TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 4,973
- 15,304
Mmeshindaje?
Siku za hivi karibuni kumejitokeza tabia ya watumiaji wa Whatsapp ku-forward picha zinazoonyesha matukio ya kutisha kama vile watu waliokatwa mapanga, waliokatwa/unguzwa sehemu za siri, waliokitwa mashoka vichwani, waliopata ajali mbaya na nyingine ambazo kwa maoni yangu sioni kama ni sawa kwa picha za aina hii kusambaa kwenye jamii. Inawezekana kabisa baadhi yetu huwa tunafowadi tu picha hizi bila hata kufikiria mara mbili kwamba zina athari gani katika jamii? Mimi binafsi sioni kama picha hizi zinatusaidia chochote sisi kama Watanzania. Ni kweli tunayo haki ya kupata habari lakini nadhani tuangalie sana aina ya vitu tunavyo izoesha jamii ikizingatiwa kwamba picha hizi zinaweza kuangaliwa hata na watoto maana hamna kizuizi chochote. Nadhani itasaidia zaidi kwa matukio tajwa kuripotiwa polisi badala ya kusambaza kwenye mitandao. Au wadau mnaonaje?