What was your worst experience with a bank? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

What was your worst experience with a bank?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Injinia, Nov 22, 2009.

 1. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakuu, hii nimeshindwa kuiweka kwenye forum ya "kero" kwa kuwa hata hivyo wahusika hawatasoma.

  Nataka kuzungumzia "my worst banking experience". Yaani benki ya Barclays London (makao makuu na matawi). Miezi 2 iliyopita nilifungua akaunti Barclays Knightsbridge (London) nikaambiwa baada ya siku 7 akaunti itakuwa tayari na nitatakiwa kuweka kiasi fulani cha fedha ili waweze kuendelea na mambo kama kunitengenezea kadi nk. Nikasubiri. Siku 7 zikapita, nikasema labda wamezidiwa kazi, mwezi ukapita (huku naendelea kufuatilia) mwishowe mwezi 1 baada ya ufunguzi huo ndio naambiwa akaunti tayari.

  Wakaanza kunitumia mara barua za faida za kuwa na akaunti kwao na mambo kama hayo...muda wote pesa iko kwao na mimi sina namna ya kuzitumia maana nia ilikuwa nitumie kadi kwa ajili ya malipo bila kutembea na fedha taslimu.

  Juzi Ijumaa, mieze 2 baadae ndio kadi inatumwa!!

  Sijawahi kuwa na "experience" mbaya kama hii hata nyumbani mikoani!! Nyumbani unafungua akaunti na muda si mrefu mambo yako tayari.

  Je kuna mwingine hapa JF aliyekutana na adha kama hii?
   
Loading...