Where do deleted data from recycle bin go?

MAHENDEKA

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2010
Posts
340
Reaction score
181
Kama tujuavyo kuwa recycle bin ndo 'jalala' la data/documents that have been deleted from computer..swali langu ni kwamba unapo delete au ku-empty.

data/documents zilizopo ndani ya recycle bin,data hizo zinakwenda wapi?,na unapofanya system recovery data hizo (zilizofutwa) zinarudi je? zinatoka wapi? And whats the concept behind this phenomenon?

-Pili nitafurahi endapo mtu atanifafanulia maana ya maneno haya. MEMORY and STORAGE katika lugha ya kiswahili manake kila nikifikiria kwa makini naona kama yana maana sawa vile
 
Unapodelete data zinaenda recycle bin na kumbuka recycle bin ni part ya system kwa hiyo basi data ndani ya recycle bin zinaendelea kuwa valid na unaweza kuzi-access bila kutumia specialized scripts zozote. Right click recycle bin chagua document gani unaihitaji then choose restore. Unapofanya system restore, system inasoma data kutoka backup folder ndani ya computer yako au kokote ulikosave.

Unapoempty recycle bin, system inadelete handle zote zinazohusiana na hizo file zilizokuwa deleted na kuifanya ile space kuwa available kwa file zingine kuandikwa juu yake. Lakini huo siyo mwisho wa hizo data, ukweli ni kwamba data ndani ya hard drives zinabaki humo mpaka hiyo hard drive iharibiwe. mfano kuna department katika serikali ya marekani unaponunua computer kutoka kwao wanakupatia bila hard drive na hard drive zenyewe zinakuwa shreded.

Kuhusu Memory na Storage ni kwamba zote zinatunza data ila tofauti yake kubwa ni kwamba Memory inatunza data kwa muda mfupi (temporary) wakati Storage inatunza kwa muda mrefu.
 
MAHENDEKA;

Memory ina maana sawa na "Storage Capacity", hivyo neno memory siyo synonymous na neno "storage" as storage. Memory however, zipo za aina nyingi! Changanya na za kwako sasa kupata maana zake za kiswahili!

More over, storage of data in any storage media is just a logical allocation of data to a particular storage space. Ukienda Ubungo Bus Terminal kwa mfano leo hii, kukata ticket ya bus la Jumapili ijayo kwenda Musoma, halafu unaambiwa kuwa basi limejaa! Sasa limejaa vipi wakati hata kuondoka halijaondoka na linatakiwa kuondoka Jumapili ijayo?

Changanaya na za kwako tena hapa! Ila swali lako ni zuri saana, nadhani wengi litakuwa lilikuwa linawasumbua!
 
Last edited by a moderator:
Kifupi. Haziendi popote . Pale unachofanya unakuwa umefuta Pointer tu ya kwenye Memory location na Memory Adress ambayo ndiyo hasa imezihifadhi.

Ni sawa niandike barua kwa Johna XYA Dodoma nifute sehemu niliondika anuani yake alafu nitumbukize posta. Huyu John XYA kweli yupo huko dodoma lakini kibidamu itakuwa vigumu kumpatia barua sababu hatujui adress yake. Wanamweza kumpata lakini bila anuani itakuwa vigumu.

Kwa Hiyo In digital languge ile Memory adress ya HDD or USB na hata Simcard inakuwa iko free kutumiwa na resouces nyingine lakini kama hijatumiwa basi zile data zilizofutwa zinakuwepo bado. Kwa hiyo kwenye hata ukifuta file fulani likaenda kwenye recyle bin kule ndani ya hard dik linakuwa liko pale pale kwenye location ile ile . Ukifuta kwenye recycle bin unakuwa ndo umefuta pointer ila file lenyewe bado linakuwepo .

Ndio maana kuna tools

  • za kusoma simcard za simu kujua message gani ziliingia zikfutwa.
  • za kurecover data zilizofuta kwa bahati kwenye HDD na USB
Hizi nyenzo zinafanya kazi vizuri tu kama ile adress bado hijatumiwa.
 
Mahendeka;
Memory ina maana sawa na "Storage Capacity", hivyo neno memory siyo synonymous na neno "storage" as storage. Memory however, zipo za aina nyingi! Changanya na za kwako sasa kupata maana zake za kiswahili!
More over, storage of data in any storage media is just a logical allocation of data to a particular storage space. Ukienda Ubungo Bus Terminal kwa mfano leo hii, kukata ticket ya bus la Jumapili ijayo kwenda Musoma, halafu unaambiwa kuwa basi limejaa! Sasa limejaa vipi wakati hata kuondoka halijaondoka na linatakiwa kuondoka Jumapili ijayo? Changanaya na za kwako tena hapa! Ila swali lako ni zuri saana, nadhani wengi litakuwa lilikuwa linawasumbua!

