Jinsi ya kufuta kila kitu kwenye computer in case unaiuza siri zisivujie nje

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
By Mnato
Jinsi ya kufuta kila kitu kwenye computer yako zikiwemo picha za uchi

Kuna watu wamekuwa wakipata hasara katika makampuni yao au hata watu binafsi kutokana na kuuza kompyuta zao kwa watu wengine .Uuzaji wa kompyuta bila kuisafisha umeawafanya watu wengi kuibiwa kumbukumbu zao za siri bila wao kufahamu na kumbukumbu hizo zinapoangukia kwenye mikono ya watu wabaya inakuwa hasara kwa aliyeuza kompyuta hiyo.

Je Unataka kuuza kompyuta yako na kununua mpya,lakini kwenye kompyuta yako kuna kumbukumbu nyingi za muhimu ambazo usingependa mtu mwingine yeyote azipate wala kuziona.Je utafanya nini?

Wapo ambao wamekuwa wakitumia mbinu za kawaida kufuta data kwenye kompyuta zao kama Kufuta(delete) au kuformat .Utafuta kila kitu kwa kubonyeza "Delete" halafu utaenda kwenye jalala(Recycle bin) na kufuta kila kitu ..

Au utaamua kuformat na kuifanya kompyuta yako ifute kila kitu.Hii Haitasaidia.
Swali ni je njia ipi ni sahihi ya kusafisha kompyuta yako kabla ya kuiuza?


Majibu ni mengi na inategemea na ufahamu wa muhusika,ila ukweli ni kuwa kwa njia zote mbili za hapo juu hakuna hata njia moja iliyo salama,kwani kama utatumia njia kama hizo na ukamuuzia mtu mwenye utaalam wa kompyuta,basi ataweza kuzirudisha(recover) .

Kabla ya kujua njia za kujikinga basi tuone ni kwa namna gani kompyuta inatunza kumbukumbu.


Jinsi kompyuta inavyohifadhi kumbukumbu

Wengi wetu wanaweza wakawa wameshaanza kujiuliza,inakuwaje sio salama wakati nimeshafuta kila kitu toka kwenye kompyuta? Je mtu ataweza vipi kuona mafaili ambayo tayari nimeshayafuta?

Ukweli ni kuwa,kwa mujibu wa uhifadhi wa kumbukumbu kwenye kompyuta.Pindi unapofuta au kufanya format(kuweka mtambo endeshi(OS) mpya),sio kweli unayafuta moja kwa moja mafaili na kumbukumbu
toka kwenye kompyuta yako.

Kitu kinachofanyika ni kuwa unaondoa taswira yake kwenye uso wa mbele wa hard disk hivyo kukufanya wewe uone kama umeyafuta ila bado yanaendelea kuwepo kwenye disk yako.

Na hii ndio maana kama kunatokea kesi,wataalam wa uchunguzi wa makosa ya kompyuta(Computer Forensic) huchukua kompyuta yako kwa ajili ya kuifanyia uchunguzi.

Siku hizi kuna program nyingi sana ambazo zina uwezo wa kurudisha mafaili hata yale yaliyokuwepo kipindi ulipoinunua kompyuta kwa siku ya kwanza, mara nyingi jinsi gani unaweza kuyarudisha
hayo mafaili hutegemea elimu ya mtu anayefanya hizo kazi ya kuyarudisha,kwani kazi ya kuyarudisha haya mafaili huwa ngumu kutegemeana na jinsi mafaili hayo yalivyofutwa.

Mfano faili lililofutwa kwa kubonyeza "Delete" ni rahisi zaidi kulirudisha kuliko lile lililofutwa kwa kuformat kopyuta, vilevile huwa ngumu zaidi kama mtumiajai alifanya mgawanyo wa hard disk (partition) baada ya kuformat.

Hivyo leo hii nitakuonesha njia thabiti za kufuta kumbukumbu toka kwenye kompyuta unayotaka kuiuza ili kuhakikisha unakuwa salama zaidi.

Nitafutaje kumbukumbu moja kwa moja toka kwenye kompyuta?
Takwimu zinaonesha kuwa mtu mmoja kati ya wanne wamekuwa wakiibiwa siri zao kutokana na kuuza kompyuta bila kufuta kumbukumbu,hivyo kama wewe hutaki kuingia kwenye hilo kundi basi unaweza kufuata hatua zifuatazo.

1.Chukua ile CD uliyopewa pindi uliponunua kompyuta yako,ambapo nyingi huitwa recovery CD.Kama umepoteza hii CD au haukupewa pindi uliponunua kompyuta,basi nenda online na tafuta programu zinazotumika kufuta kumbukumbu(disk-wiping program). Programu hizi zipo nyingi ila binafsi nimewahi kutumia Darik's Boot and Nuke (DBAN) hivyo nakushauri uijaribu hii.

2.Tumia programu kama Nero au yoyote uliyoizoea kuchoma hayo mafaili ya hii programu kwenye CD,kumbuka kuchagua mtindo wa Bootable CD.

3.Weka CD kwenye kompyuta yako halafu irestart. Kompyuta inatakiwa kuitambua hiyo CD pindi tu inapowaka,kutatokea ujumbe kwenye kioo unaosomeka "press any key to boot from CD." Hapo bonyeza kitu chochote kwenye keyboard yako.

Kumbuka: Kama hautouona huu ujumbe unaosomeka"boot from CD" inawezekanika kabisa umekosea katika kuchoma hiyo CD yako,unatakiwa kuichoka kama "Bootable CD".

Jaribu tena au wasiliana na mtaalamu wa IT aliye karibu nawe. Kama una uhakika kabisa uliichoma kama Bootable CD,basi inawezekana kuna mabadiliko unatakiwa kuyafanya ili kuiwezesha kompyuta kuitambua CD,haya kwa wasio na utaalam inabidi wawatafute wenye utaalam kidogo ili wakusaidie kubadilisha utaratibu wa BIOS.

Kama unataka kujaribu mwenyewe,basi kompyuta inapowaka tu bonyeza "Delete",baada ya hapo fuata maelekezo na kuingia kwenye "Boot Sequence",iweke CD or DVD kuwa ya juu kabisa kabla ya Hard drive,hapo mambo yatakuwa sawia.

4.Fuata maelekezo utakayopewa na hiyo programu,mara nyingi huchukua masaa kadhaa hadi siku mpaka kufuta kila kitu kilichopo kwenye kompyuta yako.

Kama haujiamini,njia salama kwa 100% ni kutoa hard disk na kuiweka kwenye jiwe,halafu chukua nyundo na ivunjevunje au imwagie petrol na kuichoma moto.

Baada ya hapo basi kompyuta yako itakuwa mbichi kabisa na unaweza kuiuza bila utata wala hofu juu ya kumbukumbuku wala usalama wako.

Hisani ya Fikra Huru
 

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,165
2,000
... Kama haujiamini,njia salama kwa 100% ni kutoa hard disk na kuiweka kwenye jiwe,halafu chukua nyundo na ivunjevunje au imwagie petrol na kuichoma moto.
...asante sana mkuu! nitakuwa natumia njia hii, ni rahisi sana!
 

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
... Kama haujiamini,njia salama kwa 100% ni kutoa hard disk na kuiweka kwenye jiwe,halafu chukua nyundo na ivunjevunje au imwagie petrol na kuichoma moto.
...asante sana mkuu! nitakuwa natumia njia hii, ni rahisi sana!

Wengi hushangaa siri zao kuvuja nje bila kujua chanzo, kumbe hard disc ya computer zao ndio source
 

SaidAlly

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
2,263
2,000
sasa nikisha ipondaponda na kuichoma moto, ntaiuza bila hard disk??
 

