William Mwamalanga: Napendekeza kura ya siri kuwataja wauaji wa albino

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,678
68,662
Umofia kwenu wana JF,
Mwenyekiti wa wachungaji,Ndugu Mchungaji William ameshauri serikali ifanye mkakati wa kura ya siri ili wamanchi wawataje wauaji wa albino maana wanajulikana.

Source:ITV
 
Naafiki hilo kiongozi, na sidhani kama hii kura ya siri inahitajika katika baadhi ya maeneo ambayo hayajakithili kwa mauaji... Kura hizo zipigwe hasa maeneo yaliyokithili kwa mauaji hayo!!
Hofu yangu tu kura hizo kutumika vbaya kwa watu wengine kuwataja wasiohusika kama kuna ugomvi baina yao..
 
Popote ulipo taja Jina la mtu unayemhisi anahusika na unyama HUU! KWA WATU WA KIGOMA TUKUMBUSHENI YULE MGOMBEA UBUNGE ALIYEDAIWA KUJIHUSISHA NA UCHAFU HUU KTK UCHAGUZI WA 2010.KAMA TAIFA TUSHIRIKIANE KUKOMESHA AIBU HII.
 
jamaa nimemuelewa sana,kwanini kila ikikaribia uchaguzi ma albino wanauwawa sana?wauaji wanajulikana lakini hawachukuliwi hatua kikwete ana ajenda gani?daima hapendi kusikia hili jina wanaloliita eti serikali sikivu.Jamaa kafunguka
 
Naafiki hilo kiongozi, na sidhani kama hii kura ya siri inahitajika katika baadhi ya maeneo ambayo hayajakithili kwa mauaji... Kura hizo zipigwe hasa maeneo yaliyokithili kwa mauaji hayo!!

Mchungaji ametoa wazo zuri sana,hope pinda na jeshi la polisi watayafanyia kazi,yes kura zipigwe sehemu zenye rate kubwa ya mauaji.

Duh! Uko fast, hazijapita hata dk 2.

Ndio maana ya mitandao ya kijamii hata kama mtu hayupo nyumbani anajua kitu gani kinaendelea.
 
Kama wanajulikana si ataje huyo mchungaji,ana roho ya uwogo,anamanisha wanasiasa,ni vizur akawa mfano wa kuanza kutaja,hasipge porojo tu .
 
Kura za siri huwa hazina maelezo yoyote yanayoweza kumbaini muhusika wa tukio.

Ni vema mwanachi yeyote amabaye atakuwa ana elewe kwa dhati kuwa fulani ndiye anaye husika na mauaji ya maalbino aende moja kwa moja kutoa taarifa kwa viongozi wa vyombo vya dola akaeleze namna ambavyo mtuhumiwa anavyo husika na mauaji ya albino.

Maelezo ya mtoa taarifa kwa siri ndiyo yatakayo viongoza vyombo vya dola kubaini uhusika wa mtuhumiwa bila mtuhumiwa kuelewa kuwa taarifa za uhusika wake zimetokana na mtu aliyekwenda kutoa taarifa kwa siri.
 
Hata ningempigia mtu ninayemchukia lakini naamini watuhumiwa Wote serikali inawajua
 
Badilisheni serikali wekeni ukawa wauwaji watakamwatwa.himi chama na serikali yake wapo hoi hawawezi tena kuijali jamii.alipigwa dr ulimboka hadi leo afya taabani na hata hawajali hali wananchi tumebaki hatuelewi.albino zaidi ya 70 wamepotea rais hajali.waziri mkuu hajali.mkuu wa police hajali.
 
wenye chuki binafsi watatajana hapa

Wingi wa kura ndio utadetermine chuki au ukweli,kama watu wengi wamekupigia kura lazima polisi wakuchukue kwa mahojiano huko ndiko kitajulikana kama ni kweli au unasingiziwa baada ya kupigwa pinchi.
 
Kama wanajulikana si ataje huyo mchungaji,ana roho ya uwogo,anamanisha wanasiasa,ni vizur akawa mfano wa kuanza kutaja,hasipge porojo tu .

Hata angetaja usingeamini usingekosa lakukosoa...kama wewe unaona hayupo sahihi ni mwongo , toa suluhisho
 
Umofia kwenu wana JF,
Mwenyekiti wa wachungaji,Ndugu Mchungaji William ameshauri serikali ifanye mkakati wa kura ya siri ili wamanchi wawataje wauaji wa albino maana wanajulikana.

Source:ITV
Anashangaza na sijui ni mchungaji wa dini gani? Mara anasema Wauwaji wanajulikana na hapo sijui anataka kura ya siri ya nini? Anashindwa pia kujua kuwa kura hizo mara nyingi ni za chuki na kuingiza watu wasio kuwemo. Mimi nilifikiri yeye akiwa "mtumishi wa Mungu" angehimiza serikali kufanya kazi yake ya kuchunguza wa kina kubaini wanaotenda Madhambi hayo. Lakini zaidi utafiti unatakiwa kubainisha hasa chanzo ch haya maovu - je elimu yetu imeshindwa kutuelimisha na dini zetu zimeshindwa kututoa katika ujima na kutuletea ustaarabu? Yeye anakazana na kura ya siri inayochochea chuki!
 
Mwaka 2007, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bukombe na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Bwana Magesa Mulogo ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mwanza alinukuriwa kama ifuatavyo:
"Tumebaini siri nzito katika mauaji haya ya albino; na hasa baada ya kuweka mtego wilayani Kahama ambapo wahusika walijipanga, wakavaa magwanda yao na kuficha sura zao na baadaye wakampigia simu tajiri yao aliyepo wilayani Igunga mkoani Tabora kuwa wako tayari kwa shughuli hiyo na walipokusanyika wote tayari kwa mauaji hayo, tukawakamata na kuanza kuwahoji,"
Kwa kauri hiyo ya mkuu ni dhahili serikali inawafaham wauaji na wahusika wakuu wa mauwaji ya albino.
 
Wingi wa kura ndio utadetermine chuki au ukweli,kama watu wengi wamekupigia kura lazima polisi wakuchukue kwa mahojiano huko ndiko kitajulikana kama ni kweli au unasingiziwa baada ya kupigwa pinchi.
Na wewe unaona ni sahihi hivyo ukapigwa pinchi kwa Sababu tu umepigiwa kura za siri? Huko vijijini ukiwa na mali kidogo unakuwa pia na maadui wengi wanaofikiria umezipata kwa 'ushirikina'
 
Miaka ya 80 tulikuwa na kipindi cha. Mikingamo, vyombo vyetu vya usalama na Habari vikishirikiana ushenzi huu utaisha.

kura pia ni sawa kwani watu wengi wakimtaja Mtu haitakuwa wote wanamchukia.
 
Back
Top Bottom