Wirearchy imeondoa ukubwa (adults)

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,420
2,271
Ni ukweli usiofichika kuwa social network imeweza kuondoa kabisa ile ya habari ya adults, usijali sana kuhusu jukwaa la wakubwa hapa JF, bali jaribu kuangalia njinsi mambo yanayokwenda.. Mfano NN anaovyotongoza vimwali vya hapa JF, na jinsi mijimama inavyotongoza vijana hapa JF. Au angalia jinsi MKJ anavyoweza kuwatupia madongo waliopo kwenye system pasipo wasiwasi wowote!

Au jaribu kuangalia waajili wanavyohaha na kutafuta pasiwodi za watumishi wao kwenye mitandao ya kijamii! Au jinsi yule kijana(anataka uprez) alivyoweza kunukuliwa vibaya na watumia mitandao! Hebu pima kwa kiasi gani mfumo wa Hierarchy unavyoanguka katika karne hii mpya ya wire! Wenyewe wanaita Wirearchy.

Soon itatinga Tz, upuuzi, ubabaishaji, rushwa na kupigiwa magoti kwa waliokwenye system utatatoweka! Hebu fikiria kila mtz akiwa amesajiriwa kwenye data base, akijulikana anafanya nini ana kipato gani, analipa kodi kiasi gani na msharaha kiasi gani? Wala sio kujua anatoka na nani(JF style kama ilivyokuwa The Utamu).

Jaribu kufikilia TRA itapokuwa baada ya kuvamiwa na mfumo mpya wa Wirearchy... Wenye magirlfriend wazuri hawatakuwa na woga tena wa kunyang'anywa wasichana wao na maafisa wa TRA. Hii ina maana kila hesabu itakuwa hewani na kuondoa kabisa rushwa, ambayo inawafanya wafanyakazi wa TRA kuonekana ka miungu, na kero kwa maisha ya kila siku. Hapatakuwa tena uoga wa kuijua TRA na wajibu wake kwa wananchi na kwa nchi kwa ujumla.

Ufanisi katika makampuni na mashirika utaongezeka mara dufu, kumbuka hata bosi atakuwa akitegemea ushirikiano zaidi toka kw a watendaji wake kutokana na upana wa utandawazi, hivyo ile habari ya bosi kujua kila kitu kutoweka.

Sio siri Mahakama na Jeshi la ulinzi(JWTZ) itachukua muda kuona mwanga huu, hata hivyo sina shaka nao hawatokuwa mbali kwani wanastahili kulipa kodi vilevile!...

Mfumo huu mpya utaweka wazi kila ngazi ya mtanzania, hivyo itakuwa ni rahisi kwa mtanzania kujua anataka kuishi katika nafasi ipi maishani mwake.
 
Kumbe Preta ni jimama... Naona pilikapilika zake hapa jamvini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom