Hii habari mbona siielewi? Nini hasa kilichotokea? Walipigana au Sofia ndiye aliyempiga mwenzie? Tunaposema hadharani tuna maana gani? Nilidhani haya yalitokea kwenye kikao cha ndani na si kwenye public forum? Hiyo kauli chafu ilitokana na nini? Na ni nini hasa kilisemwa? Kwani kosa ni kumtukana aliyemzidi umri au kutukana period? Yaani angemtukana aliye na umri mdogo kwake ingekuwa sawa?
Hii habari nilipoiona kwanza ilikuwa imeletwa kishambenga ili kuthibitisha kuwa wanawake hawastahili nafasi za uongozi! Ilizungumzia kunyosheana vidole kimipasho na kadhalika. Wengi tukaingia kwenye mtego na wengine hata kudiriki kudaio kuwa huu ugomvi ni wa kugombania bwana (ikithibitisha kuwa wanawake hawana la maana la kugombania bali mabwana). Tunamlaumu Sofia kwa kile tunachokiita ushangingi. Angekuwa mwanaume kafanya hivyo, nae tungemsemaje
Kwangu mimi niliona haikuwatendea haki wote wawili. Hata ile ya kutaka wakina Guninita wasuhishe nalo ilizidi kuniumiza maana iliendelea kuthibitisha imani yetu kuwa mwanamke hata awe na umri au wadhfa gani ni lazima asimamiwe na mwanaume! kwa nini suala hili walishindwa kulitatua ndani ya jumuia kama wenzao vijana walivyofanya dhidi ya Nape (?)? Kwa nini wamekimbilia kwa wanaume?
Mimi nadhani kuna kitu kimejificha kwenye ishu nzima. Naomba aliyeleta mada anisaidie kwa kunieleza yaliyojiri kwenye hicho kikao au mkutano wa hadhara.