Who wounded you???

Who wounded you???

Touched thread Boflo, nitakuja baadae. Inanihusu sana hii.
 
19. My relatives refused to give support on my education after my father's death but i fought on my own now i have a bachelor degree. Nikikumbuka huwa napatwa na hasira sana

Ndio maana Tanzania tuko nyuma, hivi wewe una degree?
 
Whatever i went through in different stages of life didnt wound me, it was part of growing up and moulding me to be a better person. Pengine Mungu alitaka upite hapo ili ukikutana na mtu anaomba ada uelewe maana yake na uhakikishe haumnyimi. Lakini pengine it was to teach you how to get ready for the same situation later in life. Mfano nitonye, ulishawahi kuwaza kuandika mirathi, na kuwekea wanao education insurance? Im glad i went through all that i did, getting a life lesson out of it is the crucial part badala ya kuwa na hasira na kisirani.
 
Last edited by a moderator:
Pdidy ana Masters.

Kwi kwi kwi teh teh teh, mwambie aandike application ya kazi mbele ya uso wako, uone kazi. Ofisini kwetu ukija kwenye interview, kitu cha kwanza unapewa kalamu na karatasi, unaambiwa andika application na jieleze una ujuzi gani, unapewa dakika 15. 99% ya wenye degree za mwanzo wanaishia kukubali yaishe na wenye degree za pili 60% wanaishia kukubali yaishe. Hiyo ndio Bongo.
 
Mimi niliumizwa na mume alienioa na sio kwa kuwa alicheat ila aliniahidi kuwa akipata mwanamke wa kabila lake itanibidi nimsahau cz asingerudi kwangu kamwe. huwa anaongea sana maneno ya namna hii hadi nimeshazoea. Ila ukweli ni kwamba moyo wangu ulishachoshwa sana na nilianza kumchukulia kama mtu baki katika jitihada za kujiandaa na cheating yake. Ninachomshukuru Mungu ni kwamba nilisikia mahubiri ya mtu wa Mungu Mwakasege alisema " Ni Yesu tu ndie anaeweza kuponya majeraha ya nafsini mwako peke yake". Nilimuomba Yesu anigange nafsi yangu ambayo ilikuwa imejeruhiwa sana na mwanamume niliekuwa nimempenda sana na kumheshimu yet yeye ananiumiza. Kwa kweli sasa hivi sina kinyongo nae na nampenda hivyo hivyo alivyo hata anapoanza kuongea maneno yake namsamehe mara moja. Kama atakuja fanikisha hiyo nia yake, napo nitamsamehe vile vile.
 
Ndio maana Tanzania tuko nyuma, hivi wewe una degree?

Acha wivu hapa hatuko kwenye siasa, tatizo lako huna experience ya maisha halafu wewe inaonekana ni mtoto wa mama, halafu inaonekana wewe ni mlegevu sana Zanzibar hawajambo?
 
ENH!watu ni wakatili jamani!
bora umejiponya mwenyewe mamii!
nimehisi viatu vyako vikinibana mpenzi!
 
Kwi kwi kwi teh teh teh, mwambie aandike application ya kazi mbele ya uso wako, uone kazi. Ofisini kwetu ukija kwenye interview, kitu cha kwanza unapewa kalamu na karatasi, unaambiwa andika application na jieleze una ujuzi gani, unapewa dakika 15. 99% ya wenye degree za mwanzo wanaishia kukubali yaishe na wenye degree za pili 60% wanaishia kukubali yaishe. Hiyo ndio Bongo.
hahaha kama cover letter tu wana google na ku edit unategemea nini lazima wasepe!
 
Acha wivu hapa hatuko kwenye siasa, tatizo lako huna experience ya maisha halafu wewe inaonekana ni mtoto wa mama, halafu inaonekana wewe ni mlegevu sana Zanzibar hawajambo?
Hujamuelewa Zomba, ila ana point kubwa sana, mimi ni Form Four Graduate lakini Degree holders wengi huwa wanategemea material mengi kutoka kichwani kwangu plus application wengi sana nimewasaidia format ya kuandika.

Tulifanya Presentation Interview siku moja Holiday Inn kwa kweli kilichotokea ni aibu tupu na nilikatishwa tamaa sana na hawa tunaowaita wasomi wetu.

Sasa Wazungu wengi wanapokuja kufunguwa kampuni zao baadhi ya ajila hawahitaji vyeti bali wanataka wakufanyie Interview wewe mwenyewe binafsi, wakilizika na wewe hawahitaji vyeti, maana wengine wana vyeti lakini inaleta shida kujuwa huyu alitunukiwa vipi vyeti hivyo wakati upstais empty!!
 
I wish ningekuwa beside ya snowhite wakati analia ningempa busu 1 la forehead
j.jpg
 
Nakumbuka 1990's after my parents' death, kipindi cha kufatilia mirathi... Upande wa Mzee ukiongozwa na babu walitukataa kabisa watoto wa marehemu mahakamani wakidai ndugu yao (baba) hakuwahi kuoa wala kuwa na watoto...
Cha kushangaza zaidi baadhi yao walikulia nyumbani kwetu na kusomeshwa na mama kipindi Mzee anaugua....
 
achenu ujinga wenu nyie watu, hakuna anayemuumiza mwenzake, but unajiumiza mwenyewe. sikia nikueleweshe kitu hapa ambacho kinaweza kukusaidia sana
kinachokufanya kuumie siyo jambo ulilotendewa, bali ni jinsi wewe mwenyewe utakavyochukulia lile jambo. kwa maana hiyo kinachokufanya uumie siyo lile jambo bali ni fikra zako. kwa mfano, nimempenda sana msichana, nikamsomesha mpaka chuo kikuu au level flani kwa matarajio kuwa atakuwa mke wangu, mwisho wa siku akasepa. ukiwapa scenario hiyo watu tofauti, kuna atakaye kwambia aisee patachimbika, mwingine, atatoa ushauri tofauti, na kila kitu. sasa katika hali hii, ile reaction utakyochukua baada ya jambo hilo ndiyo itakayo kuumiza
ok, fikiria umemfumania mke wako au mume wako!, kitakachokuumiza siyo fumanizi, ni jinsi utakavyolichukulia hilo fumanizi, mwingine anaua hapo hapo, mwingine anampa pole mkewake, na kumwambia twendezetu home mpz, mwingine anadai fidia tu anasepa zake.
ndiyo mana sasa, kunakitu kinachoitwa ukomavu wa hisia, au "emotional maturity" kwa kikoloni, au kwa lugha nyingine wanasema ukubwa wa kifua. kama kifua chako kinaweza kulibeba jambo, then maumivu ni madogo, na kama haliwezi hapo utadata, kwahiyo kinachokufanya udate siyo jambo, bali imaturity yako.
jifunze kukua kihisia na trust me hautaumizwa kamwe
 
Boflo leo umetoka na uzi ambao hujawahi kuutoa hapa jamvini!!! Tumezoea zile za kwako za madoooo tu!! Ha ha ha!! thenki yu mkuu!! Walimtenda Baba, na sisi tuka fall victim wote leo hii wanatuangukia!!!!!! Hata watoto wao na wajukuu wanatutafuta, unashangaa tu unapigiwa simu ...mmi naitwa fulani ni mtoto wa mtoto wa fulani, shikamoo uncle....... ninaomba... kudadeki!!
 
kwa kusoma hizi comment unajihisi kumbe hauko peke yako uliokumbwa na matatizo.kwa yaliyonikuta,kuna baadhi ya watu nimewasamehe otherwise nisinge move on.ila kuna mmoja huyo,simsamehe maisha kwa alivyo take advantage,ilini affect mno till now,wakati ni kitendo cha miaka mingi nyuma
 
Back
Top Bottom