Why Mlimani Tv, not ITV, TBC?

Why Mlimani Tv, not ITV, TBC?

Nadhani ni chombo husika huwa kina na dress code yao kwa hiyo tusilazimishe vyombo vingine viige Mlimani TV wao wameamua hivyo lakini hata Aljazeera huoni watu wamevaa hijab pamoja na ukweli kwamba wapo sana katika kutetea maslahi ya waislamu,ukipanda Qatar au emirates huoni mtu yeyote kavaa baibui mule jamani na dhani dhana nzima ya imani iko ndani ya moyo wa mtu lakini sio mavazi
Uko sawa kabisa hizo ndege zote nilishasafiri nazo sijaona wakivaa hijab, tena tu skirt zao ni fupi tu
 
Mlimani TV inayomilikiwa na wasomi utakuona akina dada wetu ambao ni watangazaji wakiruhusiwa kuvaa hijab na huku wakiwa Live wanatangaza. hii nimeona ktk taarifa ya habari au hata katika habari nyengine
lkn baadhi ya tv hawaruhusiwi. na hii kutoruhsu uvaaji wa vazi la lazima kwa akina dada wetu wa kiiislam kunaifanya baadhi ya akdada wenye imani ya kweli na dini yao wanashindwa kujiunga na tv hizo huku wakiwa na sifa zao za utangazaji . kwa mfano niliwahi kusoma ktk moja ya gazeti kwamba Sakina dotto alikata kujiunga na Itv baada ya kukuataliwa kuvaa hijab akiwa Online.na wapo wengi tu ambao kwao hijab ni lazima lakina wanasifa zote za kutangaza.
Huku tukiwa tunapigania haki za wanawake Tanzania, yaani wawe huru bila ya kuvunja sheria, vyombo vya habri vikiwa mbele kutetea uhuru wa wanawake,yaani uhuru wa wanawake na kutowanyanyaswa .
Mbona mlimani tv inawezekana na huku Itv, star tv,Tbc haiwezekani? au mlimani tv ni ya waislam?
HIVI VYOMBO VYA HABARI VYETU HAVIONI UMUHIMU HUU HASA TUKIZINGATIA KWAMBA HUU NI WAKATI WA UTANDAWAZI?
​

niliwahi kuishi zanzibar lakini sikuweza jua hijab inamaana gani na kwa ajili ya gani...je hijab ni kwa ajili ya kufunika mwili na kuwacha wazi tabia? kipi cha kwanza mwili udhibitiwe ama tabia idhibitiwe.................oh ama ni vazi tu? vazi la kiislam!! Ok lkn mbona wanaume wavaa kanzu ama kofia wakitaka na mara nyingi ijumaa wakienda msikitini na hakuna anayefuatilia, hakuna anayejari wamevaa kiislam ama kikafri!! what is special, what is the concern hijab na akina dada?
 
kuna taarifa akina dada wengi wakiislam wanaom'ba kazi itv wanaambiwa kwanza wakiwa Live wasivae hijab jambo linawashinda. kwani kwao wanaona hijab ni vazi la lazima. lkn pia wakati huu wa utandawazi kumchagulia dada kuvaa ni kichekesho cha mwaka. kubwa zaidi ni yule dda aliejistiri na sio kimini

The way I see it is that: "If you want the rainbow you have to keep up with the rain"
 
niliwahi kuishi zanzibar lakini sikuweza jua hijab inamaana gani na kwa ajili ya gani...je hijab ni kwa ajili ya kufunika mwili na kuwacha wazi tabia? kipi cha kwanza mwili udhibitiwe ama tabia idhibitiwe.................oh ama ni vazi tu? vazi la kiislam!! Ok lkn mbona wanaume wavaa kanzu ama kofia wakitaka na mara nyingi ijumaa wakienda msikitini na hakuna anayefuatilia, hakuna anayejari wamevaa kiislam ama kikafri!! what is special, what is the concern hijab na akina dada?
aaaaaaaha, ukiwa mkiristo utachukia hijab n hutojua umuhimu wa hijab. lkn hijab kwa waislam ni lazima sawa na mkiristo kuamini yesu ni lazima. kama mkiristo humuamini yesu wewe sio mkiristo, sawa na dada wa kiislam without hijab ni makosa makubwa
 
Nimelazimika kuchangia Mada hii, Mimi ni Mkatoliki.
Hii inadhihirisha kua Elim Bado kikwazo kikubwa kwa Watanzania wengi, Nakubaliana kua Zipo sharia tofauti katika kila sehem ya kazi,
Bint wa kiislam kuvaa Hijab haidhihirish kua ni Muislam Itikad kali,, au anaijua Dini sana! Bali nitaratibu eidha ailiyolelewa nayo au kwel mwenyewe ameamua kuficha badhi ya Viungo Vyake vya mwili.
Nafaham kua wengi watanzania tunapenda kuona wakina dada wakidhihirisha viungo vyao wazi, lkn wapo wakina dada wasiopenda kuonyesha viungo vyao, Mbona masisiter wanaruhusiwa kuvaa mavaz yao mazuri kokote? SI UCHOCHEZI WA KIDINI BALI NI MTAZAMO WA KUHESHIM JAMII FULAN KUFUATA TARATIBI ZAO.
Mtoa maada hajadhihirisha kua anapigania Dini kwa lazima,, Nikweli kua Kila Muumini wa dini fulan anaegemea upande wa dini hiyo kwa sabab ni dini yake na anaheshim.
Hivyo bac maoni yamtoa maada nikua Inapendeza Mdada mwenye iman fulan eidha ya Kimasai avae kimasai kudumisha mira yake, Mkristo avae kulingana na taratibu zake, na Muislam avae kulingana na taratibu zake za kiiman kama anapenda,, Isiwe sababu ya Mmasai mwenye Ujuzi fulan akose Kazi ati hataki kuachana na Mira zake..
KAMA WEWE MUISLAM fuata taratibu za iman yako na Usivunje tarajibu za kazi,KAMA wewe Ni Mkristo kadhalika, ISIWE SABAB ya Ukristo WANGU napenda kuvaa msalaba Nizuiliwe kufanya kazi taasisis au compunny zenye kiongoz wa dhehebu lingine:
Mtoa mada hana hatia na wala JF haiwez kufuata mawazo yenu ya kiuchochezi na chuki.
Mtoa mada anashauri..
JAMAN..... TUELIMIKE.......
Jambo lingine ni kua... KAZI KWANZA, OFISINI KWANGU NINA AJILI MTU KUTOKANA NA UTASH WAKE KIKAZ SI itikad yake wala MAVAZ YAKE......

Mkuu kama ulivyoambiwa kila ofisi ina dress code yake. Hamna uniformity kwenye hii kitu. Ni kama vile kila ofisi ina values na ethics zake. Huziwezi unakua huru kuondoka unakwenda unakoona kunalingana na values/principles zako. It is the same kwa wakristo pia, ukienda shule au kufanya kazi kwa msabato kama wewe ni mlutheran au mkatoliki kuna vitu utalazimika kufuata. Unaweza jikuta unafanya kazi jumapili, lakini unatakiwa upumzike jumamosi. Kama huwezi unaondoka tu vizuri, tusilazimishe haya mambo yawe uniform haitawezekana. Mwajiri ndio ana-set boundaries and rules sio dhehebu fulani. Kuna waajiri wengine wako flexible lakini wengine wanakuwa strict kwenye work principles.
 
Labda tujiulize kwanza kwanini Asha Rose Migiro havai hijab?
Na waambie waaminio wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe "Ziinat" (mapambo) yao …. Ma Dhwahara Minha” (Isipokuwavaie yalivodhihirika katika hayo); na waangushe “Khumur” (shungi) zao mpaka “Juyuub” (vifuani) mwao, na wasionyeshe “Ziinat” (mapambo) yao ila kwa ….. me wao, au wana wao, au wana wa waume wao, au umbu zao, au wana wa maumbu wao, au wana wa dada zao, au wanawake wao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au watu wafikao mara kwa mara wasio watamanifu katika wanaume, au watoto ambao hawajajua siri za wanawake; wala wasipige miguu yao ili yajulikane wanayoyaficha katika mapambo vao; na tubieni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi waaminio, ili mpate kufaulu. (Qur'ani, 24:3O-31).
Maelezo ya Maneno Muhimu:
LABDA AMEPITIKWA NA AYA HII. LKN SIO SABABU YA KUZUIA KWENYE TV KUTOVAA HIJAB HASA TUKIZINGATIA WAMEKUWA MSTARI WA MBELE KUPIGANIA HAKI ZA WANAWAKE
 
petty things like these ndizo zinaturudisha nyuma

cant we just get along?

