Who is General Nkunda?

Poleni sana.I frankly don't know why you become fascinated by these childish games of the the West.Look here, Nkunda's assignment has been completed,that is why they are "pretending" to arrest him.They are now going into a new phase of the game!Wait and see.

I tend to agree with you on this. I am sure that with New kid in oval office the security of Nkunda was in line. I do not see Rwanda arresting one of her pawns who was dancing according to the Kigali tune, if he has been arrested then he has been "arrested" because of his security, not because he was wanted in custody. He is wanted by Kinshasa not by Kigali, he did harm to Kinshasa and not to Kigali, why would they want him arrested? You may wonder his detantion cell may be like those luxurious ones in Keko. Kagame has started to behave like we Tanzanians.
 
Safi sana, nadhani vita vya DR Congo vitaisha. Kinachonishangaza na kunifanya nijiulize maswali ni: Urafiki huu wa ghafla wa Rwanda na DR Congo dhidi ya Nkunda umekujaje?

Nami nasema safi sana. Lakini sidhani kukamatwa kwake kumekuja hivihivi tu. Kwanza, ni hili suala la Wahutu wa Kinyarwanda walioko Congo. Kinshasa na Kigali wamekubaliana wanyang'anywe silaha. Kumbuka Kinshasa ilikuwa haipendi wanyang'anywe mwanzoni kwa sababu walikuwa wanasaidia upande wa serikali dhidi ya majeshi ya upinzani na majeshi ya rwanda wakati ule na vikundi vya upinzani dhidi ya serikali ya Kinshasa. Nkunda anajua wakinyang'anywa silaha atakuwa hana sababu ya kuueleza ulimwengu kuhusu kuwepo kwake na kujidai analinda jamii ya Kitusi iliyoko Congo. Pili, inawezekana kabisa Nkunda na viongozi wa Rwanda wamezikana kwenye biashara ya almasi, colbat na madini mengine. Bila kusahau mbao. Vyote hivyo vilikuwa vinapitishwa Rwanda wakati wa kupelekwa nje. Tatu, Kitu kingine ambacho kinaweza kufanya akamatwe ni kile kilichoandikwa na mwandishi mmoja jana kuwa Nkunda alishakuwa "flippant" na "megalomaniac". Nina uhakika kama umewekwa mahali kuwa henchman na ukabadilika basi waliokuweka watakuondoa tu. Alishakuwa "liability" kwa serikali ya Rwanda.
 
Nkunda hakuwa Mkuu wa majeshi ya CNDP, alikuwa mwenyekiti tu, hivi karibuni aliondolewa madarakani kwa kupinduliwa na Mkuu wa Majeshi (Bosco Ntaganda). Nkunda alifanikiwa kukimbia akiwa na askari wachache kama 3,000 hivi kati ya askari zaidi ya 10,000. Huyo Bosco akawaambia bbc wasubiri muda si mrefu itajulikana kwamba Nkunda hayuko nao, thats revealed now. Hivyo mimi sioni cha kufurahia kwani huyo Bosco ndo anakuwa na nguvu zaidi sasa. Hapa kuna kamchezo tu kanachezwa.

Si unaona hata yale mazungumzo ya akina Mkapa na Obasanjo hayana maana tena kwani Bosco hataki mazungumzo. Silaha zote za Nkunda zimebaki kwa Bosco.
 
Tutatoa sababu nyingi za kweli na zisizo za kweli ila ukweli unabaki kuwa hakuna marefu yasiyo na nchi,labda ndugu zetu watapumzika kidogo. Mungu awajalie majirani zetu heri.
 
Wamesema kuwa watampeleka Congo. Sasa sijui ukweli uko wapi kama wanacheza game au lah. Lakini kwa hili la Wahutu kunyang'anywa silaha, litafanya Rwanda waingie (wameshaingia) kwenye vita huko Congo. Nafikiri hata Kagame hizi vita kashachoka. Anyway kama wamezikana au lah, wananchi wanasema "kifo cha panzi ..." Hii vita ina umri zaidi yangu na imeshakula vichwa zaidi ya milion 5. Imebaki kidogo ifikishe idadi ya Wayahudi waliouliwa na Wageruman. Na katika vichwa ilivyokula ni vivhwa vikubwa sana yaani Katibu mkuu wa UN, Lumumba, Kabila na wanachi kibaoooo...

Ila hata Savimbi ilikuwa hivyohivyo. Walimtungua na kumburuza kama LIMZOGA. Na hadi leo Angla wanatesa tu kwenye michezo na ki-uchimi.
 

Obama amesema
wazi kabisa kuwa hatavumilia viongozi wanaotegemea ufisadi kukaa madarakani, pia hatakubali marekani (makampuni yake) yatumie raslimali za dunia bila kujali madhara yake. Katika hali hiyo hayo makampuni yaliyokuwa yanamsupport Nkunda na serikali ya Rwanda yamejikuta yapo on the wrong side of history. Obama amesema wakibadilika tutawafungulia mikono wasipobadilika wataenda na maji.
Huo ni mwanzo; Raslimali za DRC haziwezi kuendelea kuwanufaisha wanyarwanda na makampuni ya nje na kundeleza vita DRC wakategemea Obama atakaa kimya. Angalia pia mchango wangu katika thread ya Hotuba ya Obama Full text ktk international forum.

"Obama amesema," Obama ni nani, ndie yule mfalme wa wana wa Israeli ajae kuokoa uzao wa mataifa?

Mbona hakukuwa na ufufuo wa wafu siku alipovikwa taji juu ya vyote ardhini na mbingu na chini baharini?

"Obama amesema hatavumilia..."!
 
