When it rains, it pours!!

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,242
113,619
Si muda mrefu uliopita mwanamuziki nyota wa Marekani wa miondoko ya R&B, Usher Raymond, alifunguliwa mashitaka ya kumuweka kwenye hali/ mazingira hatarishi ya kumwambukiza gonjwa la zinaa mwanadada mmoja hivi baada ya kukutana naye kimwili na kumficha kuwa yeye [Usher] ni mwathirika wa ugonjwa wa malengelenge ya neva ngozini kwenye kiungo cha uzazi [genital herpes].

Mwanadada huyo anadai fidia ya mamilioni ya dola za Kimarekani.

Mwaka 2012 Usher alimlipa mwanadada mwingine fidia ya dola za Kimarekani milioni moja na ushee nje ya mahakama kwa kumwambukiza hilo gonjwa!

Sasa wamejitokeza watu wengine watatu waliopanga kumfungulia mashitaka Usher kesho Jumatatu huko kwenye jimbo la California, nchini Marekani kuhusu kutokuwaambia yeye ni mwathirika kabla ya kukutana nao kimwili.

Wawili kati yao ni wanawake na mmoja ni mwanaume. Hapo kwa mwanaume kunaibua maswali kadhaa....

Ina maana Usher yuko kotekote? Yaani anapenda wanawake na wanaume pia?

Halafu, hivi mtu unathibitishaje kuwa kweli huyu ndiye aliyeniambukiza hili gonjwa na si mwingine?

Unathibitishaje kuwa kati ya wote uliolala nao huyu ndiye aliyeniambukiza?

Hahahaaa....pole zake huyo Usher maana naamini anapitia kipindi kigumu sasa hivi.

Nilisikia hii habari juujuu kwa Charlamagne Tha God. Huu ugonjwa si ni Kaswende? Kaswende si inatibika? Mbona anao toka 2012? Au ni ugonjwa mwingine ambao hautibiki.
 
Nafikiri kuna namna wadudu/virusi wa herpes huwa wanafanana na wale walikotoka. Mambo ya kuchunguza vinasaba yanaweza sema virusi hawa walitoka kwa Usher.
 
Mtu ukawa na pesa na bado ukaishi maisha ya ajabu ivi,... ii ni aibu kubwa sana kwa usher ajitafakari
 
Nilisikia hii habari juujuu kwa Charlamagne Tha God. Huu ugonjwa si ni Kaswende? Kaswende si inatibika? Mbona anao toka 2012? Au ni ugonjwa mwingine ambao hautibiki.

Hapana, huo ugonjwa siyo syphilis.

Syphilis kwa Kiswahili ni kaswende [au Kasie teh teh].

Mfano wa herpes ni kama vile vidonda vya homa vitokeavyo mdomoni.

Ila pia vyaweza kutokea kwenye sehemu za siri/ viungo vya uzazi na hicho ndo alonacho Usher.

Kasie
 
Nafikiri kuna namna wadudu/virusi wa herpes huwa wanafanana na wale walikotoka. Mambo ya kuchunguza vinasaba yanaweza sema virusi hawa walitoka kwa Usher.

Na hiyo inakuwa na uhakika wa kiasi gani kuwa vimetoka kwa huyu na si mwingine?
 
Kuna njaa kweli huko Usher atakuwa kabandua men wengi noma!

sijui kama ndugu zetu hawa wa box watapona?
 
Muda mfupi ulopita mmoja wa hawa watuhumu wapya watatu kaongea na waandishi wa habari.

Hahahaa...daah...sijui hata niseme nini.

Usher must like her women BBW:D:D:D

Hahahaa...daah...sijui hata niseme nini.

Usher must like her women BBW:D:D:D

Sema hivi...."huyo dada atakuwa msukuma/mnyamwezi.... ameenda hewani ni mdada wa miraba minne aka ameshiba hahaha wenyewe wanasema uzito wa nyoya..:)

Halafu sura yake imefanana na Nyonda-ako.... au mie naona vibaya?... ngoja nivue miwani nione vizuri.
 
Kafanana na nyonda wangu?

Hebu ngoja nimtazame vizuri....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom