William Lukuvi amvua nguo Tundu Lissu

William Lukuvi amvua nguo Tundu Lissu

Nahisi unataka kuhalalisha dhambi kwa kufanya dhambi.

Sitaki kuhalalisha dhambi kwa kufanya dhambi kama hisia zako zinavyokutuma bali nataka kuonesha inconsistency katika maamuzi ya Spika na Naibu wake!! Inakuwaje wabunge wengine wasiadhibiwe kwa kuliongopea bunge eti kwasababu ni wamagamba na wabunge waupinzani ndio waadhibiwe?
 
Sitaki kuhalalisha dhambi kwa kufanya dhambi kama hisia zako zinavyokutuma bali nataka kuonesha inconsistency katika maamuzi ya Spika na Naibu wake!! Inakuwaje wabunge wengine wasiadhibiwe kwa kuliongopea bunge eti kwasababu ni wamagamba na wabunge waupinzani ndio waadhibiwe?

Wengi tunajua kuwa kiti hakina usawa katika kutoa haki lakini hii isitufanye tuwatetee wabunge wanaosema uongo hata kama tupo upande wao. tuoneshe kukerwa na tabia ya uongo ili kuwafanya watembee ktk ukweli.
 
Hivi maana ya kuvuliwa nguo ndio maelezo mepesi kama haya, ama kweli kiswahili kinatumika vibaya.
 
Nilishasema humu bungeni kuwa TINDU LISSU hana uelewa wowote wa sheria zaidi anachokifanya ni kucheza na akili za wabunge wenzakekutokana na uelewa mdogo wa vifungu vya sheria ambavyo anaamini wenzake ambao hawana taaluma hiyo hawatamshtukia na hivyo huamua kukomalia huko.
Hata mimi natazama bunge sasa hivi , kwa kile walichokisema LUKUVI, PINDI HAZARI CHANA na sasa ufafanuzi anaoutoa mwanasheria mkuu wa serikali , FREDRICK WEREMA, ni dhahiri LISSU ameumbuka.

TLS inamtambu wakili wa mahakama kuu na mahakama zote za chini yake,na ndio maana hajawahi kushindwa kesi yeyote ya jinai dhidi ya serikali legelege ya ccm,wewe kilaza tu ila wananchi wanaokaa karibu na mto tigite na north mara wanamjua kama bonge la lawyer,serikali yako ya magamba inamjua kama ni mwakili msomi na makini ndo maana magamba kipindi kile kwenye kesi ya city water serikali yenu ya magamba ilimpa kazi kuitetea serikali ya tanzania,ila sio mbaya najua buku 7 +1000 inakuhusu
 
duh ngoja ntafute miwani niangalie vizuri hizo nguo alizovuliwa lissu nikikosa nakuvua wewe mtoa mada sawa ?
 
Wakati akichangia mswada wa sheria ya marekebisho ya Katiba, Mbunge wa Zanzibar amesema TINDU LISSU hajawahi kuwapenda wazanzibari na wala hapendi kuona Muungano ukidumu.

Mbunge huyo amewataka Wazanzibari kujua kuwa TINDU LISSU ni yule yule ambaye anajifanya kuwatetea wakati ni muongo mkubwa na kuwataka washikamane katika kuitengeneza katiba mpya, kuitetea Zanzibar na kumpuuza TINDU LISSU.

Mbunge huyo alienda mbali na kusema Wabunge wa CUF watakuwa wamepitiwa tu na upepo wa janja ya jana ya TINDU LISSU ya kujifanya kuwatetea na kujikuta wakiungana nao leo lakini kiuhalisia ni uongo mtupu.
 
Lissu na Mbowe ni wanafiki tu. Hata Dr Slaa alienda kuwahadaa wazanzibar
 
hakuna m.bwa hata mmoja ccm anaweza jibu hoja zakisheria za lissu!wote wametapatapa tu,tatizo litz ccm hii nchi limejiandalia wajinga wengi ili ikae madarakani mda mrefu kupitia ujinga wawatu...namm sishangai sabu najua nawanao ona lissu kaumbuliwa niwaji.nga walewale mlioandaliwa!lakini giza hata liweje tochi ndogo huliondoa...
 
Leo LISSU na CHADEMA yao wanajidhihirisha kuwa hawana mahusiano mazuri na wazanzibari
 
Wakati akichangia mswada wa sheria ya marekebisho ya Katiba, Mbunge wa Zanzibar amesema TINDU LISSU hajawahi kuwapenda wazanzibari na wala hapendi kuona Muungano ukidumu.

Mbunge huyo amewataka Wazanzibari kujua kuwa TINDU LISSU ni yule yule ambaye anajifanya kuwatetea wakati ni muongo mkubwa na kuwataka washikamane katika kuitengeneza katiba mpya, kuitetea Zanzibar na kumpuuza TINDU LISSU.

Mbunge huyo alienda mbali na kusema Wabunge wa CUF watakuwa wamepitiwa tu na upepo wa janja ya jana ya TINDU LISSU ya kujifanya kuwatetea na kujikuta wakiungana nao leo lakini kiuhalisia ni uongo mtupu.

