[22:05, 4/26/2016] ZAMIRA RIWAYA: RIWAYA: Wimbo Wa Gaidi
MTUNZI: HUSSEIN TUWA
SEHEMU YA SITA
Nyuma yao, ndege zaidi zilikuwa zikielekea
Dargah Mandi kupelekea mashambulizi zaidi…na
wakati huo huo ndege nyingine mbili zilikuwa
zikipeleka marobota mengine ya vyakula vya
msaada. Safari hii, yale marobota hayakuwa na
komando yoyote aliyejilaza juu yake…
_______________
Wakati boti ikipasua maji kufuata mkondo wa
mto ule, makomando walibadili zile nguo za
kupigia mbizi na kuvaa za kawaida. Wawili kati
yao waliokuwa na asili ya kiasia walivaa "salwan
khameez", nguo maarufu za ki-pakistani, ilhali
yule mwingine aliyejeruhiwa kwa risasi aliyekuwa
wa asili ya afrika, alikuwa akisaidiwa kutolewa
zile nguo kabla ya kupatiwa huduma haraka
haraka na tabibu mmoja waliyemkuta mle botini.
Ile risasi ilimkwaruza tu sehemu ya bega hivyo
haikuwa na madhara makubwa sana kwake. Yule
mmarekani mweusi alimtupia nguo za kipakistani
yule jamaa aliyechoropolewa kutoka kwenye
ngome ya watalebani.
"Vaa hizo nguo!" Alimkoromea.
Jamaa akatii bila kutia neno, ingawa muda wote
akili yake ilikuwa ikimtembea kwa kasi sana.
Aliona wale watu wengine kama watati hivi
waliokuwa pamja na yule mmarekani mweusi mle
botini wakiwa makini sana na bunduki zao, na
mara moja alibaini kuwa umakini wao wote
ulikuwa umeelekezwa kwake yeye, na si kwa
wale wenzake alioibuliwa nao kutoka mle mtoni.
Upande mwingine wa boti ile, mpakistani Imraan
Gopang naye alikuwa akivaa kanzu safi ya kijivu
juu ya suruali nyeupe ya "panjabi", baada ya
kutoa zile nguo za kuzamia mbizi alizokuwa
amevaa. Akiwa makini sana bila ya kujionesha
kuwa yuko kwenye hali ile, jamaa alivua fulana
mchinjo aliyokuwa ameivaa chini ya zile nguo za
kuzamia mbizi...na ndipo wale wenzake aliokuwa
nao mle ndani walipouona mwili wake kuwa
kutumia mwanga wa taa zilizokuwa ndani a lile
boti.
"Eeh...!" Mmoja wa wale makomando wa kiasia
alimaka huku kama wale wenzake na wale
walinzi waliowakuta mle botini, akilikodolea
macho kovu baya kabisa lililotambaa kutokea
upande wa kushoto wa kifua cha yule jamaa,
hadi ubavuni kwake. Lilikuwa ni kovu lenye
michirizi mitatu mizito iliyotokea kwenye vishimo
vitatu vilivyochimbwa pale kifuani na kuacha
makovu yenye vishimo. Yaani ni kama vile kuna
mtu katika siku za nyuma alimshindilia kwa reki
la kukusanyia majani kifuani, na kujaribu
kuzikusanya ngozi yake kutokea pale kifuani hadi
chini kabisa ya ubavu wake wa kushoto. Hakika
lilikuwa ni kovu baya sana.
"Nini?" Jamaa aliuliza huku akiwatembezea
macho wote mle botini, hali akiwa kidari wazi,
ameshikilia shati la kipakistani alilotupiwa na yule
mmarekani mweusi, ambaye ndiye pekee
aliyeonekana kutolishangaa kovu lile.
"Umekutwa na nini hapo komredi? Hilo kovu...."
Imraan Gopang akawasilisha swali ambalo bila
shaka lilikuwa likirindima vichwani mwa wale
wenzake. Jamaa aliinama na kujitazama pale
penye kovu, kisha akawatazama wale wenzake
kwa uso uliosajili hali ya kutokuwa na jibu kwa
swali aliloulizwa.
"Nyie ni wapiganaji halafu mnaogopa makovu?"
Aliwauliza badala ya kuwajibu, huku akilivaa lile
shati refu la kipakistani, na kulificha kovu lake.
Jamaa walichanganyikiwa kiasi kwa jibu lile.
"Ah...mimi nimepitia makabiliano ya kila namna
komredi...lakini sisi ni watu tunaocheza kwa
bunduki, risasi na mabomu kaka...hilo ulilo nalo?
Si kovu litokanalo na chochote kati ya hivyo
aisee..." Imraan Gopang alimjibu.
Kwa mara ya kwanza jamaa akaachia tabasamu,
na alivyofanya vile, sura yake ngumu ikabadilika
na kuwa ya kuvutia kwa namna fulani ya ugumu.
"Basi bado hujapitia makabiliano ya kila aina
komredi..." Alimjibu bila kujali.
"Okay...imetosha jamani..." Yule mmarekani
mweusi alidakia, akaendelea, "Tumalize hii
biashara Imraan..."
"Nyie ni kina nani kwani....?" Jamaa akauliza
lililokuwa likimtatiza kichwani mwake tangu
aporomoke kutoka kwenye dari la ule mtaro wa
majitaka.
“Hutaki kujibu maswali yetu, unataka tukujibu ya
kwako?” Komando mwenye asili ya kiafrika
alimuuliza, sasa akiwa amefungwa bandeji
kitaalamu begani. Alikuwa amevaa suruali ya jinzi
huku akiwa kidari wazi. Jamaa akamtupia jicho
fupi, kisha akageukia Imraan Gopang.
“Nilitaka niwashukuru tu kwa kunitoa mle ndani
kwa namna mlivyonitoa…sasa nisingependa
kushukuru watu nisiowajua, pamoja na kuwa ndio
mlioniokoa.” Alimueleza mpakistani yule ambaye
alishajua tangu kule mtaroni kuwa ndiye kiongozi
wa wale jamaa waliomuokoa. Jamaa
walitazamana.
“Okay sio mbaya…” Imraan Gopang alisema, na
kuendelea, “tuchukulie sisi kama matarishi tu
komredi.”