Sijakuelewa hata kidogo mkuu, thanks Juakali maana umegusa vitu vya muhimu, ulichosema ni sahihi kuhusu data ambazo zimekuwa empted from recycle bin, data hizi zinatatunzwa kwenye virtual storage ya system, lakini unapodelete tena na tena ile virtual storage nayo inaja, kwa hiyo data ambazo zilikuwa deleted mwanzo zaidi zinapotea ili kutunza hizi mpya, kwa mtindo huo unapofanya system recovery utapata zile ambazo zimekuwa deleted siku za karibuni zaidi
 
Unapodelete data zinaenda recycle bin na kumbuka recycle bin ni part ya system kwa hiyo basi data ndani ya recycle bin zinaendelea kuwa valid na unaweza kuzi-access bila kutumia specialized scripts zozote. Right click recycle bin chagua document gani unaihitaji then choose restore. Unapofanya system restore, system inasoma data kutoka backup folder ndani ya computer yako au kokote ulikosave.

Unapoempty recycle bin, system inadelete handle zote zinazohusiana na hizo file zilizokuwa deleted na kuifanya ile space kuwa available kwa file zingine kuandikwa juu yake. Lakini huo siyo mwisho wa hizo data, ukweli ni kwamba data ndani ya hard drives zinabaki humo mpaka hiyo hard drive iharibiwe. mfano kuna department katika serikali ya marekani unaponunua computer kutoka kwao wanakupatia bila hard drive na hard drive zenyewe zinakuwa shreded.

Kuhusu Memory na Storage ni kwamba zote zinatunza data ila tofauti yake kubwa ni kwamba Memory inatunza data kwa muda mfupi (temporary) wakati Storage inatunza kwa muda mrefu.

Asante Mkuu Jua Kali,huwa nasikia jamaa wakali wa data recovery wakiuliza swali hilo unapokuwa umepotelewa na data-kama umeisha save au kuifanyia kazi PC tangu last formating. Swali la ziada je formating nayo ni sawa na delete?Nikiwa na maana je ni rahisi kupata data iliyofutika kwenye formating ya HDD?au duniani hatujafikia hapo?na je pale TZ kuna wataalamu wa kazi hiyo?
 
nachanganyikiwa, acha nirejee kwenye jukwaa la siasa.
 
Wajameni thenkini sana, maana hata mimi nimelipata hilo darsa!!
 
Kifupi. Haziendi popote . Pale unachofanya unakuwa umefuta Pointer tu ya kwenye Memory location na Memory Adress ambayo ndiyo hasa imezihifadhi.

Ni sawa niandike barua kwa Johna XYA Dodoma nifute sehemu niliondika anuani yake alafu nitumbukize posta. Huyu John XYA kweli yupo huko dodoma lakini kibidamu itakuwa vigumu kumpatia barua sababu hatujui adress yake. Wanamweza kumpata lakini bila anuani itakuwa vigumu.

Kwa Hiyo In digital languge ile Memory adress ya HDD or USB na hata Simcard inakuwa iko free kutumiwa na resouces nyingine lakini kama hijatumiwa basi zile data zilizofutwa zinakuwepo bado. Kwa hiyo kwenye hata ukifuta file fulani likaenda kwenye recyle bin kule ndani ya hard dik linakuwa liko pale pale kwenye location ile ile . Ukifuta kwenye recycle bin unakuwa ndo umefuta pointer ila file lenyewe bado linakuwepo .

Ndio maana kuna tools

  • za kusoma simcard za simu kujua message gani ziliingia zikfutwa.
  • za kurecover data zilizofuta kwa bahati kwenye HDD na USB
Hizi nyenzo zinafanya kazi vizuri tu kama ile adress bado hijatumiwa.

Sasa, hard disc ikiwa formatted inatokea nini? Formatting maana yake nini hasa?
 
Unapoempty recycle bin, system inadelete handle zote zinazohusiana na hizo file zilizokuwa deleted na kuifanya ile space kuwa available kwa file zingine kuandikwa juu yake. Lakini huo siyo mwisho wa hizo data, ukweli ni kwamba data ndani ya hard drives zinabaki humo mpaka hiyo hard drive iharibiwe. mfano kuna department katika serikali ya marekani unaponunua computer kutoka kwao wanakupatia bila hard drive na hard drive zenyewe zinakuwa shreded.

Hapo inachanganya. Jee iwapo utaitumia kompyuta kwa miaka say 10, ukiwa unafuta mafaili mengi tu ili kusevu mengine - jee yote yale uliyofuta yanabaki ndani ya hiyo drive? Jee hakuna limit au capacity ya drive kubaki na hayo mafaili yanayukuwa deleted?
 
Kiukweli ni kwamba ukifuta files/documents kutoka kwenye recycle bin, huwezi ukarecover tena hayo mafaili, yaani ndo hivyo tena huwezi kuzipata unless labda kama umesave mahali mahali hata kama umefuta kwenye recycle bin lkn unaweza kurecover toka sehemu nyingine kwenye computer storage. Ukifuta documents yoyote kwenye recycle bin,kuzipata ni vigumu saaaaana! Ni sawa na kufuta kumbukumbu katika ramani ya dunia.
 
Sasa, hard disc ikiwa formatted inatokea nini? Formatting maana yake nini hasa?
Mimi nimejaribu kirahisi sana kama una muda na unataka kuua tafuta malezo ya cumputer science Kuhusu Memory au Storage Management

Recovery of data from a formatted disk

As with regular deletion, data on a disk is not fully destroyed during a high-level format. Instead, the area on the disk containing the data is merely marked as available (in whatever file system structure the format uses), and retains the old data until it is overwritten. If the formatting is done with a different file system than previously existed in the partition, some data may be overwritten that wouldn't be if the same file system had been used. However, under some file systems (e.g., NTFS, but not FAT), the file indexes (such as $MFTs under NTFS, "inodes" under ext2/3, etc.) may not be written to the same exact locations. And if the partition size is increased, even FAT file systems will overwrite more data at the beginning of that new partition.
From the perspective of preventing the recovery of sensitive data through recovery tools, the data must either be completely overwritten (every sector) with random data before the format, or the format program itself must perform this overwriting, as the DOS FORMAT command did with floppy diskettes, filling every data sector with the byte value F6 in hex.

Read full article on Disk formatting - Wikipedia, the free encyclopedia
Kwa lugha rahisi fomatting ni kama deleting. sema neno format linatumika katila level ya hardware na neno deleting linatumika katika level ya file.

Hard disk ikiwa formatted ni kuwa Storage manager (CPU ya HDD) ya Hard disk inaambiwa inaweza kuandika mafile kwenye lacation yeyote na adress yeyote. Ile adress na location ina kuwa declared kuwa wazi kutumika japo inakuwa bado ina mafaile ya zama
 
Asante Mkuu Jua Kali,huwa nasikia jamaa wakali wa data recovery wakiuliza swali hilo unapokuwa umepotelewa na data-kama umeisha save au kuifanyia kazi PC tangu last formating. Swali la ziada je formating nayo ni sawa na delete?Nikiwa na maana je ni rahisi kupata data iliyofutika kwenye formating ya HDD?au duniani hatujafikia hapo?na je pale TZ kuna wataalamu wa kazi hiyo?

Formating siyo sawa na ku-delete, unapoformat una deal na file structure wakati deleting una invalidate handle za file husika. tukirudi kwenye swali la ku-recover data baada ya ku-format HDD. Ndiyo inawezekana kabisa computer zinatumia mathematical function kuandika data kwenye face ya HDD na Inverse function zinajua jinsi ya ku-retrieve data kutoka HDD.

Sasa hivyo Data recovery Application, zinajua kabisa kuwa disk mpya inakuwa katika RAW state, then kabla ya kuitumia lazima file system iandikwe juu ya HDD (formating) na jinsi unavyo delete na kuformat ndivyo LAYERs zinavyozidi kuandikwa juu ya uso wa hard drive na hiyo haiaffect kabisa size ya Hard drive husika since Handle zikiwa deleted system inaiona hdd kuwa kama mpya. Hizo Data recovery application zina extract data kutoka current kuelekea za zamani, zinapokuta file system zinaitoa hiyo file structure zinaingia kwenye LAYER ya chini yake. Zitaendelea kufanya hivyo mpaka zifike pale HDD ilipokuwa katika RAW state.
 
Mimi nimejaribu kirahisi sana kama una muda na unataka kuua tafuta malezo ya cumputer science Kuhusu Memory au Storage Management

Kwa lugha rahisi fomatting ni kama deleting. sema neno format linatumika katila level ya hardware na neno deleting linatumika katika level ya file.

Hard disk ikiwa formatted ni kuwa Storage manager (CPU ya HDD) ya Hard disk inaambiwa inaweza kuandika mafile kwenye lacation yeyote na adress yeyote. Ile adress na location ina kuwa declared kuwa wazi kutumika japo inakuwa bado ina mafaile ya zama

Naomba ufafanuzi zaidi kuhusu CPU ya HDD pls.
 
Kiukweli ni kwamba ukifuta files/documents kutoka kwenye recycle bin, huwezi ukarecover tena hayo mafaili, yaani ndo hivyo tena huwezi kuzipata unless labda kama umesave mahali mahali hata kama umefuta kwenye recycle bin lkn unaweza kurecover toka sehemu nyingine kwenye computer storage. Ukifuta documents yoyote kwenye recycle bin,kuzipata ni vigumu saaaaana! Ni sawa na kufuta kumbukumbu katika ramani ya dunia.

Kaka...Zinatatikana hata kama ume empy deleted Item....Baada ya kufuta kwenye C drive...zinapatikana...wameenda mbali hata zile ulizo format zinapatikana....zoezi hili nimeshalifanya...kwani program flan bwana invisible aliweka humu...ni balaa...inapata data si mchezo.
 
Naomba ufafanuzi zaidi kuhusu CPU ya HDD pls.
Mkuu ndo maana nilisema kwa kwa lugha rahisi. CPU ya HDD kwa jina la kitaalam ni Storage Device Controller Storage device zote iwe CD drive, USB,HDD etc zinaunganishwa na PC kwa kitu kinaitwa kinaitwa controller
Controller kazi yake ni kuwa na instruction jinsi drive fulani inavyotakiwa kuacess au kuhifadhi data. controller ndo zina taarifa ya kiasi gani cha space ya ku allocate kwa every read/write ya device. Controller ndo zinajua data inayoandikwa kwente strorage device ikae kwenye location na adress gani. Ndo Ninasema hizi contrloler ni kama CPU ya storage devices.

Kwa lugha nyepesi Computer ni System amabyo ina subsystem nyingi. Na kila subsytem ina kifaa cha ku controll subsystem ile. Nilitumia jina CPU ili watu waelewe . CPU ndo Central or Core pocessing unit but there are other processing unit na HDD controller ni moja wapo.

Niko tayari kukosolewa au kuelimishwa
 
Ukifuta files kutoka kwenye Bin Operating system inaimark lile eneo la hard drive kuwa liko wazio kwa ajili ya matumizi mengine, ila zile data(patern ya bits) ipo pale pale, ndo maana kuna program zinaweza kurecover hizo file. Kama unataka kufuta hiyo data kabisa unatakiwa utumie program ambayo itaandika juu ya hilo eneo la hard disk ili ku overwrite data yako with garbage.

Mimi natumia Eraser ukitumia hiyo hakuna mtu anayeweza kurecover hakuna cha FBI wala CIA, haijawahi kutokea.
 
Ndiyo maana information nyingi (na mithani ya University) huwa zina-leak kirahisi!
 
Ukifuta files kutoka kwenye Bin Operating system inaimark lile eneo la hard drive kuwa liko wazio kwa ajili ya matumizi mengine, ila zile data(patern ya bits) ipo pale pale, ndo maana kuna program zinaweza kurecover hizo file. Kama unataka kufuta hiyo data kabisa unatakiwa utumie program ambayo itaandika juu ya hilo eneo la hard disk ili ku overwrite data yako with garbage.

Mimi natumia Eraser ukitumia hiyo hakuna mtu anayeweza kurecover hakuna cha FBI wala CIA, haijawahi kutokea.

Duh, Sikujua kuwa mkuu umefanya kazi FBI na CIA mpaka ukajua kuwa hawawezi kurecover data zilizodeletiwa na Eraser.
Hapa chini maneno ya wataalam wengine.
While data can technically never be fully deleted on a hard drive, so-called "government wipes" make the data all but unrecoverable. The only way to absolutely ensure that all traces of previous data are deleted is to destroy the drive and platters.
It is nearly impossible to totally delete files in a hard drive unless you destroy the disk that is in the hard drive, otherwise, with some professional tools and equipment you can still read the data.
This is a very difficult process for amateurs. If you have any doubt in your mind about what you are doing, it is much safer to find a trained professional.
There are even some professionals who can recover disks that have been for example burned, sawed in twice and then smashed with a sledge.
 
Source? Laws the Physics ni Universal FBI wala CIA hawawezi kuzivunja, hakuna example hata moja kwenye research community inayoonyesha kuwa kurecover erased data inawezekana, tena haiwezekani baada ya ku-overwrite mara moja tu, Eraser inafuta hata mara 35. Kwa kifupi hakuna sababu ya kuamini kama wanaweza, until ipatikane evidence otherwise.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom