Why CCM presidential ambitions comes 2015 relies heavily upon Prof. Anne Tibaijuka?

Mpaka sasa huyu mama kuna lolote la maana kalifanya hapa Tanzania?

Watu wanauwana kwenye kugombea viwanja kama kawaida na huku yeye ndiye Boss.

Huyu mama ana huruma sana kuwa Rais wa nchi mbovu kama Tanzania na hasa hapa tulipo.

Tunataka mtu ambaye atachokonoa hadi nyoka pangoni mwake kwa moshi wa mti mbichi ambao utawaka kwa miaka 5 bila kukoma.

Tunamtaka Putin/Kagame wetu Tanzania aje asafishe. Huyu mama huwezi kumuona hata siku moja akimuweka ndani Mkapa au Lowassa.
 
Heshima zako kaka MN! Nastahili kukugongea likes za kutosha ila nmebanwa na mtandao hapa.
Ndugu yangu Ruta na wapendwa wengine, njia pekee ya chama chetu kipendwa ambacho kiliwahi kuwa cha wakulima na wafanya kazi ni kukiondoa kwenye dola. Wakiwa pembeni nje ya dola wao watajenga chama chao na sisi tutajenga nchi yetu!
Ni uasi dhidi ya historia kutumia rasilimali za taifa eti kujaribu kutatua migogoro ndani ya chama cha siasa.
Kuna kamtazamo bado kapo miongoni mwa watz wengi hasa baadhi ya watumishi wa umma, TISS na wazee wengine eti bila ccm nchi haitasonga, hvyo kundi hili la watu limekuwa busy kutumia kila mbinu kuwa nchi inabaki mikononi mwa chama hchi ambacho ni chenyewe tu ndio kinaelewa kinapotupeleka. Chama hicho hakina nafasi tena ya kuendelea kushika dola kwa matumaini kuwa huyu atabadili hali ya chama,
je nchi itakuwa wapi??

kimsingi ninakubaliana na wewe lakini shilingi ina pande mbili....................................usifikiri ccm itaachia tonge la ugali without a fight....................kwa hisia zangu huu ndiyo mkakati wa kuwabakisha madarakani..........................ingwaje hata mimi ningependa wadondoke......ili wajifunze kumheshimu mpigakura...................
 
mimi simpigii mtu debe ninangalia mazingira yalivyo ya kisiasa na jinsi ccm inavyoweza kujipanga upya...................wanawake wemgi waliopo ninasikitika hata wewe umeshindwa kumtaja hata mmoja kwa sababu wenye mandhari ya mvuto hawapo..................

Dr. Asha Rose Migiro ilooks too lethargic and continuation of another ten years of a Moslem is unthinkable.................................part of JK campaign in 2005 ilikuwa ni zamu ya Muislamu sasa unafikiri hiyo hoja ilimnufaisha yeye pekee yake?
Watanzania hatuchagui raisi kwa matakwa ya Kikwete wala mtu mwingine yeyote aliyoko madarakani, aidha hatuchagui raisi kwa jinsia yake, dini yake, rangi yake wala kabila lake kwasababu haendi Ikulu kuimarisha dini yake, kabila lake wala rangi yake kwa hiyo basi swala la zamu ya muislamu ni "out of point". Sijashindwa kumtaja mwanamke anaye faa na asiye na tuhuma. Sijataja kwa sababu sipendi kuwaangalia hao walioko huko juu tu, waache CCM kama kweli wanania nzuri na nchi hii waachie demokrasia ifanye kazi. Mchakato uanzie "grassroot", mizengwe iachwe, nakuhakikishia mr Ruta, tutapata kiongozi aliyebora na sio hao watu unaowapigia debe saa hizi.
 
Kwa Taarifa yako Asha Rose Migiro ndio CCM wanamwandaa 2015
Tuombe Uzima

Kazi ya urais tusiifanye ya majaribio Kama Uspika.....

....samahani ninawaheshimu sana kina mama...lakini kwa nchi za afrika mashariki mwanamke kuwa rais bado sana ......mmeona mwenyewe spika ...anaboronga..Hadi ....Kule Uganda ..walimpa umakamu wa rais kwanamama...specioza kazibwe..akamfungia mumewe nje.......haya hapa nyumbani niambie kinaamama wangapi barazani walioweza kumaintain ndoa Zao baada ya kuwa mawaziri....wanawake wengi,...badohawajazoea kuwa juu ya wanaume ..hii hype ekes kuwa intimidate waume Zao..ambao ni Kiri kuwa nao bado hawajaoea Hali hiyo....

Kuna Kazi nyingi ...tu zinaowafaaa
 
kimsingi ninakubaliana na wewe lakini shilingi ina pande mbili....................................usifikiri ccm itaachia tonge la ugali without a fight....................kwa hisia zangu huu ndiyo mkakati wa kuwabakisha madarakani..........................ingwaje hata mimi ningependa wadondoke......ili wajifunze kumheshimu mpigakura...................

Sitaki kukufundisha cha kusema ila kwa maslahi ya Tanzania tunayoitaka ingekuwapoa sana kama tungeweka mijadala ya namna gani ya Tanzania bila CCM, hili la mgombea bora wa ccm 2015.... dah sijui nalionaje maana kwangu hata waweke malaika bado sitamuamini na atashindwa tu kufanyakazi kimazingira na nature ya siasa za chama chao....
 
Nchi ina matatizo mengi sana: misingi yetu ya elimu ya chini ni mibouvu, hali ya maisha ni ngumu (kwa watanzania halisi na si wa humu JF, wengi humu ndani ni longolongo tupu hila ukweli wenyewe a majority are somewhat comfortable), ajira zinachukuliwa na wageni kwa kisingizio wazawa are unprepared for the job market and we have poor work ethics, economical development plan amna despite all the natural resources we have been blessed with.

So far amna kiongozi yoyote anaeongea like a politician despite all the social problems facing us, sisi tumekazana tu na zamu sijui ya nani lakini the important aspect of a good politician is never mentioned someone who talks about his economical plans which will take us from where we are into the next stage of our development and how he/she intends to accomplish those goals. Aren't we tired of political slogans without action plans.

Embu tuache siasa za maji taka sujui nani anatufaa atuhitaji majina au elimu ya mtu kutishika what we need is a serious politician na so far no one as stood up above the rest.
 
tatizo ni mfumo wa kupata viongozi......................atakachotusaidia ni kubadilisha katiba kazi ambayo miaka minne ijayo haitafanyika kukidhi kiu iliyopo hususani ya kuleta uongozi shirikishi katika kupata viongozi madhubuti......................mfumo uliopo ni wa kujuana tu.

kwa hiyo na yeye amefikaje hapo? Ivi wewe kweli unaamini kuna msafi ccm? ndugu yangu, kile chama kimeoza. Hakuna anayefaa kuongoza nchi yetu pale. Kama kweli ni wasafi, basi watoke huko....
 
I believe we need a transition period...........................and she can fit in as that transformational figure that will encompass the opposition too.............It is not easy to discard ccm altogether no matter how virulent the party has turned out to be................

Kwa nini? Kulikuwa na transition period Zambia? Kenya je? wacha kuwa muoga wa kufikiri ndugu yangu. Dare to think the impossible, dare to be different. Be bold! Nani alidhani mwisho wa huu mwaka Gaddafi angekuwa hapo alipo?hahahaha
Nadhani ungemwita huyo mtu kichaa!
 
Mpaka sasa huyu mama kuna lolote la maana kalifanya hapa Tanzania?

Watu wanauwana kwenye kugombea viwanja kama kawaida na huku yeye ndiye Boss.

Huyu mama ana huruma sana kuwa Rais wa nchi mbovu kama Tanzania na hasa hapa tulipo.

Tunataka mtu ambaye atachokonoa hadi nyoka pangoni mwake kwa moshi wa mti mbichi ambao utawaka kwa miaka 5 bila kukoma.

Tunamtaka Putin/Kagame wetu Tanzania aje asafishe. Huyu mama huwezi kumuona hata siku moja akimuweka ndani Mkapa au Lowassa.

mawzo mazuri lakni siasa na mchezo wa kulinganisha Putin na kagame sio watanzania na Raisi lazima awe mmoja wetu..........................kuhusu kuuana kwenye viwanja si ndiyo kaanz a kazi hata miaka miwili bado.........................miaka ya tisini alisaidia kuanzisha BAWATA ambayo Rose Asha Migiro akiwa waziri wa wanawake na watoto alifuta na kesi hadi leo ipo mahakamani ikisota...................BAWATA lilikuwa chombo cha kumkomboa mwanamke.............
 
wa nini? Kulikuwa na transition period Zambia? Kenya je? wacha kuwa muoga wa kufikiri ndugu yangu. Dare to think the impossible, dare to be different. Be bold! Nani alidhani mwisho wa huu mwaka Gaddafi angekuwa hapo alipo?hahahaha
Nadhani ungemwita huyo mtu kichaa!

ukweli unabaki palepale mazingira ya Afrika yanafanana sana........kumbuka miaka ya sitini tuliona upepo wa mabadiliko ukianzia Afrika ya kaskazini na hilo lazima litajirudia na ccm nao wana wataalamu wa kuwashauri ya kuwa ngoma ya jana haichezeki tena leo...............TISS na NEC hawatakuwa na lao bao comes 2015...........................kwa hiyo ni lazima ccm wapanue wigo la demokrasia na kuwaruhusu wanachama wa kawaida kumteua mgombea uraisi ambaye anakubalika na wengi..............na hapo huyu mama ana nafasi kubwa.........masuala ya Zambia na kwingineko ya mekwisha kujadiliwa sana humu kwa hiyo saka makala husika..........ujielemisha ila sitarudia uchambuzi ambao tayari ulikwisha kufanyika kitambo................
 
kwa hiyo na yeye amefikaje hapo? Ivi wewe kweli unaamini kuna msafi ccm? ndugu yangu, kile chama kimeoza. Hakuna anayefaa kuongoza nchi yetu pale. Kama kweli ni wasafi, basi watoke huko....

wanadamu wote ni wachafu alkini kwenye kipimo linganishi kuna wengine ni nafuu
 
Nchi ina matatizo mengi sana: misingi yetu ya elimu ya chini ni mibouvu, hali ya maisha ni ngumu (kwa watanzania halisi na si wa humu JF, wengi humu ndani ni longolongo tupu hila ukweli wenyewe a majority are somewhat comfortable), ajira zinachukuliwa na wageni kwa kisingizio wazawa are unprepared for the job market and we have poor work ethics, economical development plan amna despite all the natural resources we have been blessed with.

So far amna kiongozi yoyote anaeongea like a politician despite all the social problems facing us, sisi tumekazana tu na zamu sijui ya nani lakini the important aspect of a good politician is never mentioned someone who talks about his economical plans which will take us from where we are into the next stage of our development and how he/she intends to accomplish those goals. Aren't we tired of political slogans without action plans.

Embu tuache siasa za maji taka sujui nani anatufaa atuhitaji majina au elimu ya mtu kutishika what we need is a serious politician na so far no one as stood up above the rest.

yotte uliyoataja yanasababishwa na mfumo mbovu wa kuwapata viongozi na ndiyo maana ninashauri ya kuwa presidential primaries kwa vyama vyote vya siasa ili kuwauliza wananchama hivi wanamhitaji nani?

hata kama sote ni wabovu lakini mmoja wetu lazima awe Raisi wa hao wabovu.................wenzie.............
 
