Wiki ya ubunifu Tanzania-Kanda ya Njombe

Izzi

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
553
1,107
Habari wanajukwaa,

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa WUTz kufanyika Njombe, na nikiwa ni mmoja wa waratibu wa jukwaa hili la WUTz Kanda ya Njombe nimeona ni vyema nikilileta suala hili hapa JF. Kwanza ni kwasababu ninaamini kuna wadau wengi wenye uzoefu na fikra tunduizi za kutosha zinazoweza kutusaidia kulifanya jukwaa la WUTz2022 Kanda ya Njombe lilete tija. Pili ni namna mojawapo ya kualika wadau, hususani wabunifu kushiriki WUTz2022 - Kanda ya Njombe. Naomba nitoe dondoo kidogo kwa kifupi;

NB: Popote linapotumika neno "Ubunifu" ni kwa maana ya "Innovation". Wataalamu wa Kiswahili watatusaidia tafsiri mahsusi ya haya maneno matatu: 'Innovation', 'Invention' na 'Creativity'

WIKI YA UBUNIFU NI NINI?
Sio tukio, ni jukwaa ambalo lilianza mwaka 2015 chini ya Mfuko wa HDIF (Human Development Innovation Fund) wa UKAid, likiratibiwa na UNDP kwa kushirikiana na COSTECH. Jukwaa hili huwa lipo kila mwaka na hufanyika kwa wiki moja kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ambapo wabunifu hupata nafasi ya kuonekana, wadau hupata nafasi ya kufahamiana na kutengeneza ushirikiano, maarifa ya kutosha hushirikishwa, mambo mbalimbali ya kibunifu huoneshwa na masuala nyeti ya kisera hujadiliwa. Lengo kuu ni kuujenga mfumo wa ikolojia ya ubunifu Tanzania.

IWTZ.png

MWAKA HUU ITAFANYIKA WAPI?
Kwa mwaka huu 2022, kilele cha WUTz2022 kitakuwa Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, kuanzia Tarehe 15 Mei mpaka Tarehe 20 Mei.

KWANINI INAITWA "KILELE"?
Kwasababu kabla ya Tarehe 15 Mei, kutakuwa na matukio mbalimbali katika mikoa 16, yatakayokuwa yanafanyika kwa nyakati tofauti tofauti kuanzia Aprili 23 Mpaka Mei 14 yote ni katika kuadhimisha WUTz katika ngazi za mikoa/kanda.

KUNA KAULI MBIU?
Ndio, WUTz2022 ina kauli mbiu (Main theme) ifuatayo: "UBUNIFU KWA MAENDELEO ENDELEVU" (Innovation for sustainable Development).

SDG wheel Swahili-06.jpg

Lakini kuna 'sub-themes' 5, ambazo ni: (*Samahani nitatumia lugha ya kukopa);
  • Green and blue innovations for a hunger-free future.
  • Policy and institutional frameworks for a vibrant innovation ecosystem.
  • Innovation financing for job creation.
  • Inclusive digital connectivity - Leaving no one behind.
  • Innovation for a future-proof education system.
NJOMBE INAFANYIKA LINI?
WUTz2022 kanda ya Njombe itafanyika kuanzia Tarehe 8 Mei mpaka Tarehe 14 Mei, 2022 katika maeneo tofauti tofauti, kwa Halmashauri zote zilizopo katika Mkoa wa Njombe.

OK, KWAHIYO?
Nitumie fursa hii kukaribisha mawazo, ushauri, maoni kuhusu namna bora ya kulifanya jukwaa lilete tija zaidi. Ikumbukwe, jukwaa hili kwa mikoa mingi linawalenga zaidi wanafunzi wa vyuo vikuu. Kwa Mkoa wa Njombe hali ni tofauti, hatuna vyuo vikuu zaidi ya OUT - kwa sehemu kubwa walengwa wengi ni vijana na wananchi walioishia kidato cha nne, cha sita, na vyuo vya ufundi. Hivyo, tunafahamu tunahitaji kutumia mbinu tofauti za kulifanya jukwaa hili liendane na mazingira yaliyopo. Kwa mwenye mawazo, karibu sana. Lakini pia inawezekana yapo maswali, ruksa kuniswalika pia.

Pia, nitumie fursa hii kumkaribisha yeyote anayeona anaweza kufanya chochote katika WUTz2022 kanda ya Njombe; Iwe ni mbunifu, au ni muwezeshaji, au ni mdau wa namna yoyote, tunaendelea kupokea wadau ambao tutashirikiana nao ili kufanikisha tukio. Nitumie ujumbe DM au acha maoni yako hapa na mimi nitakuwa nikipita kusoma na kujibu.

