William Lukuvi amvua nguo Tundu Lissu

William Lukuvi amvua nguo Tundu Lissu

Umeandika kishabiki sana, kumbe kajibu hoja lakini wewe unapamba, wangapi wamedanganya na hawajafanywa kitu, nawe hapa JF lazima uchukuliwe hatua kali za kiuandishi.
Ukiua kwa upanga......
 
Tundu Lissu, jana kawaingiza choo cha kike wabunge wenzake.
 
Tangu lini TEC inawakilishwa na mwanamke ha ha ha hakuna askofu mwanamke.
 
Sasa mbona Lissu hajapewa nafasi baada ya mwanasheria mkuu kuongea pumba leo mpaka tumejua dini yake,kabila lake,aliposoma seminary ilibaki kidogo angetaja mpaka jina lq mkewe chezea Lissu wewe.
 
Unajua hata sisi tunaangalia usitudanganye na ushabiki wako. Tunajua kinachoendelea. Hata kama mkijifagilia ukweli unaonekana dhahiri.

Khaa, Mlimumu...
Manye wadodo wanyaLumumba wasina mahala, nhondo yose wakusolele ng'an mchanya.
Munu mono yena mahala, siyosuma kikala yamuhulichize Lukuvi hamba Welema, wose msina chinji..!!
 
Mleta uzi mwenyewe ni thatha.unategemea nini!uhar.,..
 
Na ikidhihirika huyo LUKUVI wako na PINDI CHANA wamesema uwongo, watapewa adhabu gani? Kichwa cha habari hakiendani na yaliyoandikwa. Yale yale ya Watanzania wengi kupenda porojo. Hapo kinachoonekana ni Lukuvi na Chana kujitetea, wanaosikiliza wataangalia uthibitisho wa shutuma na utetezi wa Lukuvi, ndiyo itajulikana nani ni mwongo.

Chana nadhani ni mwongo wa kwanza. Anasema walishirikishwa Wazanzibari, si ataje walioshiriki? Wazanzibari wenyewe wanasema hawakushirikishwa. Wabunge wa CUF wa Zanzibar na hata wa CCM (japo hawakutoka) wanasema Wazanzibari hawakushirikishwa, huyo Chana Wazanzibari aliowashirikisha wanaishi nyumbani kwake hata Wazanzibari wengine wasijue kuwa kuna miongoni mwao waliowawakilisha? CCM ni chama cha waongo, na sifa moja kubwa waliyo nayo ni kusema uwongo, hata siku moja huwa hawakubali hata pale ukweli ulipo dhIhiri. Walikataa kuhusu EPA, walikataa kuhusu polisi kumwua Mwangosi,.......; hawa hawaaminiki mpaka tunapopata uthibitisho KUTOKA kwa mtu mwingine mwenye credibility, siyo LUKUVI.

Waziri wa nchi sera na uratibu wa Bunge, WILLIAM LUKUVI sasa hivi wakati bunge linaendelea ameweka wazi uongo wa TINDU LISSU, uongo uliofanya jana wabunge wa upinzani wasusie kujadili mswaada wa sheria ya marekebisho ya KATIBA. Jana LISU alisema Rais KIKWETE hakuzingatia sheria katika kuteua wajumbe wa kamati ya kushughulikia mchakato wa Katiba mpya kwa madai kuwa aliacha kuwateua wajumbe waliowasilishwa kwa barua na makundi yao, jambo ambalo LUKUVI ameliweka wazi kwa kuwataja wajumbe hao kwa majina kutoka makundi yote walivyowalishwa kwa rais na Rais kufanya uteuzi kama ambavyo sheria iliktaka kufanya. Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya mswada wa sheria ya Marekebisho ya Katiba, PINDI HAZARI CHANA naye akiweka bayana kuwa makundi yote yalihusika katika kutoa maoni yao juu ya katiba mpya tofauti na ambavyo LISSU alivyokuwa akidai kuwa wazanzibari hawakuhusishwa.

