Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,221
Namna ambavyo watumiaji wa WhatsApp wanaitumi app ya WhatsApp; itabadilika na soon WhatsApp itakuwa ni mtandao wa tofauti zaidi. Itakuwa ni sehemu ambayo sio lazima ukimaliza kuchat na rafiki yako kwenye WhatsApp, unafunga app ya WhatsApp na kufungua app ya Instagram ili kufahamu habari zinazoendelea mjini. Itakuwa unaweza kupata taarifa zote kupitia app ya Instagram bila kulazimika kwenda kwenye apps nyingine.
Kampuni ya Meta imekuwa ikifanya majaribio ya kuweka mfumo wa Channels. Mfumo huu utawezesha makampuni, content creators, wataalam na brands mbalimbali kutengeneza Channels ambazo zitakuwa zinatoa updates na taarifa mbalimbali ndani ya mtandao wa WhatsApp.
Mabadiliko haya yataleta utaratibu mpya wa kufuatilia habari, na taarifa mbalimbali moja kwa moja ndani ya WhatsApp; badala ya kwenda Twitter, Instagram na Facebook ili kupata taarifa mbalimbali kama vile habari. Itaathiri soko la Telegram, ambayo inafanya vizuri kwa kuwa na Channels nyingi na kuanzisha mfumo wa Channels kabla ya app nyingine hazijaanza kuwa na Channels.

Mambo ambayo yatakwepo katika Channels za WhatsApp
- WhatsApp itakuwa na channels za news, team za mpira, vyombo vya habari, content creators, wasanii, brands mbalimbali, channels za kiserikali na aina mbalimbali ya channels ambazo zitakuwa zinatoa updates kwa watumiaji.
- Channels zitakuwa na button ya “Follow”
- Ukitaka kujitoa kwenye Channel, itakwepo option ya “Leave”
- Channels zitakwepo kwenye tab mpya ya “Updates” ambayo itakwepo kwenye tab ya Status.
- Message za kwenye Channels zitakuwa zinafutika baada ya Siku 30
- Admins watakuwa na uhuru wa kuzuia Screenshot zisifanye kazi kwenye Channels.
- Hautaweza kuona orodha ya watu ambao wame-follow channel.
- Hautaweza kuona namba za admins wa Channel
- Admin atakuwa na uhuru Channel iwe huru kwa kila mtu kujiunga au kuzuia isipatikane kwa watumiaji wote.
- Message za Channels sio encrypted hivyo WhatsApp inaweza kuziona. WhatsApp imesema inafanyia kazi mfumo wa encryption ambao utasaidia kuboresha usalama wa chats
- Status na Channels zitakaa pamoja na zitakwepo kwenye tab ambayo itaitwa “Updates”. Utaweza kuona Status za marafiki na kuangalia updates za Channels ambazo umejiunga nazo kwa pamoja. Tab ya Updates itakuwa na Channels na WhatsApp Status kwa pamoja.
- Meta imetangaza mfumo wa Channels utaanza rasmi kwa watumiaji wa WhatsApp na utaanza kwa watumiaji wa nchi za Colombia na Singapore.
- Itakuwa ni njia rahisi ya kutuma habari, na taarifa mbalimbali kwenye WhatsApp. Watumiaji hawatalazimika kutumia Instagram, Facebook au Twitter kufahamu nini ambacho kinaendelea.
- Itakuwa njia salama kwa sababu hauwezi kuona namba za admin na watu ambao wamejiunga kwenye channel.
- Channels zitarahisisha kwa wafanyabiashara kutangaza bidhaa zao na biashara.