..wabunge wa Znz wajadili hoja, siyo mtoa hoja.

..hoja ni hii: composition ya bunge la katiba iwe 50/50 kati ya Tanganyika na Zanzibar.

..kwanini wabunge wa Znz wanapinga hoja hiyo??
 
Huu Muswada wa Rasimu ya Katiba unaweza kuwa Kama Ule wa tozo za Card za Simu ,Tutakumbuka shuka kumekucha.
 
Dah, hapo ushabiki upo wapi? tunasema mara kwa mara kuwa CHADEMA wana tabia ya kukurupuka. haya ndo madhara ya chama kuongozwa na vihiyo
Hapo ndo akili yetu wabongo ilipogota, kupenda chama bila kujali maslahi ya taifa, mtu akisemea maslahi ya taifa kakurupuka!! aya kanyaga twende....
 
[h=1]MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR AJIBU MAPIGO YA TUNDU LISU, NI KUHUSU MABADILIKO KATIBA YA ZANZIBAR.[/h]



Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman (Pichani) ameshangazwa na mwanasheria mwenzake Tundu Lisu kwa kutofahamu madhumuni na malengo ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yaliozaa serikali ya umoja wa kitaifa. Kauli ya Mwanasheria huyo aliitoa katika baraza la wawakilishi wakati akifafanua baadhi ya mambo ya kisheria baada ya wajumbe wa baraza hilo kumtaka afanye hivyo kufuatia kauli ya ya Tundu Lisu aliyoitoa bungeni wiki hii.​
"Sasa kuja kwa haya yametuonesha kwamba kuna wenzetu kumbe wana fikra kwamba Zanzibar iliwahi kutawaliwa. Maana mtu anaposema marekebisho ya 10 ya Zanzibar yamjitangazia uhuru maana yake ana fikra na huyu ni mwanasheria mtu kafika mpaka kuwa mbunge anayeaminika na chama chake lakini anasema kwa kufanya hivyo Zanzibar imejitangazia kuwa huru kwani tuliwahi kutawaliwa?," alihoji Othman.​
Akijadili bajeti ya wizara ya makamu wa rais wa jamhuri ya muungano, huko Dodoma Mbunge wa Singida Mashariki wa Chama Cha (CHADEMA) Tundu Lisu alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa Zanzibar imefanya katiba kwa kujitangazia kuwa ni nchi.​
Othman alisema marekebisho ya katika ya Zanzibar yalikuja baada ya hoja nyingi ambazo hazikuwa na majibu katika muungano ambayo ilikuwa ikisema ni Zanzibar ni sehemu ya muungano, lakini kama nini mkoa? Shehia? Kata? au kijiji?, haya hayakuwa na jibu katika katiba ya muungano.​
Kufuatia maridhiano Zanzibar ndipo wazanzibari wakamaua kufanya kukufikia marekebisho ya 10 ya katiba yao ambayo ilifafanua kuwa zanzibar ni nchi na ndivyo ilivyo kwa sababu haikuwahi kutawaliwa kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wanavyofikiria.​
"Marekebisho ya 10 ilichofanya ni kusema kwamba ikiwa mtu hatambui, maana ilikuwa imeshaonesha dalili kwamba kuna wengine hawatambui hilo tena wakubwa. Sasa marekebisho ya 10 yalipokuja ni kufafanua tu, kama kuna mtu hatambui sisi wenyewe tunajitambua" alisema mwanasheria huyo huku akiungwa mkono na wajumbe kwa kupigiwa makofi.​
Huku akishangiriwa na wajumbe wa baraza hilo mwanasheria mkuu alisema hakuna mtu ambaye atawazuwia kusema "Aaah katiba yenu isiwe namna gani au isiwe hivi na ndio maana unakuta katiba za muungano zipo nyingi lakini kila mmoja ina muundo wake kwa mujibu mlivyokubaliana nyinyi wenyewe."​
Mwanasheria mkuu alisifu muungano wa miaka mingi wa Uswizi ambao unatambulika na kuigwa duniani kutokana na kufuata misingi imara iliyowekwa na wananchi wenyewe.​
Alisema muungano ambao umedumu na unasifiwa ni Swiss Federation kwa sababu umeanza tokea mwaka 1292 na umekwenda kwa mafahamiano hadi mwaka 1874 wakatunga katiba ambayo wameifanyia mapitio upya mwaka 1999 na nchi hiyo ina serikali 26, lugha nne rasmi na ndio muungano amabo umedumu na nchi ambayo ni imetulia duniani.​
Mwanasheria huyo alisema mashirika yoye ya kimataifa yapo Uswizi kwa sababu ya muungano huo uliotumilia na kwa sababu umekuwa na misingi imara ya kuhakikisha muungano ule unaweza kuhimili mabadiliko yoyote yatakayokuja ya kisiasa.​
"Mheshimiwa Naibu Spika nitumie fursa hii hapa hapa niseme wakati tupo katika mchakato wa maoni ya katiba nadhani ni wakati mzuri kuiweka sawa ile misingi ya muugano kama Uswizi,"na kuongeza: "Wakati mwengine napata wasiwasi nasema hii khofu yangu niiseme hapa kwamba tunaanza kubishana kuhusiana na watunza nyumba wawe wangapi, waendeshaji nyumba wawe wangapi, wawili, watatu, wanane au watano? Lakini tatizo letu la msingi mimi nadhani ni nyumba yenyewe iweje. Kama tunaamua kuishi, maana mfumo wa sasa hivi mmoja anaishi nyumba kubwa na mwengine mabandani huko uwani huo sio utaratibu tunao."​
Aidha aliwaambia wajumbe hao kwamba wanzanzibari wana mambo ya msingi ya kujadili kuliko kuzungumzia idadi ya watunza nyumba akimaanisha kero za muungano zilizopo na kushindwa kuafikiwa.​
"Kwa hivyo mimi niwaombe sana waheshimiwa wajumbe, niwaombe na wazanzibari wenzangu na wananchi wote, kwamba huko mbele tusije tukalaumiana kwamba tumefanya marekebisho ya 10 kimakosa na tumejitangazia uhuru. Sasa hivi tuondoe fikra hizo lakini tunaweza kujieleza kwa hoja za msingi na mambo ya msingi katika hoja hii hapo ndipo tutakapojenga utawala bora ndani ya muungano," aliongeza Mwanasheria huyo.​
Akitoa ufafanuzi zaidi kwa wajumbe hao kuhusu muungano Othman alisema hata suala la uraia limepewa kipaumbele katika katiba ya Uswizi ambapo mtu anapozaliwa ndipo anapopewa uraia wake.​
"Pale unapozaliwa ndio panapokupa uraia, na kuna mengi ambayo nadhani tatizo liliopo kwa wenzetu ni kwamba hawajifunzi kwamba muungano ni kitu gani. Muungano ni suala ambalo nchi mbili mnapoungana, nchi zilizokuwa huru ni suala la makubaliano na mtakachokubaliana ndicho ambachi kitakuja katika katiba yenu," alisema Othman.​
Othman ambaye ni mwanasheria aliyewahi kuandika waraka (paper) aliyoipa jina ‘masuala ya yasiokuwa na majibu ndani ya muungano' aliwaambia wawakilishi hao kwamba maelezo ya Tundu Lisu yamejaa hadaa na yamejaa upotoshaji tena upotoshaji ambao umepindukia mipaka ya kweli.​
"Mimi nimepata kusoma na kuangalia hiyo hutuba ya Mhe Tundu Lisu… lakini pia nimeona majibu ambayo yalitolewa na mhehsimiwa Shamsi Vuai Nahodha aliyesema kuwa maeelzo ya Mbunge Lisu yamejaa hadaa na upotoshaji naungana naye," alisisitiza huku makofi ya wajumbe yakitawala ndani ya baraza hilo.​
Tokea kuanza kwa kikao cha baraza la wawakilishi kwa kiasi kikubwa mijadala wa bajeti umetawaliwa na suala la muungano ambapo wajumbe wengi wamekuwa wakiungana na wananchi kudai maslahi zaidi kwa zanzibar ikiwemo kurejesha kwa hadhi ya rais wa zanzibar na mamlaka kamili ndani na nje ya nchi.​
Imeandaliwa na Salma Said, Zanzibar​
 
Dah, hapo ushabiki upo wapi? tunasema mara kwa mara kuwa CHADEMA wana tabia ya kukurupuka. haya ndo madhara ya chama kuongozwa na vihiyo

CCM inawabunge wengi wenye fikra zilizotawaliwa na mambo ya kale akili mgando,na vijana waliomo ccm kubezwa na fikra mgando zisizopenda mabadiliko,wengi wametawaliwa na mawzo ya ndiyo ndiyo bila kufikiri ni kitu gani wanashabikia zaidi ya yote wanajifanya mawaziri hata kutojua wajibu wao ndani ya bunge,Ubabe wa kutumia polisi na vyombo vya usalama ndio ngao na staili ya kuendesha misimamo hata kwa jambo lisilofaa kwa wananchi.
 
Jaman hebu turuhusu akili zetu zifanye kazi. kwa maelezo ya Lukuvi tu inakujaje na hitimisho. Mie nsfikiri Lisu alipaswa kupewa nafasi ya kuthibitisha alichosema, km angeshindwa hapo ningekubaliana na hoja hii. Lakini hukumu yako imelalia zaidi kishabiki kuliko kimantiki.

Lukuvi alikuwa anarejea hotuba ya msemaji rasmi wa kambi ya upinzani masuala ya sheria na katiba Mh Tundu Lissu aliyoisoma jana Bungeni.
Kanuni za Bunge zinambana mtoa hoja kwa kusema uongo na kumkashifu rais kwa kujaribu kuwaaminisha wananchi kutokuwa na imani na rais wa nchi.
Alipaswa kupewa adhabu. Lakin kasamehewa.
 
lugha zingine amvua nguo sasa ndio nini? Yawezekana ulikuwa na nia nzuri.lakini lugha uliyo tumia haina maadili ya kitanzania.
 
Back
Top Bottom