamlaka halali. Na katika mila zote na desturi zote za Kiafrika tunafundishwa kuwaheshimu wakubwa. Na katika familia zetu tunafundishwa kuwaheshimu wazazi, waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani. Rais wa nchi ni kiongozi wako, ni mkubwa kwako na ni kama baba wa familia ya Watanzania, hivyo pamoja na yote, anastahili heshima. Hivyo mimi katika hili la heshima, nakiri kuwa mtumwa!.

P.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom