William Lukuvi amvua nguo Tundu Lissu

William Lukuvi amvua nguo Tundu Lissu

Nilishasema humu bungeni kuwa TINDU LISSU hana uelewa wowote wa sheria zaidi anachokifanya ni kucheza na akili za wabunge wenzakekutokana na uelewa mdogo wa vifungu vya sheria ambavyo anaamini wenzake ambao hawana taaluma hiyo hawatamshtukia na hivyo huamua kukomalia huko.
Hata mimi natazama bunge sasa hivi , kwa kile walichokisema LUKUVI, PINDI HAZARI CHANA na sasa ufafanuzi anaoutoa mwanasheria mkuu wa serikali , FREDRICK WEREMA, ni dhahiri LISSU ameumbuka.

Hacha umbumbumbu wa CCM leta hoja hapa. Kamati ya Bunge ilioji Taasisi zipi za Zanzibar zilizokuwa kwenye ratiba ya Kamati? Nitajie Taasisi moja iliyotoa maoni miongoni mwa zilizo kwenye List ya Kamati ya Sheria na Katiba ya Bunge Full Stop . Sio mnaleta hapa maneno ya Khanga na hoja za kuokoteza barabarani.
 
VIijana wa Lumumba mmetisha kwa kuchangia kwenye hili bandiko, mtakuwa mmeongezwa mshiko si bure
 
nilishasema humu bungeni kuwa tindu lissu hana uelewa wowote wa sheria zaidi anachokifanya ni kucheza na akili za wabunge wenzakekutokana na uelewa mdogo wa vifungu vya sheria ambavyo anaamini wenzake ambao hawana taaluma hiyo hawatamshtukia na hivyo huamua kukomalia huko.
Hata mimi natazama bunge sasa hivi , kwa kile walichokisema lukuvi, pindi hazari chana na sasa ufafanuzi anaoutoa mwanasheria mkuu wa serikali , fredrick werema, ni dhahiri lissu ameumbuka.

we mjinga kweli, ila utaelewa tu muda ukifika.
 
MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR AJIBU MAPIGO YA TUNDU LISU, NI KUHUSU MABADILIKO KATIBA YA ZANZIBAR.





Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman (Pichani) ameshangazwa na mwanasheria mwenzake Tundu Lisu kwa kutofahamu madhumuni na malengo ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yaliozaa serikali ya umoja wa kitaifa. Kauli ya Mwanasheria huyo aliitoa katika baraza la wawakilishi wakati akifafanua baadhi ya mambo ya kisheria baada ya wajumbe wa baraza hilo kumtaka afanye hivyo kufuatia kauli ya ya Tundu Lisu aliyoitoa bungeni wiki hii.​
“Sasa kuja kwa haya yametuonesha kwamba kuna wenzetu kumbe wana fikra kwamba Zanzibar iliwahi kutawaliwa. Maana mtu anaposema marekebisho ya 10 ya Zanzibar yamjitangazia uhuru maana yake ana fikra na huyu ni mwanasheria mtu kafika mpaka kuwa mbunge anayeaminika na chama chake lakini anasema kwa kufanya hivyo Zanzibar imejitangazia kuwa huru kwani tuliwahi kutawaliwa?,” alihoji Othman.​
Akijadili bajeti ya wizara ya makamu wa rais wa jamhuri ya muungano, huko Dodoma Mbunge wa Singida Mashariki wa Chama Cha (CHADEMA) Tundu Lisu alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa Zanzibar imefanya katiba kwa kujitangazia kuwa ni nchi.​
Othman alisema marekebisho ya katika ya Zanzibar yalikuja baada ya hoja nyingi ambazo hazikuwa na majibu katika muungano ambayo ilikuwa ikisema ni Zanzibar ni sehemu ya muungano, lakini kama nini mkoa? Shehia? Kata? au kijiji?, haya hayakuwa na jibu katika katiba ya muungano.​
Kufuatia maridhiano Zanzibar ndipo wazanzibari wakamaua kufanya kukufikia marekebisho ya 10 ya katiba yao ambayo ilifafanua kuwa zanzibar ni nchi na ndivyo ilivyo kwa sababu haikuwahi kutawaliwa kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wanavyofikiria.​
“Marekebisho ya 10 ilichofanya ni kusema kwamba ikiwa mtu hatambui, maana ilikuwa imeshaonesha dalili kwamba kuna wengine hawatambui hilo tena wakubwa. Sasa marekebisho ya 10 yalipokuja ni kufafanua tu, kama kuna mtu hatambui sisi wenyewe tunajitambua” alisema mwanasheria huyo huku akiungwa mkono na wajumbe kwa kupigiwa makofi.​
Huku akishangiriwa na wajumbe wa baraza hilo mwanasheria mkuu alisema hakuna mtu ambaye atawazuwia kusema “Aaah katiba yenu isiwe namna gani au isiwe hivi na ndio maana unakuta katiba za muungano zipo nyingi lakini kila mmoja ina muundo wake kwa mujibu mlivyokubaliana nyinyi wenyewe.”​
Mwanasheria mkuu alisifu muungano wa miaka mingi wa Uswizi ambao unatambulika na kuigwa duniani kutokana na kufuata misingi imara iliyowekwa na wananchi wenyewe.​
Alisema muungano ambao umedumu na unasifiwa ni Swiss Federation kwa sababu umeanza tokea mwaka 1292 na umekwenda kwa mafahamiano hadi mwaka 1874 wakatunga katiba ambayo wameifanyia mapitio upya mwaka 1999 na nchi hiyo ina serikali 26, lugha nne rasmi na ndio muungano amabo umedumu na nchi ambayo ni imetulia duniani.​
Mwanasheria huyo alisema mashirika yoye ya kimataifa yapo Uswizi kwa sababu ya muungano huo uliotumilia na kwa sababu umekuwa na misingi imara ya kuhakikisha muungano ule unaweza kuhimili mabadiliko yoyote yatakayokuja ya kisiasa.​
“Mheshimiwa Naibu Spika nitumie fursa hii hapa hapa niseme wakati tupo katika mchakato wa maoni ya katiba nadhani ni wakati mzuri kuiweka sawa ile misingi ya muugano kama Uswizi,”na kuongeza: “Wakati mwengine napata wasiwasi nasema hii khofu yangu niiseme hapa kwamba tunaanza kubishana kuhusiana na watunza nyumba wawe wangapi, waendeshaji nyumba wawe wangapi, wawili, watatu, wanane au watano? Lakini tatizo letu la msingi mimi nadhani ni nyumba yenyewe iweje. Kama tunaamua kuishi, maana mfumo wa sasa hivi mmoja anaishi nyumba kubwa na mwengine mabandani huko uwani huo sio utaratibu tunao.”​
Aidha aliwaambia wajumbe hao kwamba wanzanzibari wana mambo ya msingi ya kujadili kuliko kuzungumzia idadi ya watunza nyumba akimaanisha kero za muungano zilizopo na kushindwa kuafikiwa.​
“Kwa hivyo mimi niwaombe sana waheshimiwa wajumbe, niwaombe na wazanzibari wenzangu na wananchi wote, kwamba huko mbele tusije tukalaumiana kwamba tumefanya marekebisho ya 10 kimakosa na tumejitangazia uhuru. Sasa hivi tuondoe fikra hizo lakini tunaweza kujieleza kwa hoja za msingi na mambo ya msingi katika hoja hii hapo ndipo tutakapojenga utawala bora ndani ya muungano,” aliongeza Mwanasheria huyo.​
Akitoa ufafanuzi zaidi kwa wajumbe hao kuhusu muungano Othman alisema hata suala la uraia limepewa kipaumbele katika katiba ya Uswizi ambapo mtu anapozaliwa ndipo anapopewa uraia wake.​
“Pale unapozaliwa ndio panapokupa uraia, na kuna mengi ambayo nadhani tatizo liliopo kwa wenzetu ni kwamba hawajifunzi kwamba muungano ni kitu gani. Muungano ni suala ambalo nchi mbili mnapoungana, nchi zilizokuwa huru ni suala la makubaliano na mtakachokubaliana ndicho ambachi kitakuja katika katiba yenu,” alisema Othman.​
Othman ambaye ni mwanasheria aliyewahi kuandika waraka (paper) aliyoipa jina ‘masuala ya yasiokuwa na majibu ndani ya muungano’ aliwaambia wawakilishi hao kwamba maelezo ya Tundu Lisu yamejaa hadaa na yamejaa upotoshaji tena upotoshaji ambao umepindukia mipaka ya kweli.​
“Mimi nimepata kusoma na kuangalia hiyo hutuba ya Mhe Tundu Lisu… lakini pia nimeona majibu ambayo yalitolewa na mhehsimiwa Shamsi Vuai Nahodha aliyesema kuwa maeelzo ya Mbunge Lisu yamejaa hadaa na upotoshaji naungana naye,” alisisitiza huku makofi ya wajumbe yakitawala ndani ya baraza hilo.​
Tokea kuanza kwa kikao cha baraza la wawakilishi kwa kiasi kikubwa mijadala wa bajeti umetawaliwa na suala la muungano ambapo wajumbe wengi wamekuwa wakiungana na wananchi kudai maslahi zaidi kwa zanzibar ikiwemo kurejesha kwa hadhi ya rais wa zanzibar na mamlaka kamili ndani na nje ya nchi.​
Imeandaliwa na Salma Said, Zanzibar​

huyu mzenji ndio mpuuzi...hajui ktk mkataba uhuru unakuwa ktk mipaka ya mkataba.Zenj walipoanza fanya mambo ya nje ya mkataba ni wazi kuwa wameshakuwa huru kutumia sheria nyingine.
 
CCM inawabunge wengi wenye fikra zilizotawaliwa na mambo ya kale akili mgando,na vijana waliomo ccm kubezwa na fikra mgando zisizopenda mabadiliko,wengi wametawaliwa na mawzo ya ndiyo ndiyo bila kufikiri ni kitu gani wanashabikia zaidi ya yote wanajifanya mawaziri hata kutojua wajibu wao ndani ya bunge,Ubabe wa kutumia polisi na vyombo vya usalama ndio ngao na staili ya kuendesha misimamo hata kwa jambo lisilofaa kwa wananchi.
mnajishushia hadhi kujadiliana naye.hebu itunzeni heshima yenu wakuu.
 
Kamvuaje nguo? Nilidhani kampa matusi ya nguoni. Badili hiyo heading yako imekaa kishari sana.
 
Nilishasema humu bungeni kuwa TINDU LISSU hana uelewa wowote

Wabunge mbumbumbu kama wewe ndio mnaosababisha bunge letu kuwa la kipuuzi kwa sababu ya kutojitambua na kutotambua majukumu yenu sasa mmegeuka kuwa mapoyoyo.
Tundu Lissu anaijua sheria kuliko wabunge (mapoyoyo) wote wa ccm hata ukichanganya akili zao kwa pamoja. Tundu Lissu akishaongea bungeni mapoyoyo yote ya ccm mnasahau hoja iliyopo mezani na kujielekeza kujibu hoja zake mwisho wa siku mnajikuta mmepitisha sheria za kijinga zisizozingatia mahitaji ya wananchi.
 
huyu mzenji ndio mpuuzi...hajui ktk mkataba uhuru unakuwa ktk mipaka ya mkataba.Zenj walipoanza fanya mambo ya nje ya mkataba ni wazi kuwa wameshakuwa huru kutumia sheria nyingine.
Wewe ndiyo unaonekana mpuuzi zaidi kuliko huyo unayemuona mpuuzi na hoja yako isiyokuwa na kichwa wala mkia. Hujui kuwa Zanzibar wana sharia zao?
 
Lukuvi hana lolote mkuu.pole sana.yuko kwa maslahi yake na siyo ya taifa........tafakari.kwa kina....

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
mbona hujataja maelezo ya LISSU kuhusu kutowakilishwa kwa baadhi ya makundi,katiba ni kwa ajili ya watz wote si ya chama
 
Wakati akichangia mswada wa sheria ya marekebisho ya Katiba, Mbunge wa Zanzibar amesema TINDU LISSU hajawahi kuwapenda wazanzibari na wala hapendi kuona Muungano ukidumu.

Mbunge huyo amewataka Wazanzibari kujua kuwa TINDU LISSU ni yule yule ambaye anajifanya kuwatetea wakati ni muongo mkubwa na kuwataka washikamane katika kuitengeneza katiba mpya, kuitetea Zanzibar na kumpuuza TINDU LISSU.

Mbunge huyo alienda mbali na kusema Wabunge wa CUF watakuwa wamepitiwa tu na upepo wa janja ya jana ya TINDU LISSU ya kujifanya kuwatetea na kujikuta wakiungana nao leo lakini kiuhalisia ni uongo mtupu.

Ninyi mnaoipenda Zanzibar mbona hamkuwapa fursa ya kutoa maoni ya muswada huu? Acheni Propoganda zisizo na mashiko?
 
Wewe ndiyo unaonekana mpuuzi zaidi kuliko huyo unayemuona mpuuzi na hoja yako isiyokuwa na kichwa wala mkia. Hujui kuwa Zanzibar wana sharia zao?

mojawapo ya raha za JF ni kuwa kuwa na bogus km wewe wengi wenye confidence kuwa ni wajuaji............Zenji wana sheria sijui sharia zao....so what?km zinakinzana na za jamhuri ni kuvunja muungano.
 
Wabunge mbumbumbu kama wewe ndio mnaosababisha bunge letu kuwa la kipuuzi kwa sababu ya kutojitambua na kutotambua majukumu yenu sasa mmegeuka kuwa mapoyoyo.
Tundu Lissu anaijua sheria kuliko wabunge (mapoyoyo) wote wa ccm hata ukichanganya akili zao kwa pamoja. Tundu Lissu akishaongea bungeni mapoyoyo yote ya ccm mnasahau hoja iliyopo mezani na kujielekeza kujibu hoja zake mwisho wa siku mnajikuta mmepitisha sheria za kijinga zisizozingatia mahitaji ya wananchi.

hah..ndio maana Gayo matanzania maarufu kule kenya ktk kuchora vikatuni vya kisiasa..alichora bunge kama club ya taputapu na akina ndugai wakiwa full ktk ze ochumale, viroba ,..etc.
 
wazenj km chambo ya samaki...CCM wanawatumia km watakavyo....CUF wapo busy ktk uliberali wao..hawajui hata jana walikuwa wapi,leo na kesho watakuwa wapi.

Maliberali bwana....hawachelewei kusema fulani ni handsome, fulani nimeipenda sauti yake, fulani nimependa body lake..and the sort.CUF waondoe kansa ya kutojitambua CCM iondoshwe bara na visiwani.
 
Waziri wa nchi sera na uratibu wa Bunge, WILLIAM LUKUVI sasa hivi wakati bunge linaendelea ameweka wazi uongo wa TINDU LISSU, uongo uliofanya jana wabunge wa upinzani wasusie kujadili mswaada wa sheria ya marekebisho ya KATIBA.

Jana LISU alisema Rais KIKWETE hakuzingatia sheria katika kuteua wajumbe wa kamati ya kushughulikia mchakato wa Katiba mpya kwa madai kuwa aliacha kuwateua wajumbe waliowasilishwa kwa barua na makundi yao, jambo ambalo LUKUVI ameliweka wazi kwa kuwataja wajumbe hao kwa majina kutoka makundi yote walivyowalishwa kwa rais na Rais kufanya uteuzi kama ambavyo sheria iliktaka kufanya.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya mswada wa sheria ya Marekebisho ya Katiba, PINDI HAZARI CHANA naye akiweka bayana kuwa makundi yote yalihusika katika kutoa maoni yao juu ya katiba mpya tofauti na ambavyo LISSU alivyokuwa akidai kuwa wazanzibari hawakuhusishwa.

Kwa ushahidi huu wa LUKUVI NA PINDI CHANA ni wazi LISSU anaweza kukabiliana na adhabu kwa mujibu wa kanuni za bunge kutokana na kusema uongo na kuuaminisha umma wa watanzania kuwa alikuwa akisema ukweli

Hizo ni data za kupika. Jana huyo Lukuvi na Chana walikuwa wapi? Wana majungu wa CCM kama kawaida.
 
Nadhani wewe hukumelewa Lissu, ALICHOKISEMA ni juu ya mamlaka ya Rais ya kuteua wajumbe, Jk ni mwenyekiti wa ccm, ccm ina maslahi katika katiba mpya, hivyo ni dhahiri hata hao watakaoteuliwa na raisi toka makundi yoyote yale, watakuwa wanawakilisha mawazo ya ccm! bali kinachotakiwa kufanywa ni kila kundi kutumia utaratibu wao kumpta mtu wao, bila viongozi wa kisiasa kuingilia ili kuepuka mawazo ya chama kimoja, pia watu kuwa huru kuchangia yale waliyotumwa na sio kumtumikia CCM, kwa kulipa fadhila!
 
Back
Top Bottom