Windows 7 toleo la Kiswahili – asante Microsoft

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956

Kwa kutambua umaarufu na umuhimu wa lugha ya Kiswahili duniani,Microsoft wametoa pack ya Kiswahili kwa ajili ya Widows 7 na Microsoft Office. Pack hii inapatikana online na zaidi ya yote ni BURE. Akizungumzia toleo hili boss wa Microsoft Afrika Mashariki na Kusini bwana Louis Otieno alisema

“zaidi ya watu million 150 wanaozungumza Kiswahili Afrika sasa wanaweza kuanza kutumia technolojia kwa lugha waipendayo na kuielewa zaidi. Hii ni mojawapo ya njia za kupanua wigo wa lugha duniani”.

Tazama video ya ufunguzi huo hapa chini.

Viongozi na wabia mbalimbali Afrika na duniani kote wameipokea habari hii kwa furaha kubwa. Mkurugenzi wa elimu nchini Kenya mama Lydia Nzomo amesema Windows 7 ya Kiswahili ni ushindi kwa watoto wa shule za msingi kwani

itawasaidia kujua kutumia komputa haraka.
Microsoft wanasema toleo hili litahamasisha serikali za nchi husika kuongeza uwekezaji kwenye mambo ya IT, kupunguza ujinga na kuwavutia watu wengi zaidi kutumia komputa hasa kwenye nchi hizi ambazo utumiaji wa komputa bado ni mdogo.

Kazi ya kutengeneza toleo la Kiswahili lilifanywa na wataaluma wa lugha ya Kiswahili kutoka Afrika mashariki na kati kwa muda wa miaka miwili. Aliyeiongoza kazi hii ni mtafasiri wa lugha ya Kiswahili ndugu Mpasua Msonobari. Mpasua alisema kuna maneno zaidi ya 300,000 yliyotafasiriwa kwa Kiswahili kwenye toleo hilo jipya.
Download kwa kubonyeza hapa kupata toleo lako la Windows 7 toleo la Kiswahili
Microsoft wamekuwa wakishirikiana na nchi mbali mbali Afrika na duniani ili kuzitambua na kuzitafasiri lugha mbalimbali.

Habari hii ni nzuri lakini watanzania tujiulize, je, kuna mtanzania aliyeshiriki katika kazi hii? Tanzania inaongoza na kusifiwa kwa kukienzi na kukiendeleza Kiswahili, kama hatujihusishi kwenye project kubwa kama hizi si kazi bure. Mpasua aliyeongoza kazi hii ni mRwanda-mKenya watanzania tuko wapi? Changia mawazo yako.
 
Last edited by a moderator:
0L7C0234.jpg

​
 
Haya sasa msingizie kingereza ndio shida kutumia kompyuta, kilichobaki msingizie hela tu ya kununua kompyuta na c zaidi... Soon iOS na Android wanaleta kiswahili pia, nenda china hadi mbibi anatumia ipad kwenye train na anajidai kwelikweli, sasa bongo washindwe...
 
Ni wazo zuri la kuitafsiri hyo window 7 maana watu wengi wasiojiua lugha ya kiingereza watapata fursa nzuri za kutumia komputa bila woga, ila nimesikitika kusikia hamana Mtanzania aliyeshiriki katika mpango huo. Watanzania inabidi kuchangamkia fursa kubwa kama hizi, sa hapo kama tukikuta ina makosa kwenye baadhi ya misamiati tutamlaumu nani wakati hatukushiriki kwenye uundaji wake?
 
m nadhani ktk ligha ya kiTechnologia kwa kweli kiswahili ni kigumu sana tena sana kuna cku nlishika cm inayo run kiswaz!!!!!!!!!!!!!!!!!! duh nilchoka
:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
 
Ni kweli kabisa nakubaliana na wewe ... wewe angalia mfano wa maneno yenyewe
Muhtasari
Kipeto Lugha hiki Kiolesura cha Windows (LIP) hutoa toleo lililofasiriwa nusu la maeneo yanayotumika sana ya Windows. Baada ya kusanidi LIP, matini katika vigagula, vikasha ongezi, menyu, na mada za Msaada na auni zitaangazishwa katika lugha ya LIP. Matini ambayo hayajatafsiriwa yatakuwa katika lugha msingi ya Windows 7. Kwa mfano, kama ulinunua toleo la Kihispania la Windows 7, na ukasanidi LIP ya Kikatalani, matini mengine yatabaki katika Kihispania. Unaweza kusanidi zaidi ya LIP moja kwa lugha moja msingi. LIPs za Windows zinaweza kusanidiwa kwa matoleo yote ya Windows 7.

Maagizo
ONYO: Kama una usimbaji fiche wa BitLocker uliowezeshwa, tafadhali usitishe kabla ya kusanidi LIP. Fungua Control Panel, teua System and Security, kisha BitLocker Drive Encryption. Bofya kwenye Suspend Protection.

Kwa sababu kuna vipakuaji vya kando vya matoleo ya 32-biti na 64-biti vya Windows 7 LIP, kabla ya kuanza kupakua, unahitaji kubainisha ni toleo lipi la Windows 7 ulilosanidi. Hivi ndivyo unavyostahili kubainisha ni toleo lipi la Windows 7 ulilosanidi:

Source: Maelezo ya upakuaji: Windows 7 LIP
 
hii lugha kama ndiyo kiswahili,itachukua miaka kadhaa kuwafundisha watumiaji wa computer kuielewa.binafsi naona giza tu( mfano neno kipeto.usimbaji fiche,kikatalani)
 
Mkuu Dotworld Poa tu mimi mbona ninatumia na ipo Poa kichizi.Mkuu leo.leo Jizoesheni Lugha yenu acheni Utumwa wa lugha za wageni lugha ya kizungu jifunzeni lugah yaenu kwa njia ya Computer jamani acheni uvivu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Dotworld Poa tu mimi mbona ninatumia na ipo Poa kichizi.Mkuu leo.leo Jizoesheni Lugha yenu acheni Utumwa wa lugha za wageni lugha ya kizungu jifunzeni lugah yaenu kwa njia ya Computer jamani acheni uvivu.
Sio uvivu Mkuu MziziMkavu Unajua hii lugha ukiingia kichwa kichwa unaweza ukatoka kapa, unaweza ukajikuta unataka ku-accept command kumbe ndio una-DELETE.

Chukua kwa mfano maneno hayo hapo kwenye web page yao MOJA TU ya kiswahili imejaa maneno kama

  • Kipeto,
  • Kiolesura,
  • Kusanidi,
  • Matini katika Vigagula,
  • Vikasha ongezi,
  • Auni zitaangazishwa,
  • Kikatalani,
  • Usimbaji fiche!

Just imagine ume-hit Enter Key alafu inakuuliza Je? unataka matini katika vigagula? ... sasa what's the hell is matini katika vigagula?
 
Mkuu DotworldAcha uvivu jifunze lugha yako acha mambo ya ukoloni wa lugha za kigeni.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom