IROKOS
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 10,182
- 7,844
Habari nilizopewa kutoka Azam media ni kwamba aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema ndugu Wilbrod Slaa ameshindwa kufika ndani ya studio za Azam media bila kuwepo kwa taarifa yoyote kutoka kwake.
Kuna jambo lipo nyuma ya pazia. Soon litajulikana.
Uko sahihi sana mkuu, mimi saa 2.50 asubuhi nimetune Azam 2 nikakuta kuna mwanasheria wa AZAK anahojiwa na mdada mmoja, ambaye kipindi chake kilipoisha akasema kinafuata kipindi cha mahojiano kati ya Tido na Slaa. Nikasubiri ghafla saa 3.00 nikaona wameweka vikatuni, nikamuita mtoto wangu mpenda vikatuni aje aangalie ila yakianza mahojiano aje aniite. Mpaka karibu saa 4 sikuona kitu na wala Azam hawakutoa maelezo ya kutuomba radhi. Ila asubuhi saa 2 stat Tv walikuwa wanarudia yale mahojiano ya juzi.