Leo Zanzibar wanahadhimisha miaka 50 ya mapinduzi(yanaitwa matukufu ingawa sababu ya kuitwa hivyo siijui).
Pamoja na mambo mengine nimeiona bendera ya Zanzibar huku ikiwa na kialama kidogo cha bendera ya Jamhuri hii ya muungano wa Tanzania juu pembeni.
Kiprotokali wameingia wageni mbalimbali kabla ya rais wa taifa la Zanzibar hajaingia
Ukiangalia protokali hii utagundua kuwa wageni walioingia kabla ya rais wa Zanzibar ni pamoja na mgeni rais wa jamhuri hii ya muungano wa Tanzania
Rais wa Jamhuri hii ya muungano wa Tanzania alipigiwa wimbo wa Taifa la Tanzania
Lakini alipoingia rais wa Zanzibar naye alipigiwa wimbo wa taifa huru la Zanzibar
Mimi nina maswali ambayo naomba wana jf munijibu kiufasaha kwani yananichanganya sana!!
1....Kiitifaki rais wa Zanzibar na rais wa Jamhuri hii ya Muungano wa Tanzania nani yuko juu ya mwenzake kimadaraka?
2...Rais wa Zanzibar akija Tanzania bara huwa anakuja kama nani na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akienda Zanzibar anaenda kama nani?
3..Rais wa Zanzibar anaruhusiwa kuingia ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kama nani pale ambapo rais wa Jamhuri ya Muungano anahutubia bunge?
4..Wabunge wa Zanzibar wanaingia ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Taznaina kama akina nani?
5..Endapo sherehe za muungano zitafanyika Zanzibar mgeni rasmi atakuwa nani?
Mods naomba msiondoe uzi huu wala msiuchanganye na uzi mwingine ili tupate majibu kutoka kwa waelewa wa haya mambo,
Mods nawaomba sana kwa hili!!!