While Zitto is being attacked pls read here

While Zitto is being attacked pls read here

Chintu, usichanganye mambo. Msimamo na fikira ni vitu viwili tofauti kabisa. Kama chama tunapaswa kuwa na msimamo mmoja katika mambo ya msingi, lakini hatupaswi kufanana kifikra. Narudia tena, ni ujinga wa kutisha kutaka Watu wafanane kifikra kwa sababu ni kujaribu kywafanya wasiwe binadamu!

M4C ni jambo la msingi na ni dira ya kukijenga chama nadhani unatakiwa umshauri ZITTO aungane na wenzie kujenga chama sababu kama kufikiri tofauti ni kuacha kukitumika chama na kwenda kuzunguka na SPIKA na kufanya mikutano ya mara kwa mara na KIKWETE basi ni bora afikiri kitofauti kwa niaba ya familia yake si CHADEMA.
 
Mkuu nadhani utakubaliana na mimi kua hiyo sera ya ukweli na uwazi ilikua katika maneno tu
na si katika matendo. Sisi tunataka sera ya ukweli na uwazi katika matendo na si katika maneno.

Sasa swali la kujiuliza ni je Sera hii hii ya Uwazi na Ukweli ambayo iliimbwa sana na Serikali ya awamu ya tatu chini ya CCM na haikuwekwa kwenye vitendo itatekelezwaje chini ya Serikali ya watu walewale na wa chama kilekile? Ndiyo maana watu wanahoji Zitto anautafutaji Uwazi kwenye mikataba ya madini/nishati kwenye Serikali ya watu walewale na chama kilekile kilichoshindwa kuiweka kwenye vitendo Sera ya Ukweli na Uwazi? Tafakari.
 
Mwambie ZItto akuambie yeye Ana mahusiano gani na hayo makampuni ya kutafuta Mafuta na Gesi , MWambie akuambie yeye ni nani kwa MKono ADvocate na anahusika vipi na mikataba husika , akishakuambia njoo hapa umtetee! Nasubiri ajiingize kwenye 18 zaidi. Tafakari

Nasema tena nasisitiza kwako Kitila ambae ni rafiki mkubwa sana na ZItto KAbwe , mwambie akuambie yeye Kama mshauri maelekezo ( consultant) wa MKono anamasilahi gani kuhusiana na mikataba iliyosainiwa? Alishiriki kwa kuwa go gani? Je? Alikoenda na kukutana na baadhi ya mabalozi Jana aliongea nini na wanufaika aw mafuta na gesi alipokuwa na nao? Chunguzeni hili jambo ni kubwa kuliko

bora umesema..unajua watanzania tuna ushabiki tu..mtu akiwa na 5mins of fame basi kila mtu anamshabikia hatujui really nini kinachoendelea behind the scenes...kila mtu alikua anasema JK ni mtu wa watu kijana mwenzetu atamtoa kila mtanzania kwenye umaskini..akapewa kura zote zile 2005...i think we all know what happened next!!
 
Watu wanamchukia Zitto bila sababu yoyote ile

Sidhani kama kuna mtu anayemchukia Zitto Kama Zitto. Kinachochukiwa kutoka kwa Zitto ni tabia yake ya kukubali kununuliwa kirahisi. Zitto anadhani peke yake anaweza kuleta mabadiliko katika Nchi yetu. Kupata mabadiliko ya kweli; Lazima aunganishe nguvu zake na zawenzake ili ushindi wa kweli upatikane. Dhambi ya kupanga mipango ya kuihujumu CDM lazima imwandame hadi mwisho wa maisha yake. Anatamani sana kuanza kutembea kabla ya kuanza kutambaa. Zitto lazima atambue kuwa maisha ni hatua na haihitaji haraka kwani mambo mazuri lazima yaje kwa wakati.
 
M4C ni jambo la msingi na ni dira ya kukijenga chama nadhani unatakiwa umshauri ZITTO aungane na wenzie kujenga chama sababu kama kufikiri tofauti ni kuacha kukitumika chama na kwenda kuzunguka na SPIKA na kufanya mikutano ya mara kwa mara na KIKWETE basi ni bora afikiri kitofauti kwa niaba ya familia yake si CHADEMA.

Tatizo la Zitto anauota Urais hata akiwa barabarani anatembea. Tamaa ya fisi.
 
Zitto aachane na Mkono!

