Moja ya matatizo yetu kama nchi na wananchi ni kuchukia watu wanaofikiri tofauti.
Tumezoea mazoea; ukiona mtu anaenda tofauti na mazoea tunaanza kumpa majina kibao: kanunuliwa, msaliti, anajipendekeza, hana ushirikiano, n.k.. Lazima tubadilike na kujua kwamba binadamu tu tofauti kimwili, kiakili na kila kitu.
Ili tutoke hapa tulipo lazima turuhusu akili zifikirii sawasawa na tena tuhangaike kufikiri kitofautitofauti. Kama tunataka kila mtu afikiri kama sisi ni kuendeleza utamaduni wa kutumia akili za kuazima.
Zitto ni miongoni mwa watu wachache hapa nchi aliyeamua kujipambanua na kuamua kufikiri kitofautitofauti. "Kosa" lake ni kwamba ameamua kuacha kufanya mambo kwa mazoea na ameamua kuhangaika kufikiri kitofautitofauti. Zitto analaaniwa kwa kudiriki kwake kuhangaika kufikiri na kuachana na mazoea. Atabambikizwa majina yote ya ovyo kama usaliti, kujipendekeza, n.k. Tunamtia moyo aendelee kuhangaika kufikiri, wapo watakaomuelewa.