Kuna baadhi ya watu hawataelewa ulichoandika! Hili ndilo lakusikitisha zaidi!
Masikitiko yako ni kama yangu niliposikia tu huyu mzee anapewa ubalozi.
Mimi kwa uelewa wangu nilijua kwamba hizi kazi za ubalozi zina watu wake hasa waliobobea katika maswala ya kidiplomasia
Kwa haraka haraka mimi hili la huyu dokta naliona kama "kudumaza" taaluma na malengo yake
Nchi makini zinathamini sana na kuendeleza vipawa na maono ya wananchi wake!
Mtu muhimu kama huyu kwenye sekta yenye wataalamu wachache kama afya unaanzaje kumpa ubalozi!? Ila huwezi jua huenda anaenda kututafutia fursa za vijana wetu kusoma masomo ya afya huko aendako! Vinginevyo watu kama hawa ndio walitakiwa kutumia tafiti zao na maono yao ili kuongeza ufanisi na wataalamu katika sekta ya afya!
Nchi nyingine watu kama hawa wanafungiwa maabara kabisa kutafuta majawabu ya matatizo mbalimbali kwenye jamii!
Kama ulivyosema, hata mimi sitaki kuamini katika maswala yasiyo na ushahidi usioshikika kwamba kuokoa maisha ya Lisu yaweza kuwa sehemu ya sababu ya ubalozi Wake! SITAKI KUAMINI KATIKA HILO HATA KWA BUNDUKI!
Sent using
Jamii Forums mobile app