Wimbi la kuvunjika kwa ndoa

Wimbi la kuvunjika kwa ndoa

Sister kama kuna kitu siku hizi watoto hawaogopi tena ni wazazi wao kwasababu wazazi wanafanya matendo mabaya kwahiyo hata wao hawajiamini kukosoa,sasa mie naonelea kanisa lianzishe harakati za kuita wazazi wenye vijana ili wafanyiwe reinassance na kwasababu ndoa inasimamiwa na kanisa bado ndo lenye uwezo wa kureshape wanandoa waweje na matokeo yake,tusirushiane mpira,kanisa lifundishe ndoa kama kozi na wahusika waive. nalog off.
 
Kwahiyo kama wazazi wamefika sehemu na wao wakawa ni tatizo ndo na kanisa liache kufanya kazi yake?? inamaana mmeamua kufeli nyote siyo?

Viongozi wa makanisa mnaogopa kukemea na kufundisha sasa na nyie mnakuwa mzigo na sehemu ya tatizo,kwa mtindo huu wa viongozi wanaoogopa lawama hakika kila kitu kitafeli ..mmepewa mamlaka lakini mnaogopa,why this? ndoa ni sakramenti na nyinyi ndo mnafungisha ndoa,swali,mnafungishaje ndoa watu ambao bado hamna uhakika kama wameelewa juu ya kitu mnachowafanyia,tena agano?
 
Mwaka jana kuna mshkaji ndoa yake imekufa hadi leo kisa ni jamaa kumsema mkewe mara nyingi kuhusu mavazi!!!!!!!!
Shemeji anapenda mavazi ya kisasa hasa ya kuanika sehemu nyeti za mwili na jamaa aliamini angembadili ndani ya ndoa!! Binti anasema amechoshwa na ugomvi wa mavazi ambayo yeye anaona kawaida!
Vijana hawaelewi maana ya ndoa!!
 
hela imekuwa mungu wa wanadamu kwa hiyo umuhimu wa mwenza umepungua kwani kwa sababu hakuna mamlaka za jamii yenyewe ambazo zinaweza kuwabana na kuwawajibisha wanandoa na makundi ya namna hii zamani yalikuwa na nguvu sana lakini baada ya huyu mungu mgeni hakuna mtu yuko tayari kuwajibishwa including fine. jambo lingine thamani ya utut hasa mwanamke imekuwa replaced kwa kutamaniwa kwa ajiri ya uzinzi na wanawake wako radhi kwa hilo kwani ni nadra sana leo hii mwanamke kuwa na affection ya ndani kwa mume kapuku. yaani kwa maana nyingine mwanamke kwa sasa ni commodity na yeye ndie wa kwanza kuhalalisha hali hiyo ya biashara mwili ambapo si lazima kusimama kinondoni makaburini ndo uonekane unauza mwili.

ila kikubwa kabisa ni kupotea kwa hofu ya Mungu kwa wanadamu. na uking'ang'ania kutokubali ndoa yako ivunjike hasa endapo mwenzako keshaamua kukutupa. kwanza atakuchafua na kukutwisha kila uchafu wewe ambaye unafanya kila njia kutokubali kuvunjika kwa hiyo ndoa basi jiandae kuchafuliwa na kutukanwa lakini bora kuwa mjinga kwani ukweli ni kwamba BWANA atarudi na kisasi mkononi mwake. ISAYA 35 8-10 Biblia Takatifu inasema hao wanaotembea kwenye njia ya utakatifu japokuwa wataonekana kuwa ni wajinga lakini hawatapotea katika njia hiyo

(Isa 35:8 [ESV2011])
And a highway shall be there, and it shall be called the Way of Holiness; the unclean shall not pass over it. It shall belong to those who walk on the way; even if they are fools, they shall not go astray.

(Isa 35:9 [ESV2011])
No lion shall be there, nor shall any ravenous beast come up on it; they shall not be found there, but the redeemed shall walk there.

(Isa 35:10 [ESV2011])
​And the ransomed of the LORD shall return and come to Zion with singing; everlasting joy shall be upon their heads; they shall obtain gladness and joy, and sorrow and sighing shall flee away.
 
hapo sasa mdogo wangu,sio rahisi kwa kweli,mi mzima sijui wewe mgogo wangu na familia yako.
Mzima dada....?
Ni kweli siku hz mtu anaingia kwenye ndoa na kauli mbiu moja tu ni kula raha......sasa mtu huyo apate shida unadhani atakaa...
 
tumrudie Mwenyezi Mungu tu na mambo yote yatakuwa sawa....kila mmoja amuombee mwenzake na kuuombea uhusiano uliopo udumu kwa furaha, upendo, amani, uaminifu na kheri nyingine zote.....na ninaamini kuwa sio ndoa zote ni majanga au wanataka kuachana, NO! kuna ndoa zimejaa raha hadi wahusika wanajiuliza HIVI NI KWA NINI HATUKUOANA MAPEMA? .....kama ya kwangu...!!
 
Ndoa kwa sasa zina changamoto nyingi na mtu anaingia kwenye ndoa eti kwa sababu kaona umri umeenda, ma age mate wake wameolewa wote sasa akikutana na mtu hata kama anaona hajampenda kivile basi tu anaolewa baada ya muda timbwili zinaanza na ni vigumu sana kumvumilia au kumsamehe mtu ambaye hukumpenda kwa moyo wa dhati. Ushauri wangu ni huu wadada oleweni kwa sababu mmepata watu mnaowapenda kwa dhati na mko tayari kuishi nao kwa upendo na uvumilivu na sio kuolewa kwa sababu umri umesonga au marafiki wameolewa. Pia tukumbuke sehemu ya tendo la ndoa ni muhimu lakini muda wa kushiriki tendo ni mchache na muda mwingine ni kufarijiana na kupanga maisha na kulea watoto kama mkijaliwa hivyo kuolewa ni umpendae kwa dhati ndo vema. Pia ili ndoa zidumu ni vema mungu atangulizwe mbele ili ayaongoze maisha. Mungu aliweka ndoa akikusuudie iwe paradiso ndogo na sio uwanja wa vurugu.
 
mashini, tulisha lizungumza hili sana kiasi watu wanaweza kuchoka kusoma tena comments!

Ila kwa kifupi, kwa mtazamo wangu, wengi wao huwa hawajafahamiana vizuri (wale wanaokutana kwa muda mfupi) au hawajajiandaa kuishi maisha ya ndoa kisaikolojia (wamelazimishwa na familia, kupeana mimba, mazingira nk) au kuiga (kwa sababu age mate wake wote wameoa/kuolewa) au kwa nia ya kupata mtoto tu au kwa nia ya kupata mali tu toka kwa mpenzi wake, kutokujuana tabia halisi mapema, kudanganyana nyakati za uchumba na ukweli kujulikana baadaye nk.

pia kuoa/kuolewa kwa kufuata hisia za papo kwa papo, kukimbizana na muda ni tatizo lingine pia
 
Back
Top Bottom