Why CCM presidential ambitions comes 2015 relies heavily upon Prof. Anne Tibaijuka?

Ndugu yangu Rutashubanyuma, naona unasahau kuwa Mhaya haruusiwi kuwa kiongozi wa ngazi ya urais, kadhalika Msukuma na wale wote watokao katika makabila makubwa hapa Tanzania!

hizi ni hisia tu hakuna mahali ambapo hili limeandikwa...............................na kama wananchama wa kawaida ndani ya ccm wakipewa uhuru wa kuchagua viongozi wawapendao..............................hisia hizi zitafikiwa mwisho wake.......
 
Serikali ya Tanzania haina dini hilo lipo kikatiba, sioni kwanini dini ichukue ujiko hapa. Hata hivyo watanzania tusio na dini au ambao ni "atheists" tutawakilishwaje kama kweli dini mhimu kiasi hicho. Tukubaliane kimsingi kama marehemu Nyerere kwamba tumchague kiongozi kwa uwezo wake na sio dini yake. Visingizio vya dini, jinsia, usawa, kabila n.k. mara zote huletwa na watu au viongozi mbao huwa wamebeba agenda za siri nyuma yao. Hili lilifanywa na mafisadi katika kumuengua fisadi mwenzao katika kugombea uspika wa bunge la muungano. Lilirudiwa ktk uchaguzi mdogo wa Igunga waliponyapalia swala la hijabu ya mkuu wa wilaya. Watanzania tukatae mitazamo hii. Tumewakosa viongozi wengi wazuri kwa ujuha huu, ofisi inaongozwa hovyo kwa sababu kiongozi aliwekwa sio kwa ubora na uwezo wake bali kwasababu ni mwanamke, shit!

hizi ni nadharia lakini inapokuja kiutekelezaji watanzania wanazo dini zao, makabila yao na jinisia zao.......................kwa hiyo wanapopiga kura nyanja hizi huwaongoza kufanya maamuzi ambayo mengi yao hayana hekima...........................be real sisi ni wakabila na wadini.......
 
Inaonekan huna taarifa sahihi kuhusu BAWATA na mgogoro ilikokuwa nao na serikali. Kwa taarifa yako kesi ya BAWATA na Serikali ilikaa mahakamni kwa miaka 12. Kesi hiyo ilifikia tamati mwaka 2009, pale BAWATA ilipoibwaga serikali. Kwa kujikumbusha rejea taarifa hii ya Daily news
:

tatizo lako unafikiri hii serikali ya mamluki hufuata sheria.................hadi leo BAWATA bado hawajarudishiwa haki walizopewa na High Court kwa hiyo itbidi warudi mahakamani kudai utekelezaji wa hiyo hukumu.............................la muhimu hapo ni kuwa Asha Rose Migiro ndie aliyekuwa Waziri wa Wizara ya akina mama na alishiriki katika kuwakandamiza wanawake wenzie.......................hakupaswa kushiriki katika kuifuta BAWATA angelikuwa ni mzalendo na mkereketwqa angelijiuzulu uwaziri....................hakufanya hivyo kwa sababu analitumikia tumbo lake............
 
ukweli unabaki palepale mazingira ya Afrika yanafanana sana........kumbuka miaka ya sitini tuliona upepo wa mabadiliko ukianzia Afrika ya kaskazini na hilo lazima litajirudia na ccm nao wana wataalamu wa kuwashauri ya kuwa ngoma ya jana haichezeki tena leo...............TISS na NEC hawatakuwa na lao bao comes 2015...........................kwa hiyo ni lazima ccm wapanue wigo la demokrasia na kuwaruhusu wanachama wa kawaida kumteua mgombea uraisi ambaye anakubalika na wengi..............na hapo huyu mama ana nafasi kubwa.........masuala ya Zambia na kwingineko ya mekwisha kujadiliwa sana humu kwa hiyo saka makala husika..........ujielemisha ila sitarudia uchambuzi ambao tayari ulikwisha kufanyika kitambo................

nadhani umeshajijibu. Kama siasi za Africa zinafanana, basi hatuko mbali na Zambia au Kenya. Hatuhitaji mjinga mwingine aje kutuongoza. For me, she is nothing but thief kwa maana yupo ccm. Sina muda wa kujielimisha na analysis za walalahoi hapa jf. Maana utaweza kudai hii nayo ni analysis.
 
who is not a thief...........................give me just one name
 
Dhambi moja liyonayo ni kuwa mhaya. Kwanini wewe hujui kuwa nchi ina ukabila mbaya sana wa kisirisiri. Hata awe na sifa zote mhaa hawezi kupata urais.
 
Huyo mama ingawa ni mhaya na mkatoliki mwenzangua dhambi yake ni gamba(CCM). Watanzania wenzangu ni lazima tuanze upya na watu wapya,wenye mawazo mapya. Kama anataka kwenda Ikulu basi atoke ktk kichaka(CCM) nitamuunga mkono.
 
