Wilson Oruma: Viongozi Simba wafanye maamuzi magumu kwa Chama

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
Mchambuzi wa soka Wilson John Oruma amesema umefika wakati wa Simba SC kuachana na kiungo wao mshambuliaji, Clotous Chama kwani hakuna cha ziada atakachowapa.

Oruma amezungumza hayo ikiwa ni siku chache baada ya Chama kuubeba mchezo wao dhidi ya Jwaneng Galaxy na kuibuka na ushindi wa 6-0.

Oruma amesema, Chama amekuwa akicheza ana akili za viongozi kwani hufanya vizuri pindi mkataba wake unapokuwa unaelekea ukingoni.

“Chama ana jambo lake ndio maana anafanya hivi alivyofanya, baada ya muda atarudi kwenye desturi yake kama kawaida.

Ni wakati sasa viongozi kuchukua maamuzi magumu ya kuachana naye ili walete mchezaji anayeweza kuwavusha zaidi ya hapa,” alisema Oruma.
 
Unatakiwa ueleze kama huyu ni Wilson Oruma wa Nigeria au wa pale Ukonga Mazizini.

Wakati mnaandika andikeni stori zinazoeleweka ikiwemo na source ya habari na ikiwa bila source inakuwa tu kama stori za vijiweni.
 
1706701034523.jpg
 
Ni kweli. Simba inatakiwa itafute mrithi wa Chama kipindi hiki ambacho nguvu zake zinaelekea ukingoni. Maeneo mengine kibao ikiwemo mafoward yanahitaji usajili wa maana.

Sehemu ya Simba yenye uhai zaidi ni mabeki. Washambuliaji wanatia huruma
 
Back
Top Bottom