Wife kanizidi kipato lakini kila wiki lazima aniombe elfu 20 ya kusukia

kyanyangwe

Senior Member
Oct 31, 2018
114
500
Habari wakuu.

Mke wangu ni muajiriwa kwenye moja ya entities hapa Tanzania, kipato chake kwa mwezi ni around 1.9m baada ya makato yote ya serikali.

Mimi kipato changu ni around 500k kwa mwezi na kiukweli kama mwanaume najitahidi sana pamoja na kipato changu kidogo kuhudumia familia yangu vizuri.

Sasa kilichonifanya kuandika huu uzi ni kisa kilichotokea juzi Jumamosi, wife ameninunia sababu ikiwa kwamba aliniomba pesa ya kusukia kama 20k hivi nikamwambia sina, nikamwambia yeye anakosaje hiyo elfu 20 wakati mahitaji yote ya nyumbani natoa mimi. Kanuna mpaka leo.

Nimeambatanisha ushahidi wa salary yake hapa, nishaurini, huyu mwanamke yuko sahihi kuniomba hela ya kusukia wakati kanizidi kipato karibia mara 4?
20210201_160523.jpg
 

T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,021
2,000
Yuko sahihi sana. Kwenye hiyo laki 5 toa elfu 20 akasuke tena hizo nywele za gharama ndogo. Angekuwa hana ajira bado ungetoa, kwa hiyo hapa hutoi kwa vile anakuzidi hela sio kwa vile huna hela kwa sasa. Ndio maana unautaja mshahara wake kama sababu ya kutompa.

Fedha zake mshirikiane kuendesha familia ila kumjali usiache. Cha msingi asikimbie na pesa yake, atapeleka kwa nani?
 

Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
5,777
2,000
Wanawake hela mnazotafuta ni kwaajili ya nini?
 

Ngishi

Senior Member
Sep 17, 2018
133
250
Jamani vitu vingine si vya kuomba hata ushauri, kama unayo unampa kwa upendo kabisa na hiyo inamfanya ajisikie na kujiona kuwa mume unamjali. Tena usisubiri uombwe ukiwa nayo unamwambia tu mke wangu naona nywele hizo zimechoka kasuke zingine hela hii hapa.

Nawe ukikosa siku mshirikishe tu kwamba mke wangu leo iko hivi na hivi, hela sian nimekwama kama uko vizuri naomba nisupport akiwa nayo atakupa tu sio unamsubiri uombwe au mke azungumzie suala la pesa ndio uanze kubwabwaja maneno.Angekuwa ni mchepuko wako kakuomba ungetoa zaidi ya hapo hata km kakuzidi kipato
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom