DIZZO MTAWALA
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 240
- 769
Anaandika Dr Christopher Cyrilo
Dr. Mpoki Ulisubisya, aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya Afya ameondolewa kwenye nafasi hiyo na kupewa ubalozi.
Bila shaka Dr. Mpoki aweza kupangiwa kuwa balozi wa ubalozi mpya wa CUBA. Kabla ya Tanzania kufungua ubalozi Cuba, shughuli za kibalozi nchini humo zilitekelezwa na balozi wa Tanzania nchini Canada.
Kwa wasiojua, Ubalozi ni nafasi nyeti kwa nchi kama Marekani, China, Urusi, na zingine zinazojua dhumuni la nafasi hiyo katika ulimwengu wa leo. Kwa Tanzania, ubalozi waweza kuwa zawadi kwa mwanasiasa, hongo au wakati mwingine kuepuka lawama kwa mtu anayeondolewa mahali fulani. Au kupunguza minon'gono.
Kwa nadharia hiyo, Dr. Mpoki hakutendewa haki. Sitaki kuwa 'delusional' kiasi cha kuamini kwamba nafasi yake katika kuokoa maisha ya Mh.Tundu Lissu kule Dodoma kabla ya kusafirishwa Nairobi imepelekea haya. Sitaki kuamini kabisa mambo hayo yasiyo na ushahidi wa kushikika. Lakini najua Mh. Rais Magufuli akimkubali sana ndio maana akamuhamisha kutoka kuwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kumfanya kuwa katibu mkuu wa wizara ya Afya.
Wanafunzi na madaktari waliopitia mikononi mwa Dr. Mpoki wanajua uwezo wake. Huyu sio mtanzania wa kwenda kufanya kazi za kidiplomasia, wakati kuna mamilioni ya watanzania wanahitaji huduma yake. Moja kati ya madaktari bingwa wa kwanza nchi Tanzania katika eneo la Anestheology/Usingizi. Moja kati ya malengo yake ilikuwa ni kuhakikisha wataalamu wa Anesthesiology/usingizi wanapatikana katika hospitali nyingi za Tanzania.
Ukiacha ubingwa wa eneo hilo la Anestheology, pia ni mtaalamu wa huduma za dharura, mtafiti katika maeneo ya vimelea vya magonjwa na udhibiti wa maradhi ya kuambukiza. Pia ana shahada ya udhamiri/'masters' ya usimamizi wa biashara (MBA).
Je! Ni sawa kumpeleka Dr. Mpoki kwenye shuguli za kidiplomasia? Si sawa. Tunawahitaji maelfu ya wataalamu wa aina ya Dr. Mpoki, lakini waliopo hawafiki kumi.
Ikiwapendeza wanasiasa tuliowapa nguvu ya kuamua watakavyo, basi nawaomba waamue kumbakiza Dr. Mpoki Tanzania.
Asante.
Sent using Jamii Forums mobile app