“Matarishi?”
“Yah…kazi yetu kubwa ni kusafirisha vifurushi
kutoka sehemu moja kwenda nyingine…kwa
malipo, of course….”
“Na kwenye swala hili la leo, kifurushi chetu
kilikuwa ni wewe…wajibu wetu ulikuwa
kuhakikisha kuwa tunakutoa kwa watalebani na
kukufikisha kwenye hili boti…ukiwa hai.” Yule
komando aliyemvuta mkono kule mtaroni wakati
wanashambuliwa na watalebani alidakia.
“Oh? Kwa hiyo nyie ni mamluki…mercenaries?”
Jamaa alisaili.
“Matarishi ni sahihi zaidi…” Imraan akasisitiza,
kisha akaendelea, “Hatujui umefanya nini na wala
ni kwa nini umejipatia umuhimu wa kulazimisha
sisi tupewe kazi ya kwenda kukuchoropoa kule
ulipokuwa, kwa namna ya hatari namna ile…na
hatujali. Ndivyo matarishi walivyo. Wao hulipwa
kwa kubeba na kuifikisha bahasha mahala
patakiwapo pasina kujua ndani ya bahasha ile
kuna ujumbe gani…”
Jamaa akaafiki kwa kichwa na kumgeukia yule
mmarekani mweusi.
“Ina maana wewe ndiye uliyeandaa mkakati huu
wa kunitoa mle ndani kwa kuwatumia hawa…
matarishi.” Alimwambia, na bila kusubiri
uthibitisho kutoka kwake akaendelea, “Basi
ahsante sana. Nilijua tu kuwa msingeweza
kuniacha mle ndani…ingawa mmekawia sana.
Hali ilikuwa ngumu sana kule…hasa baada ya
kuuawa kwa yule mwenzangu…sikujua kama
hangenitaja, ilikuwa ni hali tete kwa kweli…”
“Ni kweli. Ilitubidi tubahatishe kufuata ile ile
kanuni mliyowekewa na mwenzako aliyewahiwa
na watalebani…kuwa siku ya kuja kuwachomoa
mle ndani itatangazwa sana maredioni hapa
Pakistani kwa wiki nzima…kuwa idara ya hali ya
hewa inawatahadharisha wananchi wote dhidi ya
kimbunga kikali…kitakachoipiga pwani ya
Pakistani kwenye siku, tarehe na saa maalumu…
tulitaraji tu kuwa utakuwa umesikia tangazo hilo
ukiwa mle ngomeni mwa watalebani, na utajua
kuwa hiyo ndiyo siku na saa ambayo tutakuja
kukuchomoa mle ndani…” Mmarekani alimjibu.
“Ni kweli…na ndipo nilipoanza kujinadi kushikwa
na tumbo la kuhara…nikawa naenda chooni mara
kwa mara, nikikichimba kidogo kidogo kile choo
ambacho tangu awali nilishaelekezwa na
mwenzetu aliyeuawa kuwa ndio ingekuwa njia
yangu ya kutokea mle ndani pindi hali ikifikia
pabaya…”
“Okay, tutaongea zaidi mimi na wewe…kwanza
wacha nimalizane na matarishi wetu hapa…”
Mmarekani alisema.
Kwa dakika kumi na tano zilizofuatia jamaa
alimshuhudia yule mmarekani mweusi
akihamishia pesa kwenye akaunti za wale
mamluki wanne waliokuwa wakiongozwa na
mpakistani Imraan Gopang, kwa kutumia
kompyuta mpakato maalum aliyokuwa nayo mle
botini. Alipomaliza alipeana mikono na wale
jamaa mmoja baada ya mwingine, akimalizia na
Imraan Gopang.
"Ilikuwa ni faraja kufanya tena biashara na wewe,
Imraan." Alimwambia, na kwa mara nyingine
jamaa akaelewa kuwa ile haikuwa mara ya
kwanza kwa wale jamaa kufanya pamoja kazi
kama ile.
"Na mimi vile vile, kamanda! Ukija tena kwenye
nchi yetu hii ya majanga usisite kunipigia...tuk
utane japo kwa kikombe cha kahawa..." Imraan
alimjibu.
"Ha ha ha haaaa...Okay poa, Imraan haina
shida.Ila unue umipokea simu yangu haitakuwa
kwa ajili ya kuoanga miad ya kupata kikombe
cha kahawa kaka...itakuwa ni kwa kazi tu".
Imraan akacheka pamoja naye, na walipomaliza
kucheka, mmarekani mweusi akamwambia, "Basi
sasa nyinyi na sisi tutagawana njia baada ya
kama dakika kumi hivi...helikopta maalum
itawafikisha Karachi...na pale kila mmoja
atatawanyika kivyake...mimi na ninyi hatujaonana
kabisa jamani...na siku hii haipo kabisa katika
historia zenu...sawa?"
"Kama kawaida..." Mmoja wale makomando alini
u wakati Imraan akiafiki kwa kichwa tu swala lile.
"Good. Basi mpaka hapo tutakapohitajiana
tena...kama ikibidi." Mmarekani mweusi alisema.
"Poa."
______________
Dakika kama saba baadaye boti liliegeshwa
kwenye ukingo wa pili wa mto ule, likiwa
limesafiri kiasi cha kama kilometa kumi na tano
kutokea pale ambapo lilipokuwa likiwasubiria
wale makomando. Kutokea mle kwenye boti
zilionekana helikopta mbili zikiwa zimeegeshwa
umbali fulani kando ya mto ule.
“Okay Imraan…nyie mtaingia kwenye ile helikopta
ya kushoto…itawafikisha Islamabad na huko kila
mtu ataangalia ustaarabu wake…sisi tutaingia
kwenye ile ya kulia na kuelekea Karachi …”
Mmarekani mweusi alisema.
Lakini haikuwa hivyo...
***MNH, Leo tumepata jipya...lile kovu baya, vipi
habari yake...? Na kwa nini haikuwa kama
Mmarekani mweusi alivyopanga?
NJOO TUSOME ZAIDI hizi beti za wimbo huu
hapo kesho...
