Wikileaks' release on Tanzania Tanzania; August 2011

Wikileaks' release on Tanzania Tanzania; August 2011

Status
Not open for further replies.
Hizi habari ningefurahi sana kama zingeandikwa na kutangazwa na vyombo vyetu vya habari,ili watanzania wengi zaidi wayafahamu haya....lakini mmh!

Natabiri yatakayojiri wiki ijayo kuanzia kesho!!!!!!!!!

1. Magazeti ya bongo kuna baadhi yataitoa habari hii, maana is just quoting wikileaks.

2. Magazeti kama habari leo, uhuru nao wanaweza kuja nayo kinamna nyingine ya kuipotosha.

3. Mwanahalisi au raia mwema kama kawaida wataingia deep juu ya habari hii.

4. Habari ikipamba moto kama kawaida wale jamaa wa kurugenzi ya habari ya ikulu watatoa press release kukanusha.

5. Kwa mara ya kwanza watanzania walio wengi watamuona mmiliki wa Kempiski luningani na kwenye magazeti naye akikanusha.

6. Dili ya kuibomoa forodhani hotel (mahakama ya rufaa) kupisha upanuzi wa Kempiski itatangazwa na waziri aidha wa sheria au kigogo mwingine kwamba haipo/ imesitishwa ili kupoteza the suspected link na hii scandal.

7. Huyo the so called Pile kama yupo bongo ndiyo kwa heri hiyo

8. Litaibuka liwaziri au jimwanasheria mkuu kutoa mwongozo kwamba habari kutoka wiki leaks zisichapishwe magazetini maana nyingi zinahusu usalama wa taifa mfano hii ya suti za JK
 
Mi nadhani taarifa yao hiyo iko sahihi, kwa ukerewe huo ndo ukweli wenyewe. Mbunge wao yule wa muda mrefu nadhan alichangia kudumaa kwa maendeleo! Alikuwa busy sana na mambo ya kimataifa akasahau jimbo lake.
 
Wakuu, naomba mwenye taarifa za ziada ili nijiridhishe kabla sijahitimisha katika kichwa changu.
Je, yalikuwepo makampuni/watu wengine waliokuwa washindani katika kuimiliki Hotel hiyo kabla ya kukabidhiwa mmiliki wa sasa? Ni akina nani,na wana asili za nchi gani?
Chemsha bongo kabla hujapagawa
!
Msulujenda natoka kwa muda,kama kawaida yangu!
 
During colonial times, we were told, some of the kings sold their land with piece of clothes! More than a century later, we want to use the same style to sell our country! Eehhh! Makubwa haya
 
Sina shaka tena kwamba wewe ni Great Thinker. Lakini nakulaumu sana kwa kutosema lolote juu ya;

1. Fisadi Jairo atakavyokua kutokana na kutajwa tena humu,

2. Wala husemi kitu kwamba Mzee Mukama wa CCM atakunja uso au atacheka kitendo cha CCM kuonekana kuuza nchi kwa mwarabu kupitia vijizawadi na bahasha ya khaki;

3. Sijaelewa kwa nini umesita kusema MACHALII WOTE waliojazana vijiweni bila ajira na WALAZWAHOI wote kwa ujumla wetu jinsi itakavyokua hata kule kwenye machimbo Mara au mbugani Serengeti baada ya KUBAINISHIWA wazi kiasi hiki CHANZO CHOTE NA TABIA ZA VIONGOZI WETU na jinsi zinavyotusababisia ugumu wa maisha.

4. Wala sijaelewa ni kwa nini hujasema lolote juu ya Mhe Lema kule A-Town na uongozi wa CHADEMA kwa ujumla watakachomwambia Mhe Tendwa na vyombo vyetu vyote vya ulinzi juu ya mikono ya Waarabu kujipenyeza kufadhilifadhili na hat kutafuta kutia ushawishi juu ya siasa zanchi yetu na mwenendo wake wote, kutuvuruga KUTAKA KUJENGA hoteli na barabara kule kusiko ...

banae, hebu rudi tena jikoni ili ukarefushe kidogo orodha yako na kutueleza pia kwamba ni kwa nini kazi zimekua hazienda hasa kwa Mhe Hosea na Taasisi yake kuendelea kulilia kufungwa mikono kiutendaji ...

Natabiri yatakayojiri wiki ijayo kuanzia kesho!!!!!!!!!

1. Magazeti ya bongo kuna baadhi yataitoa habari hii, maana is just quoting wikileaks.

2. Magazeti kama habari leo, uhuru nao wanaweza kuja nayo kinamna nyingine ya kuipotosha.

3. Mwanahalisi au raia mwema kama kawaida wataingia deep juu ya habari hii.

4. Habari ikipamba moto kama kawaida wale jamaa wa kurugenzi ya habari ya ikulu watatoa press release kukanusha.

5. Kwa mara ya kwanza watanzania walio wengi watamuona mmiliki wa Kempiski luningani na kwenye magazeti naye akikanusha.

6. Dili ya kuibomoa forodhani hotel (mahakama ya rufaa) kupisha upanuzi wa Kempiski itatangazwa na waziri aidha wa sheria au kigogo mwingine kwamba haipo/ imesitishwa ili kupoteza the suspected link na hii scandal.

7. Huyo the so called Pile kama yupo bongo ndiyo kwa heri hiyo

8. Litaibuka liwaziri au jimwanasheria mkuu kutoa mwongozo kwamba habari kutoka wiki leaks zisichapishwe magazetini maana nyingi zinahusu usalama wa taifa mfano hii ya suti za JK
 
Kumbe kununuliwa nguo nayo ni rushwa? Angalia mazingira ya kununuliwa hizo nguo..hata wewe mwenyewe ukikutana na waziri akiwa shopping unaweza ukampa offer.