Makoye Matale

JF-Expert Member
May 2, 2011
6,491
2,000
sasa nikisha ipondaponda na kuichoma moto, ntaiuza bila hard disk??

Hard disk zinauzwa madukani, baada ya kuifanyia 'total destruction' unaweza kununua HD mpya isiyokuwa na madhara kwako, bei yake utaiongeza katika masalia ya kompyuta yako. Ukiuza masalia ya kompyuta bila HD huenda hutapata mnunuzi.
 

Prince Nadheem

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
1,189
2,000
Hii post nimeiona jana kama sio juzi kule fikra huru forum kama sikosei. So ingependeza sana kama ungetoa na credits maana hata huku kuna baadhi ya topics huibwa na kupelekwa forums zingine au blogs na huwa tunalalamika sana kuwa hatupewi credits na hao watu.
So we have to do what we preach
 

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
7,358
0
Hii post nimeiona jana kama sio juzi kule fikra huru forum kama sikosei. So ingependeza sana kama ungetoa na credits maana hata huku kuna baadhi ya topics huibwa na kupelekwa forums zingine au blogs na huwa tunalalamika sana kuwa hatupewi credits na hao watu. So we have to do what we preach
mbona ameandika hapo chini, na kule mwanzo kaandika jina la mwandishi (Mnato.. teh teh!). Bloggers wa Bongo ndy mabingwa wa kukopi na kupesti, akijitahidi sana anabadili lugha tu, na hatoi credit! Blogu za Bongo hazina habari original, ndiyo maana zooote zina habari zinazofanana!
 

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
7,358
0
Njia salama siyo kuwipe, unaweza ukawipe vizuri tu, lakini kama wanaume wanajua kulikuwa na madini ndani lazima yatarejeshwa tu!!!....njia salama ni kuiharibu kabisa (HAKIKISHA IMEHARIBIKA HASWAA, SIYO UNAIVUNJA MARA MOJA NA KUTIA KWENYE DUT BIN!). Lakini mpaka uhangaike hivyo basi kweli una vitu vya SIRI haswaa, na ujue unaweza kuwa unahangaika kudestroy wakati wenzio walishanyonya zamaani wametulia tu, computer yoyote ukishaiunganisha kwenye internet tu basi kwishnei, mtu akiamua kuchukua data zako anachukua tu!
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,773
2,000
... Kama haujiamini,njia salama kwa 100% ni kutoa hard disk na kuiweka kwenye jiwe,halafu chukua nyundo na ivunjevunje au imwagie petrol na kuichoma moto.
...asante sana mkuu! nitakuwa natumia njia hii, ni rahisi sana!

heeee hii mbinu ina walakini, sidhani kama waweza uza kompyuta bila hard disk
 

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
13,673
2,000
Thanks mkuu japo sensitive data zangu hua naziweka kwenye flash yangu moja ambayo hua natembea nayo popote though no one notices it as a flash! Kwa hdd ni mainly entertainment stuffs!
 

Blackman

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
788
500
Thanks mkuu japo sensitive data zangu hua naziweka kwenye flash yangu moja ambayo hua natembea nayo popote though no one notices it as a flash! Kwa hdd ni mainly entertainment stuffs!

siku ikiharibika hiyo flash au kupotea utalia
 

Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,893
2,000
Pia ukiformat, formated hard disk zaidi ya mara tatu mfululizo data kuonekana huwa vigumu sana.
 

FASHIST

JF-Expert Member
Aug 22, 2013
246
0
... Kama haujiamini,njia salama kwa 100% ni kutoa hard disk na kuiweka kwenye jiwe,halafu chukua nyundo na ivunjevunje au imwagie petrol na kuichoma moto.
...asante sana mkuu! nitakuwa natumia njia hii, ni rahisi sana!

mwishowe mtatuambia tuchome hadi computer 2nayoiuza!!" ..........
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom