Which is better: Single or Unhappily Married?

Dadangu hakuna kitu kizuri kama maisha ya ndoa(kama ukipata ubavu wako), ila ukikosea au ukaolewa kama fasheni tu, maana siku hizi mtu anaolewa kwasababu kaona umri unaenda, au rafiki zake wote wameolewa au kafata kitu fulani(like pesa na vitu kama hivyo), sasa ukiolewa kwa sababu kama hizo hapo, stress utazikwepa vipi au utaenjoy vipi? maana hapo hakuna mapenzi ya kweli. ukimpata yule wa kwako kabisa(ubavu wako) utajiona ka uko peponi maana mnapendana kwa dhati na kwenye penzi la dhati hakuna kuumizana wala nini, ni kujiachia tu na raha!

Ahsante sana Mperwa! :)
 
Tumeumbwa tuoe/tuolewe. Hii ndiyo sheria ya Mungu na hulka ya mwanadamu: kwamba kuwe na mume na mke (watu wa ndoa). Mpaka utakapooa/olewa ndipo moyo wako utaridhika. Bila kuoa/olewa hata kama mtu utakuwa na rafiki wa kudumu bado utaona kuna kitu una-miss, kuna kitu kimepungua katika maisha yako; hata kama huyo partner wako mnapendana kiasi gani!

Halafu kuna huduma ambazo huwezi kuzipata kwa partner asiye mume/mke wako isipokuwa tu katika ndoa. Ndoa inakuhakikishia: kampani ya daima kutoka kwa mwezi wako (katika shida na raha). Inakuhakikishia matunzo ya kudumu mpaka uzeeni kama mnajaliwa maisha marefu. Ndoa inakuhakikishia malezi mazuri ya pamoja ya watoto wenu, mkijaliwa. Niambie nje ya ndoa utapata huduma hizo kweli? Si rahisi.

Maisha single yana raha yake na nafasi yake, lakini si kwa maisha yote ya mtu hasa kama anayachagua kwa hiari yake. Utafika mahali mtu utaona kwamba unahitaji mtu wa kuingia naye kwenye commitment.

Mi nafikiri afadhali uoe/uolewe. Mwombe Mungu akujalie mume/mke mwema. Hilo ndiyo la maana.
 
Marriage isn't everyone's cup of tea, that's why some people prefer coffee, others coco, others tea with a touch of gin... and then that's where the problem starts.
 
Wajameni ndoa raha we acha tu....hao wanaofurahia usingle, bado wako kwen 20, wakifikisha 30s hasa wasichana wanaanza 'kutusumbua' tuli kwen ndoa zetu mara ooh 'nataka mtoto na umri unaenda' and the like,
 
Acha hizo lahazizi!...mtu anafanya vile roho napenda!
 
Tangu utotoni nimeambiwa the ultimate goal for a woman ni kuolewa.Kusema kweli nilikuwa natamani kumeet Mr Right and walking down the isle but what Ive seen around me has made me wonder if marriage is for me.Sitaki kuingia kwa maisha ya majonzi na majuto like most married women I know of.Ofisini kwetu yuko mama mmoja everyday analia kwa sababu ya domestic problems.Sasa mimi nina jiuliza, haya ni maisha ya aina gani.Si heri yule mtu single who is living in peace na heshima zake than mwenye ameolewa na ako na stress zisizoisha.What is happening to the institution of marriage.Wako watu wanaozifurahia ndoa zao kweli?Ama nikuvumilia tuu nakuvaa smile fake wakilia moyoni.

...bora kuwa single after unhappy marriage(s)!
 
Ukichoka kukaa single basi uniPm nitakupa company ya kudumu maana hata mi bado sana hapa.
 
Despite all the problems facing the married couples i wouldnt advise one to remain single. The positive effects of marriage outweigh the negative ones. The fact ni kwamba unapokuwa single, u happen to be so free na mara nyingi too much of freedom is harmful. Remaining single will make you happy for sometimes, but kumbuka kuna maisha haswa baada ya kuchoka when you need someone to talk to and help one another. Sasa endelea kusema unakula raha ukiwa single then itokee umri umeenda na ukaugua uone moto wake.
 
Tatizo unaweza ukatafuta weeee na usipate. Sasa usipopata ufanyeje? Settle for less? No way Jose....I'd rather stay single and mingle whenever I want to....

na unaweza ukampata lakini ni kwa nje tu...utamu wa ngoma ni uingie ucheze.....mkiwa bado mpo mpo kila m2 ataona mwenzio ndio Mungu kampangia, cjui inakuwagaje, ngoja muingie ndani...mambo kibao! nimetokea huko mie, niliona wangu ni mr rite kweli kweli...lakini mambo kumbe mseto mseto...hajatabiriki....ni kuomba Mungu tu.....ndoa ni tamu na kuna machungu yake pia....cdhani kama kuna mtu yupo perfect so ni suala la kuchukuliana mlivyo tu but yaczidi uwezo.
 
Dadangu hakuna kitu kizuri kama maisha ya ndoa(kama ukipata ubavu wako), ila ukikosea au ukaolewa kama fasheni tu, maana siku hizi mtu anaolewa kwasababu kaona umri unaenda, au rafiki zake wote wameolewa au kafata kitu fulani(like pesa na vitu kama hivyo), sasa ukiolewa kwa sababu kama hizo hapo, stress utazikwepa vipi au utaenjoy vipi? maana hapo hakuna mapenzi ya kweli. ukimpata yule wa kwako kabisa(ubavu wako) utajiona ka uko peponi maana mnapendana kwa dhati na kwenye penzi la dhati hakuna kuumizana wala nini, ni kujiachia tu na raha!

mhh cku hizi bado lipo kweli?watu cku hizi wanaoana baada ya miezi kadhaa ndoa imejifia.....bwana eee ndoa haitabiriki hakuna cha kuingia kwa ajili ya kitu fulani au cjui nini, tuliingia kwa mapenzi na baada ya muda limtu linakubadilikia haswaa, aaahh tena mie naweza sema bora hao wanaoingia kwa ajili ya kitu fulani mana sie tulioingia kwa mapenzi then unakuja umizwa inaudhi sana, mwenye kuingia kwa njia yoyote ile aingie tu sekta haitabiriki hii.
 
Tafuta mtu ambae atakua kweli mumeo ndio utaona utam wa ndoa,ukipata kimeo umeliwa dadaa!!

jamani mkiwa nje ni tofauti na ndani, ndani kila mtu anatoa makucha yake wajamaa, ukimpata leo utamshukuru Mungu kwa kukupa mume/mke bora huwezi tabiri litakalotokea mbele, anaweza akawa mwema sana mwanzoni kati akawa shubiri....cdhani kama kuna mtu anaeweza sema ndoa yake inateleza tu......hata umpate wa namna gani mabadiliko yapo tu.
 
kuna article moja niliisoma inasema "maambukizo ya AIDS kwa wanandoa yameongezeka" sasa hapo yupi kati ya single na mwanandoa anaweza kuepuka nadhani kwa single muda wote unajikinga na mwanandoa hapo utajikinga vp? Bora single tuu hapo

kweli kabisa, ndio mana napendaga kusema mliopo nje chonde chonde mtembee na zana zenu, sie wa ndani li baba limetoka huko limejilewea limesagura huko limesahau zana likija home huwezi kuliambia litumie zana na mke wake wa ndoa....ndio balaa linapoanzia.
 
I'm in dillema, I don't know which is better.

oooh babe babe....maisha ndio haya, kila kitu na raha/karaha zake, ndoa ni tamu lakini ina mambo yake mengine yanaudhi/kera sana! cshahuri m2 awe cngle kabisa napo kuna u lonely fulani hivi.
 
na unaweza ukampata lakini ni kwa nje tu...utamu wa ngoma ni uingie ucheze.....mkiwa bado mpo mpo kila m2 ataona mwenzio ndio Mungu kampangia, cjui inakuwagaje, ngoja muingie ndani...mambo kibao! nimetokea huko mie, niliona wangu ni mr rite kweli kweli...lakini mambo kumbe mseto mseto...hajatabiriki....ni kuomba Mungu tu.....ndoa ni tamu na kuna machungu yake pia....cdhani kama kuna mtu yupo perfect so ni suala la kuchukuliana mlivyo tu but yaczidi uwezo.

Unaona Nyamayao, mimi na wewe have something in common! Hata mimi nimepitia huko huko ulikotoka wewe...
 
Tangu utotoni nimeambiwa the ultimate goal for a woman ni kuolewa.Kusema kweli nilikuwa natamani kumeet Mr Right and walking down the isle but what Ive seen around me has made me wonder if marriage is for me.Sitaki kuingia kwa maisha ya majonzi na majuto like most married women I know of.Ofisini kwetu yuko mama mmoja everyday analia kwa sababu ya domestic problems.Sasa mimi nina jiuliza, haya ni maisha ya aina gani.Si heri yule mtu single who is living in peace na heshima zake than mwenye ameolewa na ako na stress zisizoisha.What is happening to the institution of marriage.Wako watu wanaozifurahia ndoa zao kweli?Ama nikuvumilia tuu nakuvaa smile fake wakilia moyoni.

Ni hivi mama:

  • Wapo watu married na wanafurahia sana maisha yao, nadhani hata wewe mifano unayo. Huyo mama wa ofisini kwako asikutie hofu, ni mfano wa wanaotesekea ndoa zao, kama ilivyopo pia mifano mingi tu ya wanaofurahia ndoa zao.
  • Kuwa single sio mwisho wa domestic problems (and other problems). Wako watu wengi tu single na wanasota vibaya sana kwa matatizo yao mbalimbali. Of course wapo pia wanaofurahia hayo maisha ya kuwa single. Lakini raha ya kuwa single inaonekana tu kipindi kile ambacho you are able to mingle, ikifika muda ambako mingling ni shida basi pepo la upweke linakuvamia, unateseka mbaya! Wenzetu wazungu kipindi hicho ndipo hufuga paka au mbwa na kumfanya ndiye companion wake!
  • Kwa hiyo kuwa married kuna potential ya kupata raha au karaha au vyote kwa vipimo/uwiano tofauti. Hali kadhalika, karaha hazikwepeki hata ukibakia single. Sasa sijui kwako karaha zipi zina uzito? Au raha zipi bora? The choice is yours, but remember you will be responsible for your choice, it is about risk taking. Be ready for whatever consequences za choice utakayofanya.
 
Single is better than unhappily married.. Usiolewe au kuoa eti kwa sababu fulani kaoa au kaolewa.. ndoa si mchezo wa kuigiza kuna machungu na matamu kiasi katika ndoa zisizo na mpangilio.. kwa hivi ni bora kuishi mwenyewe kuliko kuishi kwa mateso..Kuna mambo mengi yanayochangia unhappy marriage tofauti ya UMRI, DINI, KABILA,KIPATO etc. ni issue kubwa katika ndoa nyingi
 
Wandugu, kwanza niwaambie: Hakuna maisha yaliyo marahisi au yaliyo ya raha tu toka A mpaka Z. Maisha ni mapambano ndugu zangu, maisha ni magumu. Maisha ni uteguzi wa kudumu wa vitendawili mbele yetu. Na daima mtu utakutana na uchungu, changamoto, na pia raha fulani (faraja). Kumbe maisha ya ndoa ni magumu. Lazima mtu unapoingia ujue unaenda kujifunza ku-face magumu na pia kupata faraja zake. Kumbe usitegemee kupata raha tu. Hilo halimo! Kuna yote mawili: raha na machungu.

Panapokuwa na raha, basi mshukuru Mungu. Panapotokea machungu (ambayo daima yatakuwepo) basi jifunze kunesa, kuvumilia. Ujue huwezi kumpata mtu (mume/mke) ambaye mtaelewana kwa kila kitu na wakati wote. Tumeumbwa kila mtu tofauti na mwenzake. Kila mmoja kalelewa kivyake (ana historia yake). Kila mtu anabadilika daima: kuelekea wema au kuelekea ubaya. Katika haya yote ujue kwamba lazima mtagongana tu. Kumbe lazima kujitahidi kuvumilia, kumchukulia mwingine alivyo, kusaidiana na kurekebishana kwa upendo. Ukiona mtu anafanya Jubilee ya ndoa ya miaka 25, au 50 nk mwulize atakueleza shida alizopitia naye atakueleza. Mwulize raha alizozipata ni nyingi pia na atakusimulia.

Kumbe tusikwepe ndoa kwa kuogopa shida zilizomo. Kama hutaki kuoa/kuolewa uwe na sababu nyingine nzito lakini kama ni kuwepa shida/magumu ni kujidanganya tu kwa sababu huko kwenye u-single nako kuna moto wake hasa utakapozeeka ambapo si wengi watakupapatikia tena. Au pale utakapopata ugonjwa wa maisha yote na kuhitaji mtu wa kuwa karibu nawe daima na hayupo kwa vile hukuoa/hukuolewa kwa ubabe tu. Utashangaa! Nani atakutunza asiye na commitment nawe? Ujue commitment ya ndoa ina uzito sana, inamwajibisha mtu kisheria na hata kimaadili. Mtu atakuwa tayari kuwa nawe uzeeni au katika ugonjwa wa kudumu mpaka ufe. Lakini kama mtu anaishi kihuni tu asitegemee wakati wa shida au uzee wahuni wenzake watakuwa na muda naye. Wapi bana! Waache kutafuta wazima au vijana.

Ndoa imewekwa ili wawili waweze kukaa pamoja tena katika shida na raha, na si katika raha tu. Kwa hiyo ukiwa na nia ya kuoa/kuolewa tafadhali mwombe Mungu akusaidie na uingie katika maisha hayo ukijua kwamba unaenda si kupata raha tu bali kujifunza pia kujitoa.
 
Kwa wanaumme wa sikuhizi , mhhh afadhali nibaki single. Maana vimada, mara vi msg kwenye simu, mara kalala nje lol! Kuna wachache sana wamepata bahati ya wanaumme wanaujiheshimu lkn wengi ni michezo tuu . Hakuna mwanamme hatoki nje ya ndoa
 
Back
Top Bottom