Mar 29 · Public · in Timeline Photos
View Full Size · Send as Message · Report
Zainab Jamal and 328 others like th
[22:07, 4/26/2016] ZAMIRA RIWAYA: RIWAYA: Wimbo Wa Gaidi

[22:14, 4/26/2016] ZAMIRA RIWAYA: Next
KONA YA Riwaya Reloaded
RIWAYA: Wimbo Wa Gaidi
MTUNZI: Hussein Tuwa
SEHEMU YA NANE
“Sio kazi bure komredi…akaunti zetu zimenona…
tuombe tunusurike tu hapa…” Imraan alimjibu.
“Kweli kaka…”
Safari yao iliendelea bila ya tukio lolote…
________________
Saa moja baadaye helikopta ilitua pembezoni
mwa jiji la Islamabad, na mara baada ya Imraan
na kundi lake kuteremka,rubani aliirusha tena ile
helikopta na kutokomea angani.
Imraan aliwaongoza wenzake kimya kimya,
wakikata mitaa kadhaa kabla ya kutokea kwenye
kituo cha teksi. Walionekana kama wenyeji
watatu tu waliokuwa na mgeni wao mmoja wa
kiafrika wakitoka kwenye moja ya sehemu
kadhaa za starehe, ambazo kwa mazingira ya
nchi ile zilikuwa ni za siri sana.
"Okay makomredi...mimi naelekea kwangu sasa.
Ninyi mtarudi kwenye mahoteli yenu na
kukipambazuka mtoweke nchi hii...si tiketi na
pasipoti zenu viko sawa?" Imraan aliwaambia na
kuwauliza wenzake.
"Yah...tuko vizuri..."Mmoja alijibu.
"Okay..tutawanyike. Ikiwa kutatokea kazi
nyingine ninajua nitawasiliana vipi na nyie..."
"Kuna kazi tena na dalali wako wa madili
keshadunguliwa kule?" Mwenzake mmoja
alimuuliza.
Imraan akafyatua kicheko kifupi, kisha akamjibu,
"Kufa ndio sehemu kuu ya kazi yetu kaka…ndio
maana hata kama mmoja wetu angeuawa leo hii,
bado hela yake ingetumwa tu kwenye akaunti
yake, familia yake ikanufaika. Kafa yeye...sio
harakati, bwana. Atawekwa mwingine wa
kusimamia mambo haya badala yake...na
atanitafuta tu muda ukifika..." Alimjibu.
Kila mmoja akachukua teksi yake na kuelekea
kwenye hoteli aliyofikia. Imraan alimuelekeza
dereva wa teksi yake amrejeshe nyumbani
kwake...ambako alipaacha kwa siku kadhaa
alipokuwa ameenda kwenye misheni ile ya hatari.
________________
CNN ndio walikwa wa mwanzo kutangaza juu ya
shambulizi lile kubwa kabisa la ndege zisizo na
rubani dhidi ya ngome kuu ya wataleban
iliyokuwa kilomita saba kutoka kwenye kile kijiji
cha Dargah Mandi.
Kupitia taarifa ile, dunia ilihabarishwa kuwa
kiongozi mkuu wa wataleban ndani ya Waziristan
alikuwa ameuawa pamoja na wafuasi wake
wengi wakiwemo wale wa Al-Qaida waliokuwa
wamehifadhiwa kwenye ngome ile.
Aidha, CNN ilihabarisha kuwa katika kampeni ile
ya mashambulizi iliyofanywa kwa ushirikiano kati
ya jeshi la marekani na lile la Pakistani, jeshi la
shirikisho lilifanikiwa kumtia mbaroni gaidi
muhimu aliyehusika katika ulipuaji mabomu
ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 98,
aliyekuwa akisakwa sana, Nouman bin
Fattawi...lakini helikopta aliyokuwa akisafirishwa
nayo kutoka Pakistani ilidunguliwa na vikosi vya
wapiganaji wasiojulikana na yeye pamoja na watu
wengine saba waliuawa. Mpaka muda habari ile
inarushwa hewani, hakukuwa na kundi lolote
lilojinadi kuhusika na udunguliwaji wa helikopta
ile. Habari hii ilidakwa na vyombo vingine vya
habari na kusambaa dunia nzima.
Ni habari iliyoleta kizaazaa kikubwa nchini
Tanzania...
___________________
Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam, Tanzania.
Wiki moja baadaye:
Umma wa watu ulikuwa umefurika kwenye
makaburi ya kisutu. Muda ulikuwa ni saa kumi za
alasiri. Ufurikaji wa umma makaburini pale
haukutokana na kwamba kulikuwa kuna mtu
maarufu aliyekuwa akizikwa siku ile, La Hasha.
Mfuriko ule ulitokana na ukweli kwamba kulikuwa
kuna marehemua watano waliokuwa wakizikwa
siku na wakati ule, na hivyo kulikuwa kuna
makundi matano ya ukubwa tofauti kwenye
makaburi matano yaliyochimbwa sehemu tofauti
ndani ya uzio wa eneo lile la makaburi maarufu
jijini.
Ni kutokana na ujumla wa makundi yale matano
yenye ukubwa tofauti kuwa ndani ya eneo lile
kwa wakati mmoja, ndipo taswira ya umma wa
watu kufurika ilipopatikana makaburini pale.
Nje ya uzio wa makaburi yale magari mengi
yalikuwa yameegeshwa pande zote za barabara
finyu, kiasi kwamba ilikuwa ni shida kwa magari
mengine kupita tu pale barabarani, wachilia mbali
kupishana.
Kwenye kaburi lililochimbwa pembeni kabisa ya
eneo lile la makaburi, upande wa kushoto mara
baada ya kuingia kwenye geti la makaburi yale,
kulikuwa kuna kundi la wastani la wanandugu
waliokuwa wakimzika mpendwa wao,
wakiongozwa na sheikh aliyekuwa mjuzi katika
taratibu za kuendesha maziko. Lilikuwa ni kundi
lenye huzuni kwa kuondokewa na ndugu na
jamaa yao ambaye hata hivyo wamekuwa mbali
naye kwa muda mrefu, siku zote hizo kabla ya
umauti kumkuta mpendwa wao, wakiwa
wamegubikwa mashaka mazito juu ya hatma
yake…mpaka habari zilipowafika kuwa hatimaye
mpendwa wao alikuwa ameuawa kwenye kifo
kibaya kabisa, huko ughaibuni.
Walikuwa wamekusanyika kumzika Nouman
Fattawi.
Kaka, mwana, mjomba, rafiki, mpenzi…na kwa
wengine, ndugu yao katika imani.
Hata hivyo, hawa wote walikuwa ni sehemu moja
tu ya wale waliokuwapo kwenye mazishi ya
Nouman Fattawi siku ile.
Pamoja nao walikuwepo wana usalama wa taifa,
ambao walikuwa pale kushuhudia maziko ya gaidi
aliyekuwa akisakwa na wamarekani kwa udi na
uvumba, akihusishwa na ulipuaji wa ubalozi wa
marekani jijini Dar miaka kumi na minane
iliyopita… na pia kuwatazama kwa makini wote
waliokuwa wamefika kwenye mazishi ya mtu yule
hatari sana kuwahi kutokea kwenye historia ya
Tanzania tangu vita dhidi ya kile kilichokuja
kunadiwa na kutambulika kama “ugaidi” inadiwe
duniani. Na ni kutokana na kulijua au kulitarajia
hilo ndio maana hata kundi lililokuwa kwenye
maziko ya Nouman Fattawi jioni ile pale kisutu
ndilo lilikuwa dogo kuliko yale mengine manne
yaliyokuwa pale makaburini siku ile.
Ni nani anayetaka kuhusishwa na gaidi?
Hakuna…isipokuwa kama ni ndugu wa damu au
wa karibu sana…au ambaye yuko bega kwa bega
na harakati za marehemu kiasi kwamba hajali
iwapo na yeye atahusishwa na harakati hizo.
Na ni hawa wa mwisho ndio ambao
wanausalama waliojipenyeza kwenye maziko
yale, wakiwa wamejivika kanzu na vibaraghashia
ili kufanana na waombolezaji halisi wa tukio lile,
ndio waliokuwa wakijaribu kuwabaini kwenye
mkusanyiko ule. Walitaraji kupata cha
kuwaongoza kwenye azma yao ile kutoka kwenye
mawaidha ya mwisho yatakayotolewa na yule
shekhe atakapomaliza kuongoza maziko yale.
Lakini pia walikuwepo watendaji wa shirika la
ujasusi la marekani, C.I.A., ambao nao walikuwa
ni weusi kama wengine pale kaburini, wakiwa
wamejivika mavazi muafaka kwa tukio lile, na
ambao pia walijua namna ya kuitikia dua
zilizokuwa zikielekezwa na shekhe mazikoni pale.
Lengo lao lilikuwa ni kujithibitishia kuwa kweli
gaidi waliyekuwa wamemtamani kwa miaka
mingi, hakika alikuwa amezamishwa ndani ya
tumbo la ardhi jijini Dar…ili watakapopeleka ripoti
huko kwenye makao yao makuu kule Langley,
Virginia, wawe na ushahidi wa dhahiri kabisa kwa
kile walichokishuhudia. Lakini vilevile, uwepo wao
pale ulikuwa na lengo la kujaribu kuona iwapo
kutakuwa kuna atakayepandwa na jazba pale
makaburini na kubwabwaja kulipiza kisasi kwa
wamarekani kwa kifo cha yule mshirika wao…au
kuona yeyote ambaye angeelekea kuwa alikuwa
akishirikiana na marehemu kwa namna moja au
nyingine.
_________________
Maziko yaliendelea kama ilivyotakiwa. Kutokana
na namna mwili wa marehemu ulivyoharibika,
ulizikwa kwa shida sana, kilichozikwa kikiwa ni
mabaki yaliyopatikana ya mwili wake. Baada ya
mwili kuingizwa kaburini na kuzikwa, shekhe
alitoa mawaidha kwa wafiwa kuwa wawe
wastahamilivu, na kuwa Nouman Fattawi alikuwa
ameshakunywa kifo chake kutoka kwenye gilasi
ya umauti, ambayo sote hapa duniani
tumeahidiwa kunyweshwa baada ya muda
fulani…hivyo wote waliobakia pamoja na yeye
mwenyewe walikuwa wana gilasi zao
zinazowasubiri.
“Siku gani…saa ngapi…mahala gani na sisi
tutaletewa gilasi zetu za umauti haijulikani.
Mwenzetu kapelekewa gilasi yake Pakistani,
lakini huenda kuna miongoni mwetu ambaye ya
kwake inamsubiri hapo morogoro road akiwa
njiani kutoka hapa mazikoni…basi na tushike
ibada ndugu zangu, tumrejee mola wetu na
tuchukulie kifo cha ndugu yetu, mpendwa wetu,
mwana imani mwenzetu, raia mwezetu huyu…
kuwa ni ukumbusho kwetu sisi tuliobaki…”
Shekhe alimalizia. Akapiga “Fat-ha”, kisha
akaomba dua ndefu kwa lugha ya kiarabu. Watu
wakaitikia dua. Alipomaliza akaruhusu watu
kutawanyika kwa maelezo kuwa wanafamilia
wamesema kuwa hakutakuwa na matanga
nyumbani kwao. Hakuongelea hata neno moja
kuhusu ugaidi wa Nouman Fattawi wala namna
alivyokufa.
Maziko yakaisha.
Watu wakatawanyika.
Wanausalama wa taifa na wenzao wa C.I.A.
wakaambulia kunufaika na mawaidha tu ya
shekhe kwenye maziko yale.
Kutokea chini ya mti uliokuwa hatua kadhaa
kutoka kwenye kaburi la jirani ambako napo
maziko mengine yalikuwa yakiendelea, mtu
mmoja mrefu aliyevaa suruali nyeupe ya
kitambaa chepesi, viatu vyeusi vya ngozi bila ya
soksi na shati jeupe la mikono mirefu ambalo
hakulichomekea, wala hakuwa amelifunga
vifungo kiasi cha kuionesha fulana nyepesi
nyeusi aliyoivaa chini ya shati lile, alikuwa
akifuatilia kwa makini sana kile kilichokuwa
kikiendelea sio pale kwenye yale maziko
aliyokuwa amesimama karibu nayo, bali kule
kwenye maziko ya gaidi Nouman Fattawi.
Usoni alikuwa amevaa miwani ya jua iliyoficha
macho yake, na kichwani alikuwa amevaa
barghashia moja ghali sana. Kwa pale alipokuwa
amesimama kando ya mti, uso wake ulikuwa
umeelekea pale kwenye yale yaliyokuwa
yakiendelea kwenye maziko yaliyokuwa jirani na
ule mti aliokuwa amesimama chini yake,
miongoni mwa wazikaji wengine, lakini macho
yake yaliyokuwa nyuma ya miwani ile myeusi, na
masikio yake vilikuwa kule kwenye kilichokuwa
kikifanyika kwenye kaburi la Nouman Fattawi.
Na sasa alibaki pale pale chini ya mti wakati
akiwatazama watu waliokwenda kumzika
Nouman wakitawanyika, ilhali wale waliokuwa
wakimzika marehemu wa kwenye kaburi
alilokuwa amesimama kando yake, wakimalizia
kumfukia yule marehemu wao pale kaburini.
Alibaki akiwa amesimama pale pale chini ya mti
hata pale wale watu waliokuwa wakimzika yule
marehemu mwingine walipomaliza na
kutawanyika…
****Doh, katoka Nouman, kaja mzee wa chini ya
mti...nini hii sasa?
NJOO TUSOME zaidi khabari hizi hapo kesho,
muda kama wa leo.
[22:33, 4/26/2016] ZAMIRA RIWAYA: ONA YA Riwaya Reloaded
RIWAYA: Wimbo Wa Gaidi
MTUNZI: Hussein Tuwa
SEHEMU YA TISA
Alibaki akiwa amesimama pale pale chini ya mti
hata pale wale watu waliokuwa wakimzika yule
marehemu mwingine walipomaliza na
kutawanyika…
__________________________
Kiasi cha kama saa moja na nusu baada ya watu
wote kutawanyika pale makaburini, kaburi la
marehemu Nouman Fattawi likapata mgeni. Jua
lilikuwa limeshazama na mwanga ulikuwa
unatowekea kutoka kwenye hafifu kwenda
kwenye kiza, na umbile la mtu likafika pale
kaburini kama mzuka tu na kusimama wima
upande ambapo miguu ya marehemu aliyelala
chini ya tuta lile la udongo ingekuwapo.
Kutokea pale chini ya mti alipokuwa
amechutama baada ya kuwa ameshasimama kwa
zaidi ya saa tatu, tangu wakati mwili wa Fattawi
unaletwa, unazikwa na kuachwa peke yake pale
chini ya udongo, mtu mrefu aliyekuwa amevaa
nguo nyeupe alimakinika vilivyo, huku akijibanza
zaidi nyuma ya mti ule. Alijifuta machozi
yaliyokuwa yakimtiririka na kukaza macho
kukitazama kile kiumbe kilichokuwa kimesimama
pale mbele ya kaburi la hayati Nouman.
Kutokea pale nyuma ya mti, jamaa alibaini vitu
viwili. Kwanza yule mtu alikuwa ana umbo dogo…
halafu, kutokana na mavazi yake, alikuwa ni wa
jinsia ya kike.
Umakini wake ukapanda daraja.
Yule mwanamke alikuwa amevaa vazi la dera
lenye rangi iliyojificha, aidha buluu au kahawia…
au nyeusi… hakuweza kujua kwa urahisi kutokea
pale alipokuwa. Alikuwa amesimama wima hali
mikono yake akiwa ameishika pamoja kwa mbele,
chini kidogo ya kitovu chake, na kichwa chake
akiwa amekiinamisha kwa mbele kama
anayeomba dua fulani kwa marehemu yule.
Jamaa alizidi kumfuatilia huku kwa wakati huo
huo akitembeza macho huku na huko ili kuona
iwapo yule mwanamama alikuwa amekuja na
watu wengine pale makaburini muda ule.
Hakuona mtu mwingine yeyote.
Kisha, ghafla kama alivyoibuka, yule mwanamke
aligeuka na kuondoka pale kaburini kwa mwendo
wa haraka.
Jamaa akajichomoa nyuma ya mti na kuanza
kumfuata kwa mwendo wa tahadhari. Nje ya uzio
wa makaburi yale mwanadada alikunja kulia na
kutembea kwa mwendo mfupi kabla hajalifikia
gari dogo ambalo jamaa hakuweza kulitambua
mara moja lilikuwa ni la muundo gani, na dakika
moja baadaye lile gari likaondoka eneo lile kwa
mwendo mdogo.
Bila kujishauri zaidi, jamaa akafungua mnyororo
uliokuwa umeifunga pikipiki yake aina ya boxer
aliyokuwa ameipaki pale nje, na kuiingiza
barabarani, akilifuata lile gari.
Baada ya kulifuata lile gari kwa muda, likikata
mitaa kadhaa wa kadhaa ya jiji, hatimaye lile gari
ambalo sasa alibaini kuwa lilikuwa ni Toyota
Duet, liliashiria kukata kona kuingia kwenye jengo
la hoteli moja nzuri sana ya ghorofa tano
iliyokuwa maeneo ya sinza. Jamaa alipitiliza na
pikipiki yake hadi kwenye maegesho yaliyokuwa
nje ya hoteli ile, akamkabidhi mlinzi wa kimasai
pale kwenye maegesho yale, na kuelekea kwenye
lango kuu la hoteli ile, akiliona lile gari la yule
dada bado likiwa pale nje ya geti la hoteli ile
likisubiri geti lifunguliwe ili liingie.
Jamaa akapitiliza hadi sehemu ya mapokezi ya
hoteli ile na kukuta watu kadhaa wakijiandikisha
pale. Akaketi kwenye moja ya makochi ya pale
mapokezi akiwa makini sana.
Dakika chache baadaye alimuona yule
mwanamke mwenye umbo dogo akiingia mle
hotelini na kupita moja kwa hadi kaunta ya
mapokezi.
“Naomba ufunguo wangu dada…namba mia tatu
na saba…” Dada alipaaza sauti kumwambia binti
wa mapokezi. Binti alimkabidhi ule ufunguo na
mwanadada akaongoza kwenye lifti
iliyompandisha huko juu.
Jamaa akakunja uso. Hakuwa amepata kumuona
yule dada hata siku moja hapo kabla, na wala ile
sauti yake haikumletea kumbukumbu yoyote.
Lakini jambo moja lilimfunukia wazi wazi akilini
mwake, na ndilo lililomfanya akinje uso.
Yule mwanamke aliitaja namba ya chumba chake
kwa sauti makusudi…kwa faida yake yeye…ili
yeye ajue kuwa yule dada yuko kwenye chumba
namba mia tatu na saba.
Kwa nini?
Ina maana yule dada alijua kuwa yeye
angekuwepo pale makaburini muda ule? Na alijua
kuwa alikuwa akimfuata kwa pikipiki muda wote?
Kama ndivyo…ni kwa nini basi?
Kwanza anahusika vipi na Nouman Fattawi yule
dada?
Akili ilimuwamba mtu mwenye nguo nyeupe, au
mzee wa chini ya mti.
Hatua gani ifuate sasa?
Jamaa alijiuliza akiwa ametulia kwenye kochi la
pale mapokezi. Jibu lilijileta kwake dakika tano
baadaye.
___________
Sehemu nyingine ya jiji, mzee Fattawi, baba wa
hayati Nouman alikuwa kwenye wakati mgumu
sana. Vijana waliombeba kwa gari lao wakati
wakitokea makaburini akiamini kwa ni miongoni
mwa waombolezaji kwenye msiba ule wa
mwanaye aliyemkosa kwa miaka mingi, walikuwa
wakimuongelesha maneno ambayo hakuwa
akiyaelewa.
“Mzee…tunajua kuwa uko kwenye msiba mzito…
sisi pia tuna masikitiko na kifo hiki. Letu kwako ni
moja tu…elewa kuwa mwanao amekufa kishujaa,
hivyo asitokee mtu yeyote akaja kukuletea habari
za kuwa eti alikuwa gaidi…yeye amekufa kwenye
njia iliyo sahihi. Na tuko wengine pamoja naye
kwenye njia hiyo hiyo aliyoenda yeye…” Mmoja
wao alimwambia. Mzee akapagawa.
“Wanangu…mbona siwaelewi? Mimi Nouman
nilishamzika miaka zaidi ya kumi iliyopita!
Nilimzika moyoni mwangu. Sikuwahi kuonana
naye tangu nimeanza kusikia hizo habari za eti
naye ni gaidi. Nilishahojiwa na watu wa kila aina
mimi…na wote jibu langu limekuwa ni hili hili…
sitambui swala la mwanangu kuwa gaidi na
siamini…sio Nouman…sasa mmeshamuua,
haitoshi kuwafanya muiache nafsi yake ipumzike
jamani? Hebu nishusheni hapa! Nishusheni
haraka tena!” Mzee alifoka.
Bila kuongea zaidi, jamaa walipaki gari kando ya
barabara na kumteremshia njiani, nao wakatia
moto gari lao na kutoweka.
Mzee wa watu akabaki akilia kwa uchungu peke
yake barabarani…
_______________
Akiwa pale mapokezi, jamaa aliona watu wawili
wenye asili ya kiajemi wakiingia mle hotelini huku
wakiangaza macho huku na huko, wakiwa na
mabegi yao ya safari. Muonekano wa watu wale
mara moja ulimjuza kuwa hawakuwa wenyeji,
lakini pia hawakuwa wema. Hakusubiri zaidi.
Aliinuka na kuziendea ngazi za miguu na
kuzikwea haraka hadi ghorofa ya tatu. Huko
akaanza kukisaka chumba namba mia tatu na
saba. Alipokifikia alisimama nje ya mlango wa
chumba kile na kutazama huku na huko, akaona
korido ilikuwa tupu. Akajaribu kusikiliza iwapo
kulikuwa kuna mienendo yoyote nyuma ya
mlango wa chumba kile. Kulikuwa kimya kabisa.
Akajaribu kushika kitasa cha mlango ule, na
ajabu mlango ukajisukuma ndani kirahisi kabisa.
Kengele za hatari zikaanza kugonga kichwani
mwake. Akili ikamwambia ageuze pale pale,
aondoke. Lakini udadisi ukamwambia vinginevyo.
Akausukuma zaidi ule mlango na kujidhihirishia
chumba kilichokuwa kimegubikwa na kiza.
Haraka akaingia ndani na kuusukuma taratibu ule
mlango nyuma yake na kuufunga. Alianza
kutafuta kitasa cha kuwashia taa kando ya
mlango ule wakati ghafla taa ya mezani
ulipowaka moja kwa moja mbele yake. Alihemka
huku akijisogeza pembeni kwa hamaniko,
akitafuta pa kujificha.
“Tulia hivyo hivyo…!” Sauti nzito ilimkoromea, na
hapo hapo ndipo alipomuona mtu mmoja
aliyekuwa ameketi kwenye kochi lililokuwa
upande wa pili wa chumba kile. Kutokea pale
alipokuwa, aliweza kuona miguu tu iliyokuwa
imekunjwa nne, na juu ya goti la mmoja kati ya
miguu ile kulikuwa kuna mkono ulioshika bastola
kubwa, ambayo ilikuwa imemuelekea yeye.
Duh!
Ule mwanga wa ile taa ulikuwa ukimmulika usoni,
na hivyo hakuweza kumuona vizuri yule mtu
mwenye bastola. Aligwaya kidogo.
“Weka mikono yako sehemu ambayo nitaiona
kwa urahisi, na usifanye utundu wowote hapo!”
Sauti ilimkoromea tena, na jamaa akahisi moyo
ukimlipuka.
Ile sauti!
Alishapata kuisikia kabla…
Akasikia mchakacho hafifu jirani na pale
alipokuwa amesimama, na ghafla, kabla hajaweza
kugeuka vizuri kutazama kule ambako
mchakacho ule ulitokea, akapigwa kwa nguvu na
kitu kizito kichwani.
Mguno hafifu ukamtoka, naye akaenda chini bila
kupenda…kiza kikatanda mbele ya uso wake…
***DOH!
Apr 1 · Public · in Timeline Photo
[22:37, 4/26/2016] ZAMIRA RIWAYA: Wimbo Wa Gaidi
MTUNZI: Hussein Tuwa
SEHEMU YA KUMI
Akasikia mchakacho hafifu jirani na pale
alipokuwa amesimama, na ghafla, kabla hajaweza
kugeuka vizuri kutazama kule ambako
mchakacho ule ulitokea, akapigwa kwa nguvu na
kitu kizito kichwani.
