kama kuna mtu ambae kashaumizwa na timu za kiafrika basi na mimi nimo,yani ukishangilia ni ugonjwa wa moyo ni sawa ukipenda sana halafu siku mwenzi wako anakufanya ukose raha na itakufanya usahau tena mambo ya kupenda,na si ajabu kuona kati ya timu 6 za afrika hakuna hata moja kuingia raundi ya 2 mana hata ghana nao naanza kuwa na wasiwasi nao kutokana na mechi yao vs watu 10 australia,na kesho wanacheza na ujerumani ambae kocha wao alikuwepo uwanjani kuwasoma ktk mechi ya ghana vs australia,mwaka 2002 kweli simba wa teranga walinifurahisha sana yani walijituma na kuweka utaifa mbele wakatolewa kwa bao la kifo robo fainali,ila sasa hivi basi tushangilie ila ukisema ndio unaziwekea dhamana hazidhaminiki utapata ugonjwa wa moyo,mfano mzuri wasauzi kocha sio tatizo,ila anapangiwa na viongozi wa tff yao yani safa,hata kuachwa benny mccarthy sio yeye bali viongozi na mashabiki,ukianzia listi anapangiwa inaenda kitimu eg kaizer chiefs wacheze kadhaa na orlando pirates,halafu siasa nyingi kuliko mpira yani hiyo black economic empowerment inaingizwa sana na kiasi hata kwanza booth hachezi,huyo sibaya nae hachezi kisa timu fulani kubwa ya sauzi lazima ktk 1eleven awepo mchezaji hata kama kiwango kidogo,cameroon etoo tu ndie anajituma anakosa msaidizi,nigeria mabrazameni sitaki hata kuwasikia,ivoria nao wanalewaga sifa sana hasa walipodroo na portugal wakaona soka wanajua na wasipoangalia wanaweza hata kufungwa na north korea mechi ya mwisho japo walikula 7-0 hao north korea jana,algeria hawatabiriki wakicheza na timu kubwa ila unaweza kushangaa wakicheza na hata bongo wanafungwa,ghana nao sio wabaya sana ila nao naona wanaambukizwa ubishoo wa kuridhika na waliidharau sijui australia baada ya kuona wamefungwa 4-0 na ujerumani?