MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 849
Wakuu wameongea mengi hapo juu ya msingi, kuhusu suala la Palestina Wamarekani walimkaba Salim kwamba atakuwaje Katibu Mkuu wa UN wakati nchi yake iko partial kabisa katika mgogoro wa Palestina, kwamba Tanzania ilikuwa inaunga mkono kwa wazi kabisa PLO na haikuwa hata na uhusiano wa kibalozi na Israel, kwa hiyo hilo kama moja ya migogoro mikubwa kabisa, Marekani iliitumia turufu hii kumkataa Salim kwamba hatakuwa na credibility kwenye hili suala nyeti.
Salim alijaribu sana kujibu hili swali lakini hakuweza kuwa convincing enough, kwani issue ilikuwa wazi.
CV ya Salim imesheheni!! Anaweza hata akawa Rais wa Marekani acha Tanzania. Ndio maana alikuwa tishio kwao!!!
CV ya Salim imesheheni!! Anaweza hata akawa Rais wa Marekani acha Tanzania. Ndio maana alikuwa tishio kwao!!!
Wayne said:Katika kuweka kumbukumbu sawa,naamini kipindi cha Dr. Boutrous Ghali ndipo mkataba wa amani wa camp david uliposainiwa na Jenerali Yitzak Rabin akiwa kama Waziri Mkuu wa Israel na Yasser Arafat kama kiongozi wa PLO,tukio la kupeana mikono ya kuashiria amani lilifanyika chini ya Rais William Jefferson Clinton.
I stand to be corrected.
Mikael, siku zote nilikuona u-mstaarabu sana. Kumwita Kikwete Jangala badala ya Jakaya inahusu nini? After all mwenzio ni President of the United Republic of Tanzania whether you like it or not?
hii ni free forum mamaaa.....
so what akiwa president ndio nini....akichanwa si anatoka damu kama mimi...anakula kama mimi [hata kama mimi nakula mlo mmoja]....na mwisho wake ni kama wangu dunia hii...
heshima haiombwi ..bali huja yenyewe....ukiwa baba ..unaheshimiwa kwa ajili ya huduma unayotoa anzia kwa mke....hadi kurudi bega moja juu na kifurushi cha kitoweo cha watoto....kama yote huwezi ndio ..utakuwa baba ..lakini watoto wako watakuita kimoyomoyo BABA OVYOOOO!!...umenisoma nadhani!!!
huwezi kumlinganisha yeyote na huyu sijui naniii huyu...jangala michosho kiwete...eti kwa ajili ..sijui akiongea watu wanalala .....sikujuwa kumbe mwaka 2005 ulichagua mchekeshaji ..sasa kwanini akiitwa jangala uje juu....nadhani ....HATA ZE KOMEDY WANAWEZA URAIS..kwa kuwa wakiongea hata walevi hawalali.......wengine huluita ZE comedy!!
Una uhakika?
Mikael, siku zote nilikuona u-mstaarabu sana. Kumwita Kikwete Jangala badala ya Jakaya inahusu nini? After all mwenzio ni President of the United Republic of Tanzania whether you like it or not?
Watanzania bwana, naanza kuamini kuwa tuko tofauti na binadamu wengine - how this came about, I must admit I have no idea at all. Tunaweza tukapewa sifa hata ya "non-existant person" tukamkubali kwamba "he is the best" hata bila kujua kama yupo ama hayupo. Tunaweza kuletewa chizi wa kutupwa lakini maadam hatujui histosia yake kwa ndani, lakini kwa kusadikishwa kuwa anafaa, tukamchagua na kumpa dhamana ya kuongoza taifa.
Na sasa tunadhani Salim angeweza kuwa hata Raisi wa Marekani kwa sababu ya unyenyekevu wake. Pamoja na kuwa ameweza kuwa kiongozi mkuu wa OAU, hakuna legacy yoyote aliyoiacha pale. Jamani katika hii karne kabla ya kumpa mtu uongozi lazima tujiulize kwa lipi.
Naamini kwa historia yetu hii ni ndoto - ndio ukweli unaouma.
Watu kama Dr. Slaa hawana nafasi katika jamii yetu - ndivyo tulivyo.
Nimesoma huu mjadala kiasi fulani nimejifunza vitu vingi; Ila kitu kinachonisikitisha ni tabia ya viongozi wetu kutokushare yale waliyojifunza na wananchi. Mtu kama Salim anatakiwa aandike kitabu kuelezea yale aliyoyafanya na pia aliyokutana nayo. Nadhani itakuwa a fascinating book to read.
Rufiji said:Nimesoma huu mjadala kiasi fulani nimejifunza vitu vingi; Ila kitu kinachonisikitisha ni tabia ya viongozi wetu kutokushare yale waliyojifunza na wananchi. Mtu kama Salim anatakiwa aandike kitabu kuelezea yale aliyoyafanya na pia aliyokutana nayo. Nadhani itakuwa a fascinating book to read.
Rufiji,
..Salim Salim ruled out mpango wa kuandika a memoir, akidai kuna viongozi wengi sana amekutana nao kikazi, na kuna mambo mengi walizungumza naye wakitegemea kwamba hatayaweka hadharani.
..kwa msingi huo basi wanahistoria wanapaswa kuchukua jukumu la kuandika kuhusu ushiriki wa Salim Salim ktk siasa za ndani na nje ya Tanzania.
..tayari kuna vitabu vimeandikwa kuhusu Mwalimu Nyerere na Kawawa. wanahistoria wanapaswa kuandika kuhusu maisha ya Sheikh Abeid Amani Karume, na wa-Tanzania wengine maarufu.
Jasusi,Mwanafalsafa,FMES,....
..je ni kweli kwamba Mkapa alimuomba Salim Salim aje kuwa Makamu wa Raisi baada ya kifo cha Dr.Omari Ali Juma?
..maneno ya mitaani ni kwamba Salim alikataa offer ya Mkapa.
..Dr.Omari alifariki ukiwa umebaki muda mchache sana Salim Salim amalize term yake kama Katibu Mkuu wa OAU.
..kama Salim Salim angechukua nafasi ya Dr.Omar nadhani leo hii tungekuwa tunamzunguzia kama Raisi wa Tanzania.
Mtarajiwa,
Ni habari ulizozisikia lakini hazina ukweli kabisa.. Salim alitakiwa kusimama kama mgombea wa urais wakati wa Mkapa (chaguo la Nyerere).. Akatolewa nje na baraza la mapinduzi iweje tena ampe kazi sehemu ambayo kura zote zilimkataa Salim..basi huyo Mkapa mwenda wazimu..
Kisha zaidi ya hapo Salim ni mjamaa mtu ambaye Mkapa asingemhitaji kabisa...na ndio maana walimtupa nje kabisa baada ya Nyerere kuondoka..
Jamani kuweni na hoja ambazo zinaleta mjadala...
Mtarajiwa,
Ni habari ulizozisikia lakini hazina ukweli kabisa.. Salim alitakiwa kusimama kama mgombea wa urais wakati wa Mkapa (chaguo la Nyerere).. Akatolewa nje na baraza la mapinduzi iweje tena ampe kazi sehemu ambayo kura zote zilimkataa Salim..basi huyo Mkapa mwenda wazimu..
Kisha zaidi ya hapo Salim ni mjamaa mtu ambaye Mkapa asingemhitaji kabisa...na ndio maana walimtupa nje kabisa baada ya Nyerere kuondoka..
Jamani kuweni na hoja ambazo zinaleta mjadala...