Sitaki kukufundisha cha kusema ila kwa maslahi ya Tanzania tunayoitaka ingekuwapoa sana kama tungeweka mijadala ya namna gani ya Tanzania bila CCM, hili la mgombea bora wa ccm 2015.... dah sijui nalionaje maana kwangu hata waweke malaika bado sitamuamini na atashindwa tu kufanyakazi kimazingira na nature ya siasa za chama chao....

ni kweli lakini ni vyema tuakatafari mbinu zipi watazitumia kujinusuru hata tujue tutawabana vipi wasipate pa kupumulia.........wazungu husema "be prepared and your time will come.........."
 
Watanzania hatuchagui raisi kwa matakwa ya Kikwete wala mtu mwingine yeyote aliyoko madarakani, aidha hatuchagui raisi kwa jinsia yake, dini yake, rangi yake wala kabila lake kwasababu haendi Ikulu kuimarisha dini yake, kabila lake wala rangi yake kwa hiyo basi swala la zamu ya muislamu ni "out of point". Sijashindwa kumtaja mwanamke anaye faa na asiye na tuhuma. Sijataja kwa sababu sipendi kuwaangalia hao walioko huko juu tu, waache CCM kama kweli wanania nzuri na nchi hii waachie demokrasia ifanye kazi. Mchakato uanzie "grassroot", mizengwe iachwe, nakuhakikishia mr Ruta, tutapata kiongozi aliyebora na sio hao watu unaowapigia debe saa hizi.

mawazo mazuri sana lakini yanahitaji kusukumwa hasa lile la kuwashirikisha grassroots kwenye zoezi la kumchagua Raisi kupitia vyama vyao vya siasa badala ya kuwaachia powerbrokers............lakni kuhusu dini, jinsia, kabila n.k huwezi kuyakwepa kwa sababu hata huko nyuma nafasi zilikuwa zinagawiwa kwa kuzinatia vigezo hivyo...............................na hoja ya muhimu ni kuwa sote tunaweza sasa haiwezekani upande mmoja uonekane ndiyo unaweza zaidi iwe jinsia, dini, kabila rangi n.k.............................upende usipende hivyo vigezo vitaendelea kutumika ili kuleta maelewano ya kitaifa.........................................
 
Ruta, Huyu mama Tibaijuka ni hatari sana kwa CCM kwa sababu she is for real, CCM haihitaji watu ambao there are for real, inahitaji watu wanaojua kupiga zengwe.

Kwa taarifa yako, Mama Tibaijuka, ameshapeleka mezani kwa JK, maombi ya kuvifutia miliki, viwanja vyote vya wazi ambavyo CCM imejimilikisha, akamsisitizia JK lazima avifute ili itakapo kuja kuwafutia umiliki wale wote waliomilikishwa maeneo ya wazi kuijanja ujanja, kusiwe na mahali pa kulilia. Sasa kama mtu huyu ndio kwanza anataka kuipokonya CCM mtaji wa kujivunia, unategemea nini?.

Prof. Tibaijuka akipewa urais, kwanza atamfikisha Ben mahakamani kwa kufanya biashara Ikulu, pia anaweza kumfikisha JK mahakamani kwa kuifanya Ikulu ni pango la walanguzi!. Huyu sio mtu wa kuaminika hata kidogo!.

Dr. Migiro pia ni kama Mama Tibaijuka kwenye ukweli, tatizo la mama Migiro, nae zengwe, fitna na unafiki hana, ambazo Dr. Migiro hana, hivyo hana sifa zinazohitajika CCM.

Mtu kama Magufuli ni hatari zaidi kuliko hao wote, anaweza kabisa kuwa dictator, ni mtu asiyeheshimu kabisa sheria, taratibu na kanuni, yeye hufikia maamuzi kwa utashi wake, kule Mwanza alivunja petrol station, serikali ikalipishwa mabilioni ya fidia. Serikali itakula tena hasara hivi karibuni kwa kulipishwa mabilioni ya fidia ya wale samaki wa Magufuli, hivyo naye hafai kabisa.

