What's the story: Ulipataje kazi unayofanya au uliyowahi kufanya?

Duuh..Umenikumbusha mbali.
Nakumbuka nilikuwa napita na bahasha mtaani huku nikiwa nawaangalia watu kwenye ofisi zao na jinsi wanavyoenjoy maisha. Siku moja nikakutana na rafiki yangu wa kitambo sana alikuwa kwenye taasisi fulani ya kifedha. Tukawa tunapiga stori mbili tatu za maisha huku nikijua atajiongeza ili walau akienda lunch na mimi anitoe kwa mchana huo.

Tukiwa tunaongea mara Meneja akapita kwani alikuwa ametoka. Rafiki yangu akaniambia yule ndio boss pale. Akanishauri nimuelezee boss hitaji langu la ajira anaweza kunisaidia. Basi nikamuacha akaenda halafu baadae tulipoachana na rafiki yangu, ushauri wake ukawa unajirudia mno akilini mwangu. Ilipofika alasiri nikawa napita tena pale nje ya ile taasisi ya fedha yaani, namshukuru Mungu kwa kunipa ujasiri. Nilimuendea yule meneja wakati akielekea kwenye gari lake na nikamueleza kila kitu na jinsi nilivokuwa na uhitaji wa kazi. Nashukuru kwani alinielewa na akaagiza CV yangu ipokelewe na iwekwe mezani kwake.

Siku moja baada ya miezi kama minne hivi kupita nikapigiwa simu kuwa nihudhurie interview. Kwa kweli nilihudhuria ni nikafaulu vizuri na wao wakanikubali. Nilipigiwa simu wiki moja baadae ya kuanza kazi baada ya kuwarudishia mkataba nilioujaza wa kazi.

Japo ilikuwa ni temporary lakini nilifurahi sana!
 
Pindi nimemaliza chuo wakati nasubiria ajira za serikali asee niliunganishiwa kazi moja hio ya part time na shem huko world vision asee kulikua na vijihela nje nje... Jamani Lile shirika acheni tu... Nilinenepa nikapasuka..
Badae ikatokea kazi permanent nikaapply nikaitwa kwenye interview hahaha kasheshe Ilikua kwenye interview field yangu haikumeet qualifications niliwekwa tu.. Nikapewa hadi possible za maswali ya written interview na shem nilifaulu songombingo Ilikua kwenye oral interview wakati huo kulikua na jopo la interviewers toka head office kama 5 hivi mweh ningepata Lile shavu saivi ningekua naongea mengine

Cc Smart911
 
Sio ya kwanza lakini kuna kazi niliwahi kupata kupitia JF jukwaa hili, kutokana na network nliyotengeneza wakati nipo hapo ikaniwezesha kupata kazi yenye maslahi zaidi ambayo ndio naendelea nayo.

JF ya siku hizi sio reliable kama ya kipindi hiko. Siku hizi kuna utapeli na matangazo ya kutembelea blog za watu.
 
Dah nmesoma hii thread nmejikuta natabasamu.... At my age ( less than 25 years ) nmeshafanya kazi sehemu tatu... Mmh mungu huyu jamaniii
Nkipata nafasi ntakuja kuelezea jinsi nlivyopata kazi zote moja baada ya nyingine sehemu zote na sababu ya kuacha.... Its interesting maana sikua na refa uko wala nna e mjua
 
zina chaji au kweupe?
 
Mimi baada ya kumaliza chuo harakati za kusaka ajira zikaanza nilisota kitaa kwa mwaka mmoja. Kipindi wakati bado nipo kitaa nikakutana mwanamke ambaye kwasasa ni mke wangu tukaanzisha uhusiano kipindi hicho, Maisha yakaendelea kusonga bila kutarajia nikampa ujauzito alipoulizwa akanitaja nikaitwa kwao kuulizwa nikakubali. Kwakuwa tulikuwa tunaishi mtaa mmoja na wazazi wangu na wake wanajuana wakakaa chini kuyajenga ikabidi nimuoe . Baada ya miezi mitatu nikiwa naishi na mke wangu tunalea mimba dada yake akaja kuniambia niende kwenye interview na copy za vyet ktk idara moja ya serikali nilipofika nilijitambulisha basi wakachukua copy wakaniambia nitoke nje baada wiki NNE nikapigiwa simu nilipoti kazini. Mpaka Leo nipo na kazi hiyo hiyo.
 
Usingempa mimba huyo binti,seem like nafasi ya kupata hiyo kazi ingekuwa ndogo..kuna vitu vinatokea kwa sababu
 
Mimi baada ya kumaliza chuo harakati za kusaka ajira zikaanza nilisota kitaa kwa mwaka mmoja. Kipindi wakati bado nipo kitaa nikakutana mwanamke ambaye kwasasa ni mke wangu tukaanzisha uhusiano kipindi hicho, Maisha yakaendelea kusonga bila kutarajia nikampa ujauzito alipoulizwa akanitaja nikaitwa kwao kuulizwa nikakubali. Kwakuwa tulikuwa tunaishi mtaa mmoja na wazazi wangu na wake wanajuana wakakaa chini kuyajenga ikabidi nimuoe . Baada ya miezi mitatu nikiwa naishi na mke wangu tunalea mimba dada yake akaja kuniambia niende kwenye interview na copy za vyet ktk idara moja ya serikali nilipofika nilijitambulisha basi wakachukua copy wakaniambia nitoke nje baada wiki NNE nikapigiwa simu nilipoti kazini. Mpaka Leo nipo na kazi hiyo hiyo.
Sometimes mlango wa mafanikio unakuja kwa njai ya ajab kabisa.
Imagine usingekutana na mke wako, mambo yangekuwaje mpaka sasa?
 
Back
Top Bottom