PreGE2025 POTOSHI Witara akimwaga machozi baada ya kuliwa kichwa na wajumbe

PreGE2025 POTOSHI Witara akimwaga machozi baada ya kuliwa kichwa na wajumbe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Waitara analia. Magufuli hayupo

Wajumbe wamemla kichwa tayari











Screenshot_20250712-120156.jpg
 
Tunachokijua
Mwita Waitara ni mwanasiasa kutokea nchini Tanzania. Kwa sasa Waitara ni mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini anayemaliza muda wake kwa tiketi ya CCM, awali amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Ukonga mwaka 2015 kupitia tiketi ya CHADEMA.

Madai

Julai 12, 2025 kumeibuka kipande cha video kikimuonesha mbunge wa Tarime vijijini anayemaliza muda wake, Mwita Waitara aikimwaga machozi mbele ya waandishi wa habari na kuelezwa kuwa tukio hilo linakuja mara baada ya yeye kukatwa jina na wajumbe.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache tangu mchakato wa kutafuta wagombea wa ubunge, udiwani na baraza la wawakilishi kwa chama cha mapinduzi kuzinduliwa rasmi.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa kipande hicho si cha hivi karibuni.

Kipande cha video kinachomuonesha Mwita Waitara mbunge wa Tarime Vijijini akilia si ya mwaka 2025 na haihusiani na mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2025.

Kipande hicho cha video ni kutoka katika sehemu ya hotuba aliyoitoa Waitara Machi 28, 2023 alipokuwa akizungumzia adha ya migogoro ya mipaka Jimboni mwake.

Aidha kwa mujibu wa ratiba ya CCM katika mchakato huo bado unaendelea katika ngazi mbalimbali.
Back
Top Bottom