Vitu vingine ni immaterial jamani!
Na habari za wikileaks siyo zote ni za kuaminika!
ficha upumbavu wako kutetea maovu. Sheria yetu ya rushwa inasema wazi kuhusu zawadi ambazo unaweza kuzipokea na zikizidi kiasi fulani lazima utolee taarifa kwa mwajiri.

Kama kikwete ndiye mwajiri mkuu na anavunja miiko ya utumishi je wakina Jairo watafanya nini? Raisi wa nchi anayepokea zawadi ya Tsh millioni moja hawezi kukataa zawadi ya dollar millioni moja, hawezi kushindwa kuuza nchi. Hili ni janga la kitaifa tunaweza kuanzia hapa kuulizana na kitu kikasanuka. Tuwaulize PCCb kama wanakubali, tuwaulize usalama wa Taifa hiki ndicho wanastahili kulinda.

Tunampenda Raisi wetu lakini lazima arudishe upendo wetu kwa kulijengea taifa heshima na kudumisha utukufu wa mamlaka yake. Wageni na wawekezaji wameifanya serikali yetu ni kitu rahisi rahisi tu. Huu mzaa ndio unaweza kufanya mfungwa kudiriki kuipigia simu "serikali" hii ni kazi kwelikweli
 
Jamani hii kwenye nchi za wenzetu ni big news lakini sijaiona kwenye vijarida vyetu (they are not broadsheet newspapers rather tabloids), hata gazeti la Uhuru(the leading tabloid newspaper) halijaandika habari kubwa kama hii, uhuru wa habari wanautaka wa nini sasa.
 
hapa bongo kichefuchefu tu mtu anapewa uongozi anaanza kujiendeleza kwanza yeye halafu ndio tunafuatia tuliompa kura ni wachache sana ambao wanatoa ipaumbele kwa wananchi wao.

kwa mfano magufuli na mnyika ndio naona wako pamoja na zile ahadi zao mpaka sasa..
 
Lazima tuwe wakweli kwa nafsi zetu at some point. Hivi mtu anayefanya kampeni za urais au hata ubunge akipata hotel fulani ikajitolea kumfanyia ukarimu wa kuhost mikutano yake for free atakataa. je, sheria ya nchi inakataza hilo? Tatizo letu tunatumia sheria za nchi nyingine kujadili masuala ya Tanzania.

Hivi mnafikiri hayo mahelkopta mnayosikia yanaruka angani wakati wa kampeni yanalipiwa na pesa za ruzuku? Au tunangoja mpaka wikileaks waje kutuambia kuwa yalilipiwa na mfanyabiashhara fulani ndio tuanze kushangaa? kwa kifupi, kampeni ni gharama na kama sheria ya nchi haikatazi kupokei mchango sio dhambi.

Itamake sense kujadili rushwa hapa iwapo tutakuwa na kidhibiti cha favor ambayo rais amewafanyia hao kempinski kutokana na fadhili waliyompa.

Hillary Clinton alipokuwa senator on New York alikuwa anapokea USD 150,000 kila mwaka toka kwa "special interests" na kampeni zake zilikuwa sponsored na special interests pia. Cha msingi ni kutokutoka nje ya mipaka ya sheria ya nchi tu.
Ni dhahiri kwamba hujaelewa hiyo cable inachozungumzia. Kwanza hakuna suala lolote linalohusiana na mambo ya kampeni za uchaguzi hapo. Pili, umewahi kusikia mtu au kampuni kubwa kama Kempinski Hotels inampa favours mwanasiasa ambaye aidha hana wadhifa mkubwa au hatarajiwi kuja kuwa na wadhifa mkubwa?

Ni wazi kabisa huyo mwarabu alikuwa ananunua favors, zingatia maelezo ya Ms. Pile kuhusu Bunge kupitisha sheria kuruhusu ujenzi wa hoteli mbugani.

Halafu zingatia jinsi neno "events" lilivyotumika hapo. Halimaanishi tukio kama ulivyoelewa wewe, ni tukio gani la kisiasa mtu anaweza akalifanyia ndani ya guest room ya hotel? Matumizi ya neno events huku likiwa limewekewa quote marks ni kwamba maana inayokusudiwa hapo si ile ya neno halisi. Hapo kinachozungumziwa ni kufanya mapenzi na mtu ndani ya chumba cha hotel, hakuna habari ya kampeni hapo.
 
Kila kitu hapo kimejieleza..sioni element yoyote ya rushwa hapo!

" I suspect giving free clothes and the campaign donation is just the way these people do business".

Hiyo sentence hapo imesummarize kila kitu

Hizo donations hazitolewi kienyeji tu na hawa tunaowaita wawekezaji kwa viongozi wetu, wanaanza kwa kununulia chupi, ukikubali hiyo offer wanakununulia shati, ukipokea wanakununulia suruali, then suti. Mwisho wa siku wanakuja na ombi fulani kwako. kwa kuwa umeshapokea "zawadi" maamuzi utayoyafanya, for sure yatarefrect mahusiano yenu, yaani utamfavour kwa kuwa unavaa chupi na suti zake, tena siku anakuja atakwambia aisee suti zile zinakupendeza kweli, utasema ahante, then atalodge ombi lake....................for sure utamfavour in a deal. Corruption impairs judgement.....................................funguka!!!!
 
Ila ukerewe nako noma. Kuna mawe yanacheza dansi kule. Ndio maana wazungu wametoa tahadhari kabla ya hatari. Inaelekea ugagula ni sehemu ya mila za kule.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom