Wimbo wa Taifa wa Zanzibar

Wimbo wa Taifa wa Zanzibar

Wakuu mimi ni miongoni mwa walioalikwa kwenye shughuli ya uzinduzi wa Hotel ya kisasa ya nyota 5 ya Azam , japo kiukweli ilishaanza kutumika kitambo kidogo kabla ya uzinduzi wenyewe, nawapongeza sana Azam kwa kuchagiza maendeleo ya Zanzibar.

Mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Tanzania Mh Magufuli kulipigwa nyimbo mbili za mataifa husika, mmoja ni ule uliyozoeleka wa Mungu ibariki ambao ni wimbo wa Taifa la Tanzania, lakini baadaye ukapigwa wimbo mwengine mzuri sana ambao tulinong'onezwa kwamba ni wimbo wa Taifa la Zanzibar!

Baada ya kuambiwa hayo binafsi nilifarijika sana na kujisikia fahari kubwa sana kwa Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964, na nichukue wasaa huu kuwapongeza sana Wazanzibar wote kwa wimbo mzuri sana wa Taifa lao.

Ningependa kujua huu wimbo wa Taifa la Zanzibar ulianza kutumika rasmi mwaka gani, ama ulikuwepo tangu Mapinduzi ya 1964?

Mungu ibariki Zanzibar

Huo wimbo ni wa CCM wazanzibari hawana muda nao kabisa.
 
Ulishindwa kuwauliza waliokualika umekimbilia kuja kujitapa humu na wewe uonekane upo juu au??? Usitusumbue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu wimbo upo tokea 64 baada mapinduzi tu.
Unasema hivi:-
MUNGU ametubarikia
Unguja na Pemba yote
Sote tunashangiria
Jamhuri kutuletea
MUNGU ametubarikia
Unguja na Pemba yoteee.
lakini kama hujui kuuimba unaweza usiuelewe.
Asante sana mkuu kombo alawi

Swali : ni kwanini miaka ya hapo kati wimbo huu ulizimwa ?
 
Back
Top Bottom