Kwa vile rais mpendwa wetu ni JK, CCM inamhitaji mtu kama JK, na kati ya waliopo, ambaye ni kama JK ni Membe, tena anamzidi JK kwa vile JK ni Mswahili, Membe sio mswahili. Kisifa, wanaendana, kitabia wanaendana, hata kimuonekano, wote ni ma HB, hivyo wanaendana, msiwe na wasiwasi kuhusu uwezo, Watanzania hatuchagui uwezo, tunachagua sura, kwa 2015, sura ya kupendeza ni Membe Pekee!.
 
Mkakati wa kujivua gamba unaelekea kuwa sasa ni kioja ndani ya ccm kwa sababu una matatizo ya ujumbe na wajumbe wenyewe kwani kuna migongano mikubwa hapo...ingawaje mjumbe hauwawi...

ujumbe wa kujivua gamba una walakani kwa kuwa siyo sera ya chama na mkakati wake siyo shirikishi...matawi ya ccm hayana taarifa na hayajui kinachoendelea....vivyo hivyo mikoani na wilayani tatizo ni hilo hilo hawajui...kipi kinaendelea...

pili uteuzi wa safu mpya ya uongozi wa juu ndani ya ccm pia ni matashi ya viongozi wa juu na huku chini wanaona wanaburutwa tu...haya si mazingira ya kukiaanda chama kubaki madarakani....na isitoshe baadhi ya vinara wa ufisadi wameachwa kundini...

mbinu za kukisafisha chama yaelekea nahivyo kueleweka na wengi ya kuwa lilikuwa changa la machoni kwani vinara wa ufisadi bado wanaendelea kutesa ndani ya chama hicho na wengine wamepata ujasiri hata kuanza kujenga ngome za kujiandaa kutwaa nchi...kwa nguvu ya pesa na na kwa gia ya dola...lakini hawaungwi mkono na wapigakura...

lakini wenye uwezo wa kutafakari ndani ya ccm wanaamini ya kuwa yaliyotokea katika uchaguzi wa 2010 hayawezi kujirudia tena mwaka 2015...ccm haiwezi kuendelea kutegemea kuokolewa na TISS na NEC katika uchaguzi ujao...

mbinu za ujumbe wa nguvu mpya, kasi mpya na ari mpya wengi wa wapigakura sasa wameushtukia kwa sababu hakuna mabadiliko na viongozi huendelea kuwa wale wale kwenye ngazi zote na hivyo kufifilisha matarajio ya wananchi....kuwa kuna malengo kweli ya kubadilisha mwelekeo wa taifa kutoka hadhi ya kujuana na kujali sifa za wahusika ili kusukuma kwa kasi maendeleo ya taifa...

kutokana na mazingira tajwa wapo wanaoamini ya kuwa mwanamke mwenye taswira ya mvuto ndani ya ccm anaweza kuwa karata ya mwisho ya kumalizana na Dr. slaa na Chadema yake...mwanamke huyo awe ana sifa zifuatazo:-

1) Asiwe na tuhuma hata moja ya ufisadi katika utumishi wake wa umma.

2) Awe Mkristu kuendeleza azma isiyo rasmi ya wakristu na waislamu kupokezana kiti cha Uraisi ndani ya ccm kwa hoja ya kujenga umoja na mshikamano bila ya kubaguana kwa misingi ya udini, ukabila au jinsia....au tofauti nyinginezo kama katiba inavyobainisha.

3) Asiwe Mnzanzibara kwa sababu wao wamekazana kuonyesha hawana imani na serikali ya Muungano kwa kurekebisha katiba yao na kujipa madaraka makubwa ambayo yanaonyesha dhahiri kuwa wanataka kujitenga...huwezi ukaendelea kuwaamini watu na masuala ya Muungano watu ambao wanadai wao ni nchi....hata hizi hongo za kuwapa vyeo kwenye masuala yasiyo ya Muungano kama u-R.C zina harufu kali ya rushwa za kisiasa...

4) Awe ni mwanamke ambaye ni mcha Mungu ili kuonyesha kwa vitendo ya kuwa kweli hizi ngonjera za ya kuwa wanawake wanaweza zinatoka moyoni.....mwanamke mwenye kashfa za ngono au mwenye tabia ya kulonga hovyo atakuwa mwiba kwa ccm...chadema watamrarua vilivyo...

5) Awe ndani ya baraza la mawaziri la JK la sasa kuonyesha ya kuwa uongozi wa kitaifa ni endelevu...hili pia litasaidia kuwatoa hofu washirika wa ufisadi ya kuwa hakuna lengo la siri la kuleta mtu mpya atakayewashughulikia....

6) Prof. Anne Tibaijuka hakuwa na upinzani katika kiti chake cha ubunge na hakuhitaji kuwawekea wapinzani mapingamizi kama viongozi wengi ndani ya chama cha magamba walivyofanya ili kujinusuru na hasira za wapigakura...huu ni uthibitisho ya kuwa hata vyama vya upinzani hususani Chadema vinamheshimu kwa sababu anajiheshimu mno...

kwa mbinu hizi ccm itatesa kwa kipindi kirefu sana....toa maoni yako bila ya shaka yoyote.......
Ndugu yangu Rutashubanyuma, naona unasahau kuwa Mhaya haruusiwi kuwa kiongozi wa ngazi ya urais, kadhalika Msukuma na wale wote watokao katika makabila makubwa hapa Tanzania!
 
Ruta, Huyu mama Tibaijuka ni hatari sana kwa CCM kwa sababu she is for real, CCM haihitaji watu ambao there are for real, inahitaji watu wanaojua kupiga zengwe.

Kwa taarifa yako, Mama Tibaijuka, ameshapeleka mezani kwa JK, maombi ya kuvifutia miliki, viwanja vyote vya wazi ambavyo CCM imejimilikisha, akamsisitizia JK lazima avifute ili itakapo kuja kuwafutia umiliki wale wote waliomilikishwa maeneo ya wazi kuijanja ujanja, kusiwe na mahali pa kulilia. Sasa kama mtu huyu ndio kwanza anataka kuipokonya CCM mtaji wa kujivunia, unategemea nini?.

Prof. Tibaijuka akipewa urais, kwanza atamfikisha Ben mahakamani kwa kufanya biashara Ikulu, pia anaweza kumfikisha JK mahakamani kwa kuifanya Ikulu ni pango la walanguzi!. Huyu sio mtu wa kuaminika hata kidogo!.

Dr. Migiro pia ni kama Mama Tibaijuka kwenye ukweli, tatizo la mama Migiro, nae zengwe, fitna na unafiki hana, ambazo Dr. Migiro hana, hivyo hana sifa zinazohitajika CCM.

Mtu kama Magufuli ni hatari zaidi kuliko hao wote, anaweza kabisa kuwa dictator, ni mtu asiyeheshimu kabisa sheria, taratibu na kanuni, yeye hufikia maamuzi kwa utashi wake, kule Mwanza alivunja petrol station, serikali ikalipishwa mabilioni ya fidia. Serikali itakula tena hasara hivi karibuni kwa kulipishwa mabilioni ya fidia ya wale samaki wa Magufuli, hivyo naye hafai kabisa.

Kwa vile rais mpendwa wetu ni JK, CCM inamhitaji mtu kama JK, na kati ya waliopo, ambaye ni kama JK ni Membe, tena anamzidi JK kwa vile JK ni Mswahili, Membe sio mswahili. Kisifa, wanaendana, kitabia wanaendana, hata kimuonekano, wote ni ma HB, hivyo wanaendana, msiwe na wasiwasi kuhusu uwezo, Watanzania hatuchagui uwezo, tunachagua sura, kwa 2015, sura ya kupendeza ni Membe Pekee!.
Umesahau kidogo mkuu, pamoja na kuchagua sura pia tunachagua chama maslahi ya taifa baadae!
 
mawazo mazuri sana lakini yanahitaji kusukumwa hasa lile la kuwashirikisha grassroots kwenye zoezi la kumchagua Raisi kupitia vyama vyao vya siasa badala ya kuwaachia powerbrokers............lakni kuhusu dini, jinsia, kabila n.k huwezi kuyakwepa kwa sababu hata huko nyuma nafasi zilikuwa zinagawiwa kwa kuzinatia vigezo hivyo...............................na hoja ya muhimu ni kuwa sote tunaweza sasa haiwezekani upande mmoja uonekane ndiyo unaweza zaidi iwe jinsia, dini, kabila rangi n.k.............................upende usipende hivyo vigezo vitaendelea kutumika ili kuleta maelewano ya kitaifa.........................................
Serikali ya Tanzania haina dini hilo lipo kikatiba, sioni kwanini dini ichukue ujiko hapa. Hata hivyo watanzania tusio na dini au ambao ni "atheists" tutawakilishwaje kama kweli dini mhimu kiasi hicho. Tukubaliane kimsingi kama marehemu Nyerere kwamba tumchague kiongozi kwa uwezo wake na sio dini yake. Visingizio vya dini, jinsia, usawa, kabila n.k. mara zote huletwa na watu au viongozi mbao huwa wamebeba agenda za siri nyuma yao. Hili lilifanywa na mafisadi katika kumuengua fisadi mwenzao katika kugombea uspika wa bunge la muungano. Lilirudiwa ktk uchaguzi mdogo wa Igunga waliponyapalia swala la hijabu ya mkuu wa wilaya. Watanzania tukatae mitazamo hii. Tumewakosa viongozi wengi wazuri kwa ujuha huu, ofisi inaongozwa hovyo kwa sababu kiongozi aliwekwa sio kwa ubora na uwezo wake bali kwasababu ni mwanamke, shit!
 
mawzo mazuri lakni siasa na mchezo wa kulinganisha Putin na kagame sio watanzania na Raisi lazima awe mmoja wetu..........................kuhusu kuuana kwenye viwanja si ndiyo kaanz a kazi hata miaka miwili bado.........................miaka ya tisini alisaidia kuanzisha BAWATA ambayo Rose Asha Migiro akiwa waziri wa wanawake na watoto alifuta na kesi hadi leo ipo mahakamani ikisota...................BAWATA lilikuwa chombo cha kumkomboa mwanamke.............

Inaonekan huna taarifa sahihi kuhusu BAWATA na mgogoro ilikokuwa nao na serikali. Kwa taarifa yako kesi ya BAWATA na Serikali ilikaa mahakamni kwa miaka 12. Kesi hiyo ilifikia tamati mwaka 2009, pale BAWATA ilipoibwaga serikali. Kwa kujikumbusha rejea taarifa hii ya Daily news:

"DailyNews by FAUSTINE KAPAMA, 3rd April 2009 @ 07:00

The High Court has declared unconstitutional the government's decision to deregister the National Women Council, commonly known as Baraza la Wanawake Tanzania (Bawata). Justices Amir Manento (rtd), Laurian Kalegeya and Juxton Mlay ruled yesterday that the decision by the Registrar of Societies and the Minister for Home Affairs in September 1996 was null and void.

They said in a judgement that the provisions of Sections 2(2), 6, 9(a), 9(d)(iii), 12 and 13 (2) of the Society Ordinance (now Section 2(2),8,14,17 and 19(2) of the current Society Act), relied upon by the government were unconstitutional. The justices, however, ruled that the said impugned provision that have been declared unconstitutional would not be struck out of the statute books. Instead, they ordered the appropriate authority within a year from the date of delivery of the judgement to take necessary steps to make the said provisions compliant with the constitution.

Furthermore, the court ordered the government to pay the petitioners costs of the suit and 20m/- as general damages following several inconveniences caused after the deregistration of the society. Petitioners in the case, apart from Bawata, were Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, Sherbanu Nasser Kabisa, Rose Temu Mushi, Mary Chonjo Marealle and Salma Khatim Kauli. In their petition, Bawata, through Prof. Issa Shivji, had argued that the government's action of deregistering the organization was unconstitutional.

This was so because such action violated Articles 13(6)(a), 18, and 20 providing for the right of fair hearing, expression, and association and assembly, respectively and other international human rights instruments. The instruments include the International Convention on Civil and Political Rights (ICCPR), the African Charter on Human Rights, and the Convention on Elimination of All Forms of Discrimination Against Women (CEDAW).

Bawata was formed in 1994 for purposes of uniting women of all economic, social, and political backgrounds and to ensure gender equity in a multiparty democratic Tanzania. With the advent of political pluralism, it was felt that women might lose rights without an organ to voice their common concerns and problems. Bawata was formerly registered on May 16, 1995.

Its early work -- as articulated in its constitution -- focused on inheritance rights, the right to own land and political representation of women in Parliament.The government, however, accused the society of being a political party and in September 1996, the government decided to deregister the Non-Governmental Organization.

Later on, the government asked Bawata to amend its constitution and operate as a research institution. In March 1997, at a General Meeting, Bawata yielded and the organization's constitution was amended in accordance with government demands. Even so, the government went ahead to deregister the society. In response, in 1997, Bawata went to the High Court to challenge the government's action and the constitutionality of the Societies' Ordinance."
 
Ruta, Huyu mama Tibaijuka ni hatari sana kwa CCM kwa sababu she is for real, CCM haihitaji watu ambao there are for real, inahitaji watu wanaojua kupiga zengwe.

Kwa taarifa yako, Mama Tibaijuka, ameshapeleka mezani kwa JK, maombi ya kuvifutia miliki, viwanja vyote vya wazi ambavyo CCM imejimilikisha, akamsisitizia JK lazima avifute ili itakapo kuja kuwafutia umiliki wale wote waliomilikishwa maeneo ya wazi kuijanja ujanja, kusiwe na mahali pa kulilia. Sasa kama mtu huyu ndio kwanza anataka kuipokonya CCM mtaji wa kujivunia, unategemea nini?.

Prof. Tibaijuka akipewa urais, kwanza atamfikisha Ben mahakamani kwa kufanya biashara Ikulu, pia anaweza kumfikisha JK mahakamani kwa kuifanya Ikulu ni pango la walanguzi!. Huyu sio mtu wa kuaminika hata kidogo!.

Dr. Migiro pia ni kama Mama Tibaijuka kwenye ukweli, tatizo la mama Migiro, nae zengwe, fitna na unafiki hana, ambazo Dr. Migiro hana, hivyo hana sifa zinazohitajika CCM.

Mtu kama Magufuli ni hatari zaidi kuliko hao wote, anaweza kabisa kuwa dictator, ni mtu asiyeheshimu kabisa sheria, taratibu na kanuni, yeye hufikia maamuzi kwa utashi wake, kule Mwanza alivunja petrol station, serikali ikalipishwa mabilioni ya fidia. Serikali itakula tena hasara hivi karibuni kwa kulipishwa mabilioni ya fidia ya wale samaki wa Magufuli, hivyo naye hafai kabisa.

Kwa vile rais mpendwa wetu ni JK, CCM inamhitaji mtu kama JK, na kati ya waliopo, ambaye ni kama JK ni Membe, tena anamzidi JK kwa vile JK ni Mswahili, Membe sio mswahili. Kisifa, wanaendana, kitabia wanaendana, hata kimuonekano, wote ni ma HB, hivyo wanaendana, msiwe na wasiwasi kuhusu uwezo, Watanzania hatuchagui uwezo, tunachagua sura, kwa 2015, sura ya kupendeza ni Membe Pekee!.

ninaafiki na hii misimmo walakini ndiyo maana nimeshauri ya kuwa lazima mchakato wa kura za maoni shirikishi ndiyo utakisaidia ccm kutoka hapo kilipo katika siasa za kujuana na kulindana........................na kuanza kumtumikia raia wa kawaida...........
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom