William Lukuvi amvua nguo Tundu Lissu

William Lukuvi amvua nguo Tundu Lissu

Kamvua nguo ipi?? Hii habari imekaa KIKUDA sana, kichwa cha habari na habari yenyewe tofauti.

Kwanza kwa akili ya Haraka Lukuvi darasa la saba anawezaje kuwa na hoja kumzidi Tundu Lissu aliyebobea kwenye sheria na anatambulika dunia nzima kwa umahiri. Mambo ya akili ndogo kuongoza akili kubwa yako CCM tu...
Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Eti anatambulika dunia nzima??? Tembea uone, nadhani huna exposure wewe. Lissu ni mtaalamu aliyebobea kwenye sheria zipi duniani???? fafanua au muulize babu slaa akupe majibu then leta hapa jamvini.
 
Waziri wa nchi sera na uratibu wa Bunge, WILLIAM LUKUVI sasa hivi wakati bunge linaendelea ameweka wazi uongo wa TINDU LISSU, uongo uliofanya jana wabunge wa upinzani wasusie kujadili mswaada wa sheria ya marekebisho ya KATIBA.

Jana LISU alisema Rais KIKWETE hakuzingatia sheria katika kuteua wajumbe wa kamati ya kushughulikia mchakato wa Katiba mpya kwa madai kuwa aliacha kuwateua wajumbe waliowasilishwa kwa barua na makundi yao, jambo ambalo LUKUVI ameliweka wazi kwa kuwataja wajumbe hao kwa majina kutoka makundi yote walivyowalishwa kwa rais na Rais kufanya uteuzi kama ambavyo sheria iliktaka kufanya.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya mswada wa sheria ya Marekebisho ya Katiba, PINDI HAZARI CHANA naye akiweka bayana kuwa makundi yote yalihusika katika kutoa maoni yao juu ya katiba mpya tofauti na ambavyo LISSU alivyokuwa akidai kuwa wazanzibari hawakuhusishwa.

Kwa ushahidi huu wa LUKUVI NA PINDI CHANA ni wazi LISSU anaweza kukabiliana na adhabu kwa mujibu wa kanuni za bunge kutokana na kusema uongo na kuuaminisha umma wa watanzania kuwa alikuwa akisema ukweli

Ni kweli huyo LISSU amelidanganya Bunge na Taifa, sijui taarifa zake anapata wapi au anafanya makusudi tu. Rais aliteuwa wajumbe kutoka miongoni mwa majina alaiyopewa na makundi maalumu. HAKIKA ALIFANYA HIVYO. KWANINI WANAKUWA WAONGO HAO UPINZANI? WHY? SHAME! NA KATIBA MPYA ITAKUJA TU, HATA MKIWEKA ROAD BLOCKS NI KAZI BURE, FUTILE!
 
Nyie wote mmelewa madaraka! Ccm haitokua madarakani daima! Lukuvi na huyo mmama Pindi Chana Ndio waongo wakubwa!
 
Kwake yeye huko ndo kuvuliwa nguo.

Sasa siku mtu akivuliwa nguo kikwelikwli yeye atadai amechunwa ngozi au ameliwa ini, sijui!
 
Tangu lini mwenye shule ya kuunga unga akamvua nguo geneous au unaota mchana kweupe?
 
Kwani wajumbe wa bunge la katiba wapo tayari au mapendekezo yalowekwa kwenye mswada yanayompa madaraka makubwa rais kuteua hao wajumbe na mswada wenyewe kukosa kujadiliwa na wazibari ndo suala lenyewe.
Mwanasheria wa Zanzibar anasema ataupitia huo muswada ulopitishwa ili alinganishe na ule walopelekewa awali kisha atakuwa na la kusema. Kwa matinki hii; sijui ni upande upi usemao kweli. Ktk hili lazima kuna mmoja anadanganya; wakati utamdhuhirisha
 
Back
Top Bottom