Hizi habari ningefurahi sana kama zingeandikwa na kutangazwa na vyombo vyetu vya habari,ili watanzania wengi zaidi wayafahamu haya....lakini mmh!
Natabiri yatakayojiri wiki ijayo kuanzia kesho!!!!!!!!!
1. Magazeti ya bongo kuna baadhi yataitoa habari hii, maana is just quoting wikileaks.
2. Magazeti kama habari leo, uhuru nao wanaweza kuja nayo kinamna nyingine ya kuipotosha.
3. Mwanahalisi au raia mwema kama kawaida wataingia deep juu ya habari hii.
4. Habari ikipamba moto kama kawaida wale jamaa wa kurugenzi ya habari ya ikulu watatoa press release kukanusha.
5. Kwa mara ya kwanza watanzania walio wengi watamuona mmiliki wa Kempiski luningani na kwenye magazeti naye akikanusha.
6. Dili ya kuibomoa forodhani hotel (mahakama ya rufaa) kupisha upanuzi wa Kempiski itatangazwa na waziri aidha wa sheria au kigogo mwingine kwamba haipo/ imesitishwa ili kupoteza the suspected link na hii scandal.
7. Huyo the so called Pile kama yupo bongo ndiyo kwa heri hiyo
8. Litaibuka liwaziri au jimwanasheria mkuu kutoa mwongozo kwamba habari kutoka wiki leaks zisichapishwe magazetini maana nyingi zinahusu usalama wa taifa mfano hii ya suti za JK
ficha upumbavu wako kutetea maovu. Sheria yetu ya rushwa inasema wazi kuhusu zawadi ambazo unaweza kuzipokea na zikizidi kiasi fulani lazima utolee taarifa kwa mwajiri.Kumbe kununuliwa nguo nayo ni rushwa? Angalia mazingira ya kununuliwa hizo nguo..hata wewe mwenyewe ukikutana na waziri akiwa shopping unaweza ukampa offer.
Vitu vingine ni immaterial jamani!
Na habari za wikileaks siyo zote ni za kuaminika!
Do we know anything of them?Kila tunapodhani tumesimama tuangalie tusije anguka. These guys know us more than we thought
Ha ha ha Hiyo EVENT Kempinski nafikiri hata mama Salma alihudhuriaYaani we acha tu, mama Salma asisikie habari hii!
Ni dhahiri kwamba hujaelewa hiyo cable inachozungumzia. Kwanza hakuna suala lolote linalohusiana na mambo ya kampeni za uchaguzi hapo. Pili, umewahi kusikia mtu au kampuni kubwa kama Kempinski Hotels inampa favours mwanasiasa ambaye aidha hana wadhifa mkubwa au hatarajiwi kuja kuwa na wadhifa mkubwa?Lazima tuwe wakweli kwa nafsi zetu at some point. Hivi mtu anayefanya kampeni za urais au hata ubunge akipata hotel fulani ikajitolea kumfanyia ukarimu wa kuhost mikutano yake for free atakataa. je, sheria ya nchi inakataza hilo? Tatizo letu tunatumia sheria za nchi nyingine kujadili masuala ya Tanzania.
Hivi mnafikiri hayo mahelkopta mnayosikia yanaruka angani wakati wa kampeni yanalipiwa na pesa za ruzuku? Au tunangoja mpaka wikileaks waje kutuambia kuwa yalilipiwa na mfanyabiashhara fulani ndio tuanze kushangaa? kwa kifupi, kampeni ni gharama na kama sheria ya nchi haikatazi kupokei mchango sio dhambi.
Itamake sense kujadili rushwa hapa iwapo tutakuwa na kidhibiti cha favor ambayo rais amewafanyia hao kempinski kutokana na fadhili waliyompa.
Hillary Clinton alipokuwa senator on New York alikuwa anapokea USD 150,000 kila mwaka toka kwa "special interests" na kampeni zake zilikuwa sponsored na special interests pia. Cha msingi ni kutokutoka nje ya mipaka ya sheria ya nchi tu.
Kila kitu hapo kimejieleza..sioni element yoyote ya rushwa hapo!
" I suspect giving free clothes and the campaign donation is just the way these people do business".
Hiyo sentence hapo imesummarize kila kitu
Hatujijui....ila tunajua ku rap kushinda wao kama jamaa mmoja alivyosemaDo we know anything of them?