William Mhando MD Mpya wa TANESCO

Tanzania bila udini haiwezekani!

Biblia na Quran zipo Ikulu. Wachaguliwa na Wateule wanaapa kwa kuvishika vitabu hivi. Udini haupo ila majina ya kidini yapo na yanawasaidia baadhi ya watu kuteuliwa.
 
Huyu MD sijui kama ndo tumepata au tumepatikana!

does it matter?

asilimia kubwa ya watanzania hawatumii umeme...ni siye wa mijini tuko concerned...tena hata humu mijiji si wote?

ni kwa muktadha huo najiuliza kama kuna tofauti yoyote kama tumepata au kupatikana?
 
Hapo roho zenu kwatu kabisa! pongezi kila kona kwanini? kwa kuw a kateuliwa William! Angekuwa Juma hapo pasinge tosha hapa.........
Mods, there's a feature whereby such-a-like comments could automatically disappear or become invisible by-default through contributors' vote of "NO THANK"! I've seen this feature in Yahoo! Online News, and could be better to borrow a leaf. Itasaidia kupunguza MIKOSI kama hii kwani ukikutana na 'contribution' kama hii mwanzo wa siku basi siku yako yote imeharibika!!

By the way, pongezi kwa bodi ya TANESCO maana wamezingatia vilio vya muda mrefu kutaka mashirika yetu yasiongozwe na wanasiasa. Muhimu ni kwa Muhando kutoa ushirikiano na ushawishi ili shughuli za huduma za umeme zitolewe na kampuni tofauti ikiwezekana TANESCO ibaki na jukumu la kuzalisha umeme pekee!

IMHO, huduma za umeme haziwezi kuwa bora kama shughuli za kuzalisha, kusambaza, kuuza, kuelimisha, na nyingine zitatekelezwa na shirika moja pekee. Kwa ufanisi ni lazima TANESCO ipunguziwe majukumu, ibakize machache ambayo hakutakuwa na 'excuse when it comes to accountability'. So far, TANESCO has lot of excuses and sometimes you could even sympasize with them amid exhaust responsibilities!!
 
Congratulations to new MD. We wait for your contributions to reducing black out in this country.

“If we are serious about winning, we have got to realize that the true test of our commitments is ahead of us, not behind us” –Bill Clinton the ex US president.


Karibu Jukwaani Mzee Tegambwage!
 
Matatizo ya umeme ni muda sasa, kabla ya u-MD alikuwa mkuu wa ugavi sasa sijui shida ilikuwa maamuzi - yaani hakuwa na uwezo huo? La sivyo naye ni wale wale!
 
BARUA YA WAZI KWA WILLIAM MHANDO

KWANZA ninachukua fursa hii kukukaribisha katika kiti cha Ukuregenzi wa TANESCO. Ninaamini utakuwa mtu wa mabadiliko na mwenye vision ya kuona Tanzania nzima ikiwa chini ya mwanga wa taa za umme unaotokana na vyanzo mbalimbali tofauti na TANEESCO ya huko nyuma.

Nakushauri uishauri serikali kwamba biashara ni biashara na governance ni governance na serikali na watumishi wake wawe wa kwanza kulipa bili zao ili shirika lijiendeshe kibiashara.

Wafurahishe wafadhili kwa kuhakikisha unajua kila shilingi ya TANESCO inayoingia inavyotumika katika kuendeleza jukumu mlilopewa la kuleta umeme sio tu mjini bali pia vijijini.

Mhesshimiwa, waangalie wafanyakazi wako ambao ni wategaji wakubwa na wanaofanya kazi inayochukua saa moja kwa siku nzima tena usiku ili tu kupata ovataimu bila ya kutambua kuwa kufanya hivyo kunaweza kuleta maafa mbalimbali ikiwemo vifo na kuvunjiwa nyumba na majambazi katika giza achilia mbali kuathiri uzalishaji mali na vifaa mbalimbali vya umeme viwandani na majumbani.

KUBWA zaidi, hata hivyo mheshimiwa ni kutokubali watu wako kufanya kazi kama vile wanatufanyia jamala au huruma bali wawe ni watumishi wa kweli kweli maana kwa uhakika hapana sababu ya shirika lako linalostahili kutunywa senti kila dakika kuwa shirika lisiloingiza faida ila kama wanasiasa wanaligeuza ni shamba la bibi.