Mguno hafifu ukamtoka, naye akaenda chini bila
kupenda…kiza kikatanda mbele ya uso wake…
No way!
Kwa namna isiyotarajiwa alijiachia kwenda chini
na hapo hapo akalikwapua kwa nguvu sana zulia
refu na jembamba lililokuwa limetandikwa pale
juu ya sakafu ya marumaru ya chumba kile,
likitambaa kutokea pale mlangoni hadi pale
kwenye kiti alichokalia yule mtu mwenye bastola,
na kubingirika nalo sakafuni.
Kile kiti kilichokuwa juu ya lile zulia kilipinduka
pamoja na yule jamaa aliyekuwa amekikalia,
ambaye aliachia mgutuko wa kutotarajia huku
akienda chini na bastola yake. Jamaa
hakuhangaika naye bali alijizungusha zaidi pale
chini akiunyooshea mguu wake kule alipohisi
kuwa pigo la kichwa lilipotokea, lakini akaambulia
patupu, kwani mtu aliyempiga lile pigo aliwahi
kuruka juu na ngwara yake ikapita patupu.
Pale pale chini akajigaragaza kufuata kule miguu
ya mtu mwenye bastola ilipokuwa na kumkumba
vibaya yule jamaa. Wote wawili wakajibabatiza
kwenye kiti alichokuwa amekalia yule jamaa
hapo awali.
Jamaa akawahi kujiinua lakini akakutana na teke
zito la ubavu kutokea nyuma yake. Akagumia
huku kwa pembe ya jicho lake akimuona yule
mtu mwenye bastola akiinuka ilhali bado ile
bastola yake ikiwa mkononi mwake. Jamaa
akachanganya miguu huku akijirusha nyuma kana
kwamba alikuwa akicheza dansi isiyojulikana,
kisha kwa namna ya ajabu mguu wale
ukafyatuka kama kofi kali la mkono na
kuipangusa vibaya ile bastola kutoka mkononi
mwa yule jamaa.
Heh!
Hapo mshirika wa yule mtu mwenye bastola
alimrushi teke jingine kali sana, na kwa mara
nyingine mzee wa chini ya mti alijigeuza kwa
wepesi wa ajabu mithili ya mtu aliyekuwa
akicheza dansi, na pigo la yule mwanadada
mwenye umbo dogo likapotea, naye akayumba
kibwege na kujikuta akiwa amedhibitiwa kwa
namna ambayo wala hakuielewa.
“Basi inatosha nyinyi…ebbo!” Jamaa alibwata, na
yule mtu aliyekuwa ameshika bastola hapo awali
alibaki akiwa amepiga mduwao usiosemeka pale
alipomshuhudia yule jamaa akiwa amemkaba
kabali kali sana yule mwanadada huku akiwa
amemuwekea kisu kooni.
E bwana we!
Walitazamana.
“Tulia mzee…huhitaji kabisa kuanzisha mambo
haya na mimi nakwambia…nielezeni ni nini
kinaendelea hapa?” Mzee wa chini ya mti alisaili
huku akiwa amemkazia macho makali sana yule
bwana aliyekuwa na bastola hapo awali.
Jamaa alikuwa akimtazama kwa makini na
kutoamini.
“Oh…okaayy…tulia basi…tulikuwa tunataka
kuongea tu…!” Yule bwana alisema kwa mashaka
huku akiwa ametawanya mikono yake kuonesha
kuwa hakuwa na silaha yoyote mikononi mwake
muda ule.
“Hivi ndivyo mnavyoongea na watu?” Mzee wa
chini ya mti akasaili.
“Sasa unaniachia au huniachii wewe?” Yule dada
naye alikoroma kwa hasira. Jamaa alimpapasa
mwilini haraka kwa ule ule mkono wake ulioshika
kisu huku bado akiwa amemkaba.
“Toa hiyo bastola uloificha pajani…taratbu sana,
kisha tuongee!” Jamaa alimkoromea yule dada.
“Dah!” Dada alinywea na kutekeleza kwa
kupitisha mkono ndani ya ile nguo iliyoonekana
kuwa kama dera, lakini kumbe ikiwa ni suruali
iliyoshonwa kwa mtimbo wa bwanga pana
aliyoivaa chini ya blauzi ya kitambaa kile kile cha
ile suruali, ambayo ilishonwa kwa mtindo wa
namna madera yanavyoshonwa, ila yenyewe
ikiishia sehemu baina ya kiuno chake na magoti
yake.
Akaitupia sakafuni ile bastola.
Jamaa akamsukuma mbele kwa nguvu
kumuendea yule bwana na wale washirika wawili
wakapamiana vibaya. Walipojiweka sawa, jamaa
alikuwa ameketi kitandani mle ndani huku akiwa
amewanyooshea ile ile bastola iliyokuwa kwenye
uvungu wa paja la yule mwanadada, ilhali kile
kisu alichokuwa nacho hapo awali hakikuwepo
tena mkononi mwake.
Loh!
Walikodoleana macho.
“Anzeni maongezi!” Jamaa alisema kwa ukali.
________________
“Ulikuwa unatafuta nini pale makaburini wewe?”
Bwana aliyekuwa na bastola hapo awali
alimuuliza.
“Hatuendi hivyo…utambulisho kwanza…sauti yako
naijua, lakini sura yako hainiletei kumbukumbu
yoyote…ni nani wewe?” Jamaa alisaili.
Swali lake lilionekana kumzidishia udadisi
mkubwa yule bwana, aliyepata umri wa kama
miaka hamsini au hamsini na miwili hivi.
“Hunikumbuki?”
“Sikujui! Ila sauti yako…? Sauti yako si ngeni
kabisa masikioni mwangu…ni nani wewe? Na
huyu dada…ni nani? Mnanitakia nini?”
“Mnh! This is interesting…kwamba hunikumbuki
kabisa ila sauti yangu unaikumbuka?” Babu
alisaili tena.
“Hebu acha mambo ya kis…nge hapa wewee! Mi
nakuuliza maswali unajitia kukomaa na hilo la
kuwa sikukumbuki? Nimekwambia sikujui na
nataka nipate maelezo ya mchezo huu haraka
sana!” Jamaa alimjia juu.
“Ondoka hapa jijini wewe, usiwe mjinga! Hutakiwi
kuwepo hapa na wala hukutakiwa kuwepo kule
makaburini leo hii…!” Yule dada alidakia kwa
hasira.
“Excuse me…na wewe ni nani tena?” Jamaa
alihoji zaidi.
“Okay Grey, nadhani tunahitaji kuwekana sawa
kwanza hapa…” Yule mtu mzima alisema, na
jamaa akaonekana kumakinika baada ya kusikia
akitajwa kwa jina lake.
“Unalijua jina langu?”
“Na zaidi ya hapo…tutulie, tuwekane sawa…”
Mzee alimjibu.
“Sawa…anza maelezo.”
“Naitwa Benson Kanga…”
“Jina geni masikioni kwangu hilo…”
“Si ajabu kuwa hivyo, lakini ridhika tu kuwa hilo
ndio jina langu na niko upande wako.”
“Mnh, sasa kama mko upande wangu…kwa nini
hamkunijia kistaarabu zaidi?”
“Ni ngumu kidogo kuelezea…ila tu ni kwamba
baada ya kifo cha Nouman Fattawi…na mchango
wako hadi kufikia kwenye kifo kile, hukutakiwa
kabisa kuonekana popote pale ambapo japo
mzuka tu wa Nouman ungekuwepo. Uwepo wako
pale makaburini leo ulikuwa unahatarisha sana
swala hili. Watu wengine watapoteza maisha yao
bure…” Mtu aliyenadi kuwa ni Benson Kanga
alimwambia.
Yule mtu aliyetambuliwa na Benson kwa jina la
Brey alimung’unya midomo kwa namna
iliyoonesha kuwa alimuelewa sana, ingawa kama
angewepo mtu mwingine anayewasikiliza wakati
ule ambaye si katika wao, hakika asingeelewa
kitu.
“Ni kweli, lakini ilikuwa ni muhimu kujihakikishia
kuwa ni kweli Nouman Fattawi amezikwa,
Benson.”
“Haikuwa lazima uwepo pale makaburini ili
kupata uhakika wa hilo. Mimi kazi yangu ni
kuhakikisha kuwa swala zima la Nouman Fattawi
linabakia kuwa limezikwa. Nouman Fattawi
anatakiwa asahaulike kabisa kwenye uso wa
dunia…uwepo wako jijini na hususan pale
makaburini leo hii hausidii sana kwenye hilo.”
Benson Kanga alimwambia.
“Kwa hiyo mliniona nikiwa pale makaburini?”
“Tulikuhisi kuwa ni wewe pale ulipoingia
makaburini ila hatukuwa na uhakika…umebadilika
sana katika miaka michache ya hapa kati, Brey…
lakini baada ya maziko hatukukuona ukitoka…
tukapata wasiwasi. Ndio ikabidi nimtume
msaidizi wangu arudi pale kukuchomoa mle
makaburini”
“Mlijua kuwa nimo mle?”
“Ndio jibu pekee lililopatikana Brey…tumeona mtu
anayeshabihiana na wewe akiingia kisha
akatupotea mle mle makaburini. Tukaweka kambi
kwenye milango yote miwili ya kutokea nje ya
makaburi, na bado hatukukuoana ukitoka…ikabidi
tubahatishe kwa njia ile. Na imesaidia…”
Brey Jabba alitikisa kichwa.
“Hivyo ndivyo ilivyokuwa…ilibidi tujihakikishie
kuwa ni wewe kweli, ndio maana ikabidi tujihami
kwa bastola namna ile pale ulipoingia humu
ndani…”
“Nimeelewa.”
“Basi sasa fanya utoweke hapa jijini…ukae mbali
sana na jiji...huo ndio ulikuwa utaratibu. Hatutaki
ya Fattawi yaje yakukute…kazi yako umeifanya
kwa hiyo sasa nenda ukaanze maisha mapya nje
ya jiji. Tayari umeshaandaliwa pa kwenda…
natakiwa nihakikishe umefika huko na nikuache
huko. Sahau kila kitu kuhusu kazi uliyoifanya
kwenye swala la Nouman Fattawi!” Benson
alimwambia.
“Nadhani mmechelewa…” Brey Jabba alimjibu.
“Ukimaanisha nini?”
“Kuna watu nimewaona wakiingia hapa hoteini…
kama dakika tano baada ya huyu msaidizi wako
kuingia…wamenitia mashaka sana.”
Wenyeji wake wote wawili wakamakinika.
“Unamaanisha nini…? Ni watu gani?”
“Wana asili ya asia wale jamaa…kimuonekano tu
ni kama wapakistani, au wa-afghanistan…lakini
sio waarabu. Hii hoteli iko sinza, sidhani kama
watu kama wale ni wa kuja kukaa hoteli ya
sinza...wangekaa angalau kariakoo huko au
katikati ya jiji…” Brey Jabba alisema.
Benson aliguna.
“Unamaanisha nini?”
“Kwamba wao, kama mimi, waliweza kumfuata
huyu msaidizi wako kutoka huko alipokuwa hadi
hapa…”
“No! Hilo haliwezekani! Nilikuwa makini sana…”
Mwanadada alimaka, na kuendelea, “…mbona
wewe nilikuona wakati unanifuata na nilikuacha
kwa kuwa nilitaka uje hapa!”
“Sawa. Ulimakinika na mimi…hukuweza
kumakinika na wale wengine…jamaa wamo humu
hotelini nawaambia.” Brey Jabba alisema.
“Lazima tutoweka hapa…sasa hivi!” Benson
alisema huku akiinuka. Akaganda kwenye hatua
zake pale wote mle ndani waliposikia mlango wa
kile chumba walichokuwamo ukabishwa hodi
kutokea nje.
Wakatazamana, wakiwa kimya, macho
yakiwatembea.
Hodi ikabishwa kwa mara ya pili, kwa nguvu
zaidi.
“Wamefika.” Brey Jabba alisema kwa utulivu wa
kuogopesha…
***mnh! Kuna usiri ndani ya usiri hapa