Hii ni Topic nzuri kiasi,Ila nijuacho mimi ni kwamba Mzee wa mji anamwandaa mtoto wa "mama mdogo" ili kuwa na vipindi atleast sawa kutoka enzi za mwalimu. Formular iko hivi mwalimu (miaka 23 pale Ikulu),Mkapa (miaka 10) Jumla yao ni 33.Sasa mtoto mwingine wa "mama mdogo" akija na kuwa ikulu kwa miaka 10,nagalau difference haitakuwa kubwa maana watakuwa na Jumla ya miaka 30. Hapo ndipo tuanze tena kupokezana upo hapo? Hiyo ni nyeti za ndani sana tena very strategic!

Haya,njia nyeupe kwa mabunduki 2015!
 
Nilimsikiliza prof. Tibaijuka jana kwenye BBC akijibu na kueleza kuhusu suala la ardhi na uwekezaji...pia tangu nianze kumsikiliza akiwa waziri hapa tz,...nimetokea kumpenda sana, na anaonekana mtu ambaye yuko committed, na anaweza kazi, ni mwaminifu na ile intergrity yake ya UN inamfanya afanye kazi kwa uaminifu ili asichafue cv ambayo alishaitengeneza.some people wanasema kale kamama ka UN Asha mingiro ndo pengine mzuri, mm naona yule ni mlaini halafu hawezi kitu na pale UN alipelekwa tu na mkubwa...Jamani nimeamua kulitoa hili moyoni mwangu, kwakweli nampenda sana uyu mama na angekuwa rais tz hata ndani ya ccm mlemle tungefika mbali....alimponda sana yule waziri wa ardhi aliyepita kwa kunyang'anya ardhi ya wananchi kwaajili ya wawekezaji uchuro....
 
Akamilishe kwanza ujenzi wa miji mipya Kigamboni, Makongo na Kibamba ili tujue utendaji wake wa ukamilifu wa mipango, akishindwa hata Urais hafai.
 
Ni marufuku kwa mhaya,mnyakyusa na mchaga kuwa RAISI bila shaka unajua ni kwa nini!
 
We huwatakii mema CCM, au ndio unapiga ndogondogo ili uwarahisishie kazi wapinzani.

Jamani kumbukeni tatizo SIYO mtu, tatizo ni system au structural damage kwa wale ma engineer wenzangu na solution siyo ku replace mtu mmoja haisadii ktk kuleta mapinduzi ya kweli ndani ya nchi yetu. kinachotakiwa ni overhaul the system kwa kutengeneza mfumo utakaotupa serikali ndogo ambao ni effective, create system which will empower people instead of govt. na tatu mfumo huo uwe na check and balance kati ya govt na other institutions ili kuweza enforce uwajibikaji. kufikiria kuwa mtu mmoja akichaguliwa atatua matatizo ni matokeo ya uvivu wa kufikiri au kutoijua system.
 
sasa kama unampenda wewe sisi anatuhusu nin.?
we unampenda ANNA mimi nampenda SLAA,wengine wanampenda LOWASSA..
OTHERWISE SUBIRI 2015 KWENYE KAMPENI RASMI..
 
haki ya nane, kama tz watakuja waweke raisi mwanamke, huyu pekee ndo anafaa.wengine hawapo...hata hivyo, sidhani kama Lowasa anamfikia huyu mama....yule mama ana akili na ni mwaminifu ati...
 
Nilimsikiliza prof. Tibaijuka jana kwenye BBC akijibu na kueleza kuhusu suala la ardhi na uwekezaji...pia tangu nianze kumsikiliza akiwa waziri hapa tz,...nimetokea kumpenda sana, na anaonekana mtu ambaye yuko committed, na anaweza kazi, ni mwaminifu na ile intergrity yake ya UN inamfanya afanye kazi kwa uaminifu ili asichafue cv ambayo alishaitengeneza.some people wanasema kale kamama ka UN Asha mingiro ndo pengine mzuri, mm naona yule ni mlaini halafu hawezi kitu na pale UN alipelekwa tu na mkubwa...Jamani nimeamua kulitoa hili moyoni mwangu, kwakweli nampenda sana uyu mama na angekuwa rais tz hata ndani ya ccm mlemle tungefika mbali....alimponda sana yule waziri wa ardhi aliyepita kwa kunyang'anya ardhi ya wananchi kwaajili ya wawekezaji uchuro....
Jamani kumbukeni tatizo SIYO mtu, tatizo ni system au structural damage kwa wale ma engineer wenzangu na solution siyo ku replace mtu mmoja haisadii ktk kuleta mapinduzi ya kweli ndani ya nchi yetu. kinachotakiwa ni overhaul the system kwa kutengeneza mfumo utakaotupa serikali ndogo ambao ni effective, create system which will empower people instead of govt. na tatu mfumo huo uwe na check and balance kati ya govt na other institutions ili kuweza enforce uwajibikaji. kufikiria kuwa mtu mmoja akichaguliwa atatua matatizo ni matokeo ya uvivu wa kufikiri au kutoijua system.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom