Wimbo wa Taifa wa Zanzibar

Katika kufuatilia kwa makini ndo utagundua ubanaishaji wa vyombo kama tbc,kama nia ni kuweka taarabu ,nadhan ingewekwa muda mwingine,

mkuu,leo ndo imedhihirika rasmi znz ni nchi. shein kukagua gwaride la jeshi na kupigiwa mizinga. serikali tatu oyeeeeeee. tanganyika oyeeeeeeer.
 
Ndiyo vinapita Vipando, kutoa salamu zao.
 
Hivi kuna wimbo wa taifa wa Tanganyika?

Swali la kipuuzi,kwani kuna benki kuu,sarafu,bendera,polisi na jeshi la Tanganyika si mlijifanya kuhodhi vitu vyote kwa jina la muungano.Pengo sasa hivi hana raha kwa sababu serikali mbili ndio matakwa ya Vatikani ili waendelee kuritadisha Wazenji na kupora ardhi.
 

Na mkiondoka tunabaki navyo nyote. .. benki kuu, hosipitali kuu, majengo ya wizara, miundombinu ya polisi, miundombinu ya jeshi, uwanja wa taifa, jengo la bunge, na vingine vyote vilivyojengwa kwa jina la muungano but mlivyokuwa hamna akili hamkupigania hata kimoja kijengwe kwenu.... masikini wakubwa nyie
 

Acha chuki zako kwa kanisa katoliki.endelea kumuabudu mungu wako.Acha wengine wamwabudu Mungu wao
 

Haaahaa mawazo mgando,serikali yeny ndo tatizo la muungano hangaikeni ni na watawala tena wote ni wa chama flani sioni sababu ya kumtaja Pengo kwani yeye ni nani kwenye serikali yenu.
 
Wabaguzi ni SMZ hata leo magari ya serikali hamjabadili number na kuandika SUK(serikali ya Umoja wa Kitaifa)bado ni SMZ serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Leo sherehe zilikaa ki CCM na mkawatenga kabisa CUF dhambi ya Ubaguzi itawatafuna milele
 
Ndiyo vinapita Vipando, kutoa salamu zao.

Duh! Vipando umenikumbusha mbali. Tafadhali anayefahamu beti za wimbo wa Tanganyika atuwekee humu kwani naona nao unakuja tena kwa kasi.
 
Ndiyo maana tunasema Muungano wetu unamatatizo, ila kwa hali ilivyo Mgeni rasmi ndo uhwa anakuwa wa mwisho kuingia ukumbini, hivyo wapo sahihi. Lakini ktk mamlaka anayoyale ya Zanzibar tu.
Mimi huwa najiuliza JWTZ, polisi, ni majeshi ya muungan iweje yakaguliwe na Rais wa Zanzibar? wakati yeye si amiri jeshi mkuu?


 
Zanzibar sio Nchi. Ni Jimbo. Laa sivyo, walikua wapi siku zote! Ah.
 
wadau!!
Ninaomba kwa mwenye mashairi ya wimbo wa taifa wa zanzibar atuwekee,niko najarib kufuatilia kwa tv lakin maneno hayasikiki!!

Nhoja nikutafutie hiyo taarabu nikuwekee usikilize, chunga mori usije ukapanda
 

ardhi gani mnayoporwa kanchi kenyewe sijui kana sijui ekari tatu zile
 
Hapa tunaigiza tu kuwa kuna muungano ila jifikra zaidi ni ukaliaji wa nchi zawatu kimafia zaidi.
 
Nadhani wimbo isiwe ishu,tujadili dhana ya huo muungano dosari na faida zake,ingawa kuna mvutano wa chinichini,
 
Leo,neno zanzibar kama nchi limetumika kwelikweli,naona ni salamu kwa mizengo pinda
 

kuritadisha ndio kufanyaje!?
 
Kuna wakati mmoja kati ya wale watangazaji alisema zanzibar leo imezizima! Mwenzake kwa haraka alidakia haijazizima! Kiswahili kinatabu!
 
Subirini hotuba ya mpemba wao huyu baadae..tunasema kuna mawaziri mizigo lakn zanzbar wanakoelekea nimzigo tena wakujitakia kwa Jamhuri ya Muungano wa Tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…