NB: Tunaandaa matukio yatakayofanyika "Physically" na "Online".

Kwa sasa naomba niishie hapa, nitaendelea kuleta masasisho (updates) kadiri itakavyoonekana inafaa. Na baadae nitakuwa nikileta masasisho kuhusu WUTz2022 kwa ujumla.

Mimi... ninashukuru.

PS: Nimeambatanisha kijarida chenye taarifa kuhusu WUTz2022 kwa ujumla.

MASASISHO: Aprili 07, 2022

View attachment IWTz 2022 Open Call-01.png

View attachment IWTz 2022 Open Call II-01.png

MASASISHO: MEI 4, 2022

Ifuatayo ni mikoa inayoandaa "events" kuelekea wiki ya Ubunifu kitaifa, sambamba na Taasisi zinazohusika katika mikoa tajwa;

1. ARUSHA: Westerwelle Foundation Tanzania - Tarehe 9 - 13 Mei, 2022.
2. DODOMA: Capital Space Limited - Tarehe 15 - 20 Mei, 2022.
3. IRINGA: R-Labs - Tarehe 12 - 14 Mei, 2022.
4. MBEYA: MUST - Tarehe 9 - 13 Mei, 2022.
5. ZANZIBAR: Cube Zanzibar - Tarehe 10 - 14 Mei, 2022.
6. MTWARA: SIDO - Tarehe 13 Mei, 2022.
7. MWANZA: SIDO - Tarehe 25 - 29 Aprili, 2022
8. TANGA: Projekt Inspire Ltd - Tarehe 6 Mei, 2022.
9. MOROGORO: The Arena of Taking Charge (TAOTIC) - Tarehe 6 - 13 Mei, 2022.
10. NJOMBE: Valiant Hands of Care (VAHACA) Foundation - Tarehe 11 - 13 Mei, 2022.
11. KILIMANJARO: Kilistart - Tarehe 6 - 7 Mei, 2022.

12. KAGERA: KADETFU - Tarehe 27 - 30 Aprili 2022.
13. KIGOMA: SIDO - Tarehe 9 Mei, 2022.
14. MARA: Buhare CDTI - Tarehe 9 Mei, 2022.
15. RUVUMA: Mlale Digital Innovation Centre - Tarehe 6 Mei, 2022.
16. DAR ES SALAAM: TAI Volunteers - Tarehe 9 - 12 Mei, 2022.

IWTZ2022 - NJOMBE.png

INNOVATION WEEK MBEYA.jpg

IWTz2022- Moro Edition.png

WhatsApp Image 2022-05-03 at 11.45.56 PM.jpeg
 
Attachments

  • IWTz2022 Information Sheet_Updated.pdf
    3.3 MB · Views: 8
KWANINI INAITWA "KILELE"?
Kwasababu kabla ya Tarehe 15 Mei, kutakuwa na matukio mbalimbali katika mikoa 16, yatakayokuwa yanafanyika kwa nyakati tofauti tofauti kuanzia Aprili 23 Mpaka Mei 14 yote ni katika kuadhimisha WUTz katika ngazi za mikoa/kanda.
Hongera sana mkuu samahani naomba kuuliza VP kwa Dar essalaam hii itafanyika wapi
 
Ahsante nashukuru sana, naomba kujua kuwa Costech wanaweza toa mchango gani kwa NG'O ya vijana watakaoamua kuungana na kuanzisha shirika la INNOVATION hasa kwa upande wa ICT?
 
Ahsante nashukuru sana, naomba kujua kuwa Costech wanaweza toa mchango gani kwa NG'O ya vijana watakaoamua kuungana na kuanzisha shirika la INNOVATION hasa kwa upande wa ICT?
Mimi sio msemaji wa COSTECH lakini naweza kujibu kama ifuatavyo;

Unaposema Shirika la Innovation hususani kwa upande wa ICT, sijajua litakuwa na utofauti gani na yaliyopo.

Kwa mfano, mimi ninaendesha NGO na tunashirikiana na COSTECH katika baadhi ya kazi zetu. Lengo kuu la NGO yetu ni kuwawezesha vijana, na ili kutimiza hilo tunalenga zaidi eneo la ubunifu kwasababu ubunifu utawafanya vijana wengi watengeze ajira badala ya kutafuta ajira. Ubunifu unaweza kuwa wa TEHAMA au usihusishe TEHAMA. Kwa mfano tumeanzisha mradi wa vijana unaowawezesha kutatua changamoto zilizopo katika jamii inayowazunguka kwa kutumia rasilimali zilizopo palepale walipo (Ambazo ni kidogo), na kila changamoto ina utatuzi wake.

