Who is INDO Power Solutions na ni nani Bw. Brian Mutembei?

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,750
4,958
Unapoambia fundi seremala kawa mpishi wa Serena Hotel, mtu unaweza tilia mashaka chakula atakachopika.

Nimejaribu sana ku Gogle hiyo kampuni iliyonunua korosho na huyo kiongozi wao aliyetia saini na naibu Waziri, kidogo nimeingiwa na wasiwasi.

1. Kenya kuna kiwanda kimoja tuu cha kubangua korosho kinacho fanya kazi, na ni kidogo sana. Hakiwezi kubangua hata tani 1 kwa wiki.

2. Indo Power haina uzoefu wa biashara ya korosho, na pia haijulikani.

3. Duniani hakuna kiwanda chenye uwezo wa kubangua tani 1 laki . Labda wawe Raw Cashew Traders.

4. Kwanini leo wamenunua korosho kwa bei ya $1800/= kwa tani na hali bei ya korosho ulimwenguni ipo chini wastani qa $1300/= ( west Africa = $1300 - 1400/=, Indonesia $1209/=, India 1450/= ) na tusisahau bado kuna kodi ya 15% ya bei ya ununuzi, usafirishaji nk...

5. Waziri wa kilimo alikwenda UAE kwenye kongamani la korosho, wanunuzi wote wakubwa duniani alikutana nao, inasemekana walishindwana bei, na hakupata hata order ya tani moja.

6. Sasa huyu Bw. Brian Mutembei kweli atakuwa muokozi wetu na malaika, kama hii deal ni ya ukweli, huyu ndugu anastahili medali ya juu Tanzania. Hakuna mfanyibiashara anayeweza kujiingizia hasara, huyu ananunua Korosho yetu kwa $178,000,000, sio mchezo, lakini tuwe macho.

Mwenye kuijua hii kampuni atujuze

=====

Baadhi ya Michango ya Wanachama;

======

===
ILANI:
Sina shida kabisa kama watu hawa wamelipa pesa walizosema watalipa ila endapo hawajatoa pesa na wamekuja kutafuta kiki kwetu ni vyema tuwachambue kwa umakini. Aidha, napata shaka kuwa kuna mtu nyuma ya kampuni hii ambaye soon tutamjua na tutajua lengo lake.
===

Mkuu Mkirindi,

Mimi Intelligence ya siku hizi inanishangaza inavyofanya kazi yake. Hakuna kitu kinasikitisha kama kuwa na Idara ya Usalama inayohangaika kudhibiti wananchi kwa maslahi ya 'tabaka tawala' badala ya kulinda maslahi mapana ya Taifa.

Ninachokijua mimi ni hiki:

1) Kampuni ya INDO Power Solutions imesajiliwa nchini Kenya mwaka 2016 ikionyesha inamilikiwa na watu wawili:
a) Joyce Waithira Gatoho na
b) Alice Wanjiku Gatoho

View attachment 1010458

Lakini, kinachoshangaza kidogo hapa ni kuwa pamoja na uchanga wa kampuni hii; Joyce anayedaiwa kuwa shareholder ni marehemu kitambo sana. Sasa, endelea kunisoma chini uelewe nini maana yake

View attachment 1010459

Ukisoma hapo juu utabaini kuwa Alice kwa mantiki hii ni sole shareholder ambaye akijua wazi kuwa Joyce hayupo hai (kwa nia ovu naweza kusema) aliamua kutumia jina lake ili atimize azma yake.

Taarifa za kampuni hii ambazo nimezipata ndani ya dakika 25 hivi nilitarajia vyombo vyetu vingeweza kuzipata kwa urahisi na kuepusha aibu mbeleni.

2) Twende kwa huyu ndugu Brian Mutembei

Namfahamu huyu jamaa kwa uzuri tu. Brian ni dalali maarufu na kwa waliokaa katika jiji la Nairobi watakuwa wanamfahamu.

Dalali huyu ni mtu wa karibu na Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto (ambaye wakenya wanamjua kama mmoja wa watu mafisadi wa kutupwa).

Brian ana rekodi ya makosa ya jinai na amewahi kufungwa. Kumbukumbu zake zipo kila sehemu (mtu akijiongeza):

View attachment 1010461

Aidha, dalali huyu anajulikana kwa mbwembwe zake za kumwaga mafedha kuonyesha 'jeuri ya pesa' hivyo siwezi kumtofautisha na kina "Ndama Mutoto ya Ng'ombe" au "Jackie Pemba" hivyo yeye kutumika kwenye hili deal haishangazi.

Simsingizii, soma hii story (event hii nzi wetu alikuwepo) na utaona maneno haya hapa:

View attachment 1010475

Naishia hapa kwa leo.

UPDATE, Feb 9, 2019

View attachment 1018644
Habari ya kwamba Indo Power Solutions ya Kenya ni fake lkn ndiyo imesaini deal la kununua tani laki moja za korosho hapa Tanzania, imetrend sana mitandaoni.

Nilitegemea kusikia AG wa Tanzania awe amejiuzulu. Anasubiri nn? Au jiwe ndiye aliwapigia simu?

Indo power Solutions ni kampuni iliyoshinda zabuni ya kuwa mnunuzi wa tani 100,000 za korosho za Lindi na Mtwara kwa bei ya Dola za kimarekani milioni 180. Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Joseph Buchweishaija alisema historia ya kibiashara haikuwa kigezo kikubwa cha kampuni kupewa zabuni.

Gazeti la Kenya la East African lilifanya uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo na kubaini kuwa usajili wa Indo Power Solutions unaonesha ilisajiliwa 2016 hata hivyo haikuwahi kupata zabuni iliyozidi Dola milioni 10. Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Brian Mutembei anajulikana zaidi kisiasa. Kamuni hiyo haijulikani, na ilibainika kuwa walikuwa ni madalali na sio wanununuzi.

Na hata baada ya kushinda zabuni hiyo kamuni hiyo ilienda kutangaza kuuza korosho kwenye tovuti ya Alibaba. Tangazo hilo waliliweka kabla ya kulipia korosho hali iliyoleta sintofahamu kwa watanzania.
 
===
ILANI:
Sina shida kabisa kama watu hawa wamelipa pesa walizosema watalipa ila endapo hawajatoa pesa na wamekuja kutafuta kiki kwetu ni vyema tuwachambue kwa umakini. Aidha, napata shaka kuwa kuna mtu nyuma ya kampuni hii ambaye soon tutamjua na tutajua lengo lake.
===

Mkuu Mkirindi,

Mimi Intelligence ya siku hizi inanishangaza inavyofanya kazi yake. Hakuna kitu kinasikitisha kama kuwa na Idara ya Usalama inayohangaika kudhibiti wananchi kwa maslahi ya 'tabaka tawala' badala ya kulinda maslahi mapana ya Taifa.

Ninachokijua mimi ni hiki:

1) Kampuni ya INDO Power Solutions imesajiliwa nchini Kenya mwaka 2016 ikionyesha inamilikiwa na watu wawili:
a) Joyce Waithira Gatoho na
b) Alice Wanjiku Gatoho

INDO-Powe-Solutions(KE).jpg

Lakini, kinachoshangaza kidogo hapa ni kuwa pamoja na uchanga wa kampuni hii; Joyce anayedaiwa kuwa shareholder ni marehemu kitambo sana. Sasa, endelea kunisoma chini uelewe nini maana yake

Joyce_Gatoho_DEAD.jpg

Ukisoma hapo juu utabaini kuwa Alice kwa mantiki hii ni sole shareholder ambaye akijua wazi kuwa Joyce hayupo hai (kwa nia ovu naweza kusema) aliamua kutumia jina lake ili atimize azma yake.

Taarifa za kampuni hii ambazo nimezipata ndani ya dakika 25 hivi nilitarajia vyombo vyetu vingeweza kuzipata kwa urahisi na kuepusha aibu mbeleni.

2) Twende kwa huyu ndugu Brian Mutembei

Namfahamu huyu jamaa kwa uzuri tu. Brian ni dalali maarufu na kwa waliokaa katika jiji la Nairobi watakuwa wanamfahamu.

Dalali huyu ni mtu wa karibu na Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto (ambaye wakenya wanamjua kama mmoja wa watu mafisadi wa kutupwa).

Brian ana rekodi ya makosa ya jinai na amewahi kufungwa. Kumbukumbu zake zipo kila sehemu (mtu akijiongeza):

BrianMutembei.jpg

Aidha, dalali huyu anajulikana kwa mbwembwe zake za kumwaga mafedha kuonyesha 'jeuri ya pesa' hivyo siwezi kumtofautisha na kina "Ndama Mutoto ya Ng'ombe" au "Jackie Pemba" hivyo yeye kutumika kwenye hili deal haishangazi.

Simsingizii, soma hii story (event hii nzi wetu alikuwepo) na utaona maneno haya hapa:

BrianMutembeiKE.jpg

Naishia hapa kwa leo.

UPDATE, Feb 9, 2019

A95275B8-0BE7-4919-9771-23564E3A84B3.jpeg
 
Geresha. Mkataba utakuwa feki ili sifa zipatikane. Hizo korosho anazichukua kwa robo bei kwani zinaozeana na kuota huko walikozilundika.

Tatizo CAG hatahisika kukagua haya mauzo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana huo ni uongo na unafiki, Wako watu tayari kununua kwa $1400 -1500/=, haiwezekani kwa robo bei. Korosho za Tz ni bora kwa ukubwa na uzito

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kampuni ya RICHMOND iliyoingia mkataba na Serikali ya Tanzania kwani ilitokea wapi...??

Ukilijua hilo basi usiwe na hofu kwanini hiyo kampuni ya kununua hizo tani laki moja imekuja pasikojulikana....

Eaters are within us.
Very true, but we need to be cautious, mkulima wetu apate chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana huo ni uongo na unafiki, Wako watu tayari kununua kwa $1400 -1500/=, haiwezekani kwa robo bei. Korosho za Tz ni bora kwa ukubwa na uzito

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkirindi nisaidie. Wasomi wa nchi hii siwaelewi. Nahisi na wewe mmoja wao. Tukiache Kiingereza cha ajabu ulichoandika hapo chini. Ulishikiwa fimbo! Haikuwa lazima kuandika yasoeleweka. Hukuyaona? Ungefanya editing angalau. Bei hata iwe kamili, tumefikaje huko? Hii ndio kununua korosho zote kwa siku tatu? Kuna aliyemlazimisha? Mbwembwe kibao. Makofi na maandamano ya pongezi vimeishia wapi? Wasomi wa nchi hii huona mwisho wa pua. Palamagamba anaaminisha watu tutakaa na Barrick kugawana faida pasu kwa pasu. Alikuwa anatoa macho huyo. Nilihisi Kiswahili kinampa tabu Prof kazoea Kiingereza. Nikamwamini. Tukapiga hesabu ya Noah. Ndoto mbaya sana ilipita. Jinamizi. Labda kama umo kwenye rindi la ujinga unaweza tetea sakata la korosho kama Mkirindi!
 
hahahahah naona umepata wivu kweli..... bora unywe sumu lakini korosho zimesha nunuliwa hahahahaha
Kuhusu wewe yatosha tu kukwambia Rutashobolwa=Rutashobokelwa. Kudanganya ni dhambi. Kudanganya mtu mwingine ni balaa. Kujidanganya mwenyewe nuksi. Naona hata kujicheka mwenyewe umeanza. Mkosi mkubwa. Hata hivyo nilitaka maelezo kutoka kwa wasomi. Unaingiza rindi lako la ujinga kwenye usomi? Kweli sio kila Rutta ni nshomile.
 
Mkirindi nisaidie. Wasomi wa nchi hii siwaelewi. Nahisi na wewe mmoja wao. Tukiache Kiingereza cha ajabu ulichoandika hapo chini. Ulishikiwa fimbo! Haikuwa lazima kuandika yasoeleweka. Hukuyaona? Ungefanya editing angalau. Bei hata iwe kamili, tumefikaje huko? Hii ndio kununua korosho zote kwa siku tatu? Kuna aliyemlazimisha? Mbwembwe kibao. Makofi na maandamano ya pongezi vimeishia wapi? Wasomi wa nchi hii huona mwisho wa pua. Palamagamba anaaminisha watu tutakaa na Barrick kugawana faida pasu kwa pasu. Alikuwa anatoa macho huyo. Nilihisi Kiswahili kinampa tabu Prof kazoea Kiingereza. Nikamwamini. Tukapiga hesabu ya Noah. Ndoto mbaya sana ilipita. Jinamizi. Labda kama umo kwenye rindi la ujinga unaweza tetea sakata la korosho kama Mkirindi!
Sijakuelewa, if u r quoting me kuhusu kuwa haiwezekani bei iwe a quater of the price mentioned in the media, than we are spreading lies na unafiki.

Kama umewahi kusom michango yangu kwenye hili sakata la korosho basi ungejua msimamo wangu. I am an authority on ghis issue la biashara ya korosho. Mimi nimekuwa nikinunua minada ya ushirika na kusafirisha kadri ya uwezo wangu, so i know the market.

Ninaunga mkono serekali kuwatetea wakulima, lakini the way they are handling the situation is very pathetic. Kuna mengi wamekosea, hawakuwa n planning ya maana ama madhubuti.

Leo serekali ikitangaza bei ya $1500 hadi $ 1600/= ,itanunuliwa within 10 bays, lakini ifikapo feb 21 bei itaanguka, kwani mavuno ya India yataingia sokoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kampuni ya RICHMOND iliyoingia mkataba na Serikali ya Tanzania kwani ilitokea wapi...??

Ukilijua hilo basi usiwe na hofu kwanini hiyo kampuni ya kununua hizo tani laki moja imekuja pasikojulikana....

Eaters are within us.

Sent using Nokia 8 Plus
Labda amesahau kuwa Rostam alienda magogoni na ana biashara zake kenya
 
Back
Top Bottom