WITO: Bi Sophia Simba Jiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WITO: Bi Sophia Simba Jiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bowbow, Sep 16, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanabodi,

  Waziri Sofia Simba anashika wadhifa mkubwa sana kwenye serikali ya awamu ya nne, kwani wizara yake ndio kioo cha viongozi wote yaani Utawala bora. Wizara hii ndio inayongalia mienendo na maadili ya viongozi wote wa umma. Inakemea ukiukwaji wote wa haki za watumishi wa umma.

  Je Sofia Simba anastahili tena kuiongoza wizara hii???????

  Je kupigana hadharani na kiongozi mwenzako ni maadili ya uongozi????

  Je kujichukulia sheria mkononi ni utawala boraa??????

  Kutoa kauli chafu mbele ya hadhara tena kumtukana mtu aliyekuzidi umri ndio maadili ya mwanamke wa kitanzania?????????

  Kutokupeleka malalamiko yako kwenye mamlaka husika kabla ya kujichukulia sheria mkononi ndio maadili ya utawala bora?????

  Hayo pamoja na mengine mengi uliyoyafanya HUSTAHILI TENA KUWA KIONGOZI WA HIYO WIZARA WALA UONGOZI WOWOTE WA UMMA

  Bi Sofia Simba JIUUUZULU, JUIZULU JIUZULU
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  umemuandikia?au yumo humu?if not ssa ujumbe ataupataje?
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Umetumwa na Janet Kahama?

  Kama kuna mtu kampiga huyo mtu aende pilisi ili ukweli ujulikane, vinginevyo hizi ni Kampeni za uchaguzi tu hakuna lolote la maana.
   
 4. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwl Nyerere aliwahi kusema katika moja ya speech zake kuwa "kiongozi huwezi kuishi kihuni huni tu"....Naona siku hizi hawa mawaziri wa JK adabu zero kabisa.......Namshauri hata Mama kahama akaripoti polisi kwa shambulio la aibu inaweza kuwa fundisho kwa wengine....Huyo Sophia Simba uswahili mwingi ndio tatizo.
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Mh! Makubwa...kwa nchi za wenzetu hawa walitakiwa wajiuzulu kwanza..wakapigane wamalize ndo warudi kweny utawala. Kwani anayedai kupigwa karipoti kituo kipi cha polisi?
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mawaziri wote wahuni tokana na RAISI NAYE MUHUNI. Tutegemee nini?
   
 7. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Give me a break! Kwa nini sasa huyo Janeth naye asiambiwe ajiudhuru. Wagombane wawili ajiuzudhuru mmoja! Hizi ni porojo za kampeni tu, hakuna kitu. Kwanza logically Kahama alikosa adabu kwa waziri
   
 8. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  First Lady

  nakuhakikishia ujumbe ataupata tena very soon
   
 9. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kama kila mtu atatumwa na wanasiasa kuja kumsea hapa JF,

  basi na wewe utakuwa umetumwa na Sofia if I can say so.

  kikubwa ni kuangalia nguvu ya mada na sio nani katoa mada.
   
 10. M

  Masatu JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wamethibitisha WOTE hawafai kugombea uenyekiti uwt
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Aripoti polisi tena aonekana mambo ya chama anayatoa nje ya utaratibu?
  To aliyepigwa this is a golden ticket to win the race! The fact that amempeleka kwenye vikao vya chama na sio polisi - ni ushindi tosha.Atabakiza kazi ndogo sana.Aliyeonyesha umwamba ana kazi ya kujisafisha mbele ya UWT na CCM. Kazi kwake.
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hapa ni ulingo wa UWT - Janet ni mwenyekiti UWT mkoa..hakuna cha uwaziri hapa.... Sophia alipaswa kumheshimu mwenyekiti wake!
  tusichanganye mambo.
   
 13. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #13
  Sep 16, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  hizi ni siasa za mwaka 2010...unajua kikwete anataka kuhakikisha anadhibiti jumuia zote za chama kwa kuweka watu wake ..ili kuweza kuwazima wanaotaka kuchukua fomu kupinga kipindi chake cha pili....

  huyu sophia simba anazo baraka za kikwete kugombea hii nafasi...ila kosa kubwa alilofanya ni kuleta dharau kwa mwenyekiti wake wa mkoa ikiwemo tabia ya kishangingi ya kutukana na kupigana ...hii ni tabia ambayo haifai hasa ukizingatia sophia ni WAZIRI WA UTAWALA BORA...[wizara muhimu inayosimamia mambo nyeti nchi hii..maadili,usalama wa taifa,na TAKUKURU...]....waziri wa wizara hii ana nguvu kubwa nyuma yake akiamua kuitumia wagombea wezake hawatamuweza.......

  ...kuna uwezekano mkubwa wajumbe kwenye mikutano mikuu ya jumuia wakapiga kura za chuki kuwakataa wagombea wa kikwete....utakuwa uchaguzi kipimo cha nguvu ya kikwete chamani na kwenye jumuia ambayo inaelekea kushuka ...hasa kutokana na kitendo cha kuwepo mpasuko mkubwa....lets wait and see...
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Kweli nami nakubaliana na mtoa mada hapo juu kuwa Sophia ni chaguo la JK kwenye nafasi hiyo ya Mwenyekiti...ila jamani huyu Mama ana nini?mbona hana uwezo na inajulikana wazi kabisa?anataka nini?anataka wanachama hao wamueleweje?kwani hajatosheka alipo?au anataka watu tumdharau kwa kutompa hata ubunge wa kuteuliwa?namshangaa sana ila kwa sababu serikali na chama chao wote uozo mtupu..............
   