ONDOKANA NA UJINGA WA KUNYIMA wenye maduka umeme eti kwa sababu mpangaji wa zamani hakulipa bili yake. Au kwa kuwa kuna deni la nyuma lisilowahusu wapangaji wa sasa basi complex nzima ya maduka ikanyimwa umeme. MTANGULIZI wako hakuangalia hili kabisa kwa upande wa hasara inayoipata TANESCO wakati inawanyima wateja watarajiwa umeme eti kwa kumuadhibu mwenye nyumba au mpangaji wa zamani. HIi sio akili hata kidogo.

Kama kuna complex ya maduka inayokosa umeme kama zile za TABATA shule ambako kuna maduka zaidi ya 10 yanakoseshwa umeme kwa makusudi kwa sababu wenye nyumba walikuwa na ugomvi wenyewe kwa wenyewe na sasa wateja wapya wanataka umeme lakini TANESCO inawanyima bila kigezo wala sababu ya msingi mara moja hakikisha wateja hao watarajiwa wanapata umeme kwa LUKU ili shirika liongeze kipato chake fumba na kufumbua.

NInawashauri kuwa oanishe TIN number ya kila mfanyabiashara ili muwakamate wahuni wachache wanaotuharibia sisi wengine biashara zetu ambazo bila umeme ni kama vile mtu unatumbukiza shilingi ******.

Nimalizie kwa kukupa tena hongera nikiamini utakuwa ni MD wa kwanza atakayekuja na sera ya USIMNYIME ASIYE NA KOSA UMEME na shirika lako lisiwe la kunyima watu umeme bali la kuongeza kwa kasi kubwa iwezekanavyo watumiaji wa umeme kila mahala nchini- Mungu awe nawe, Mungu Ibariki TANESCO mpya.
 
Nasikia Muhimbili hospitali nao wamepata CEO mpya na anaanza juni 1, 2010. ebu mliyopo jikoni kama mna data mzirushe hapa kama ilivyo kawaida ya jamii forum.
 
CEO Engineer Mhando hongera unaieelwe Tanesco na nina uhakika unaelewe kiundani matatizo ya Tanesco toka kuzalisha umeme mpaka kumfikia mteja ( power generation,transmission,distribution).Wadau wanasubiri vitendo sahihi.Nakutakia heri.
 
tatizo kubwa kwenye mashirika ya jinsi hii, ni watendaji wa ngazi za chini ya huyo mkuu aliyeteuliwa. anaweza akaja na mipango yake lukuki, lakini watendaji wake wakamuangusha kwa kuzoea kufanya kazi kwa mtindo wa enzi za 47! namuunga mkono mchangiaji aliyesema kuwa MD aanze kwa kuikomalia serikali yenyewe, kwa sababu ndio mdeni mkubwa wa Tanesco! Laiti angefanikiwa kuwafungia LUKU, angemaliza mchezo. Kwa sababu hata madeni serikali inajiuliza kuilipa Tanesco kwa kujiona kama ndio mmiliki wake! Lazima Tanesco yenyewe nayo ijiendeshe kibiashara, kimsingi Tanesco haikupaswa kushindwa kujiendesha!
 
Ana undugu na Tido wa TBC?

inawezekana ni ndiyo au hapana...

itoshe kujua kuwa Mhando ni majina maarufu kwa wabondei kutoka mkoani Tanga na Wazigua ambao wanapatikana katika maungio ya mikoa ya tanga, morogoro na pwani.

Tido ni mtu wa tanga, sifahamu huyu William ni wa wapi?
 
Congratulations to new MD. We wait for your contributions to reducing black out in this country.

“If we are serious about winning, we have got to realize that the true test of our commitments is ahead of us, not behind us” –Bill Clinton the ex US president.

Mzee karibu sana Ukumbini..mchango wako unahitajika sana hapa JF

Sad but true my friend, sad but true.
Msitegemee kipya kwasbabu naye alikuwepo miaka yote hio iliyopita ya uzembe wa TANESCO na alikua katika management board!

........Mkuu hiyo ni kweli kabisa............inawezekana kabisa kuw ahuyu bwana akawa na msimamo tofauti na kiongozi aliyepita.......hebu tumpe nafasi................
..............Nakumbuka wakati ule Magufuli alipokuwa naibu Waziri hatukumsikia sana...........alipopewa uwaziri kamili....nafikiri kila mtu alimkubali kwa kazi aliyoifanya...............

Mkuu Nyamgluu....usipotee sana namna hiyo...........
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom