While Zitto is being attacked pls read here

While Zitto is being attacked pls read here

I would never waste my valued time criticising a leader whom I do not have HIGH REGARDS TO.

Therefore by shear dint of the fact that most of us here would never hesitate off-loading scarthing attacks on certain UNBECOMING CHARACTER TRAITS IN OUR LIFE-LONG FRIEND, ZITTO ZUBERI KABWE, that simply owes to the fact that he matters a lot to us thence no slightest wayward veering would go unscrutinised thoroughly about this gentleman, Dr Mkumbo and even Dr Slaa himself.

Constructive criticism is here to stay those who matter a lot to us, and Zitto for one in this instance. I, for one, would always NOT HESITATE, today or tomorrow, to turn RED HOT on any of the political leaders that Iplace of an exceptional stature, only choosing to become FAST-RATE POLITICAL MERCHANTS of some sorts, perfectionists in DOUBLE-SPEAK, and a bull of a lion in INCONSISTENCIES, LONE-RANGING and unwarranted popularity seeking tendencies.

Naam, in a nutshell, Zitto can still be a VALID CHAQUE to cash on some days as long as he resets his new-found political passions into a public-friendlier social justice warrior with predictable steps and dependable moves both in public eye or in private.

Gentlemen, if you truely have so political love for our buddies like Kitila Mkumbo, John Mnyika, William Malecela, Zitto Kabwe, Deus Malya, Muhingo Rweyemamu, Mzee Mwanakijiji and the like, TELL THEM THE MOST CHOKING TRUTH so that only truth and truth alone remain the strong foundation of your friendship and NOT otherwise.


Kwanza nimpongeze kakangu Dr. Mkumbo kwa jinsi alivojaribu kufafanua juu ya alivyo zito. Mi nafikiri tusiwe na conclusive statements juu ya Zitto kisa tu eti anafikiri tofauti na sisi, hatutaenda haki kwa Ndg yetu Zitto hata kidogo. Zitto ni mwanasiasa mchanga wengi wanaomfahamu toka yuko sekondari na Chuo pale mlimani ni mtu makini anayependa kusimamia anachokiamini, na mda mwingine huwa yuko tayari hata kusimama peke yake kutetea anachokiamini na hii ndio sifa kubwa ya viongozi wengi duniani ilimradi tu anachokisimamia na kukiamini kiwe na maslahi kwa waliowengi. Tumeona hivyo kwa Mwal. kipindi cha uongozi wake kuna kipindi aliotofautiana na wenzake ndani ya chama akawambia CCM sio mama yake kwa kuwa alijua anachosimamia, vivyo hivyo mapema miaka ya mwanzoni kuna hata waliotaka kumpindua kwa kufikiri tofauti na yeye. Na kwa CDM mimi nafikiri ili chama hiki imara kiwe imara we need a diverse of views and sometimes our ideas may differ as far as we think differently. Zitto asihukumiwe kwa lolote kwa sasa, personaly bado namuona Zitto kama kiongozi shujaa, makini, visionary, mzalendo, na wa mfano kwa vijana wengi na ambae atakisaidia sana chama huko mbele. Mfano mzuri ni katika kutetea rasilimali za nchi kutonufaisha wachache. Tutafute taarifa sahihi kumhukumu kiongozi huyu sio uvumi unaletwa na wasioitakia mema CDM tutakuja kujuta baadae.

Na kwako zitto huu ni wakati wa changamoto ndio wakati wa kusimama imara katika kuwatumikia watanzania, tunakuamini chapa kazi.
 
Wajameni hebu tuendelee kuchambua mambo ya msingi humu ndaani ya JF tujaribu kuleta nyuzi ambazo zitasaidia kupata ufumbuzi wa mambo madogo madogo hadi yale makubwa na tuache kujadili vitu ambavyo havina tija na maendeleo ye nchi yetu tukumbuke kuwa 2015 ni mbali/simbali so kuhusu kauli za Mh Zitto Zuberi Kabwe zisituweke busy na tukaacha kuchambua mambo yenye tija kwa wakati huu pia tukumbuke kuwa CHADEMA kina katiba ambayo ndio inaongoza kupata viongozi so kwa nini enyi watu/wabongo mnashadadia kila kitu/mtu akiibuka tu na kusema mie nitagombea Urais basi watu matumbo motooo Lol!!hivi kwa nini tunakuwa hivi wajameni hebu tumuuache Mh Zitto Zuberi Kabwe aendelee na mambo yake huu sio wakati wa kupata nani agombee URAIS
Kama kipindi kikifika na akachaguliwa kugombea Urais basi si haba tutampa kura zetu si ndio Makamanda so now hebu leteni nyuzi kali ili tuzichambue kikubwa na kisomi zaidi hili la ooh mie nitagombea Urais tuliache kwani kipindi kikifika tutaona nani anafaa na nani hafai finito.
Kila mtu ana haki ya kusema mie nitagombea Urais kwani ndio ile tunaita fredom of speech kama sikosei hapa kuna wasomi huenda wakaweka mambo sawa zaidi kuhusu masuala ya kujieleza.
 
Acha upuuzi, umetumwa na Zitto? Hujui kuwa" Mchelea mwana kulia, hulia yeye? Tumwache zitto aendelee kutusumbua?? Hatukubali, kwa umoja wetu na nguvu zetu tutamkabili mpaka tumtokomeze kabisa.
 
Kiongozi siku zote lazima ajue anaongoza nini na anaowaongoza wakoje. Zito zuberi Kabwe ni kati ya viongozi wa chadema walioshiriki bila shaka kuing'arisha nyota ya chadema kwa miaka kumi sasa. Hayamkini wapo wengi waliofanya kazi ndani ya chama bila kuwa viongozi na kukifanya chama kiwe hivi kilivyo sasa na hawa ni pamoja na wewe msomaji.

Naona wengi wamekuwa wakitaka kutumia kauli za Zito kumgombanisha na chadema au na wanachama wa chadema. Huwa inanipatabu sana kuoanisha kauli hizi na uasi kama wengi wanavyotaka isomeke. Ni kweli wengi tumehamaki na kauli au vitendo vya Zito ila ukitulia unaona yapo mengi zaidi ya tunavyotafsiri.

Ni haki ya mwanachama yeyote kutangaza nia yake ya kugombea cheo chochote ndani ya chama na nje havunji katiba wala hamuudhi mtu. nafikiri kinacholeta tabu ni timming inayotumika. Na nikweli wengi tunapenda watu bold ambao hawageuki na kauli zao, kwa mfano mimi binafsi ninawazimia sana Mwl J. Nyerere kwa misimamo yake na kauli zake zisizoyumba, Raisi wazamani wa USA George Bush Jr kwa kauli zake thabiti ambazo akizitoa hazibadiliki. Lakini wengine watasema hakuna rigidity kwenye maisha binadamu anabadilika na wakati, matukio na akijua zaidi ya alivyojua mwanzo, anaweza kubadilika chanya au hasi. Ila wengine watasema akibadilika atakuwa hakufanya utafiti wa kutosha ndio maana anamisimamo inayoyumba.

Zito Kabwe kwa kauli zake ni mwanachama mwaminifu wa chama chake, anakipenda, anatamani kifikie malengo yake makuu ya kumwokoa mtanzania kwenye umasikini na kukamata dola.

Njozi hizi zinamfanya atoe kauli ambazo zinanyanyua hisi za wengi na kuwachanganya sio wapenzi, wananchi tu bali hata viongozi wenzake. Hili linatokea kwa sababu mfumo wa demokrasia bado unakuwa na mabadiliko yanatokea kila kukicha na kasi ya mabadiliko haya ni kubwa sana kwa wananchi wa kawaida.

Kupishana misimamo ni jambo la kawaida kabisa, ila kushindwa kuelewana kwenye sera ni hatari. kisera CDM wako bold, Sioni Tatizo la Zito kugombea uraisi, sioni tatizo wa kauli za Zito tata au zisizo tata, anahaki zote za kufanya atakalo. Kazi kubwa ni kwa wanachadema kufanya kazi kwa bidii ili kuingia ikulu 2015. Wapo wengi wanatamani kuwa viongozi ila sio wote wanakarama ya uongozi, kiongozi atapimwa kwa uwezo wake wa kuongoza kwa sasa, kusaidia kukuza chama, kusaidia wananchi kiutawala, hekima na busara.

Mitazamo isiwe kisa cha kumwona mmoja hafai bali iwe changamoto ya makuzi ya demokrasia yetu.
Zito Zuberi Kabwe hana mgogoro wowote na chama, chama kinakuwa na sasa kazi kubwa ni kuwafikia wananchi wote kuanzia ngazi ya chini kabisa. Ikumbukwe tu hakuna atakayeweza kuwa raisi kama hajengi chama kuanzia ngazi ya msingi na kazi hii lazima ifanywe kwa vitendo.

Kuwa na njozi na kufanya kwa vitendo ni vitu viwili tofauti. Atakayepeperusha bendera ya chadema 2015 ni yule aliyewaunganisha wanachama wote viongozi wote wa chadema na kuonyesha uongozi uliotukuka na kuwaunganisha watanzania wote.

Chief Mkwawa wa Kalenga
CDM ikulu 2015 ni lazima
 
Hivi kuna possibility ya mtu kuvaa GWANDA ilhali mwili umejaa MAGAMBA??!! Tafakari, chukua hatua. take care!
 
Sipendi umbwenelehi wa kisiasa wa zitto but i think this move is perfect for CDM.......... swinging and spinning

sometimes we live with spouses we dont trust, he could be one of those similar scenarios

you stay with him/her, but sleep with an eye open
 
Zito kabwe nilikuwa naheshimu sana kazi zake na juhudi zake kubwa za kushiriki mapambano ya mabadiliko,kwa taarifa yako ni kwamba keshaingia kwenye matatizo ya kutofautiana na wenzake,na hilo lipo wazi kwani hata sisi wanachama wa kawaida tumeligundua,hivi itakuwaje siku Kikwete anasafiri safari zake halafu wapande ndege moja na Dr Slaa halafu wawe na mazungumzo ya siri,jaribu kufikiri siku hiyo sisi tunaounga mkono jitihada zao itakuwaje/??Mkuu zito keshapotea kwenye ulimwengu wa siasa za Tanzania tunasubiri tu wakati ufike apotee moja kwa moja kwani dalili zinaonyesha wazi,hata kama ana haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya chama kuna taratibu za kufata kaka,Zito ni kama hafanyi tena kazi Chadema,hatumwoni kwenye mapambano na wenzake,leo Dr slaa yupo mwanza,kuna mengi yanamsubiri dar na arusha kuja kutatua,Zito angekuwa smart anamsaidia ili kazi ziende haraka,Zito kushiriki kujenga Chadema kwa miaka kumi kama unavyodai haisaidii kama ataharibu mwishoni,mwanadamu anaangaliwa sana mwisho wa safari yake kuliko mwanzo wa safari yake!
 
kwa hiyo wewe binti yako wa miaka 5 akitangaza nia ya kuolewa na fulani ilihali bado yu masomoni bado utasema ni haki yake kikatiba kuolewa?
 
kwa maoni yangu ndio maana hatuendelei kwa sababu ya unafiki tu. Mtu anaulizwa vipi utagombea urais 2015? Bila aibu anajibu hapana hilo halipo kabisa kichwani mwangu kwa sasa namsaidia Rais, mara daraja likifika tutalivuka kumbe kichwani mwake anmipango lukuki mingine isiyo halali ya kuingia Ikulu. Hivi kati ya Zitto na hao wengine nani mnafiki wakuu? Na je kutangaza nia unakuwa umevunja katiba au sheria ya chama? Embu tujadiliane hili
 
Kuna jamaa yangu yupo Interpol Nchini Rwanda kanieleza kuwa kuna linaloendelea baina ya Zitto Anayetaka urais na Paul Kagame na alishapata kushuhudia zitto akitinga pale Ikulu ya Rwanda mapema mwaka huu.what is behind the scene?
 
Zitto anajifunza sana kwa marais na watu anaowaona yeye ni ma star...huwa anaenda hadi nje nchi malaysia hata ujerumani kujifunza na kubadilishana uzoefu na ma rais na PM wengi tu!sio mbaya sana...
 
Kuna jamaa yangu yupo Interpol Nchini Rwanda kanieleza kuwa kuna linaloendelea baina ya Zitto Anayetaka urais na Paul Kagame na alishapata kushuhudia zitto akitinga pale Ikulu ya Rwanda mapema mwaka huu.what is behind the scene?

Sasa tumechoka na habari zenu hizi kila siku zitto zitto zitto hamchoki kumchokonoa.muachen na yy apumzike jamani.kma ana hiyo influence ya kwenda kigali na kufanya maongezi na mtu kma kagame ambaye ni Rais anayeonyesha angalau mwelekeo nadhan ni vizur kwenda kujifunza kwake na sio zitto waende wote wanaotaka kufanya mema tz
 
Wana JF,

Nimeona umuhimu wa kurejea nukuu za Zitto ili watu wasome na kuamua wenyewe juu ya unadhifu na uthabiti wa kauli za Zitto. La haraka ninaloweza kusema, Zitto naye kajiunga kusimama katika nadharia mufilisi kuwa kila Mtanzania ni Msahaulifu na akipenda jambo au akimpenda mtu basi ashirikishi ubongo wake!

Ninaanza na hili la Zitto kumiliki magari ya kifahari kisha akayakana hivi karibuni kwa kisingizio cha kushindwa kuyamudu. Na kwamba Salum (Kaka yake) ndiye humlazimisha kuyachukua. Hebu tuona Zitto mwenyewe aliwahi kusema nini miaka ya nyuma:

Zitto Zuberi Kabwe
- Nimekuwa Mbunge miaka 4 sasa. Kweli siwezi kuwa na pesa za kununua VX mbili tatu nk? Mwaka 2007 nilinunua gari ya kifahari kabisa (pamoja na msaada wa marafiki wa nje) aina ya Hummer, nayo nilihongwa na nani? Nimekuwa mjumbe wa Kamati ya Afrika Mashariki kwa miezi 6 nalipwa kila siku 200,000 shs. Pia nimekuwa mjumbe wa Kamati ya Madini ya Bomani kwa miezi 4 na nusu na kulipwa 350,000 kila siku. Kweli ndugu zangu nishindwe kununua VX ya 60m, tena second hand pale AfriCarriers? Mbona mnanitukana ndugu yenu? Nimesomea kiasi cha kutosha Biashara ya Kimataifa na kufanya kazi za 'consultancy' Wizara ya fedha na wizara ya Biashara na Viwanda kuandaa mkakati wa nchi katika mazungumzo ya Economic Partnership Agreements dhidi ya EU. Nimekuwa nikilipwa vizuri tu. Nimefanya kazi kwa Mwaka mmoja na Rais Kohler kuhusu mpango wa Ujerumani kuhusu Afrika. Nimefanya consultancy na EU kuhusu nafasi ya Zanzibar katika Biashara ya Kimataifa....... Kweli jamani, hata kama mtu ana ajenda ya siri, siwezi kupata fedha za kununua gari ninayoipenda? Hivi sasa nina gari 5 - Prado 2 (zote sasa nimezigawa kwa Wagombea Ubunge watarajiwa wa CHADEMA mwakani, Nissan Patrol 1 ambayo inatumika Jimboni kwangu, Prado 2 moja anayotembelea Jacquiline, my partner na VX ambayo ninaitumia mimi kwa ziara ndefu za Chama. Gari zote nimeziorodhesha katika fomu za maadili na zile za kuzitoa nitazitoa baada ya kubadili umiliki.
Achieved at: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/38079-kauli-hizi-za-zitto-zinatupa-picha-gani-print.html

Na Je, mwaka 2012 anasemaje katika suala lile lile la kumiliki magari ya kifahari?

Zitto Zuberi Kabwe
Akizungumzia Utitiri wa magari ya kifahari anayodaiwa kuwa nayo anasema "Watu wanaishi maisha ya kufikirika sana, hayo magari wanayodai ninayo sina, iko hivi; mimi nina gari moja dogo aina ya Toyota Vista na nina Land Rover, Free Lander ambalo nimelichukua kwa mkopo, bei yake ni Dola 30,000, sijamaliza kulipa. Hayo mengine yanayosemwa ninayo ni ujinga tu wa watu.

Baada ya kuwa mbunge, nakumbuka April 2007 niliingiza nchini gari aina ya Hammer na nadhani nilikuwa mtu wa pili kuingiza gari hilo hapa nchini. Kaka yangu Salum anayefanya biashara ya magari ndiyo aliyeniletea na hili sikuliendesha zaidi ya wiki mbili, likanishinda. Lilikuwa la kifahari mno, nikamwambia alichukue aliuze na hela yangu anirudishie.
Nakumbuka nilikwenda nalo Dodoma nikiwa naendesha na nilikwenda na Dk. Slaa na siku moja mwenyekiti wangu Mbowe baada tu ya kuletewa tukiwa Protea Hotel iliyo karibu na Kanisa la mtakatifu Petro, alijaribu kuliendesha akaniambia ni gari zuri sana. Hili nililikataa. Mwaka 2008 nilinunua Toyota Land cruiser V8. Hili nililitumia hadi kwenye kampeni mwaka 2010 na baada ya hapo nililiuza.

Salum alipoona sina gari kwa sababu nadhani ya kujua mimi ni mbunge akaniletea tena Range Rover Vogue Sport nililitumia kidogo likanishinda kwa sababu ni la kifahari sana, sikuweza kuligharamia. Nina akaunti mbili tu moja benki ya NMB na nyingine benki ya CRDB na zote hazina fedha zaidi ya shs Mil. 15 kila moja."- Zitto Kabwe
Source: HABARI MOTOMOTO: ZITTO KABWE 'AANIKA' UTAJIRI WAKE
Achieved at: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/319298-mzee-pinda-mh-zitto-na-ridhiwan-kikwete-5.html

Namba 2: Kuhusu Kugombea Nafasi Mbalimbali

Miaka ya Nyuma alisema haya kwa kupaza kama kawaida yake:

Mwanzoni nilipoona mada hii na majibu ya baadhi ya watu hapo awali sikuona umuhimu sana wa kujibu kwani ni mada ya zamani sana, mwaka 2007. Nilisema kwa mara ya kwanza kuwa sitagombea ubunge mwaka 2010 mwezi September mwaka 2006 na kuripotiwa na gazeti la SundayNews. Nilirejea tena kauli hiyo mwezi March mwaka 2007 nikiwa Wilayani Maswa mkoani Shinyanga na kuleta mjadala mkali sana wakati huo.

Mwezi March mwaka 2008 nilihojiwa na gazeti la The EastAfrican na kusisitiza kuwa nia yangu ni kutumikia kipindi kimoja tu cha Ubunge na kupumzika kwa miaka mitano kabla sijarudi tena Bungeni...... soma hapa ...allAfrica.com: Tanzania: Zitto Kabwe - The Country's One-Man Backbench (Page 1 of 2)

Mara zote nilisema kuwa sababu kubwa ya kuamua kuwa Mbunge wa kipindi kimoja ni kurudi kusoma zaidi na kupata fursa ya kufanya kazi maana toka nimemaliza shule nimefanya kazi mwaka mmoja tu (Shirika la Friedrich Ebert Foundation) na hivyo kujiona kuwa ninakosa 'some skills' za uongozi ili kutumia kipaji changu 'to the fullest' na kutumikia nchi yangu. Hata siku moja sijawahi kutia shika nia yangu ya kutumikia Taifa. Lakini siku zote nimekataa kuwa carrier politician. Ninapenda nikimaliza kazi zangu za kisiasa niweze kuwa na uwezo wa kufundisha katika vyuo vikuu taaluma yangu nitakayobobea. Baada ya kuwa Mbunge kwa takribani miezi 9 tu (na hasa baada ya kikao cha bajeti cha mwaka 2006/2007) niliona dhahiri kuwa kwa Bunge letu hili, mabadiliko ni nadra sana. Hivyo nikasema mapema kabisa kuwa nitakuwa Mbunge wa 'term' moja. Nilisema mapema ili watu wa Kigoma Kaskazini wenye mawazo ya kutaka kugombea wajue 'incumbent' hatagombea. Nilifanya kwa nia njema kabisa. Ninadhani nina uhuru wa kuamua kutogombea kama nilivyoamua kugombea bila kusukumwa na mtu. Mimi sikuombwa kugombea ubunge. Niliamua mwenyewe…..

Full article at: MTWARA KUMEKUCHA: ZITTO KASEMA UBUNGE BASI BAADA YA 2010 NINI KITAFUATA ?

Na leo kaja na hii:
"Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola," alisema Zitto.

Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ge-2015-nitagombea-urais-kupitia-chadema.html

Zitto anahitaji msaada wa kupata Consistent Lying Machine! Siamini kijana aliyekuwa makini kama Zitto ghafla na kwa kasi ya ajabu anakwenda nje ya mstari wake wa utambulisho, maandiko yake na kauli zake! Omar Ilyas yuko wapi amsaidie rafiki yetu? Kitila Mkumbo, Saanane na wengineo mko wapi mmusaidie kijana wetu kurudi kwenye mstari wake?!
 
Naona Zitto anatafuta mbinu ya Julias Marema maana amepoteza supporters wengi kwenye chama chake

Je hii mbinu yake ya kutaka kureview hii mikataba itamsadia?
We kupeng'e kalale hujui lugha ndo maana comments zako kwenye mada za kiingereza ni too general
 
Nilishawahi kusema njaa zinasababisha mambo mengi sana kwa Zitto hamkuamini ila as time goes on we will be on the same pace. Hapa hatogombea urais kwa ticket ya CDM bali ataenda kwenye chama kingine na wakati wa kampeni za urais ataipaka uchafu sana CDM akizunguka nchi nzima kwa pesa za mafisadi. Nao CCM watakuwa wanafanya reference kwake kama alikuwa CDM huyu wananchi mnamsikia?. Atafanya hayo akijua kuwa hatopata urais ila atakuwa amewakwamisha CDM kwa kiasi fulani kama dili yake itafanikiwa.

Huu ni mtazamo wangu.

Zitto ni parasite wa ukombozi Tanzania.
 
Ameshachukua fungu sasa unategemea nini hapo? Maisha yake kwanza utaifa baadae
 
Low battery n No network coverage.......Nitarudi baadaye!
 
Ni kweli mkuu, hayo ni mawazo yako! Sibishani na wewe, ngoja nisepe!
 
Back
Top Bottom