Kwa ushahidi huu wa LUKUVI NA PINDI CHANA ni wazi LISSU anaweza kukabiliana na adhabu kwa mujibu wa kanuni za bunge kutokana na kusema uongo na kuuaminisha umma wa watanzania kuwa alikuwa akisema ukweli
 
Kamvua nguo ipi?? Hii habari imekaa KIKUDA sana, kichwa cha habari na habari yenyewe tofauti.

Kwanza kwa akili ya Haraka Lukuvi darasa la saba anawezaje kuwa na hoja kumzidi Tundu Lissu aliyebobea kwenye sheria na anatambulika dunia nzima kwa umahiri. Mambo ya akili ndogo kuongoza akili kubwa yako CCM tu...

''Mambo ya akili ndogo kuongoza akili kubwa yako CCM tu''
nimeipenda hii
 
Mnamwonea Lukuvi, namfahamu sana ni mtu wa kwetu. Siyo darasa la saba, alifika form 4 ila hakufanya vizuri mtihani wa Form 4. Baada ya kuona hana kingine cha kufanya na Form 4 isiyo na credit aliamua kutumia muda wake wote kwenye TANU Youth League na baadaye UVT (siku hizi UVCCM), na imemsaidia kwa kiasi kikubwa maana amefika hapo alipofika japo uwezo wake wa kuchungua mambo ni mdogo sana, nadhani amefit vizuri tu kwenye uongozi wa safari hii maana karibu wote, waliosoma na wasiosoma, wapo hivyo hivyo.

Darasa la saba ulimsomesha wewe? acha unafiki
 
hahahahahahahahhahaha,watoto wa LUMUMBA WANAKUWA MAZEZETA WEWE KWA AKILI YAKO LUKUVI ANAMMUDU TUNDU LISSU??HIYO NI SAWASAWA KULINGANISHA GOBOLE NA AK-47,MH.TUNDU LISSU NI HABARI NYINGINE LUKUVI HANA JEURI YA KUJIBU HOJA ZA TUNDU LISU AU MH.LEMA HATA MOJA.
 
mtoa mada bila shaka una mtoto tumboni, bado miezi mitatu itimie tisa utapata auheni!
 
Baada ya Zitto kabwe mwanachama mwengine mwenye nafuu ndani ya chadema ni Tundu Lissu ila sikuhizi kageuka muimba kwaya bungeni,hana hoja kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Bila shaka wewe utakuwa ccm ambaye mnadhani watu ni wajinga.
 
Dah, hapo ushabiki upo wapi? tunasema mara kwa mara kuwa CHADEMA wana tabia ya kukurupuka. haya ndo madhara ya chama kuongozwa na vihiyo

Kichaa umefika na huku pia!
 
Lissu alisema Kikwete hakuteua Mjumbe kutoka TEC yaani mjumbe kutoka Kanisa Katoliki kuwa mjumbe wa Tume ya Katiba,ukweli ni kwamba mmoja wapo wa wajumbe hao anatoka TEC yupo kwenye tume na nimiongoni mwa majina matatu yaliyo pendekezwa na TEC kwenda kwa Rais,pia alisema CSO na Bakwata haina wajumbe ukweli ni kwamba CSO na Bakwata zina wajumbe ndani ya Tume ya Katiba! Ni upotosha alio ufanya Tundu Lissu akijua watanzania sio wadadisi wa mambo!
 
hatuwezi kutengenezewa katiba na maccm,labda wakatengeneze yao pale lumumba,serikali dhaifu na wabunge dhaifu wa magamba hawawezi kututengenezea katiba ya kiccm ccm.CDM HAKIKISHENI WATANZANIA WANAPATA KATIBA WAITAKAYO,NA UMMA WA WATANZANIA UMEWAAMINI NA UPO NYUMA YENU
 
Back
Top Bottom