Poleni sana.I frankly don't know why you become fascinated by these childish games of the the West.Look here, Nkunda's assignment has been completed,that is why they are "pretending" to arrest him.They are now going into a new phase of the game!Wait and see.

Kwa Kauli ya Kagame mwenyewe alishakanusha kuwa na uhusiano na Nkunda wala kumfahamu za ya kumuona kwenye Luninga kama wamuonavyo wengine. Sasa yeye anam arrest pasipo kumfikisha kwenye vyombo vya UN ili achukuliwe hatua? Pasipokufanya hivyo kwamba ni mkakati wa nia njema kwa DRC?.

Kagame amesoma alama za nyakati. Jumuia ya Kimataifa ilikuwa against Nkunda na Kagame na ilishaanza kugundua ushirika wao.

Hakika Nkunda amekamilisha kibarua chake alichopewa na Kagame !
 
Hi ni kwa nini Kagame amemgeuka?

Safi sana, nadhani vita vya DR Congo vitaisha. Kinachonishangaza na kunifanya nijiulize maswali ni: Urafiki huu wa ghafla wa Rwanda na DR Congo dhidi ya Nkunda umekujaje?

...naona kama changa la macho tu...

kakamatwa akiwa njiani kukimbilia Rwanda?, huh!!! ...let 'em handover him kwa serikali ya Congo tuone.
 
...naona kama changa la macho tu...

kakamatwa akiwa njiani kukimbilia Rwanda?, huh!!! ...let 'em handover him kwa serikali ya Congo tuone.

bbc jioni hii wameeleza vizuri, amekamatwa kwa msaada wa aliyekuwa mkuu majeshi yake Bw. Bosco Ntaganda. Huenda sasa amani ikapatikana Kongo.
 
Si kumkamata tu,naona bora wangemwua kabisa kuliko kumpandisha kizimbani,hawa ndio dictetor wa Africa,na wanotumia kuturudisha nyuma,nashauri wampige shaba mapema kama ilivyokuwa kwa Jonas Savimbi.
 
that is perfect, watu wakiwa madarakani bwana hawajali kabisa nafsi ya wanajamii ndio hawa akina Nkunda, na aende Haag huyo akakione hata kama malipo ya mauaji aliyo ya fanya kamwe hayalipiki, cha msingi yeye asiendelee kutanua na kujiona Generali mbabe wakati amesababisha vifo vya maelfu ya wasiona hatia.
 
kijamaa chembambaaaaa kikorofiiii korofiiiiiii
Kagame kamgeuka
 
that is perfect, watu wakiwa madarakani bwana hawajali kabisa nafsi ya wanajamii ndio hawa akina Nkunda, na aende Haag huyo akakione hata kama malipo ya mauaji aliyo ya fanya kamwe hayalipiki, cha msingi yeye asiendelee kutanua na kujiona Generali mbabe wakati amesababisha vifo vya maelfu ya wasiona hatia.

Unamaanisha The Hague in the Netherlands siyo?
 
KUKAMATWA KWA NKUNDA KUSICHUKULIWE KUWA NI MWISHO WA VITA DRC.
BADO WAFUASI WAKE HAWAJA NYANGANYWA SILAHA.
Exaud J. Makyao
 
Profile: General Laurent Nkunda Rebel commander Laurent Nkunda studied psychology at university Rebel General Laurent Nkunda has long sought to portray himself as the only man who can protect his Tutsi community in eastern Democratic Republic of Congo from Hutu forces

This led to accusations that he was a stooge of the Tutsi-led Rwandan government. But in a surprising about-turn, it is the Rwandans who have finally arrested him.

- Nimesikiliza kwa makini sana waziri wa habari wa Congo, Kinshasa akihojiwa na BBC, amesema kwamba hivi karibuni Kabila alifanya mabadiliko ya cabinet, na kuingiza mawaziri wengi wapya akiwemo wa nje na ulinzi, ni hawa mawazri wawili wapya ndio waliokuja na a new plan ya kushirkiana na Kagame for the best of their nation and its people. Na ni only last week waliruka na kwenda Kigali ku-make a deal na Kagame, ya kumruhusu kuingia Congo na kutafuta the Hutu's na wao wakamtaka awape Nkunda, na pia wakaamua kuanzisha jeshi la pamoja la kuhakikisha amani huko Eastern Congo.

- Nkunda amekuwa akipoteza nguvu za uongozi wake katika majeshi yake kutokana na tabia zake mbaya za ubinafsi, wanajeshi wake walianza kumgeuka kitambo sasa wakiongozwa na chief wake of staff bwana Bosco, ambaye sasa yeye na wanajeshi wote wamejiunga na jeshi la Congo.

Waziri huyu amesema kwua ni a matter of time kabla Nkundahajakabidhiwa Kinshasa. Kama ni kweli tunasema saafi sana maana sio rahisi kumuamini Kagame ana michezo mingi sana ya kutawala.
 
......hii ni strategy ya kina Kagame kuokoa CNDP wasaidiane kuwatandika hutu extremist waliojificha Congo,Nkunda hana command tena ndani ya CNDP maana wanajeshi wengi wanamsikiliza Ntaganda,na tatizo lingine alianza story za kupiga mpaka kinshasa wakati nia ya CNDP ni safety ya banyamurenge,sasa Ntaganda,Congolese army na Rwandese forces kazi yao ni moja tuu kuwafagia hutu extremist na ndio wanachofanya sasa...sometimes to sacrifice one of your guy ili kupata amani kwa milions sio kitu mbaya,lakini sioni Kagame akiwakabidhi huyu jamaa Kinshasa,labda UN pressure ikiwa kubwa
 
Back
Top Bottom