Kuna interests nyingi nyuma ya jitihada hizi japo ni kwa maslahi ya Taifa lakini ni vigumu sana kwa ZZK kuaminika for the time being!
 
KWA HIYO TUNAJADILI JINA la ZITTO ZUBERI KABWE(MBUNGE) AMA ISSUE?KWA TAARIFA YENU UKITAMKA REVIEW KWA WACHIMBA MADINI WAKIJUA UNA NGUVU FULANI WANAKUTUMIA UJUMBE WA KHERI HAPO HAPO NA UKIZIDI KUKUNJA SHINGO WATALETA AJALI,MAJAMBAZI AMA SUMU YA RUSSIA,HILO NENO REVIEW LIMEWATAJIRISHA WENGI!
 
... ??????????????????????????

KWA HIYO TUNAJADILI JINA la ZITTO ZUBERI KABWE(MBUNGE) AMA ISSUE?KWA TAARIFA YENU UKITAMKA REVIEW KWA WACHIMBA MADINI WAKIJUA UNA NGUVU FULANI WANAKUTUMIA UJUMBE WA KHERI HAPO HAPO NA UKIZIDI KUKUNJA SHINGO WATALETA AJALI,MAJAMBAZI AMA SUMU YA RUSSIA,HILO NENO REVIEW LIMEWATAJIRISHA WENGI!
 
The problem with our hero is his inconsistency over the same issue. He was vociferous in the forefront to demand review of the same contracts he pointed out to Tanzanians as unfair, corrupt and that benefited investors more than us. And he did this with the full backing of his party to which he was and is still the Deputy Sec Gen.

Today he comes with a different stance that appears to be pro investors, this time without the official backing of his party. A common thinker has to ask him/herself what made this same man contradict his stance within a short spell of time.
This is what makes Tanzanians to act cautiously with our once super hero.
 
Tatizo la Zitto anauota Urais hata akiwa barabarani anatembea. Tamaa ya fisi.

Katongozwa katongozeka sana kwa kubinyiwa jicho tuu na MSACKY..sasa anaota ndoa na tamaa zake zinazidi kua hakuan cha kukata kiu,anaamini ndoa tuu ndio itakaa hiyo kiu.Huku ajajua tofauti ya "infatuation" na "Love" kwa i dunia yake inakimbia haraka sana,tena sana kiasi cha kumfanya ashindwe tofautisha sana mambo.
 
Moja ya matatizo yetu kama nchi na wananchi ni kuchukia watu wanaofikiri tofauti. Tumezoea mazoea; ukiona mtu anaenda tofauti na mazoea tunaanza kumpa majina kibao: kanunuliwa, msaliti, anajipendekeza, hana ushirikiano, n.k.. Lazima tubadilike na kujua kwamba binadamu tu tofauti kimwili, kiakili na kila kitu. Ili tutoke hapa tulipo lazima turuhusu akili zifikirii sawasawa na tena tuhangaike kufikiri kitofautitofauti. Kama tunataka kila mtu afikiri kama sisi ni kuendeleza utamaduni wa kutumia akili za kuazima. Zitto ni miongoni mwa watu wachache hapa nchi aliyeamua kujipambanua na kuamua kufikiri kitofautitofauti. "Kosa" lake ni kwamba ameamua kuacha kufanya mambo kwa mazoea na ameamua kuhangaika kufikiri kitofautitofauti. Zitto analaaniwa kwa kudiriki kwake kuhangaika kufikiri na kuachana na mazoea. Atabambikizwa majina yote ya ovyo kama usaliti, kujipendekeza, n.k. Tunamtia moyo aendelee kuhangaika kufikiri, wapo watakaomuelewa.

Mkuu Kitila naomba nitofautianae na mtazamo wako kwasababu kuu moja kumekuwa na kundi ambalo linatumia hizo movement za zitto kuudharirisha uongozi wa juu wa CDM kama Mbowe, Dr Slaa, BAVICHA, mambo ya udini na ukanda ktk chama na hiyo ndio imesababisha zitto aonekane mnafki na majina mengi. Nyie kama viongozi mnatakiwa muangalie hizo weakness kwa ustawi wa CDM.
 
Hivi niulize swali moja ambalo sijawahi kusikia mtu akilizungumzia. Kuna wakati wowote Zitto amewahi kuzungumzia siasa za Ukanda na Udini ndani ya Chadema?
 
Kosa la zito ni moja na dogo 2 na anaweza kujirekebisha,ni kupenda kusimama pembeni ya chama,haya mambo yote anatakiwa kuyafanya kwa kushirikiana na chama na kupata ushauri na baraka za chama.kutofanya hivi kunaleta wasiwasi juu ya maslahi aliyonayo huko mpaka afanye peke yake au kwa kushirikiana na watu wanaojulikana kwa uchafu wao (mafisadi).
 
Naona Zitto anatafuta mbinu ya Julias Marema maana amepoteza supporters wengi kwenye chama chake

Je hii mbinu yake ya kutaka kureview hii mikataba itamsadia?

Just doing for the sake of a poor country and your grandsons. Polepole mtamuelewa tu.
 
i don't know who to believe anymore..and kitila's statement ,somehow,i mean wassira is almost right,let's pray the party is not broken into pieces before 2015..
 
Great thinker naona wengi wameanza poteza muelekeo na wamekuwa waongeaji sana bila vitendo na wengine wamekuwa hata wasemaji wa vyama au kundi la watu, mimi ningependa kuona mwaleta ushahidi za tuhuma za zzk hapa si porojo na kama mnasema yupo karibu na serekali na chama kimekuwa kimya then kunajambo kina pata kwa ukaribu huo wa zzk na serekali, pia watu wengi mnapiga porojo za m4c kwa zzk but mimi najua wabunge wengi sana wa chadema ambao hawafanyi shughuli hii ukianza na shibuda then why zzk? Pia kwenye chaguzi zote ndogo za wabunge na madiwani zzk huwa hakosi je hapa anatumikia chama gani? Mwisho Kama zzk ni mzigo hope chama kingekuwa kimesha mwita na kumuonya juu ya uwajibikaji wake but sijawahi sikia mwenyekiti wala katibu mkuu wakimnyoeshea kidole zzk then nyie Mliyo nje ya chumba mtikisiko wa kitanda unawatisha nini ? chadema nw is strong than ever let us know new face and talent, so zzk atulie na afanye anayo fanya kwani na imani chama kinanufaika kwa anayoona huko serekalini
 
Rafiki yangu Mkumbo heshima mbeeeele kama tai kwanza kwako na kwa mwenzetu Zitto Zuberi Kabwe. Ila tu nikutahadharishe mkuu; huyu Zitto umuonaye wala si yule wa wakati ule wa harakati za kweli na wala usipoteze muda wako kwani hatuwezi kumpata tena.

Hakika tumempoteza mpiganaji kwa kujichagulia kujiunga na manyang'au wa uchumi wa nchi hii kwenda kuficha Uswisi.
Kwanza nimpongeze kakangu Dr. Mkumbo kwa jinsi alivojaribu kufafanua juu ya alivyo zito. Mi nafikiri tusiwe na conclusive statements juu ya Zitto kisa tu eti anafikiri tofauti na sisi, hatutaenda haki kwa Ndg yetu Zitto hata kidogo. Zitto ni mwanasiasa mchanga wengi wanaomfahamu toka yuko sekondari na Chuo pale mlimani ni mtu makini anayependa kusimamia anachokiamini, na mda mwingine huwa yuko tayari hata kusimama peke yake kutetea anachokiamini na hii ndio sifa kubwa ya viongozi wengi duniani ilimradi tu anachokisimamia na kukiamini kiwe na maslahi kwa waliowengi. Tumeona hivyo kwa Mwal. kipindi cha uongozi wake kuna kipindi aliotofautiana na wenzake ndani ya chama akawambia CCM sio mama yake kwa kuwa alijua anachosimamia, vivyo hivyo mapema miaka ya mwanzoni kuna hata waliotaka kumpindua kwa kufikiri tofauti na yeye. Na kwa CDM mimi nafikiri ili chama hiki imara kiwe imara we need a diverse of views and sometimes our ideas may differ as far as we think differently. Zitto asihukumiwe kwa lolote kwa sasa, personaly bado namuona Zitto kama kiongozi shujaa, makini, visionary, mzalendo, na wa mfano kwa vijana wengi na ambae atakisaidia sana chama huko mbele. Mfano mzuri ni katika kutetea rasilimali za nchi kutonufaisha wachache. Tutafute taarifa sahihi kumhukumu kiongozi huyu sio uvumi unaletwa na wasioitakia mema CDM tutakuja kujuta baadae.

Na kwako zitto huu ni wakati wa changamoto ndio wakati wa kusimama imara katika kuwatumikia watanzania, tunakuamini chapa kazi.
 
Back
Top Bottom