Wimbo wa DESPACITO ulipataje hawa viewers zaidi ya Billioni 5?

Labda mtu mmoja anauangalia ktk simu, desktop ma tablet. 3 viewa hizo kwa mtu mmoja.
 
Na huo ndiyo ukweli bro........... ingekuwa mtu ukitazama kitu youtube mara 1000 then ina count kama views 1000 mbona kungekuwa hakuna fairly katika ushindani wa views za youtube
aliyekwambia kuna ushindani wa views nani? Ile si biashara watu wameweka matangazo... kwani tangazo nitakaloliona leo nikiangalia video husika ni hilo hilo nitalikuta kesho??
 
unaweza ukaweka hapa hayo mahojiano.. isitunishe tu misuli mkuu!!
 
Kutazamwa mara bilioni 7 haimaanishi kuwa waliotizama wanafika hiyo idadi, mtu mmoja anaweza tizama hata mara mia
kuna watu bado hawaelewi.. nimeamini watz ni wagumu sana kuelewa
 
Jamani muwe waelewa... YouTube inahesabu device na si mara ngapi umeangalia.. Fanya research ndogo tu.. Ingia You tube tafuta video yenye viewrs wachache na ni yazamani kidogo nikimaanisha haitrend Right now.. Kisha iangalie uwezavyo utapata majibu
 
Tofautisha kati ya views na viewers

Bila ubishi bandiko lako limelenga katika views billion 5. Je nini maana ya hivyo vitu viwili hapo juu.

Kwa tasfiri ya haraka

■Views ni idadi ya kiasi gani content (video) imetazamwa.
■Viewers ni idadi ya watumiaji mtandao waliotazama.

Hiyo bilion 5 ni idadi ambayo Despacito imetazamwa ila sio idadi ya watu waliotazama, inawezekana watu milion 900 ndiyo wameitazama ila wakairudia rudia mpk kufikia jumla ya views hizo (huu ni mfano tu)

Hivyo basi kile youtube wanachoonesha chini ya video mfano 2M views ni idadi kiasi gani video imetazamwa ila si idadi ya watazamaji.

Hitimisho:
Ulichokiona hapo kwako kipo sahihi kwakuwa ni views.. ila ingekuwa viewers ningekataa kwasababu dunia haina watu bilion 5 walio na uwezo wa kuaccess internet (youtube).
 
Upo sahihi mkuu.

Pia nimejikita kwenye views tu
 
yes, mtu mmoja unaweza tizama zaidi ya mara 1 kwa kupitia gadgets tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…