Wiki hii katika #SimuliziZa116

Sema Tanzania

JF-Expert Member
May 18, 2016
251
465
Mwezi Februari, 116 ilipokea simu kutoka kwa Rahma, mwanafunzi wa shule ya sekondari iliyopo
Unguja Kaskazini A. Mwalimu wao wa sayansi alikuwa hajaja kuwafundisha kwa wiki kadhaa,
jambo ambalo lilimfedhehesha yeye na wanafunzi wenzake. Alielezea kwamba mwalimu wao
alikuwa haji darasani na hatoi taarifa yoyote wakati alipaswa kuwafundisha mara mbili kwa wiki
siku ya Jumatatu na Ijumaa.


Rahma alimueleza mshauri nasaha wa 116 kwamba walijifunza kuhusu Huduma ya Simu kwa
Mtoto skuli walipokuwa wanajifunza kuhusu haki zao na jinsi ya kulinda haki hizi. Waliamua
kupiga 116 na kuomba ushauri kuhusu mwalimu wao ili waweze kupata haki yao ya elimu kama
watoto wengine. Huduma ya Simu kwa Mtoto ilipeleka kesi yao kwa mwenyekiti wa kamati yao ya
shule (Kamati ya Kuzuia Udhalilishaji wa Watoto) inayofanya kazi ya kuhakikisha wanafunzi
wanapata haki zao ndani na nje ya skuli.
 
Back
Top Bottom