Nakuunga mkono, si ajabu mtoa mada ni msomi na bado anafikiri kuwa kufunika kichwa ndo udini. kwa kweli inashangaza mno:msela:
 
Mlimani TV inayomilikiwa na wasomi utakuona akina dada wetu ambao ni watangazaji wakiruhusiwa kuvaa hijab na huku wakiwa Live wanatangaza. hii nimeona ktk taarifa ya habari au hata katika habari nyengine
lkn baadhi ya tv hawaruhusiwi. na hii kutoruhsu uvaaji wa vazi la lazima kwa akina dada wetu wa kiiislam kunaifanya baadhi ya akdada wenye imani ya kweli na dini yao wanashindwa kujiunga na tv hizo huku wakiwa na sifa zao za utangazaji . kwa mfano niliwahi kusoma ktk moja ya gazeti kwamba Sakina dotto alikata kujiunga na Itv baada ya kukuataliwa kuvaa hijab akiwa Online.na wapo wengi tu ambao kwao hijab ni lazima lakina wanasifa zote za kutangaza.
Huku tukiwa tunapigania haki za wanawake Tanzania, yaani wawe huru bila ya kuvunja sheria, vyombo vya habri vikiwa mbele kutetea uhuru wa wanawake,yaani uhuru wa wanawake na kutowanyanyaswa .
Mbona mlimani tv inawezekana na huku Itv, star tv,Tbc haiwezekani? au mlimani tv ni ya waislam?
HIVI VYOMBO VYA HABARI VYETU HAVIONI UMUHIMU HUU HASA TUKIZINGATIA KWAMBA HUU NI WAKATI WA UTANDAWAZI?
​
kiogokichungu waambie hao madada waachane na hizo tv waende tv zenji kule hata wakivaa lile vazi la ninja poa tu,maana kuna wamasai nao wanadai wavae mashuka maofisini lakini wanakataliwa.Si unajua kila mahala kunataratibu zake,kunasehemu wakina dada wanatakiwa wavae kimini,sehemu nyingine suruali,sehemu nyingine bikini kwa hiyo mtu lazima ufuate taratibu za sehemu usika ukiona azikufai nenda panapo kufaa hakuna haja ya kulazimisha.
 
jamani mbona ni hoja nzuri tu, kama una la kuchangia changia hio hoja sio kumshambulia mtoa mada

kiukweli kuna haja kuheshimu mila na dini za watu wengine

Na kwahiyo wewe huhitaji kuheshimu kazi za watu?!, Unaleta udini na elimu duni yako kwenye kazi za watu?, hao akina dada unaotaka wavae hijabu kwenye Tv za watu wafungulie Tv yako wavae kininja ufurahi.
 
tukubali mawazo pinzani ili tupate suluhu ya jambo...mara zote anayebisha asikilizwe zaidi ya anayekubali jambo kirahisi
 
aaaaaaaha, ukiwa mkiristo utachukia hijab n hutojua umuhimu wa hijab. lkn hijab kwa waislam ni lazima sawa na mkiristo kuamini yesu ni lazima. kama mkiristo humuamini yesu wewe sio mkiristo, sawa na dada wa kiislam without hijab ni makosa makubwa

muhogo mchungu wewe unataka kuwaletea matatizo waislam, hiyo dini sijui umejifunzia wapi, hijab siyo vazi la kiislam ni vazi la jadi la mashariki ya kati. Harafu wewe unakoelekea ni kubaya, soon utataka askari wa kike wakiislam wavae hijab maana kwao ni lazima, hivi kinacho kufanya usijue kuwa kila mahali/taasis ina code of conduct ni nani?/nini: ni inferiority complex au ni uelewa duni wa mambo?,
 
Back
Top Bottom