COSTECH wao kama chombo kilicho chini ya Serikali wana-support ubunifu, lakini msisitizo ni ubunifu unaoweza kuwa endelevu (Yaani ufike mahali ujiendeshe wenyewe bila kutegemea msaada). Mara nyingi NGO hazina 'sustainability', fedha za mradi zikiisha unakuta NGO inashindwa kufanya shughuli zake kwa kukosa pesa. Kwahiyo, COSTECH wao kama ilivyo kwa Serikali yote kwa ujumla, inashauri vijana wafikirie ubunifu utakaotatua changamoto iliyopo katika jamii, lakini pia waanzishe biashara za kibunifu.

Bila shaka, mkija na ubunifu unaolenga TEHAMA, kama ni endelevu basi COSTECH, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Serikali kwa ujumla itawasaidia. Hiyo ni bila kujali kama mtasajili NGO au la.

Naamini nimejibu swali lako. Kufahamu zaidi unaweza kuingia kwenye tovuti ya COSTECH - hii hapa
 
A

Ahsante sana mkuu umenikuna nitakufuata pm
 
Bila kufuta wanasiasa chumia tumbo uvumbuzi utaishia kuwaneemesha wahuni
 
Bila kufuta wanasiasa chumia tumbo uvumbuzi utaishia kuwaneemesha wahuni
Duniani kote Mabepari huwezi kuwakwepa, 'opportunists' hawakosekani, wahuni wamejaa kila kona ya dunia hii na hakuna kitu utafanya kuwaondoa. Kwahiyo, ni maamuzi ya mtu binafsi... unaacha kuvumbua kwasababu wahuni watafaidika na kubaki kulalamika au unavumbua na kutafuta namna ya kuzuia wahuni wasifaidike?

Nina uzi wangu mmoja unazungumzia Mbinu mbalimbali za kukuza biashara; na hii ni moja ya hoja niliyoiweka mle.

MBINU YA 9: USIPIGANE NA MFUMO, PIGANA NDANI YA MFUMO. (DON'T FIGHT THE SYSTEM - FIGHT IN THE SYSTEM.)
Hakuna wa kukuonea huruma hapa, kwahiyo usitie huruma. Kuna wengine kule nyuma hawajasikia.... nimesema hivi... NOBODY GIVES A F*** what you are going through bro, you either compete or die.

Pia lawama siku zote hazijengi, kwahiyo usijaribu kumlaumu yeyote; yaani hata wewe mwenyewe usijilaumu - futa kabisa neno lawama kwenye kamusi yako. Kulalamika pia ni rahisi sana, kila mtu anaweza kulalamika - na ndo mwisho wa siku tunajikuta tumekuwa nchi ya walalamikaji; Mwananchi anamlalamikia kiongozi wake, kiongozi anailalamikia mamlaka iliyo juu, mamlaka iliyo juu inamlalamikia Mungu, Mungu tu ndo sijawahi sikia amelalamika hata siku moja. Swali la kijinga unaloweza kuniuliza ni kwamba - kwahiyo tufanyaje? Ntakujibu - pambana ndani ya mfumo.

Sikia, wakati UBER inaanzishwa ilikutana na upinzani mkali toka kwa madereva taksi za kawaida na mamlaka za kiserikali. Madereva taksi walikuwa wanalalamika kuwa madereva wa UBER wanapiga hela ndefu wakati hawana leseni za biashara za 'udereva taksi' ambazo ni gharama. Mamlaka za kiserikali zilikuwa zinaibana UBER iwatambue madereva wake kama wafanyakazi rasmi na sio 'wakandarasi'. Pia mamlaka zilikuwa zinashindwa kuamua UBER iwekwe kundi gani; Taxi company au Technology company?. Kwa ambae haelewi - UBER haiajiri madereva, inatoa mikataba ya muda mfupi. Kwamba umejisajili UBER haimaanishi umeajiriwa na UBER. Kwahiyo, kwasababu haiwaajiri madereva imeepuka kuwa responsible kama mwajiri. Wengi wetu tunafahamu - waajiri wana mambo mengi ambayo wanapaswa kuyatimiza kwa wafanyakazi wao - UBER walikwepa hiyo since day 1. *Hiyo ndo inaitwa DISRUPTION / Challenging the status quo.
 
Back
Top Bottom