Windows 7 toleo la Kiswahili – asante Microsoft

Windows 7 toleo la Kiswahili – asante Microsoft

0L7C0234.jpg

​

cheki hilo zee hapo pembeni na kibagalashia chake hivi linaelewa somo kweli hapo?? au ndio bora liende? maana limekaa kama linataka kusinzia vile
 

Mkuu FaizaFoxy ,embu tupe maelezo basi kuhusu hii picha ,maana binafsi sielewi elewi hapo yupo Mkulu wa Nchi, Mwigulu n a huyo sijui Mohamed Dewji. Sasa hao wengine kina nani? na wanafanya nini hapo? Je ndio wataalamu wa Kiswahili wenyewe waliokuwepo kwenye hilo jopo la microsoft project?
 
hii lugha kama ndiyo kiswahili,itachukua miaka kadhaa kuwafundisha watumiaji wa computer kuielewa.binafsi naona giza tu( mfano neno kipeto.usimbaji fiche,kikatalani)

Mkuu Dotworld Poa tu mimi mbona ninatumia na ipo Poa kichizi.Mkuu leo.leo Jizoesheni Lugha yenu acheni Utumwa wa lugha za wageni lugha ya kizungu jifunzeni lugah yaenu kwa njia ya Computer jamani acheni uvivu.

Hiyo translation ni upuuzi mtupu na imejaa ubinafsi kwani imelenga kundi dogo sana la watumiaji wa Kiswahili. Kama hazingekuwepo element za ubinafsi, wangepanua wigo wa ushirikishwaji katika kupata tafsiri inayokubalika na watumiaji walio wengi wa lugha adhimu ya Kiswahili. Naweza kusema waliojitosa ku translate waliongozwa na motives ovu za kupata ajira bila kujali ujuzi wao, na Microsoft wameingizwa mjini kwa sababu hiyo software haitapata soko walilotarajia.

Kama wewe unaitumia bila matatizo, that is coincidence. Usiwashauri Watanzania kupoteza muda wa thamani kujifunza kiswahili cha porini cha wawindaji Wakikuyu wakati Kiswahili halisi kipo. Ni bora niendelee kutumia English for the time being, nitaelewa haraka na nitaokoa muda kwani muda ni mali.

Sitafanya bidii ya kujibadili kutoka utumwa ya lugha ya wazungu ili nijitie kwenye utumwa wa lugha ya wakikuyu. Tusipokuwa macho kuna siku tutaanza kuagiza kamusi toka nairobi ili tujifunze maana ya usanidi, matini, usimbaji fiche, kipeto, kikatalani, vigalula, auni, nywila na upuuzi mwingine.
 
Sio uvivu Mkuu MziziMkavu Unajua hii lugha ukiingia kichwa kichwa unaweza ukatoka kapa, unaweza ukajikuta unataka ku-accept command kumbe ndio una-DELETE.

Chukua kwa mfano maneno hayo hapo kwenye web page yao MOJA TU ya kiswahili imejaa maneno kama

  • Kipeto,
  • Kiolesura,
  • Kusanidi,
  • Matini katika Vigagula,
  • Vikasha ongezi,
  • Auni zitaangazishwa,
  • Kikatalani,
  • Usimbaji fiche!

Just imagine ume-hit Enter Key alafu inakuuliza Je? unataka matini katika vigagula? ... sasa what's the hell is matini katika vigagula?

Ha ha ha ha! Mkuu umenifurahisha sana hasa kwa hiyo sentensi yako ya mwisho! Hivi hili linaweza kumaanisha kwamba sisi ni waswahili lakini wakati huo huo hatukijui kiswahili chenyewe? Chukulia umekutana na mzungu kwa mfano ambaye anataka kujifunza kiswahili halafu amekuomba umsaidie kujua maana ya hayo maneno!! Sipati picha jinsi utakavyopanga mbinu ya kumkwepa.

Hivi hilo neno vigagula halina maana fulani ya akina bibi wazee!?
 
Back
Top Bottom