 15. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  FM ES,

  Naomba uje mkuu umchambue huyu mama. Tupeni wasifu wake huyu waziri.
   
 16. Lasthope

  Lasthope Senior Member

  #16
  Sep 17, 2008
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu sofia simba mbona ana tabia za kishangingi hivi< mi nakuabaliana yeye ndo ajiuzulu coz alitakiwa awe na heshima japo kidogo kutokana na nafasi aliyonayo ila tabia za kitaarab taarab, uswahili bin mtupu ndo anaonyesha. Ndo maana wanawake tunadharaulika kila siku na kuonekana tuna upeo mdogo sababu ya watu kama hawa kina sofia. na uwaziri wote lakini hajui hata kujiheshim
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hii habari mbona siielewi? Nini hasa kilichotokea? Walipigana au Sofia ndiye aliyempiga mwenzie? Tunaposema hadharani tuna maana gani? Nilidhani haya yalitokea kwenye kikao cha ndani na si kwenye public forum? Hiyo kauli chafu ilitokana na nini? Na ni nini hasa kilisemwa? Kwani kosa ni kumtukana aliyemzidi umri au kutukana period? Yaani angemtukana aliye na umri mdogo kwake ingekuwa sawa?

  Hii habari nilipoiona kwanza ilikuwa imeletwa kishambenga ili kuthibitisha kuwa wanawake hawastahili nafasi za uongozi! Ilizungumzia kunyosheana vidole kimipasho na kadhalika. Wengi tukaingia kwenye mtego na wengine hata kudiriki kudai kuwa huu ugomvi ni wa kugombania bwana (ikithibitisha kuwa wanawake hawana la maana la kugombania bali mabwana). Tunamlaumu Sofia kwa kile tunachokiita ushangingi. Angekuwa mwanaume kafanya hivyo, nae tungemsemaje?

  Kwangu mimi niliona haikuwatendea haki wote wawili. Hata ile ya kutaka wakina Guninita wasuluishe nalo ilizidi kuniumiza maana iliendelea kuthibitisha imani yetu kuwa mwanamke hata awe na umri au wadhfa gani ni lazima asimamiwe na mwanaume! Kwa nini suala hili walishindwa kulitatua ndani ya jumuia kama wenzao vijana walivyofanya dhidi ya Nape (?)? Kwa nini wamekimbilia kwa wanaume?

  Mimi nadhani kuna kitu kimejificha kwenye ishu nzima. Naomba aliyeleta mada anisaidie kwa kunieleza yaliyojiri kwenye hicho kikao au mkutano wa hadhara.
   
  Last edited: Sep 17, 2008
 18. L

  Lorah JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2008
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0  issue ni kwamba jamii inajua amepigana hadharani siko upande wowote lakini ni aibu hasa kutokana na wizara aliyonayo sasa naweza kuelewa kwanini viongozi wetu hawana maadili muongozaji wizara mbovu, mimi kama mwanamke nawomba wote watupishe tunataka kuchukua nnchi hii kwani wanaume wameshashindwa sasa hao ni mfano mmbaya hatuko tayari kuendelea nao KIKWETE VIPI JAMANI ndo wanawake uliowaona? mhh! nimechoka kabisa na li kadi lenu la CCM nawarudishia
   
 19. K

  Kandambili Member

  #19
  Sep 17, 2008
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nina wasi wasi na FIRST LADY, mbona unaelekea kuwatetea sana akina mama wa CCM, jana nimemsikia kiongozi wao eti KAMA KUNA WANAOWATISHA WAAMBIAENI WAKAWATISHE WATOTO WAO NA WAUME ZAO.....
  du nilishangaa kwa kicheko kuona kiongozim mzima anatoa vijembe vya taarabu. kumbe sio tu wanaume wa CCM ni vituko hata wake zao pia.
   
 20. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hi ni treak ya washindani wa Aunt Sophy, kimsingi ktk wagombea wote yeye ndie aliyekuwa na nafasi ya kushinda nafasi kiulaini sasa ninashindwa kuelewa ni nani amemwingiza ktk trap hiyo? Yeye mwenyewe si mtu ushari kiasi ila ni lazima nikiri kuwa chaguzi za CCM ktk mikoa ya DAR -Morogoro mchezo huu ni wa kawaida sana ila kuna kitu behind hapa ambacho sisi hatujaonyeshwa na mlalamikaji na mlalamikiwa. Huenda PM anachosema kina ukweli ila ni vema tukajikita ktk kuichunguza hii hali vizuri maana akina Mamuya wako jiii nao wamechukua form pia.

  Aunt Sophy , simama imara ktk hili maoni yako yahifadhi uyatumie ktk vikao halali vya chama na si magazetini maana kwa kuyaanika magazetini yalojiri kikaoni ni kukihujumu chama.

  Steak ktk msimamo wako,
  Tumia dada zako na kaka zako jipange uishinde vita hii ambayo tayari ishaonyesha adui zako wako tayari kukuangamiza kwa silaha yoyote ile.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...